2010–2019
Kumtafuta Bwana
Aprili 2015


Kumtafuta Bwana

Ufahamu wetu wa Mwokozi unapopata kina, tutakuwa na ongozeko la hamu ya kuishi kwa furaha na imani kwa furaha inaweza kupatikana.

Wapendwa kaka na dada zangu, ni kwa furaha kubwa nasimama mbele yenu tunavyoshiriki katika huu mkutano mkuu kwa pamoja. Tukisikiliza maneno ya hekima, ushauri, ufariji, na maonyo yaliyotolewa kwenye mkutano mkuu kwa miaka mingi imekuwa baraka kubwa kwa Dada Teixeira, kwa familia yetu, na mimi mwenyewe.

Katika hiki kipindi muhimu cha mwaka, hasa katika Sabato hii ya Pasaka, Ninaweza kufikiria umuhimu wa mafundisho ya Mwokozi na mfano wa wema na upendo Wake katika maisha yangu.

Uelewa wa kina wa Yesu Kristo utatupa tumaini kuu kwa ajili ya siku za usoni na, bila kujali mapungufu yetu, kujiamini zaidi katika kutimiza malengo yetu ya haki. Hii itatupa hamasa kubwa katika kuwatumikia wanadamu wenzetu.

Bwana amesema, “Nitafute katika kila wazo; usiwe na shaka, usiogope.”1 Kutamfuta Bwana na kuhisi uwepo wake ni lengo la kila siku, ni juhudi zinazostahili.

Akina kaka na akina dada, leo zaidi ya wakati mwingine wo wote, tunazo mbele yetu fursa na rasilimali za kutuongezea uelewa wa mafundisho ya Yesu Kristo na Upatanisho wake. Kwa kutumia rasilimali hizi inavyofaa itatusaidi kuishi maisha yenye matunda na yaliyojawa na furaha.

Katika sitiari ya Mwokozi ya mzabibu na matawi, alisema: “Kaeni ndani yangu, nami ndani yenu. Kama vile tawi lisivyoweza kuzaa peke yake, lisipokaa ndani ya mzabibu; kadhalika nanyi, msipokaa ndani yangu.”2

Tunavyoelewa zaidi jukumu lisilo la kawaida la Kristo katika maisha yetu, ndivyo tunavyoelewa zaidi dhumuni la maisha katika dunia hii, ambalo ni kuwa na furaha. Furaha hiyo, hata hivyo, haituzuii sisi kupata majaribu na matatizo, hata mengine ni makubwa na magumu ambayo yanaweza kutusabishia kufikiria kwamba furaha haiwezekani katika mazingira kama haya.

Ninajua kwa uzoefu wangu binafsi kwamba furaha ya kuishi katika haki na kubaki ndani ya Kristo kunaweza kuendelea licha ya matatizo ya hali ya maisha ya duniani. Mwishowe, matatizo haya mara kwa mara yanaweza kuboresha, kutusafisha, na kutuongoza kwenye uelewa wa kina wa sababu ya kuishi kwetu na ya Upatanisho wa Yesu Kristo. Hakika, utimiilifu wa furaha unaweza kupatikana tu kupitia Yesu Kristo.3

Alisema, “Mimi ni mzabibu; ninyi ni matawi, akaaye ndani yangu nami ndani yake, huyo huzaa sana; maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lo lote.”4

Ninaamini kwamba tunavyomuelewa kwa undani Mwokozi, tunakuwa na matamanio yaliyoongezeka kuishi kwa furaha na uhakika kwamba furaha inawezekana. Matokeo yake, tutakuwa na uwezo mkubwa kuishi kila siku tukiwa na furaha ya maisha na kutii amri za Mungu, hata katika mazingira yenye changamoto.

Na tusiahirishe hadi kesho yale tunayoweza kufanya leo. Ni sasa tunapolazimika kuja kwa Kristo kwa sababu “kama tunamwamini, tunafanya kazi wakati bado inaitwa leo.”5

Kila siku, tufikirie kujumuisha maingiliano kila mara na mafundisho ya Kristo. Ishara ndogo na rahisi na matendo yanayofanywa kila siku yata:

  1. Ongeza uelewa wetu kwa kina wa umuhimu wa Bwana katika maisha yetu, na

  2. Utasaidi kushiriki uelewa huu na kizazi kinachochipuka, ambao kwa hakika watahisi upendo wa Baba Yetu wa Mbinguni na Mwanaye, Yesu Kristo, wanapoona mfano wetu wa kuishi injili kiukweli.

Kwa hivyo ni zipi baadhi ya tabia rahisi katika nyakati hizi za kisasa ambazo zitakuwa faraja katika mioyo yetu katika kuimarisha shuhuda zetu juu ya Kristo na huduma yake?

Picha
Woman on a train with a cell phone illuminating her face.

Mnamo mwaka 2014, mashindano ya National Geographic yalipokea maombi 9,200 ya wapiga picha wenye weledi na mashabiki kutoka Zaidi ya nchi 150.  Picha iliyoshinda inaonyesha mwanamke akiwa katikati ya gari moshi lililojaa abiria. Mwanga unaotoka kwenye simu yake ya rununu inaangaza uso wake. Anawapokeza abiria wengine ujumbe wazi: licha kuwa yupo hapo kimwili, kwa kweli hayupo hapo.6

Data ya vifaa vya mkononi, simu za kisasa, na mitandao ya kijamii vimebadilisha kwa kiasi kikubwa jinsi ya kuwa duniani na jinsi tunavyowasiliana na wengine.

Katika kipindi hiki cha digitali, tunaweza kujisafirisha kwa haraka sana kwenda sehemu na kuwa na shughuli ambazo zinaweza kwa haraka kutuondoa kutoka kwenye yale yaliyo muhimu kwa maisha yaliyojawa na furaha isiyo na mwisho.

Maisha haya yaliounganishwa yanaweza, kama hayataangaliwa, yanaweza kuwapa nafasi ya kwanza watu ambao hatuwajui au hatujakutana nao, badala ya watu ambao tunaishi nao---familia zetu wenyewe!

Kwa namna nyingine, wote tunajua kwamba tumebarikiwa na rasilimali nzuri sana za mitandao, ikijumuisha zile ambazo zimetengenzwa na Kanisa kama vile matoleo ya maandishi na sauti ya maandiko matakatifu na mkutano mkuu, matengenezo ya video ya maisha na mafundisho ya Yesu Kristo, apu ya kunakili historia ya familia zetu, na fursa ya kusikiliza miziki wenye kuinua.

Uamuzi na vipaumbele tunavyofanya na muda wetu tukiwa kwenye mitandao yanaleta hamasa. Inaweza kuamua ukuaji wetu kiroho na kukomaa katika injili na matamanio yetu kuchangia katika kuboresha dunia na kuishi maisha yaliyo na mazao.

Kwa sababu hizo, ningependa kutaja tabia tatu rahisi ambazo zitaleta shughuli nzuri za mitandaoni. Tabia hizi zitajenga tathimini ya kila siku katika maisha ambazo ni muhimu kwetu kukua na kuwa karibu na mafundisho ya Baba Yetu wa Mbinguni na Mwanaye, Yesu Kristo.

Tabia ya 1: Tembelea Mtandao Rasmi wa Kanisa kwa ajili ya Raslimali.

Mara kwa mara kutembelea wakati wa wiki katika raslimali hizi zitatusaidia daima kuwa makini kwenye mafundisho ya injili na kuwatia moyo wanafamilia na marafiki kufikiria na kuangalia nini cha muhimu zaidi.

Tabia ya 2: Jiunge na Mitandao Rasmi ya Kijamii ya Kanisa

Maamuzi haya yataleta kwenye scrini zetu maudhui ambayo ni muhimu katika kuongeza uangaliaji na kumtafuta Bwana na mafundisho Yake na yataimarisha dhamira yako ya kuielewa injili. Cha muhimu zaidi, hii yatakusaidia kukumbuka kile ambacho Kristo anakitegemea kwa kila mmoja wetu.

Kama vile “Hakuna udongo mzuri bila mkulima mzuri,”7 vivyo hivyo hakutakuwa na mavuno ya mtandaoni mpaka tutoe kipaumbele kutoka mwanzo ambacho kinafikika katika vidole vyetu na katika akili zetu.

Tabia namba 3: Kuwa na Muda wa Kuweka Vyombo Vyetu vya Mkononi Pembeni.

Inafurahisha kuweka pembeni vyombo vyetu vya mkononi kwa wakati na badala yake kufunua kurasa za maandiko au kuwa na muda wa kuzungumza na familia na marafiki zetu. Hasa katika siku ya Bwana, pata amani ya kushiriki katika mikutano ya sakramenti bila hamu ya kuona kama una ujumbe au posti mpya.

Tabia ya kuweka vyombo vyetu vya mkononi pembeni kwa wakati itaboresha na kutanua mtazamo wetu wa maisha, kwani maisha hayawekwi kwenye scrini ya inchi nne (10 cm).

Bwana Yesu Kristo alisema, “Kama vile Baba alivyonipenda mimi, ndivyo nami nilivyowapenda ninyi, kaeni katika pendo langu.”8 Mungu anataka tuwe na furaha na kuuhisi upendo Wake. Kristo anafanya furaha hiyo kuwezekana kwa kila mmoja wetu. Tunayo njia ya kumjua zaidi na kuishi injili Yake.

Natoa ushuhuda wangu wa furaha iliyopo tunapotii amri na amani na usalama tunayopata wakati tunapoishi katika upendo wa Baba Yetu wa Mbinguni na Mwanae, Mwokozi wetu. Katika jina la Yesu Kristo, amina.