2010–2019
Tutapaa Pamoja
Aprili 2015


Tutapaa Pamoja

Kama wanawake na wanaume washikao maagano, tunahitaji kuinuana na kusaidiana kuwa watu Bwana angetaka tuwe.

Pamoja na hotuba za kuvutia, muziki, na maombi ambayo daima hugusa mioyo yetu wakati wa mkutano mkuu, nimeambiwa na kina dada wengi kwamba kile wanachokipenda zaidi ni kuwatazama Urais wa Kwanza na Akidi ya wale Kumi na Wawili wanapoondoka jukwaani na wenzi wao wa milele. Na Je, hatupendi sote kusikia kina Ndugu hawa wa Ukuhani wakielezea kwa upole upendo wao kwao wenzi wao?

Picha
President Boyd K. Packer and his wife, Donna, at the Brigham City Utah Temple cornerstone ceremony, 23 September 2012.

Akimzungumza kuhusu mke wake, Donna, Rais Boyd  K. Packer alisema, “Kwa sababu ya jukumu nililonalo, nina wajibu mtakatifu wa kusema ukweli: Yu mkamilifu.”1

Picha
President Dieter F. Uchtdorf and his wife.

“Yeye ndiye uchangamfu wa maisha yangu,” 2 alisema Rais Dieter F. Uchtdorf kumhusu mke wake, Harriet.

Picha
President Henry B. Eyring and Sister Eyring at their wedding.

Rais Henry B. Eyring, akitoa mrejeo kwa mke wake, Kathleen, alisema, “Ni mtu ambaye daima amenifanya kutaka kuwa bora sana kadiri niwezavyo.”3

Picha
LDS Church President Thomas S. Monson gives his wife, Frances, a kiss at their 60th anniversary celebration, 10/6/2008, at the Lion House. The two met in 1944 and were married in the Salt Lake Temple on Oct. 7, 1948.

Na Rais Thomas S. Monson, akimzungumzia mpendwa wake Frances, alisema: “Alikuwa mpenzi wa maisha yangu, mwenzi wangu niliyemuamini, na rafiki yangu wa karibu kabisa. Kusema kwamba nitamkosa haianzi hata kuelezea kina cha hisia zangu.”4

Mimi pia ningependa kuelezea upendo wangu kwa mwenzi wangu mpendwa, Craig. Yeye ni zawadi ya thamani kwangu! Nikifanya marejeo kwa mume wangu, fungu la thamani na tukufu katika baraka yangu ya kipatriaki inaahidi kwamba maisha yangu na ya watoto wangu “yatatunzwa vyema naye.” Ni wazi kwangu kwamba Craig ni timizo la ahadi hiyo. Nikitumia maneno ya Mark Twain, ninasema kwamba “maisha bila [Craig] hayangekuwa maisha.”5 Ninampenda, moyo na roho!

Nafasi na Wajibu Mtakatifu

Leo ningependa kuwapa heshima waume, kina baba, ndugu, wana, na wajomba ambao wanajua wao kina nani na wanafanya wawezavyo ili kutekeleza wajibu wao waliopewa na Mungu kama ilivyoelezewa katika tangazo la familia, ikiwa ni pamoja na kuongoza kwa haki na kukimu mahitaji ya familia na kulinda familia zao. Tafadhali jueni kwamba nina ufahamu wa kina kwamba mada ya ubaba, umama, na ndoa yaweza kutatanisha wengi. Ninajua kwamba baadhi ya waumini wa Kanisa wanahisi nyumba zao hazitawahi kufikia kile wanachodhania kuwa bora. Wengi wanaumia kwa sababu ya kupuuzwa, kupigwa, ufungwa, na mila na tamaduni zisizo-sahihi. Sikubaliani na vitendo vya wanaume ama wanawake ambao kwa mapenzi yao ama kwa kupuuza wamesababisha uchungu, dhiki na kukata tamaa katika nyumba zao. Lakini leo ninazungumzia jambo lingine.

Ninaamini kwamba mume huwa havutii zaidi kwa mke wake kuliko wakati anahudumu katika wajibu wake aliopewa na Mungu kama mwenye ukuhani anayestahili---muhimu kabisa nyumbani. Ninapenda na kuamini maneno haya kutoka kwa Rais Packer kwa wanaume na kina baba wanaostahili: “Mna nguvu ya ukuhani moja kwa moja kutoka kwa Bwana kulinda nyumba yenu. Kutakuwa na nyakati ambapo chote kinachosimama kama ngao kati ya familia yenu na uovu wa adui kitakuwa nguvu hiyo.”6

Viongozi na Walimu Kiroho katika Nyumba

Mapema mwaka huu nilihudhuria mazishi ya mtu asiye wa---kawaida, aliyekuwa wa kipekee, mjomba wa mume wangu Don. Mmoja wa wana wa Mjomba Don alitusimulia tukio alilokuwa nalo kama mtoto mdogo, punde baada ya wazazi wao kununua nyumba yao ya kwanza. Kwa sababu kulikuwa na watoto watano wadogo wa kuwalisha na kuwavalisha, hakukuwa na pesa za kutosha kuweka fensi. Akichukuwa kwa uzito mojawapo wa wajibu wake mtakatifu kama mlinzi wa familia yake, Mjomba Don aliweka vikingi kadhaa vidogo vya mbao kwenye ardhi, akachukua kamba kiasi, na kufunga kamba kutoka kigingi kimoja hadi kingine kuzunguka eneo la nyumba. Kisha aliwaita watoto wake kwake. Aliwaonyesha vigingi na kamba na akawaelezea kwamba wakibaki ndani ya eneo lililojengwa, wangekuwa salama.

Siku moja walimu watembeleaji walitazama kwa mshangao walipokuwa wanakaribia nyumba na kuona watoto watano wadogo wakisimama kwa kutii kwenye mpaka wa kamba, wakiangalia kwa tamaa mpira uliokuwa umepita mpaka wao na kufikia barabarani. Mtoto moja mdogo alikimbia kumchukua baba yao, ambaye, alitoka, na kukimbia na kuuchukua ule mpira.

Baadaye katika mazishi, mwana mkubwa kabisa kwa majonzi alielezea kwamba yote aliyowahi kutumaini maishani mwake ni kuwa kama babake mpendwa.

Picha
Sister Burton's son and grandson reading together.

Rais Ezra Taft Benson alisema:

“Enyi, waume na kina baba katika Israeli, mnaweza kufanya mengi kwa ajili ya wokovu na kuinuliwa kwa familia zenu! …

Kumbuka wajibu wako mtukufu kama baba katika Israeli---wajibu wako muhimu zaidi duniani na milele---wito ambao kamwe hautawahi kupumzishwa.”

Picha
Sister Burton's son and grandson on a bed together.

Lazima usaidie kuunda makazi ambamo ndani yake Roho wa Bwana anaweza kuishi.”7

Maneno hayo ya kinabii yanatumika kweli siku za leo.

Ni lazima itakuwa vigumu sana, kama inawezekana, kwa wanaume wa agano kuishi katika ulimwengu ambao si tu haukandamizi nafasi na majukumu yao matakatifu lakini pia unatuma ujumbe usio kweli kuhusu kile kinachomaanisha kuwa “ni mwanaume wa kweli.” Ujumbe moja wa uongo ni kwamba “Yote yananihusu mimi.” Kwenye upande mwingine ni ujumbe wa kudharau na kukejeli kwamba waume na kina baba hawahitajiki tena. Ninawaomba msisikilize uongo wa Shetani! Amekosa fursa tukufu ya kuwahi kuwa mume ama baba. Kwa sababu ana wivu juu ya wale ambao wana wajibu mtukufu ambao hatawahi kuwa nao, ana nia ya kufanya “wanadamu wote … na huzuni kama yeye alivyo!”8

Kuinua na Kusaidia katika Wajibu Wetu Unaosaidiana

Kaka na dada zangu, kila mmoja anamhitaji mwenzake! Kama wanawake na wanaume wa agano, tunahitaji kuinuana na kusaidiana kuwa watu ambao Bwana angetaka tuwe. Na tunahitaji kufanya kazi pamoja kuinua kizazi chipukizi na kuwasaidia kufukia uwezo wao wa kiungu kama warithi wa maisha ya milele. Tunaweza kufanya kama vile Mzee Robert D. Hales na mkewe, Mary, wamefanya na kufuata mithali “Niinue nami nikuinue, na tutapaa pamoja.”9

Tunajua kutoka katika maandiko kwamba “si vyema kwa mtu … awe peke yake” Hiyo ndio sababu Baba Yetu wa Mbinguni aliumba “msaidizi wa kufanana naye.”10 Kishazi msaidizi wa kufanana naye kinamaanisha “msaidizi aliyekuwa bora kwake, aliyemstahili, ama sawa na yeye.”11 Kwa mfano, mikono yetu miwili inafanana lakini si sawa kabisa. Kwa kweli, ni kinyume ya kila moja, lakini inasaidiana na inafaana. Ikifanya kazi pamoja, inakuwa na nguvu zaidi.12

Katika sura juu ya familia, kitabu cha mwongozo wa Kanisa kuna kauli hii: “Asili ya roho za kiume na kike ni kwamba zinakamilishana.”13 Tafadhali tambua kwamba inasema “zinakamilishana,” si ”kushindanana”! Tuko hapa kukusaidiana, kuinuana, na kushangiliana kila mmoja tunapojaribu kuwa bora tuwezavyo. Dada Barbara B. Smith alifundisha kwa busara, ”Kuna furaha zaidi wakati tunapoweza kufurahia katika mafanikio ya mtu mwingine na si tu katika mafanikio yetu wenyewe.”14 Tunapotafuta ‘kukamilishana” badala ya ”kushindana,” ni rahisi sana kuhimizana kusonga mbele!

Nilipokuwa mama kijana wa watoto kadhaa wadogo, mwisho wa siku iliyojaa kubadilisha nepi, kuosha sahani, na kufundisha nidhamu, hakuna aliyeimba kwa msisitizo zaidi wimbo wa Msingi ”I’m Happy When Daddy Comes Home.”15Ninasikitika kukubali sikuwa na furaha kila mara wakati Craig alipoonekana kuingia nyumbani baada ya siku ya kazi ngumu. Daima alitusalimia sote kwa kutukumbatia na busu na alizigeuza siku nyingi ngumu na wakati mwingine mbaya kuwa nyakati za kupendeza za baba. Natamani ningeshughulika kidogo tu na orodha isiyoisha ya vitu vya kufanya ambavyo havikuwa vimefanywa bado na ningehimiza kwa busara zaidi, kama alivyofanya yeye, vitu vilivyo na maana zaidi. Ningesimama mara nyingi na kufurahia nyakati tukufu za familia na ningemshukuru mara nyingi zaidi kwa kubariki maisha yetu!

Acha Tusemezane Maneno Mema Kila Mara

Si kitambo sana, dada mwaminifu katika Kanisa alinisimulia wasiwasi mkubwa aliokuwa anaombea kwa muda. Wasiwasi wake ulikuwa juu ya baadhi ya kina dada katika kata yake. Aliniambia jinsi ilivyomvunja moyo kuona kwamba wakati mwingine walikuwa wakiwazungumzia bila heshima waume wao na kuhusu waume wao, hata mbele ya watoto wao. Kisha aliniambia jinsi kama msichana aliyekuwa ametamani kwa dhati na kuomba kupata na kuolewa na kuhani aliyestahili na kujenga familia yenye furaha pamoja naye. Alikuwa amelelewa katika nyumba ambapo mamake alikuwa amedhibiti nyumba na babake alikuwa amejinyenyekeza katika matakwa ya mamake ili kuendeleza amani nyumbani. Alihisi kwamba kulikuwa na njia bora. Hakuwa ameona kielelezo chake katika nyumba aliyolelewa, lakini aliomba kwa moyo wake kwa ajili ya mwongozo, Bwana alimbariki kujua jinsi ya kujenga nyumba na mumewe ambapo Roho angealikwa vyema. Nimekuwa ndani ya nyumba hiyo na ninaweza kushuhudia ni mahali pa takatifu!

Dada zangu na kaka zangu, ni mara ngapi kwa kusudi sisi “huneneana “maneno mema”?16

Tunaweza kujitahini wenyewe kwa kujiuliza maswali machache. Kwa kubadilisha kidogo, maswali haya yanaweza kutumika kwa kila moja wetu, iwe tumeoa au kuolewa ama hatujaoa na bila kujali hali yetu ya nyumbani.

  1. Ni lini mara ya mwisho nilimsifu mwenzi wangu kwa dhati, aidha peke yangu ama mbele ya watoto wetu?

  2. Ni lini mara mwisho nilimshukuru, nilielezea upendo wangu kwake, ama kuomba kwa dhati na kwa imani kwa ajili yake katika sala?

  3. Ni lini mara ya mwisho nilijisimamisha mwenyewe kusema jambo nililojua lingemuumiza?

  4. Ni lini mara ya mwisho nilimwomba msamaha bila kuongeza maneno “lakini kama unge” ama “lakini kama tu haunge”?

  5. Ni lini mara ya mwisho ulichagua kuwa na furaha badala ya kudai kuwa “sahihi”?

Ikiwa swali lolote miongoni mwa haya linakusababisha kuhisi vibaya ama kuwa na hatia, kumbuka kwamba Mzee David A. Bednar amefundisha kwamba “hatia ni kwa roho zetu kama vile uchungu ni kwa miili yetu---tahadhari ya hatari na ulinzi kutokana na uharibifu zaidi.”17

Ninamwalika kila mmoja wetu kutii ombi la kweli la Mzee Jeffrey R. Holland “Kaka zangu na dada zangu katika jitihada hii ndefu ya milele ya kuwa zaidi kama Mwokozi wetu, tujaribuni kuwa wanaume na wanawake ‘wakamilifu’ katika angalau njia hii moja kwa kutojikwaa katika kunena, ama ikisemwa kwa njia mzuri zaidi, kwa kuzungumza kwa lugha mpya, lugha ya malaika.”18.

Nilipojiandaa kwa ajili ya fursa hii leo, Roho amenifundisha, na nimeamua kunena maneno mema mara nyingi zaidi kwa mwenzi wangu ninayemthamini na juu yake yeye, kuwainua wanaume katika familia yangu na kuelezea shukrani kwa njia wanavyotekeleza wajibu wao wa kiungu na wa kusaidia. Na nimeamua kufuata mithali “Niinue nami nikuinue, na tutapaa pamoja.”

Je, mtaungana nami katika kutafuta usaidizi wa Roho Mtakatifu kutufundisha jinsi tunavyoweza kuinuana vyema zaidi katika wajibu wetu unaosaidiana kama wana na binti wa agano wa wazazi wetu wa mbinguni?

Ninajua kwamba kupitia nguvu ya kuwezesha ya Upatanisho wa Yesu Kristo na imani yetu katika Yeye, tunaweze kufanya hivyo. Ninaomba tuweke tumaini letu katika Yeye ili kutusaidia kusaidiana kuishi kwa furaha na milele tunapopaa pamoja, katika jina la Yesu Kristo, amina.

Muhtasari

  1. Boyd K. Packer, katika “Donna Smith Packer Receives Family History Certificate from BYU,” news.byu.edu/archive12-jun-packer.aspx.

  2. Dieter F. Uchtdorf, in Jeffrey R. Holland, “Elder Dieter F. Uchtdorf: On to New Horizons,” Ensign, Mar. 2005, 12; Liahona, Mar. 2005, 10.

  3. Henry B. Eyring, in Gerald N. Lund, “Elder Henry B. Eyring: Molded by ‘Defining Influences,’” Ensign, Sept. 1995, 14; Liahona, Apr. 1996, 31.

  4. Thomas S. Monson, “I Will Not Fail Thee, nor Forsake Thee,” Ensign or Liahona, Nov. 2013, 85.

  5. Mark Twain, Eve’s Diary (1905), 107.

  6. Boyd K. Packer, “The Power of the Priesthood,” Ensign or Liahona, May 2010, 9.

  7. Ezra Taft Benson, “To the Fathers in Israel,” Ensign, Nov. 1987, 51, 50.

  8. 2 Nefi 2:27.

  9. Ona Robert D. Hales, “Strengthening Families: Our Sacred Duty,” Ensign, May 1999, 34; Liahona, July 1999, 40; see also LaRene Gaunt, “Elder Robert D. Hales: ‘Return with Honor,’” Ensign, July 1994, 51; Liahona, Apr. 1995, 31.

  10. Mwanzo 2:18.

  11. Mwanzo 2:18, tanbibi b.

  12. Ona Bruce K. Satterfield, “The Family under Siege: The Role of Man and Woman” (presentation given at Ricks College Education Week, June 7, 2001), 4; emp.byui.edu/SATTERFIELDB/PDF/RoleManWoman2.pdf.

  13. Handbook 2: Administering the Church (2010), 1.3.1.

  14. Barbara B. Smith, “Hearts So Similar,” Ensign, May 1982, 97.

  15. “Daddy’s Homecoming,” Children’s Songbook, 210.

  16. “Let Us Oft Speak Kind Words,” Hymns, no. 232.

  17. David A. Bednar, “We Believe in Being Chaste,” Ensign or Liahona, May 2013, 44.

  18. Jeffrey R. Holland, “The Tongue of Angels,” Ensign or Liahona, May 2007, 18.