2010–2019
Sala za Ukuhani na Binafsi
Aprili 2015


Sala za Ukuhani na Binafsi

Mungu anaweza kutupa nguvu katika ukuhani kwa hali yoyote tutakayokuwepo. Ila tu inatupasa tuombe kwa unyeyekevu.

Nina shukuru kwa kuaminiwa kuzungumza na wenye ukuhani wa Mungu katika ulimwengu mzima. Ninaujua uzito wa fursa hiyo kwa sababu ninajua kitu fulani cha imani ambacho Bwana amekiweka ndani yenu.-Pamoja na ridhaa yenu ya kukubali ukuhani, mlipokea haki ya kusema na kutenda katika jina la Mungu.

Haki hiyo inaweza kuwa ya uhakika tu mnapopokea maongozi kutoka kwa Mungu. Ndipo tu wakati huo mtaweza kusema katika jina Lake. Na wakati huo tu mnaweza kutenda katika jina Lake. Mnaweza kuwa mlifanya makosa ya kufikiri, “Ee, hiyo siyo ngumu sana. Ninaweza kupata maongozi ya kiungu tu kama nitaombwa nitoe hotuba au kama nitatakiwa kutoa baraka ya ukuhani.”Au shemasi mdogo, au mwalimu anaweza kuwa na faraja katika wazo, “Wakati nitakapo kuwa na umri mkubwa au nitakapoitwa kama mmisionari, ndipo nitakapojua nini Mungu angesema na nini Mungu angefanya.”

Tafakari siku ambapo lazima ujue nini Mungu angesema na nini Yeye angefanya. Imeshakuja kwetu sote po pote ulipo katika wito wako wa ukuhani. Nilikulia katika eneo la misheni katika Marekani mashariki wakati wa Vita Kuu vya Pili. Waumini wa Kanisa waliishi mbali mbali, na kulikuwa na mgao mkali wa mafuta ya Petroli. Nilikuwa shemasi pekee katika tawi. Waumini walitoa bahasha za matoleo ya mfungo kwa rais wa tawi wakati walipokuja kwenye mkutano wa mfungo na ushuhuda katika nyumba yetu.

Nilipokuwa na umri wa miaka 13, tulihamia Utah kuishi katika kata kubwa. Nakumbuka uteuzi wangu wa kwanza kutembelea majumbani kukusanya matoleo ya mfungo. Niliangalia jina kwenye moja ya bahasha na nikagundua jina la mwisho lilikuwa sawa na mmoja wa Mashahidi Watatu wa Kitabu cha Mormoni. Niligonga mlango kwa kujiamini. Mwanaume alifungua mlango, aliniangalia, alikuwa na hasira kwenye sura yake, na kisha akanifokea nimwondokee mbali. Niliondoka nimeinamisha kichwa chini .

Hiyo ilikuwa takribani miaka 70 iliyopita, lakini bado nakumbuka hisia nilizokuwa nazo siku ile juu ya ngazi za mlangoni na kwamba kulikuwa na kitu fulani nilipaswa kukisema au kufanya. Kama wakati ule ningesali kwa imani wakati naondoka kwenda kukusanya matoleo ya mfungo siku ile, ningeweza kupata maongozi ya kiungu na kusimama kwa muda zaidi kwenye ngazi zile za mlangoni, kutabasamu, na kusema kitu kama: “Imekuwa vizuri kukutana nawe. Asante sana kwa vile ambavyo wewe na familia yako mmeitoa siku zilizopita, Ninatazamia kuonana nanyi mwezi ujao.”

Ningesema na kufanya hivyo, angeweza kuwa amekasirishwa zaidi na hata kuudhika. Lakini najua jinsi ambavyo ningejisikia. Kuliko kujisikia huzuni nilipokuwa naondoka, Ningeweza kujiona mwenye sifa mzuri katika akili na moyo wangu: “Vizuri sana”

Sisi wote lazima tuseme na kutenda katika jina la Mungu katika wakati ambao maamuzi yetu yasio na msaada hayatatosha bila maongozi ya kiungu. Nyakati hizo zinawezakuja kututokea wakati hatuna muda wa kufanya matayarisho. Haya yamenitokea mara kwa mara. Yalinitokea miaka mingi iliyopita katika hospitali ambako baba alisema kwamba madaktari walikuwa wamemwambia kwamba binti yake wa miaka mitatu aliyeumia vibaya angekufa katika muda wa dakika chache. Wakati nilipomwekea mikono yangu kwenye eneo moja la kichwa chake lisilo funikwa na mabendeji, ilibidi nijue, kama mtumishi wa Mungu, nini angefanya na kusema.

Maneno yalikuja kwenye akili yangu na midomo kwamba angeishi. Daktari amesimama akidhihaki kwa sauti kubwa ya maudhi na akaniomba niondoke nimpishe. Nilitoka nje ya chumba cha hospitali ile nikiwa na hisia za amani na upendo. Msichana aliishi na alitembea katikati ya viti ndani ya mkutano wa sakramenti kwenye siku yangu ya mwisho katika jiji lile. Bado nakumbuka furaha na kuridhika nilikohisi kutokana na kile nilichosema na kufanya katika huduma ya Bwana kwa msichana yule mdogo na familia yake.

Tofauti katika hisia zangu pale hospitalini, na huzuni niliosikia wakati nikitembea kutoka mlango ule kama shemasi, zilikuja kutokana na kile nilichojifunza kuhusu uhusiano wa sala na nguvu za ukuhani wakati nilipokuwa shemasi, nilikuwa bado sijajifunza kwamba nguvu ya kusema na kufanya katika jina la Mungu inahitaji ufunuo, na kuwa nao wakati tunapouhitaji inataka kusali na kufanya katika imani kwa uwenza wa Roho Mtakatifu.

Jioni kabla sijaenda kwenye mlango ule kwa ajili ya matoleo ya mfungo, nilikuwa nimesali wakati wa saa ya kulala. Lakini kwa wiki kadha na miezi kabla ya mwito wa simu ile kutoka hospitalini, nilikuwa nimefuata mpangilio wa sala na nikafanya juhudi ambayo Rais Joseph F. Smith alifundisha itamruhusu Mungu kutupa maongozi ambayo ni yanafaaili kuwa na nguvu katika ukuhani. Yeye alisema wazi:

“Hatupaswi kumlilia kwa maneno mengi. Hatuna haja ya kumchosha kwa sala ndefu. Nini tunatakiwa kufanya, na nini tunapaswa kufanya kama Watakatifu wa Siku za Mwisho, kwa faida yetu, ni kwenda mbele zake mara kwa mara, kushuhudia kwake kwamba tunamkumbuka na kwamba tuko radhi kujichukulia juu yetu jina lake, kushika amri zake, kufanya kazi kwa haki.”1

Na kisha Rais Smith alituambia nini tunatakiwa kuomba, katika wajibu wetu kama watumishi wake tuliahidi kusema na kutenda kwa ajili ya Mungu. Alisema: “Nini unachokiomba? Unaomba kwamba Mungu aweze kukutambua, kwamba aweze kusikia sala zako, na kwamba anaweza kukubariki wewe na Roho Yake.”2

Sio sana jambo la maneno gani ya kutumia, lakini inatakiwa kuwa na subira kiasi. Ni mtazamo kwa Baba yako wa Mbinguni kwa dhamira ya kutambuliwa na Yeye binafsi. Yeye ni Mungu juu ya wote, Baba wa wote, na bado yuko tayari kutoa usikivu kwa mmoja wa watoto Wake. Hiyo inaweza kuwa kwa nini Mwokozi alitumia maneno, “Baba yetu uliye Mbinguni, jina lako litukuzwe.”3

Ni rahisi sana kupata hisia kamili za staha wakati unapopiga magoti au kuinamisha kichwa chako, lakini inawezekana kuhisi kwamba unamkaribia Baba yako wa Mbinguni katika njia kidogo isiyo rasmi na hata katika sala ya kimya, kama mara kwa mara utakavyofanya katika huduma yako ya ukuhani. Patakuwa na kelele na watu waliokuzunguka wakati wa muda wote unapokuwa umeamka. Mungu anasikia sala za kimya, lakini unaweza kutakiwa kujifunza kupuuza kuvutwa mawazo kwa sababu muda mfupi unaotaka kuungana na Mungu unaweza usije katika nyakati za ukimya.

Rais Smith alipendekeza kwamba utahitaji kusali ili Mungu aweze kutambua wito wako wa kumhudumia. Tayari anajua kuhusu wito wako kwa undani mkamilifu. Alikuita, na kwa kumwomba Yeye, kuhusu wito wako, atakufunulia zaidi ili uweze kujua.4

Nitawapeni mfano wa nini mwalimu wa nyumbani anaweza kufanya wakati anaposali. Unaweza kuwa tayari unajua kwamba unahitajika kufanya nini:

“Tembelea nyumba ya kila muumini, mkiwasihi kusali kwa sauti na kwa siri na kushughulikia wajibu wote katika familia. …

“ … Kulinda kanisa siku zote, na kuwa pamoja na kuwaimarisha;

“Na angalia kwamba hakuna uovu katika kanisa, wala ugumu baina yao, wala kudaganya, kusengenya, wala kusemeana maovu;

“Na ona kwamba kanisa linakutana pamoja mara kwa mara, na pia ona kwamba waumini wote wanafanya wajibu wao.”5

Sasa, hata kwa mwalimu wa nyumbani mwenye uzoefu na mwenza wake mdogo, hio ni wazi kabisa haiwezekani bila msaada wa Roho Mtakatifu. Fikiria juu ya familia au hata watu binafsi ulioitwa kuwahudumia. Kwa hukumu ya kibinadamu na dhamira nzuri bado havitatosha.

Kwa hiyo utasali kwa ajili ya njia ya kujua mioyo yao, kujua kwamba vitu gani visivyo vizuri katika maisha na mioyo ya watu usio wajua vizuri. Utahitajika kujua ni kitu gani Mungu angetaka ufanye kuwasaidia na kufanya yote kwa uwezo wako wote pamoja na kujua upendo wa Mungu kwa ajili yao.

Ni kwa sababu una umuhimu kama huu na miito migumu ya ukuhani ambayo Rais Smith anapendekeza kwamba wakati unaposali, siku zote umsihi Mungu ili akubariki ili uwe na Roho Wake. Utamhitaji Roho Mtakatifu, sio mara moja daima kama Mungu atakavyomruhusu kwako awe mwenza wako wa daima. Ndiyo sababu lazima siku zote tusali ili Mungu aweze kutuongoza katika huduma zetu kwa watoto Wake.

Kwa sababu hauwezi kuwa na nguvu za ukuhani bila Roho kuwa pamoja nawe, wewe ni lengo binafsi kwa adui wa furaha yote. Kama anaweza kukujaribu wewe kutenda dhambi, anaweza kupunguza nguvu yako ya kuweza kuongozwa na Roho na matokeo yake kupunguza nguvu yako katika ukuhani. Hiyo ndiyo sababu Rais Smith alisema kwamba hamna budi kila siku kusali ili Mungu aweze kukuonya na kukulinda dhidi ya uovu.6

Anatuonya katika njia nyingi. Maonyo ni sehemu ya mpango wa wokovu. Manabii, mitume, marais wa vigingi, maaskofu, na wamisionari wote wanapaza sauti ya kuonya ili kuepuka maafa kupitia imani katika Yesu Kristo, toba, na kufanya na kushika maagano matakatifu

Kama mwenye kushikilia ukuhani, wewe unatakiwa uwe sehemu ya sauti ya kuonya ya Bwana. Lakini unahitaji kusikiliza maonyo wewe mwenyewe. Wewe hautaweza kupona kiroho bila ulinzi wa wenza wa Roho Mtakatifu katika maisha yako ya kila siku .

Lazima usali kwa ajili ya hilo na mfanye kazi ili kumpata. Ni kwa mwongozo huo pekee ndivyo mtakavyoweza kuona njia hii nyembamba iliyosonga katikati ya ukungu wa giza. Roho Mtakatifu atakuwa kiongozi wenu anapofunua ukweli wakati unapojifunza maneno ya manabii.

Kupata mwongozo huo itahitaji zaidi ya kusikiliza na kusoma kwa kawaida. Utahitaji kusali na kufanya kazi kwa imani kuyaweka maneno ya ukweli chini katika sakafu za moyo wako. Lazima usali ili Mungu aweze kukubariki wewe kuwa na Roho Wake, kwamba atawaongozeni kwenye ukweli wote na kuwaonyesha njia sahihi. Hivyo ndivyo Yeye atakavyokuonya na kukuongoza kwenye njia sahihi katika maisha yako na katika huduma yako ya ukuhani.

Mkutano mkuu unatoa fursa kubwa kumwacha Bwana aimarishe nguvu yako ya kuhudumia katika ukuhani wa Mungu. Unaweza kujitayarisha mwenyewe kwa sala. Unaweza kuunganisha imani yako pamoja na hao ambao watasali. Watasali katika mkutano huu kwa ajili ya baraka nyingi juu ya watu wengi.

Watasali ili Roho aje juu ya nabii kama msemaji wa Bwana.Wataomba kwa ajili ya Mitume na watumishi wote walioitwa na Mungu. Hiyo inajumuisha na wewe kutoka shemasi mpya mpaka kuhani mkuu mwenye uzoefu na baadhi walio wazee na vijana ambao hivi karibuni watakwenda ulimwengu wa roho, ambako watasikia, “Vizuri sana, ewe mtumishi mwema na mwaminifu.”7

Maamkizi hayo yatakwenda kwa baadhi ambao watashangazwa nayo. Kamwe hawakushika ofisi ya juu katika ufalme wa Mungu duniani. Baadhi wangeweza kuhisi kwamba waliona matokeo madogo kutoka kwenye kazi yao au kwamba baadhi fursa za kusaidia kamwe hawakupewa.Wengine watahisi kwamba muda wao wa kuhudumia katika maisha haya haukuwa mrefu kama walivyotegemea.

Haitakuwa ofisi walizokuwa nazo au muda walio hudumia ambao utafikiriwa na Bwana. Tunajua hii kutoka Fumbo la Bwana la vibarua katika shamba la mizabibu ambako malipo yalikuwa sawa bila kujali muda gani walihudumia au wapi. Watazawadiwa kwa jinsi walivyohudumia.8

Ninamjua mtu, rafiki mpendwa, ambaye huduma yake katika shamba la mzabibu iliisha usiku wa jana saa 5:00. Amekuwa anatibiwa saratani kwa miaka mingi.Wakati wote wa miaka hii ya matibabu, na maumivu makali, matatizo, alikubali wito kuhudhuria mikutano ya kila wiki pamoja na kuwajibika kwa waumini katika kata yake ambayo watoto wao wameondoka mbali na nyumbani kwao; baadhi walikuwa wajane. Wito wake ulikuwa kuwasaidia kupata faraja katika jumuiya na mafunzo ya injili.

Wakati alipopata utabiri wa makini kwamba alikuwa na muda mfupi tu wa kuishi, askofu wake alikuwa mbali kwa matembezi ya kibiashara. Siku mbili baadaye, alituma ujumbe kwa askofu wake kupitia kiongozi wa kundi la makuhani wakuu. Yeye alisema hivi kuhusu kazi yake: “Ninaelewa askofu yupo nje ya mji, kwa hiyo ninafanya mipango nafikiria juu ya mkutano wa kikundi chetu jumatatu ijayo. Waumini wawili wanaweza kututembeza Kituo cha Mikutano. tunaweza kuwatumia baadhi ya waumini kuwaendesha katika gari na baadhi maskauti kusukuma viti mwendo. Kutegemea nani anajiandikisha, tunaweza kuwa na wazee wa kutosha kufanya hivyo wenyewe, lakini ingekuwa vizuri kujua tuna watu wa ziada wanaoweza kusaidia kama tukiwahitaji. Ingeweza pia kuwa usiku mzuri wa familia kwa wasaidizi kuleta familia zao vile vile. hata hivyo nifahamisheni kabla sijatuma mpango … Asanteni.”

Na kisha alimshangaza askofu kwa mwito wa simu. Bila kujali hali yake au juhudi zake za kijasiri, alisema, “Askofu, kuna chochote naweza kufanya kwa ajili yako?” Ni Roho Mtakatifu pekee angeweza kumruhusu kuhisi mzigo wa askofu wakati mzigo wake ulikuwa mkubwa mno., Na Roho pekee ndiye angeweza kufanya iwezekane kwa yeye kutengeneza mpango wa kuwa hudumia kaka zake na dada zake kwa usahihi ule ule aliotumia katika kupanga matukio ya Kiskauti wakati alipokuwa kijana.

Pamoja na sala ya imani, Mungu anaweza kutupa nguvu katika ukuhani kwa ajili ya hali yoyote tutakayokuwemo. Kiurahisi inahitaji kwamba tuombe kwa unyenyekevu ili Roho atuoneshe nini Mungu angependa sisi tuseme na kufanya, fanya hivi, na endelea kuishi ukiwa mwenye kustahili kipawa hicho.

Ninawatolea ushuhuda wangu kwamba Mungu Baba anaishi, anatupenda, na anasikia sala zetu. Ninatoa ushuhuda kwamba Yesu ndiye Kristo anaeishi, ambaye Upatanisho wake unafanya kuwezekana kwa sisi kusafishwa na kuweza kustahili wenza wa Roho Mtakatifu. Ninashuhudia kwamba pamoja na imani yetu na bidii tunaweza siku moja kusikia maneno ambayo yatatuletea furaha, “Vizuri Sana, ewe mtumishi mwema na mwaminifu.”9 Ninaomba kwamba tupokee hitimisho la ajabu kutoka kwa Bwana tunayemtumikia. Katika jina la Yesu Kristo, amina.