2010–2019
Kwa hivyo Wakatuliza Woga Wao
Aprili 2015


Kwa hivyo Wakatuliza Woga Wao

Tofauti na woga wa kilimwengu ambao huzua taharuki na hofu, woga kiungu ni chanzo cha amani, hakikisho na kujiamini.

Ninakumbuka kwa dhahiri uzoefu niliokuwa nao nilipokuwa mvulana mdogo. Siku moja nikiwa ninacheza pamoja na rafiki zangu, kwa bahati mbaya nilivunja dirisha la duka karibu na nyumbani kwetu.Wakati kioo kilipovunjikavunjika na king’ora cha ulinzi kikalia kwa sauti kubwa, hofu ya kuduwaza ikajaa katika mawazo yangu na fahamu zangu. Nilitambua mara moja kwamba nimetiwa hatiani kuishi salio la maisha yangu jela.Wazazi wangu hatimaye walinishawishi kutoka kwenye sehemu niliyojificha chini ya kitanda changu na wakanisaidia kukubali makosa yangu. Kwa bahati mzuri, sikuhitajika kwenda jela kwa kosa langu.

Hofu niliyoisikia siku ile ilikuwa ya kuangamiza na halisi. Bila shaka mmewa hikupata uzoefu wa hisia kubwa za woga baada ya kuelewa kuhusu suala la changamoto ya afya binafsi, kugundua kwamba mwanafamilia anapitia matatizo au yuko hatarini, au kuangalia matukio yanayovuruga ya Ulimwengu. Katika mifano kama hii mshituko unaotia hofu unatokea kwa sababu ya tishio la hatari, kutokuwa na uhakika, au maumivu na uzoefu kamili ambao hautegemewi, wakati mwingine ghafla, na yaelekea kutoa matokeo hasi.

Maisha yetu ya siku zote,taarifa za makosa ya jinai, njaa, vita, ufisadi, ugaidi, kupotea kwa uadilifu, ugonjwa, na nguvu uharibifu za asili zinaweza kusababisha woga na wasiwasi. Hakika tunaishi katika wakati ambao Bwana alitabiri: “Na katika siku ile … ulimwengu wote utakuwa katika ghasia, na watu watavunjika mioyo kwa hofu” (M&M 45:26).

Kusudi langu ni kueleza jinsi woga unavyoondolewa kupitia imani na uelewa sahihi katika Bwana Yesu Kristo. Naomba kwamba Roho Mtakatifu atubariki kila mmoja wetu wakati tunapofikiri pamoja mada hii muhimu.

Hofu ya Mauti

Waliposikia sauti ya Mungu baada ya kula tunda lililokatazwa,Adamu na Hawa walijificha katika bustani ya Edeni. Mungu alimwita Adamu na akamwuliza, “Uko wapi? Na [Adamu Alijibu], Nilisikia sauti yako… na niliogopa” (Mwanzo 3:9–10). Iwekwe maanani kwamba, mojawapo ya matokeo ya anguko ilikuwa ni kwa Adamu na Hawa kupata uzoefu wa woga. Msisimko huu mkubwa ni msingi muhimu wa kuwepo kwetu duniani.

Mfano kutoka kitabu cha Mormoni unatilia maanani nguvu ya uelewa kuhusu Bwana (ona 2 Petro 1:2–8; Alma 23:5–6) katika kuondoa woga na kutoa amani hata kwa wakati tunapokumbana na matatizo mazito.

Katika nchi ya Helamu,Watu wa Alma walitishwa na jeshi la Walamani ambalo lilikuwa linawajia.

“Na Alma aliwaendea na kusimama miongoni mwao, na kuwasihi kwamba wasiogope, lakini … wamkumbuke Bwana Mungu wao na atawakomboa.

“Kwa hivyo wakatuliza woga wao” (Mosia 23:27–28).

Tazama Alma hakutuliza woga wa watu. Isipokuwa, Alma aliwashauri waumini kumkumbuka Bwana na ukombozi Yeye tu angetoa (ona 2 Nefi 2:8). Na uelewa wa Mkombozi kuwalinda kwa uangalifu uliwawezesha watu kutuliza woga wao.

Uelewa sahihi na imani katika Bwana unatuimarisha kutuliza woga wetu kwa sababu Yesu Kristo ni chanzo pekee cha kudumu cha amani. Alitangaza, “Jifunze kwangu, na sikiliza maneno yangu; enenda katika unyenyekevu wa Roho wangu, na utapata amani kwangu” (M&M 19:23).

Bwana pia alieleza, “Lakini, jifunzeni kwamba yule afanyaye kazi za haki atapokea ujira wake, hata amani katika ulimwengu huu, na uzima wa milele katika ulimwengu ujao.”(M&M 59:23).

Imani na matumaini katika Kristo na utayari wa mategemeo kwenye matendo Yake mema, rehema, na hisani yanaongoza kwenye mategemeo kupitia upatanisho Wake, katika ufufuo Wake na maisha ya milele (ona Moroni 7:41). Imani kama hii na mategemeo vinakaribisha katika maisha yetu dhamiri njema ya amani ya kufurahisha ambayo sote tunatamani kuwa nayo. Nguvu ya upatanisho inafanya toba kuwezekana na inatuliza kukata tamaa kunakosababishwa na dhambi, pia inatuimarisha kuona, na kuwa wema katika njia ambazo hatungeweza kutambua au kufanikisha uwezo wetu mdogo. Kwa kweli, mojawapo wa baraka kuu ya ufuasi wa uaminifu ni “amani ya Mungu, ipitayo akili zote” (Wafilipi 4:7).

Amani ambayo Kristo anatoa inatuwezesha sisi kutazama maisha ya hapa duniani kupitia taswira ya thamani ya milele na hutoa uthabiti wa kiroho Wakolosai 1:23) ambao unatusaidia sisi kudumisha daima kuzingatia kwenye makusudio yetu ya kimbinguni. Hivyo, tunaweza kubarikiwa kutuliza woga wetu kwa sababu fundisho lake linatoa sababu na mwelekeo katika vipengele vyote vya maisha yetu. Maagizo yake na maagano yanaimarisha na kufariji katika wakati wa mzuri na mabaya. Na mamlaka ya ukuhani Wake yanatoa uhakika kwamba mambo ambayo ni muhimu zaidi yanaweza kuendelea kwa wakati huu na milele.

Lakini tunaweza kutuliza woga ambao kwa urahisi na mara kwa mara unatusumbua katika ulimwengu wetu wa kisasa? Jibu kwa swali hili ni wazi ndio. Kanuni tatu kuu za msingi za kupokea baraka hii ya kutuliza woga katika maisha yetu(1) Kumtazamia Kristo, (2) ) kujenga juu ya msingi wa Kristo, na (3) kusonga mbele na imani katika Kristo.

Kumtazamia Kristo

Ushauri ambao Alma alimpa mwanawe Helamani kwa uhakika unahusu kila mmoja wetu leo: “Ndio, ona kwamba umeelekeza jicho kwa Mungu na uishi.” (Alma 37:47). Hatuna budi kutegemea na kuwa na uzingativu wetu umelenga imara juu ya mkombozi wakati wote na katika sehemu zote.

Kumbuka jinsi Mitume wa Bwana walipokuwa kwenye meli, ikirushwarushwa katika bahari. Yesu aliwaendea, akitembea juu ya maji; lakini hawakumtambua, wakapiga mayowe kwa woga.

“Yesu akasema nao, akasema, muwe wenye furaha; ni mimi; msiogope.

“Na Petro akamjibu na akasema,Bwana, kama ni wewe, niambie mimi nije kwako juu ya maji.

“Na alimwambia, njoo” (Mathayo 14:27–29).

Kisha Petro akatembea juu ya maji kwenda kwa Yesu.

“Lakini alipoona upepo wa nguvu, akawa na woga, alianza kuzama,” na akapiga yowe: “Bwana, niokoe.

“Na mara moja Yesu akanyoosha mkono wake, na akamshika,na akamwambia, Ewe mwenye imani haba mbona uliona shaka?” (Mathayo 14:30–31).

Ninamwona Petro akijibu kwa shauku kubwa na mara moja kwa mwaaliko wa Mwokozi. Akiwa macho yake amekaza kwa Yesu, Alitoka kwenye mashua na kimuujiza akatembea juu ya maji. Ni wakati ule tu macho yake yalipovutiwa kwingine kwa upepo na mawimbi ndipo alipokuwa mwoga na kuanza kuzama.

Tunaweza kubarikiwa kushinda woga wetu na kuimarisha imani zetu tunapofuata maelekezo ya Bwana : “Nitegemeeni katika kila wazo; msitie shaka, msiogope.” (M&M 6:36).

Kujenga juu ya Msingi wa Kristo

Helamani aliwaasa wanawe Nefi na Lehi, “Na sasa wanangu, kumbukeni, kumbukeni kwamba ni juu ya mwamba wa Mkombozi wetu, ambaye ni Kristo, Mwana wa Mungu, kwamba lazima mjenge msingi wenu; kwamba ibilisi atakapotuma mbele pepo zake kali, ndio, mishale yake kimbungani, wakati wa mvua yake ya mawe na dhoruba kali itapiga juu yenu, hautakuwa na uwezo juu yenu kuwavuta chini kwenye shimo la taabu na msiba usioisha, kwa sababu ya mwamba ambako kwake mmejengwa, ambao ni msingi imara, msingi ambako watu wote wakijenga hawataanguka” (Helamani 5:12).

Ibada na maagano ni matofali ya kujengea tunayoyatumia kujenga maisha yetu juu ya msingi wa Kristo na Upatanisho Wake. Tumeunganishwa kwa uthabiti kwenye na pamoja na Mwokozi wakati tunapostahili kupokea maagizo na kuingia kwenye maagano, kwa uaminifu tukikumbuka na kuheshimu ahadi hizo takatifu, na kufanya kadiri ya uwezo wetu kuishi kwa kukubaliana pamoja na wajibu tuliokubali. Na kwamba sharti hilo ni chanzo cha nguvu ya kiroho na udhabiti katika hali zote za maisha yetu.

Tunaweza kubarikiwa kutuliza woga wetu tunapojenga kwa imara matamanio yetu na matendo juu ya msingi wa uhakika wa Mwokozi kupitia ibada zetu na maagano.

Kusonga Mbele kwa Imani katika Kristo

Nefi alitangaza: “Kwa hiyo, lazima msonge mbele mkiwa na imani imara katika Kristo, mkiwa na mn’garo mkamilifu wa tumaini, na upendo kwa Mungu na wanadamu wote. Kwa hiyo, kama mtasonga mbele, mkila na kusherehekea neno la Kristo na mvumilie hadi mwisho, tazama, hivi ndivyo asema Baba: Mtapokea uzima wa milele.” (2 Nefi 31:20).

Uvumilivu wa nidhamu iliyoelezwa katika aya hii ni matokeo ya uelewa wa kiroho na ono, msimamo, uvumilivu, na neema ya Mungu. Kuwa na imani katika na juu ya jina takatifu la Yesu Kristo, kwa unyenyekevu kujitolea kwa mapenzi Yake na wakati Wake katika maisha yetu, na kwa unyenyekevu kukubali ushawishi wake katika matokeo ya mambo yote ukweli kuhusu ufalme wa Mungu unaojenga amani ya Mungu ambao unaleta furaha na uzima wa milele (ona M&M 42:61). Hata wakati tunapokumbana na matatizo na kukabiliana na mashaka ya baadaye, tunaweza kuvumilia kwa furaha na kuishi “maisha ya utulivu na amani, katika utawala wote na ustahivu” (1 Timotheo 2:2).

Tunaweza kubarikiwa kutuliza woga wetu tunapopokea nguvu ambazo zinakuja kutokana na kujifunza na kuishi kanuni za injili na pamoja na uamuzi wa kusonga mbele katika kufanya na kuweka maagano pamoja na Bwana.

Woga kuhusu Bwana

Tofauti na lakini wenye uhusiano na woga tunaokumbana nao ni ule ambao maandiko yanauelezea kama “Ufalme usioweza kutetemeshwa” (Waebrania 12:28) au “Woga wa Bwana” (Ayubu 28:28; Mithali 16:6; Isaya 11:2–3). Tofauti na woga wa kilimwengu ambao husabisha hofu na dukuduku, ufalme usioweza kutetemeshwa ni chanzo cha amani, uhakika, na matumaini.

Lakini ni vipi chochote kinachohusishwa na woga kiadilishe au kuwa chenye msaada kiroho?

Woga wa kiadilisha ninaojaribu kuuelezea unajumuisha hisia ya ndani ya unyenyekevu, heshima na kumcha Bwana Yesu Kristo Zaburi 33:8; 96:4), utii wa amri Zake (ona Kumbukumbu la Torati 5:29; 8:6; 10:12; 13:4; Zaburi 112:1), na matazamio ya Hukumu ya Mwisho na haki mikononi mwake. Hivyo, woga wa Mungu unakuwa kutoka kwenye uelewa sahihi wa utukufu wa asili na ujumbe wa Bwana Yesu Kristo, utayari wamapenzi yetu kumezwa na mapenzi Yake, na uelewa kwamba kila mwanaume na mwanamke atawajibika kwa dhambi zake mwenyewe Siku ya Hukumu (ona M&M 101:78; Makala ya Imani 1:2).

Kama maandiko yanavyoshuhudia, woga wa kiuungu “ni mwanzo wa maarifa” (Mithali 1:7), “maelekezo ya hekima” (Mithali 15:33), “tumaini imara” (Mithali 14:26), na chemichemi ya maisha” (Mithali 14:27).

Tafadhali kumbuka kwamba kumcha Mungu kumeunganishwa na hakuwezi kutenganishwa kutoka uelewa wa Hukumu ya Mwisho na uwajibikaji wetu binafsi kwa tamaa zetu, mawazo, maneno na matendo Mosia 4:30). Kumcha Bwana si uoga wa wasiwasi kuhusu kuja kwenye uwepo Wake kuhukumiwa. Siamini kwamba tutamwogopa Yeye hata kidogo. Badala yake, ni wazo kwamba tutakuwa katika uwepo wake kukabiliana na mambo katika uhalisia wake kuhusu sisi wenyewe na kuwa na “ufahamu kamili” (2 Nefi 9:14; ona pia Alma 11:43) kwenye urazini wetu wote, unafiki, na njia ambazo tumejidanganya wenyewe, hatimaye tutakuwa hatuna kisingizio.

Kila mtu aliyeishi au atakayeishi duniani “ataletwa kusimama mbele ya kiti cha hukumu cha Mungu, kuhukumiwa na yeye kulingana na matendo yake kama ni mema au kama ni maovu” (Mosia 16:10). Kama hamu zetu zimekuwa zenye haki na matendo yetu mema, basi kiti cha hukumu kitakuwa ni tukio la kufurahisha (ona Yakobo 6:13; Enoshi 1:27; Moroni 10:34). Na katika siku ya mwisho “tutazawadiwa kwa haki” (Alma 41:6).

Hata hivyo, kama tumetamani maovu na matendo yetu ni maovu, basi kiti cha hukumu kitatutia woga. Hatutaweza kumwangalia Mungu wetu katika hali hii mbaya; na tutukuwa na furaha kama tungeweza kuamuru miamba na milima ituangukie ili itufiche kutoka kwa uwepo wake” (Alma 12:14). Na katika siku ya mwisho tutapata zawadi [yetu] ya uovu” (Alma 41:5).

Kama ilivyofupishwa katika Mhubiri:

“Mwogope Mungu, na tii amri zake; kwani hii ni kazi nzima ya mtu.

“Kwa maana Mungu ataleta hukumuni kila kazi, pamoja na kila neno la siri, likiwa jema au likiwa baya. (Mhubiri 12:13–14).

Ndugu na dada zangu wapendwa, woga wa kiungu huondoa na maisha ya mauti. Hata kunashinda jambo ambalo kamwe hatuwezi kuwa angalau wema kiroho na kamwe hatuwezi kukamilisha mahitaji na mategemeo ya Bwana. Kwa kweli, hatuwezi kuwa angalau wema kidogo au kutimiza kile tunachohitaji tukitegemea u uwezo wetu wenyewe na utendaji. Kazi zetu na matamanio yetu peke yake havituokoi sisi. “baada ya kutenda yote tunayoweza.” (2 Nefi 25:23), tunafanywa kamili tu kupitia huruma na neema vinavyopatikana kupitia dhabihu ya upatanisho ya Mwokozi isiyo na kikomo na ya milele (ona Alma 34:10, 14). .Kwa hakika, “tunaamini kwamba kwa njia ya upatanisho wa Kristo, wanadamu wote wanaweza kuokolewa, kwa kutii sheria na ibada za injili” (Makala ya Imani 1:3).

Kumcha Mungu ni kupenda na kumwamini Yeye. Tunapomcha Mungu zaidi kabisa, kikamilifu zaidi. Na “upendo ulio kamili hutupa nje hofu” (Moroni 8:16). Ninaahidi mwanga angavu wa kumcha Mungu utafukuza mbali vivuli vyeusi vya woga wa maisha ya mauti (ona M&M 50:25) Tunapomwangalia Mwokozi,jenga juu Yake kama msingi wetu,na songa mbele juu ya njia yake ya maagano pamoja na ahadi iliyotukuka.

Ushuhuda na Ahadi

Ninampenda na kumstahi Bwana. Uwezo wake na amani ni vya kweli.Yeye ni Mkombozi wetu, na ninashuhudia kwamba anaishi. Na kwa sababu Yake, mioyo yetu isifadhaike wala tusiwe na woga (ona Yohana 14:27), na tutabarikiwa kuzuia woga wetu. Ninashuhudua kwamba hii ni kweli katika jina takatifu la Yesu Kristo, amini.