2010–2019
Kipawa cha Neema
Aprili 2015


Kipawa cha Neema

Leo na milele neema ya Mungu inapatikana kwa wote ambao mioyo yao imevunjika na ambao roho zao zimepondeka

Siku ya Jumapili ya Pasaka tunaadhimisha tukio kuu tukufu liliosubiriwa zaidi katika historia ya ulimwengu.

Ni siku ambayo ilibadilisha kila kitu.

Siku hiyo,maisha yangu yalibadilika

Maisha yako yalibadilika

Kudra ya watoto wote wa Mungu ilibadilika..

Siku ile iliyobarikiwa, Mwokozi wa wanadamu, ambaye alikuwa amejichukulia mwenyewe minyororo ya dhambi na kifo ambavyo vilitushika mateka, alivunja ile minyororo na kutuweka huru.

Kwa sababu ya dhabihu ya mpendwa Mkombozi wetu, kifo hakina uchungu, kaburi halina ushindi,1 Shetani hana nguvu ya kudumu, na sisi ni wale “tuliozaliwa … mara ya pili ili tupate tumaini lenye uzima kwa kufufuka kwake Yesu Kristo.”2

Kwa kweli, Mtume Paulo alikuwa sahihi wakati aliposema tunaweza “kufarijiana kwa maneno haya.”3

Neema ya Mungu

Mara nyingi tunasema kuhusu Upatanisho wa Mwokozi---na ni sahihi kufanya hivyo!

Katika maneno ya Yakobo, “Kwa nini usizungumziwe upatanisho wa Kristo, na kupata ufahamu kamili kwake? ”4 Lakini “tunazungumza kuhusu Kristo, … tunafurahia katika Kristo, … tunahubiri kuhusu Kristo, [na] tunatoa unabii kumhusu Kristo”5  katika kila fursa,  lazima tusipoteze kamwe akili zetu za heshima na shukrani kuu za dhabihu ya milele ya Mwana wa Mungu.

Upatanisho wa Kristo hauwezi kuwa wa kawaida katika mafundisho yetu, mazungumzo yetu, au katika mioyo yetu. Ni mtukufu na mtakatifu, kwani ulikuwa kupitia dhabihu hii kubwa na ya mwisho kwamba Yesu Kristo alileta wokovu kwa wale ambao wataamini katika jina lake.”6

Ninastaajabu, kufikiri kwamba Mwana wa Mungu angejishusha hadhi kutuokoa sisi, wanadamu tusiowatimilifu, wachafu, wenye kuelekea kufanya makosa, na tusio na shukrani kama tulivyo kila mara. Nimejaribu kuelewa Upatanisho wa Mwokozi kwa akili zangu finyu, na maelezo pekee ninayoweza kutoa ni kwamba Mungu anatupenda kwa kina sana, kikamilifu, na kwa milele. Na siwezi hata kuanza kukisia “upana, na urefu, na kina, na kimo…  [cha]upendo wa Kristo.”7

Onyesho la nguvu la upendo huo ni kile maandiko kila mara yanakiita neema ya Mungu—usaidizi wa kiungu na endaumenti kwa uwezo ambao tunakua kutoka viumbe walio na kasoro na wenye ufinyu sasa hata kuwa viumbe vilivyotukuzwa vya “kweli na nuru,mpaka [tutakapo] tukuzwa katika kweli na [kujua] mambo yote.”8

Neema hii ya Mungu ni ya ajabu sana. Ila, kila mara imekuwa haieleweki.9 Hata hivyo, tunapaswa kujua kuhusu neema ya Mungu kama tunadhamiria kurithi kile kilichotayarishwa kwa ajili yetu katika ufalme Wake wa milele.

Kwa sababu hiyo ningependa kuzungumza kuhusu neema. Hususani, kwanza, jinsi neema hufungua milango ya mbinguni   na pili, jinsi hufungua madirisha ya mbinguni.

Kwanza: Neema Hufungua Milango ya Mbinguni

Kwa sababu sote tumetenda “dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu”10 na kwa sababu “hakuna kitu chochote kichafu kinachoweza kuingia katika ufalme wa Mungu,”11 kila mmoja wetu hastahili kurudi kwenye uwepo wa Mungu.

Hata kama tulikuwa tumhudumie Mungu kwa roho zetu zote, haitoshi; kwani tutakuwa bado “watumishi wasioleta faida.”12 Hatuwezi kupata njia yetu kwenda mbinguni; madai ya haki yanasimama kama kizuizi, ambacho hatuna nguvu ya kukishinda sisi peke yetu.

Lakini vyote havijapotea

Neema ya Mungu ni matumaini yetu makubwa na ya milele.

Kupitia kwa dhabihu ya Yesu Kristo, mpango wa rehema unatosheleza matakwa ya haki13 “na [inasababisha] njia kwa wanadamu kuwa na imani ya toba.”14

Dhambi zetu, hata zikiwa nyekundu, zinaweza kuwa nyeupe kama theluji.15 Kwa sababu Mwokozi wetu mpendwa “alijitoa fidia kwa wote,”16 mlango wa kuingikia ufalme Wake wa milele umetolewa kwetu.17

Mlango umefunguliwa!

Lakini neema ya Mungu haiturejeshi tu kwenye hali yetu iliyopita isiyo na hatia. Kama wokovu unamaanisha kufuta makosa yetu na dhambi tu, basi wokovu---wa ajabu kama ulivyo---haukamilishi malengo makubwa kwa ajili yetu. Lengo lake ni la juu zaidi: Anataka wana na mabinti wake kuwa kama Yeye alivyo.

Kwa zawadi ya neema ya Mungu, njia ya uanafunzi haiturudishi tu nyuma kwenye hali ya mwanzo bali inatusaidia kuwa bora zaidi.

Inaongoza kwenye viwango vya kina ambavyo hatuwezi kuelewa! Inaongoza kwenye kuinuliwa katika ufalme wa selestia wa Baba yetu wa Mbinguni, ambako sisi, tukizungukwa na wapendwa wetu, tunapokea utimilifu wake, na wa utukufu wake.”18 Vitu vyote ni vyetu, na sisi ni wa Kristo.19 Kwa hakika vyote alivyonavyo Baba yangu vitatolewa kwetu.20

Ili kurithi utukufu huu, tunahitaji zaidi ya mlango uliofunguliwa; ni lazima tuingie kupitia mlango huu kwa tamaa ya moyo kubadilishwa---mabadiliko ya kuvutia ambayo maandiko yanaelezea kama kuzaliwa mara ya pili; “ndio wazaliwe na Mungu, wabadilishwe kutoka katika hali yao ya [kimwili] na ya kuanguka, kwa hali ya utakatifu na kukombolewa na Mungu, na kuwa wana na mabinti zake.”21

Pili: Neema Hufungua Madirisha ya Mbinguni

Sifa nyingine ya neema ya Mungu ni ufunguzi wa madirisha ya mbinguni, kupitia hayo Mungu humwaga baraka za uwezo na nguvu, kutuwezesha sisi kutimiza vitu ambavyo vinginevyo vitakuwa mbali tusikoweza kufika. Ni kwa neema ya kushangaza ya Mungu ambayo watoto wake wanaweza kushinda mikondo chini kwa chini na kinamasi cha mdanganyifu, kushinda dhambi, na “wakamilishwa katika Kristo.”22

Ingawa sisi wote tuna udhaifu, tunaweza kuushinda. Kwa kweli ni kwa neema ya Mungu kwamba, kama tunajinyenyekeza wenyewe na kuwa na imani, vitu dhaifu vinaweza kuwa vya nguvu.23

Kote maishani mwetu, neema ya Mungu inatoa baraka ya maisha haya na vipawa vya kiroho ambavyo vinaongeza uwezo wetu na vinarutubisha maisha yetu. Neema Yake inatutakasa. Neema Yake inatusaidia sisi kuwa bora zaidi wenyewe.

Nani anaweza Kustahili?

Katika Biblia tunasoma kuhusu ziara ya Kristo nyumbani kwa Simoni Mfarisayo.

Kwa nje,Simoni alionekana kuwa mwema na mtu mwadilifu. Mara nyingi alikamilisha orodha ya wajibu wote wa kidini ambao alikuwa nao: alitii sheria, alilipa zaka, aliitakasa Sabato, alisali kila siku na kwenda katika singagogi.

Lakini wakati Yesu alipokuwa pamoja na Simoni, Mwanamke aliwakaribia, akaosha miguu ya Mwokozi kwa machozi yake, na akapaka miguu Yake kwa mafuta mazuri

Simoni hakufurahishwa na onyesho hili la kuabudu, kwani alijua kwamba mwanamke huyu ni mwenye dhambi. Simoni alifikiri kama Yesu hakujua hili,lazima hawezi kuwa Mtume au Asingeweza kumwacha mwanamke huyu amguse.

Akitambua mawazo yake, Yesu alimgeukia Simoni na alimwuliza swali. “Palikuwa na mkopeshaji fulani ambaye alikuwa na wadeni wawili,” Mmoja alimdai senti mia tano, mwingine hamsini.

Na wakati [wote] walikuwa hawana chochote cha kulipa, kwa kusema kweli aliwasamehe wote wawili. Niambie baada yahapo,Yupi kati yao atakayempenda zaidi?”

Simoni alijibu kwamba alikuwa yule aliyesamehewa zaidi.

Kisha Yesu akafundisha somo la maana sana: “Unamwona mwanamke huyu? … Dhambi zake ambazo ni nyingi, zimesamehewa; kwani alipenda sana: bali kwa yule aliyesamehewa kidogo, huyo huyo hupenda kidogo.”24

Yupi kati hawa watu wawili tunayefanana naye?

Je! Tuko kama Simoni? Tunajiamini na tumefarijika katika matendo yetu mazuri, tukiamini katika wema wetu wenyewe? Huenda hatuna subira na hao ambao hawafanyi mambo yote mazuri ambayo tunafanya tukiruhusu matendo yetu kujiongoza yenyewe, kufanya vitu fulani bila kuvifikiria, kuhudhuria mikutano yetu, darasa la Kanuni za Injili hata kama tunaliona linachosha na kuangalia simu zetu za viganjani wakati wa ibada ya Sakramenti?

Au tuko kama mwanamke huyu, ambaye alifikiri alikuwa kabisa na bila tumaini lolote amepotea kwa sababu ya dhambi?

Je! Tunapenda sana??

Je! Tunaelewa deni letu kwa Baba wa Mbinguni na kusihi kwa nafsi zetu zote kuomba neema ya Mungu?

Wakati tunapopiga magoti kusali, je ni kukumbuka mambo bora tuliyofanya ya wema wetu wenyewe, au ni kuungama makosa yetu, kukiri kwa ajili ya neema ya Mungu, na kutoa machozi ya shukrani kwa ajabu ya mpango mkuu wa ukombozi?25

Wokovu hauwezi kupatikana kwa sarafu ya utii; unanunuliwa kwa damu ya Mwana wa Mungu.26 Kufikiria kwamba tunaweza kupata wokovu kwa sababu ya kazi zetu nzuri ni kama kununua tiketi ya ndege na kisha kudhania tunamiliki shirika la ndege. Au kufikiri kwamba baada ya kulipa pango kwa nyumba yetu, sasa tunashikilia hati miliki kwa sayari yote ya dunia.

Kwa Nini Basi Tutii?

Kama neema ni kipawa cha Mungu, kwa nini basi utii kwa amri za Mungu ni muhimu sana? Kwa nini kusumbuka na amri za Mungu---au toba, kwa njia hiyo? Kwa nini tusikubali kwamba tuna dhambi na kumwacha Mungu atuokoe?

Au, kuweka swali katika maneno ya Paulo, “Tuendele katika dhambi,ili neema iweze kujaa?”Jibu la Paulo lilikuwa rahisi; “La, Hasha.”27

Ndugu na akina dada, tunatii amri za Mungu---kwa sababu ya mapenzi yetu Kwake!

Kujaribu kuelewa zawadi ya neema ya Mungu kwa mioyo yetu yote na akili inatupa sisi sote sababu nyingi zaidi kumpenda na kumtii Baba yetu wa Mbinguni kwa upole na shukrani. Wakati tunapotembea njia ya ufuasi, inatutakasa, inatuendeleza, inatusaidia sisi kuwa zaidi kama Yeye alivyo, na inatuongoza sisi turudi kwenye uwepo wake. “Roho ya Bwana [Mungu wetu]” inasababisha mabadiliko makuu ndani yetu, … kiasi kwamba hatuna mpango kufanya uovu, bali kuendelea kufanya mema.”28

Kwa hiyo, utii wetu kwa amri za Mungu unakuja kama matokeo ya asili upendo wetu usioisha na shukrani kwa wema wa Mungu. Desturi hii ya upendo wa kweli na shukrani kimiujiza utaungana na kile tunachokifanya kwa neema ya Mungu. Siku zote kitakuwa ndani ya mawazo yetu na imani yetu itakuwa yenye nguvu katika uwepo wa Mungu.29

Wapendwa ndugu na akina dada, kuishi injili kwa imani sio mzigo. Ni mazoezi ya furaha---matayarisho ya kurithi utukufu mkuu wa milele. Tunajitahidi kumtii Baba yetu wa Mbinguni kwa sababu roho zetu zitakuwa zenye kupokea mambo ya kiroho. Tutaelewa mambo ambayo hata hapo hawali kamwe hatukuyafikiria. Elimisho na uelewa unakuja kwetu wakati tunapofanya mapenzi ya Baba.30

Neema ni kipawa cha Mungu, na hamu yetu kuwa watiifu kwa kila amri ya Mungu ni njia tunayomwachia Baba wa Mbinguni kujua tunataka kupokea zawadi hii ya takatifu kutoka kwa Baba yetu wa Mbinguni

Yote Tunaweza Kufanya

Nabii Nefi alifanya mchango muhimu kwa uelewa wetu wa neema ya Mungu wakati alipotangaza: “Tunafanya kazi kwa bidii… kuwashawishi watoto wetu, na pia ndugu zetu, kumwamini Kristo, na kupatanishwa na Mungu; kwani tunajua kwamba ni kwa neema kwamba tunaokolewa, baada ya kutenda yote tunatoweza.31

Hata hivyo, ninashangaa kama wakati mwingine tunatoa tafsiri isiyo sahihi ya msemo “baada ya yote tunayoweza kufanya.”Lazima tuelewe kwamba “baada” haina maana sawa na “sababu ya”

Hatuokolewi “kwa sababu” ya yote yale ambayo tunaweza kufanya. Kuna yoyote kati yetu amefanya yote ambayo tunaweza kufanya? Je Mungu anasubiri mpaka tumetumia nguvu zote kabla hajaingilia kati ya maisha yetu na neema yake ya uokoaji?

Watu wengi hujisikia kukatishwa tamaa kwa sababu wanashindwa kufanya yote ambayo yanategemewa.Wanajua kutoka uzoefu binafsi kwamba “Roho kwa kweli imedhamiria, bali mwili ni dhaifu.”32  Walipaza sauti zao pamoja na Nefi katika kutangaza, “Roho yangu unahuzunika kwa sababu ya uovu wangu.”33

Nina hakika Nefi alijua neema ya mwokozi inaturuhusu na inatuwezesha kushinda dhambi.34 Hii ndiyo sababu Nefi alifanya kazi kwa bidii sana kushawishi watoto wake na ndugu “kuamini katika Kristo, na kupatanishwa na Mungu.”35

Hata hivyo, hiyo ndiyokile tunachoweza kufanya! Na hiyondiyo kazi yetu katika maisha haya!

Meema Inapatikana Kwa Wote

Ninapofikiri ya kile Mwokozi alichofanya kwa ajili yetu muda mfupi kabla Jumapili ile ya Kwanza ya Pasaka, ninataka kupaaza sauti na kupiga kelele za sifa kwa Mungu Aliye juu na Mwanawe, Yesu Kristo!

Milango ya mbinguni inefunguliwa!

Madirisha ya mbinguni yako wazi!

Leo na milele neema ya Mungu inapatikana kwa wote ambao mioyo yao imevunjika na ambao roho zao zimepondeka.36 Yesu Kristo alisafisha njia kwa ajili yetu kufanikisha kiwango cha kukua ambacho akili zetu za maisha hata haziwezi kuelewa.37

Ninaomba kwamba tutapata kuona kwa macho mapya na mioyo mipya umuhimu wa milele wa dhabihu ya upatanisho ya Mwokozi. Ninaomba kwamba tutaonyesha upendo wetu kwa Mungu na shukrani zetu kwa zawadi isiyo na kikomo ya neema ya Mungu kwa kutii amri zake na kwa furaha “tuenende katika upya wa uzima.”38  Katika jina takatifu la Bwana wetu na Mkombozi,Yesu Kristo, amina.