2010–2019
Kaa karibu na Mti
Aprili 2015


Kaa karibu na Mti

Ono la Lehi la mti wa uzima ni fumbo la nguvu la kuvumilia hadi mwisho.

Muda mfupi kabla ya Rais Heber J. Grant kufariki, mmoja ya Wazee alimtembelea nyumbani kwake. Kabla ya kuondoka, Rais Grant aliomba, “Ee Mungu, nibariki kwamba nisipoteze ushuhuda wangu na niwe mwaminifu hadi mwisho!”1 Baada ya karibu miaka 27 kama Rais wa Kanisa, hii ilikuwa sala yake ya dhati. Mfano wake ni ukumbusho wenye nguvu ambao hakuna mtu, katika miaka hii, ambaye ana kinga ya vishawishi vya shetani. Vifaa viwili vya nguvu vya shetani ni kuchanganya na ulaghai.

Kuvumilia hadi mwisho ni sifa bainifu ya ufuasi wa kweli na ni muhimu kwa maisha ya milele. Lakini majaribu na changamoto zijapotujia, mara kwa mara tunaambiwa kwa urahisi “shikilia hapo hapo.” Acha niwe wazi, “kuskikilia hapo hapo” siyo kanuni ya injili. Kuvumilia hadi mwisho inamaanisha kuja kwa Kristo kila mara na kufkamilishwa ndani Yake.

Kama kuvumilia hadi mwisho ni muhimu kwenye uzima wa milele. Kwa nini tunatatizika kuwa waaminifu? Tunapata kutatizika tunapokuwa na vipaumbele vinavyoshindana. Utii bila kuwa na umakini na ahadi vuguvugu hudhoofisha imani. Kuvumilia hadi mwisho kunahitaji sharti kamili kwa Mwokozi na kwenye maagano yetu.

Ono la Lehi la mti wa uzima fumbo la nguvu la kuvumilia hadi mwisho. Tafadhali kwa maombi jifunze na kutafakari ndoto ya Lehi; halafu ifananishe nawe. Ufanyapo hivyo, kwa makini fikiria kanuni sita za muhimu ambazo zitakusaidia kuvumilia hadi mwisho.

1. Usisahau kusali

Tunaanza na Lehi peke yake “penye giza na ukiwa wa jangwa.”2 Kila mmoja wetu hupata vipindi vya kiza na upweke. “Maisha yanapokuwa kiza na kuchosha, usisahau kusali.”3 Fuata mfano wa Rais Heber J. Grant. Sali kwa ajili ya nguvu kuendelea kuvumilia hadi mwisho. Mwombe Baba wa Mbinguni, “Ungetaka nifanye nini zaidi?”

2. Njoo kwa Kristo na Ukamilishwe Ndani Yake.

Mti wa uzima ni kiini cha ndoto ya Lehi. Kila kitu kinalenga mti wa uzima, Mti unawakilisha Kristo, ambaye ni dhihirisho wazi la upendo wa Mungu. Tunda ni Upatanisho usiokuwa na mwisho na ni ushahidi mkuu wa upendo wa Mungu. Maisha ya milele na wapendwa wetu ni matamu na yanatamanisha zaidi ya kitu chochote. Kupata kipawa hiki, sharti “tuje kwa Kristo na tukamilishwe ndani Yake.”4 Yeye ndiye njia, kweli na uzima.”5 Tunaweza kujaza maisha yetu na ufanisi wetu na mema yetu, lakini mwishowe, kama hatutaingia katika maagano matukufu kumfuata Kristo kwa imani kuyaweka, tutakuwa tumeshindwa kuelewa kabisa lengo letu.

3. Songa Mbele kwa Imani

Kuna njia inayoongoza mpaka kwenye mti wa uzima, kwa Kristo. Ni njia nyoofu na nyembamba, kali na halisi. Amri za Mungu ni kali lakini hazina kizuizi. Zinatulinda kutoka kwenye hatari za kiroho na kimwili na kutuzuia tusipotee.

Utii hujenga imani katika Kristo. Imani ni kanuni ya tendo na nguvu. Kufuata mifano ya Kristo kila mara hujenga nguvu ya kiroho na uwezo. Bila nguvu ya kuimarisha na kuwezeshwa ya Upatanisho, haiwezekani kukaa katika njia na kuvumilia.

“Songa mbele ukiwa imani imara katika Kristo.”6

2. Kitabu cha Mormoni ni Ufunguo wa Kunusurika Kiroho

Safari ya maisha ni changamoto. Ni rahisi kuchanganywa, ukatangatanga nje ya njia na kupotea. Matatizo lazima yatakuja na ni sehemu muhimu ya kukua kwetu milele. Dhiki inapokuja, usiruhusu kitu ambacho haukielewi kikamilifu, kuharibu kila kitu unachojua. Kuwa na subira, shikilia ukweli; uelewa utakuja. Majaribu ni kama kiza kinene ambacho kinaweza kutupofusha na kuifanya mioyo yetu kuwa migumu. Isipokuwa “tushikilie sana”7 kwenye neno la Mungu, na kuliishi, tutapofushwa kiroho badala ya kuwa na mtazamo ya kiroho. Tafuta katika Kitabu cha Mormoni na maneno ya manabii wanaoishi kila siku, kila siku, kila siku! Ni ufunguo wa kuponwya kiroho na kuyashinda majaribu. Bila hiyo, tumepotea kiroho.

5. Usichanganywe na kudanganywa

Kujihadhari ni kuwa makini sana. Kujihadhari na wale ambao hawaamini katika Kristo haitakusaidia kumpata. Kutafuta #jengopana kwa ajili ya uelewa haitakupelekea kwenye ukweli. Haipatikani pale. Mwokozi pekee ndiye mwenye “maneno ya uzima wa milele.”8” Kila kitu kingine ni maneno tu. Jumba kubwa na lenye nafasi linaashiria “mawazo yasiyofaa na kiburi”9” cha dunia, kwa maneno mengine, kuchanganya na udanganyifu. Limejaa na watu waliovalia vizuri ambao wanaonekana kuwa na kila kitu. Lakini wanamdhihaki Mwokozi na wale wanaomfuata. “Wakijifunza siku zote, ila wasiweze kabisa kuufikia ujuzi wa kweli.”10 Wanaweza kuwa sahihi kisiasa, lakini wamepotea kiroho.

6. Kaa kwenye Mti

Ujumbe wa Lehi ni kukaa kwenye mti. Tunakaa kwa sababu tumeongolewa kwa Bwana. Alma alifundisha, “Tazama, aliibadilisha mioyo yao; ndio, aliwaamsha kutoka katika usingizi mzito, na wakaamka katika Mungu.”11 Tunaposalimisha mioyo yetu kwa Mungu, Roho Mtakatifu anabadilisha uhalisi wetu, tunaongolewa kindani kwa Bwana, na hatutafuti jengo pana. Kama tutaacha kufanya mambo haya ambayo hutuletea uongofu wa ndani, tunarudi nyuma kiroho. Ukengeufu ni kinyume cha uongofu

Kwa wamisionari wote wa wakati uliopita na wa sasa: Wazee na kina Dada, humwezi kamwe kurudi kutoka katika misheni yenu, na kuruka kama bata katika Babeli, na kutumia masaa yasiyoisha ukipata alama zisizo na maana katika michezo ya video isiyo na maana bila kuanguka katika usingizi mzito kiroho. Wala humwezi kujiingiza katika ponografia za mitandaoni na kudharau maadili na usafi bila matokeo mabaya ya kiroho. Kama utapoteza Roho, umepotea. Usichanganywe na kulaghaiwa.

Wafuasi wa kweli wanaendelea kuamka katika Mungu kila siku katika sala binafsi ya maana, kusoma maandiko kwa maana maalumu, utiifu binafsi, na huduma isiyo na choyo. Kaa karibu na mti na ukae macho.

Miaka michache iliyopita, Dada Pearson nami tuliitwa kusimamia kwenye misheni ya Washington Tacoma. Mwito huu ulikuwa wa kushangaza sana. Nikiwa na wasiwasi kiasi nilikutana na mwenyekiti na Mkuu wa kampuni ambako nilikuwa nimeajiriwa na kuwaarifu kuhusu wito wangu. Kiwaziwazi walikasirishwa na uamuzi wangu wa kuachana na Kampuni. “Ulifanya lini maamuzi haya, na kwa nini hukujadiliana nasi mapema?” walitaka kujua.

Katika wakati wa uwazi, jibu la ajabu lilikuja akilini mwangu. Nilisema, “Niliufanya uamuzi huu nilipokuwa kijana wa miaka 19, nilipofanya maagano matakatifu na Mungu hekaluni ya kumfuata Mwokozi. Nimejenga maisha yangu yote katika maagano hayo, na ninakusudia kabisa kuyatii sasa.”

Mara tuingiapo kwenye agano na Mungu, hakuna kurudi nyuma. Kukubali kushindwa, kuacha na kupoteza nguvu siyo mbadala. Katika ufalme wa Mungu, kuna kanuni ya ubora kwa ajili ya kuinuliwa. Inahitaji wafuasi jasiri! Hakuna sehemu ya wafuasi wa wastani au wasiojali. Wastani ni adui wa ubora, na sharti la wastani litakuzuia kuvumilia hadi mwisho.

Kama unasumbuka, umechanganyikiwa, au umepotea kiroho, nakuomba ufanye kitu kimoja kitakachokufanya urudi kwenye njia sahihi. Anza tena kwa maomi kusoma Kitabu cha Mormoni na kuishi mafundisho yake, kila siku, kila siku, kila siku! Nashuhudia nguvu ya ajabu iliyopo kwenye Kitabu Cha Mormoni kwamba itabadilisha maisha yako kutia nguvu matamanio yako kumfuata Kristo. Roho Mtakatifu atabadilisha moyo wako, na kukusaidia kuona “vitu kama vilivyo.”12 Atakuonyesha kile unachohitaji kufanya baada ya hapo. Hii ni ahadi ya Nefi kwako:

“Na nikawaambia kwamba….yeyote atakayesikiliza hilo neno la Mungu na alizingatie hataangamia; wala majaribu na mishale ya moto ya adui kuwalemea na kuwapofusha ili kuwaelekeza kwenye maangamio.

“Kwa hivyo, Mimi…niliwasihi kwamba wasikilize neno la Mungu na wakumbuke kutii amri zake kila wakati katika vitu vyote.”13

Akina Ndugu na Dada, kuvumilia hadi mwisho ni mtihani mkubwa wa ufuasi. Ufuasi wetu wa kila siku utaamua hatima ya milele. Amkeni katika Mungu, mshikilie ukweli, kushika maagano matakatifu ya hekaluni, na kaa karibu na mti!

Nashuhudia kuhusu Kristo aliyefufuka, anayeishi. Ninajua kuwa Yeye anaishi. Tamanio langu kuu ni kwamba niwe mkweli na mwaminifu hadi mwisho katika kufuata mifano yake iliyotukuka. Katika jina takatifu la Yesu Kristo, amina.