2010–2019
Kaa katika Eneo la Bwana!
Aprili 2012


Kaa katika Eneo la Bwana!

Kwa hivyo, swali letu la kila siku lazima liwe “Je, matendo yangu yananiweka katika eneo la Bwana1 ama eneo la adui?”

Rais Thomas S. Monson wakati mmoja alisema: “Acha nipeane mwongozo rahisi ambao kwao mnaweza kupima chaguzi zinazowakabili. Ni rahisi kukumbuka: ‘huwezi kuwa sahihi kwa kutenda mabaya; huwezi kukosa kwa kutenda mema’” (“Pathways to Perfection,” LiahonaLiahona, July 2002, 112; Ensign, May 2002, 100). Mwongozo wa Rais Monson ni rahisi na wazi. Unafanya kazi sawa na Liahona aliyopatiwa Lehi. Ikiwa tutatumia imani na kujitahidi kutii sheria za Bwana, tutapata kwa urahisi njia iliyo sahihi ya kufuata, haswa tunapokabiliwa na chaguzi zetu za kila siku.

Mtume Paulo anatusihi juu ya umuhimu wa upanzi katika Roho na ujuzi kuhusu kutopanda katika mwili. Alisema:

“Msidanganyike, Mungu hadhihakiwi; kwa kuwa cho chote apandacho mtu, ndicho atakachovuna.

“Maana yeye apandaye kwa mwili wake, katika mwili wake atavuna uharibifu; bali apandaye kwa Roho, katika Roho atavuna uzima wa milele.

“Tena tusichoke katika kutenda mema: kwa maana tutavuna kwa wakati wake, tusipozimia roho” (Wagalatia 6:7–9).

Kupanda katika Roho kunamaanisha kwamba mawazo yetu yote, maneno, na matendo lazima yatuinue kwa kiwango cha uungu wa wazazi wetu wa mbinguni. Hata hivyo, maandiko yanataja mwili kama maumbile ama kiumbe cha mwili wa mwanadamu wa kawaida, ambao unaruhusu watu kuvutiwa na hisia kali, tamaa, hamu, na motisha ya mwili badala ya kutafuta mwongozo kutoka kwa Roho Mtakatifu. Tusipokuwa makini, mvutio huu pamoja na msukumo wa maovu ulimwenguni unaweza kutufanya kutwaa tabia za kishenzi na kizembe ambazo zinaweza kujumuisha mojawapo wa tabia zetu. I kuzuia tabia hizo mbaya, ni lazima tufuate kile ambacho Bwana alimwagiza Nabii Joseph Smith juu ya umuhimu wa kupanda siku zote katika Roho: “Kwa hiyo, msichoke kutenda mema, kwa kuwa mnaijenga misingi ya kazi kubwa. Na kutokana na mambo madogo huja yaliyo makuu” (M&M 64:33).

Ili kujenga roho yetu, inapaswa kwamba tuache “uchungu wote, na ghadhabu, na hasira, na kelele, na ghasia yaondoke [kwetu], pamoja na kila aina ya ubaya” (Waefeso 4:31) na “muwe na hekima katika siku za majaribio; jiondoeni kutoka kwenye uchafu” (Mormon 9:28).

Tunavyojifunza maandiko, tunajifunza kwamba ahadi zilizowekwa na Bwana kwetu zinategemea utiifu wetu na zinahimiza maisha maadilifu. Hizo ahadi lazima zistawishe nafsi zetu, kutuletea matumaini kwa kutuhimiza kutolegea hata katika uwepo wa changamoto zetu za kila siku za kuishi katika ulimwengu ambao tabia na thamani ya maadili inapotea, hivyo kusababisha watu kupanda katika mwili hata zaidi. Lakini tunawezaje kuwa na hakika kwamba chaguzi zetu zinatusaidia kupanda katika Roho na wala sio mwili?

Rais George Albert Smith alirejelea ushauri kutoka kwa babu yake, aliwahi kusema: “Kuna mstari wa mtengano unaojulikana vyema kati ya eneo la Bwana na eneo la shetani. Ikiwa utakaa katika upande wa Bwana utakuwa chini ya uongozi wake na hutakuwa na shauku ya kutenda mabaya; bali ikiwa utavuka upande wa shetani wa mstari huo mwingine inchi moja uko katika uwezo wa shetani na ikiwa atafaulu, hutaweza kufikiria au hata kuamua vyema kwa sababu utakuwa umepoteza Roho wa Bwana” ( Teachings of Presidents of the Church: George Albert Smith [2011], 191).

Kwa hivyo, swali letu la kila siku lazima liwe “Je, matendo yangu yananiweka katika eneo la Bwana ama eneo la adui?”

Nabii Mormon aliwatahadharisha watu wake juu ya umuhimu wa kuwa na uwezo wa kubainisha mema na mabaya:

“Kwa hivyo, vitu vyote vilivyo vizuri vinatoka kwa Mungu; na kile kilicho kiovu hutoka kwa ibilisi; kwani ibilisi ni adui wa Mungu, na hupigana dhidi yake siku zote, na hukaribisha na hushawishi kufanya dhambi, na kufanya kile kilicho kiovu siku zote.

“Lakini tazama, kile kilicho cha Mungu hukaribisha na hushawishi kufanya mema siku zote” (Moroni 7:12–13).

Nuru ya Kristo pamoja na urafiki wa Roho Mtakatifu lazima utusaidie kujua kama njia yetu ya kuishi inatuweka katika eneo la Bwana au la. Ikiwa mitazamo yetu ni mizuri, imeongozwa na Mungu, kwani chochote kizuri kinatoka kwa Mungu. Ingawaje, ikiwa mitazamo yetu ni mibaya, tunashawishiwa na adui kwani yeye hushawishi watu kutenda maovu.

Watu wa Kiafrika wamegusa moyo wangu kwa sababu ya azimio lao na bidii wa kukaa katika eneo la Bwana. Hata katika hali ngumu za maisha, wale ambao wanakubali mwaliko wa kuja kwa Kristo wanakuwa nuru kwa ulimwengu. Wiki chache zilizopita nikitembelea mojawapo wa kata katika Afrika Kusini, nilipata fursa ya kuwasindikiza vijana wawili makuhani, askofu wao, na rais wao wa kigingi kutembelea vijana wasioshiriki kikamilifu wa baraza lao. Nilivutiwa sana na bidii na unyenyekevu ambao makuhani hao wawili walionyesha walipowaalika vijana wasioshiriki kikamilifu kurudi kanisani. Walipokuwa wakiongea na vijana hao wasioshiriki kikamilifu, nilitambua kuwa nyuso zao ziliakisi nuru ya Mwokozi, na wakati huo huo ziliwajaza nuru wote waliowazunguka. Walikuwa wanatimiza wajibu wao wa “wasaidie wadhaifu, inyooshe mikono iliyolegea, na yaimarishe magoti yaliyo dhaifu. (M&M 81:5‎)‎. Mtazamo wa makuhani hao wawili uliwaweka katika eneo la Bwana, na walihudumu kama vyombo katika mikono Yake walipowaalika wengine kufanya vivyo hivyo.

Katika Mafundisho na Maagano 20:37 , Bwana anatufundisha kile kinachomaanisha kupanda katika Roho na hasa kile kinachotuweka katika eneo la Bwana kama ifuatavyo: tujinyenyekeze mbele ya Mungu, kushuhudia kwamba tumekuja kwa mioyo iliyopondeka na roho zilizovunjika, kushuhudia kwa Kanisa kwamba tumetubu dhambi zetu zote kwa hakika, tujichukulie juu yetu jina la Yesu Kristo, tuwe na azimio la kumtumikia Yeye mpaka mwisho, tuonyeshe kwa matendo yetu kwamba tumepokea Roho wa Kristo na kupokelwa kwa ubatizo katika Kanisa Lake. Ukubalifu wetu wa kutimiza maagano haya unatutayarisha kuishi katika uwepo wa Mungu kama viumbe vilivyotukuzwa. Ukumbusho wa maagano haya lazima uongoze tabia zetu katika uhusiano na familia zetu, katika mikutano yetu na watu wengine, na hasa katika uhusiano na Mwokozi.

Yesu Kristo alitengeneza utaratibu mkamilifu wa tabia ambao kwao tunaweza kujenga mitazamo yetu ili kuweza kutimiza maagano haya matakatifu. Mwokozi aliondoa kutoka maishani mwake mvuto wowote ambao ungebadilisha mtazamo wake kutoka kwa misheni yake takatifu, hasa alipojaribiwa na adui ama wafuasi wake alipohudumu hapa duniani. Ingawa hakuwahi kutenda dhambi, alikuwa na moyo uliopondeka na roho iliyovunjika, akiwa na wingi wa upendo kwa Baba yetu wa Mbinguni na kwa wanadamu wote. Alijinyenyekeza mbele ya Baba wetu wa Mbinguni, akijinyima mapenzi yake mwenyewe ili kutimiza kile Baba alimwomba katika vitu vyote mpaka mwisho. Hata katika wakati wa uchungu mwingi wa mwili na kiroho, akibeba mizigo ya dhambi zote za wanadamu kwenye mabega yake na kumwaga damu kupitia vinyweleo vyake, alimwambia Baba Yake, “Walakini, si kama nitakavyo mimi bali utakavyo wewe” (Mark 14:36).

Ombi langu, ndugu na kina dada tunapofikiria juu ya maagano yetu ni kwamba tuweze kujiweka wima dhidi ya “mishale ya moto ya adui” (1 Nephi 15:24), tukifuata mfano wa Mwokozi ili tuweze kupanda katika Roho na kujiweka katika eneo la Bwana. Acha tukumbuke mwongozo wa Rais Monson: “huwezi kuwa sahihi kwa kutenda mabaya; huwezi kukosa kwa kutenda mema.” Nasema haya yote katika jina la Yesu Kristo, amina.