2010–2019
Kuongolewa katika Injili kupitia Kanisa Lake
Aprili 2012


Kuongolewa katika Injili kupitia Kanisa Lake

Dhamira ya Kanisa ni kuweza kutusaidia kuishi injili

Naipenda injili ya Yesu Kristo na Kanisa La Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho. Wakati mwingine tunatumia maneno injili na Kanisa kwa kubadilishana, lakini hayana maana sawa. Ingawaje, yanahusiana vilivyo na tunayahitaji yote.

Injili ni mpango mtukufu wa Mungu ambao kwao sisi, kama watoto Wake, tumepewa fursa ya kupokea yote ambayo Baba anayo (ona M&M 84:38). Hii inaitwa uzima wa milele na inaelezwa kama “kipawa ambacho ni kikuu katika vipawa vyote vya Mungu” (M&M 14:7). Sehemu muhimu ya mpango katika maisha yetu ya dunia, wakati wa kujenga imani (ona Moroni 7:26), ili kutubu (ona Mosia 3:12), na kupatanishwa na Mungu (ona Yakobo 4:11).

Kwa sababu ya udhaifu wetu wa kimwili na “upinzani katika vitu vyote” (2 Nefi 2:11), ungefanya maisha haya kuwa magumu sana, kwa sababu hatungeweza kutakasa dhambi zetu wenyewe, Mwokozi alihitajika. Wakati Elohi, Mungu wa Milele na Baba wa roho zote, alipopeana mpango Wake wa wokovu, kulikuwa na mmoja kati yetu aliyesema, “Niko hapa, nitume mimi” (Ibrahimu 3:27).

Kwa kuzaliwa na Baba wa Mbinguni, kwote kiroho na kimwili, alimiliki uwezo mkuu wa kushinda ulimwengu. Kwa kuzaliwa na mama wa dunia, angetawaliwa na uchungu na mateso ya dunia. Yehova mkuu pia aliitwa Yesu na pia kupewa jina la Kristo, maana yake Masiya ama Yule aliyepakwa Mafuta. Mafanikio Yake makuu yalikuwa ni Upatanisho, ambao kwao Yesu Kristo “alishuka chini ya vitu vyote” (M&M 88:6), kumwezesha kulipia thamana ya ukombozi kwa kila mmoja wetu.

Kanisa lilitengenezwa na Yesu Kristo wakati wa huduma Yake ya dunia, “likijengwa juu ya msingi wa mitume na manabii” (Waefeso 2:20). Katika haya, maongozi ya Mungu ya ujalivu wa nyakati(D&C 128:18), Bwana alirejesha kile kilichokuwa, bayana kumwambia Nabii Joseph Smith, “Nami nitalianzisha kanisa kwa mkono wako; (M&M 31:7). Yesu Kristo alikuwa na ndiye kiongozi wa Kanisa, akiwakilishwa duniani na manabii, waonaji, na wafunuaji wakimiliki mamlaka ya utume.

Hili ni Kanisa la ajabu. Utengenezaji wake, thamani yake, wema wake kamilifu unaheshimika na wote wanaotaka kwa kweli kulielewa. Kanisa lina mipangilio kwa watoto, vijana, wanaume na wanawake. Kuna majumba ya kupendeza ya mikutano yanyopata zaidi ya 18,000. Mahekalu ya ajabu, jumla ya 136 sasa, yanapatikana kote duniani, na mengine 30 chini ya ujenzi ama kutangazwa. Kikosi kamili cha zaidi ya wamisionari 56,000, wakijumuhisha vijana na wadogo, wanahudumu katika mataifa 150. Kazi ya ufadhili ya Kanisa ulimwenguni kote ni onyesho la ajabu la wema wa washiriki wetu. Mfumo wetu wa ustawi unatunza washiriki wetu na huhimiza kujitegemea kwa njia isiolinganishwa popote duniani. Katika Kanisa hili tuna viongozi wanyenyekevu wasiojipenda na jamii ya Watakatifu waliotayari kutumikia mmoja kwa mwengine kwa njia ya ajabu. Hakuna chochote kama Kanisa hili ulimwenguni kote.

Nilipozaliwa, familia yetu iliishi katika nyumba ndogo kwenye uwanda wa mojawapo wa jumba kuu na la kihistoria la Kanisa, Tabenakulo ya Honolulu. Sasa naomba radhi kwa marafiki wapendwa katika Uaskofu Simamizi, kwamba kama kijana nilipanda juu na chini na kupitia kila sehemu la jengo hilo, kutoka chini ya bwawa la maji mpaka juu ya mnara angavu. Pia tulibembea (kama Tarzan) kwenye miti mrefu ya mzabibu iliyoko pale.

Kanisa ilikuwa kila kitu kwetu. Tulienda kwa mikutano mingi, hata zaidi ya tulivyoenda leo. Tulihudhuria Msingi siku ya alhamisi. Mikutano za Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama ilikuwa siku ya jumanne asubuhi. Mapatano kwa vijana ilikuwa Jumatatu usiku. Jumamosi ilikuwa shughuli za kata. Jumapili wanaume na vijana wangehudhuria mkutano wa Ukuhani asubuhi. Mchana tulihudhuria Shule ya Jumapili. Halafu jioni tulirudi kwa mkutano wa sakramenti. Kwa kurudi na kuenda kwa mikutano, inaonekana muda wetu ulimalizika kwa shughuli za Kanisa siku nzima ya Jumapili na siku zingine nyingi za wiki.

Zaidi nilivyopenda Kanisa, ilikuwa ni siku zile za ujana ambapo, kwa mara ya kwanza, niligundua kwamba kulikuwa na kitu hata zaidi hivyo. Nilipokuwa wa umri wa miaka mitano, mkutano mkubwa ulifanyika katika tabenakulo. Tulitembea njiani tulimoishi na kupitia daraja ndogo inaoelekeza kwa nyumba kuu ya mkutano na kuketi kwenye laini ya 10 ndani ya kanisa kubwa. Aliyeongoza na aliyekuwa akiongea katika mkutano huo alikuwa David O. McKay, Rais wa Kanisa. Siwezi kukumbuka chochote alichosema, bali kwa umbali nakumbuka kile nilichoona na kuhisi. Rais McKay alivalia suti ya rangi malai na kwa nywele zake nyeupe zenye wawimbi alionekana kama mfalme. Kwa kitamaduni cha visiwa, alivalia mkufu wenye maua mekundu. Alipoongea, nilihisi kitu chenye nguvu na kibinafsi. Baada nilielewa kwamba nilikuwa nikihisi mwongozo wa Roho Mtakatifu. Tuliimba wimbo wa kufunga.

Ni nani aliye upande wa Bwana? Nani?

Sasa ndio wakati wa kuonyesha.

Tunauulizia kwa ujasiri:

Ni nani aliye upande wa Bwana? Nani?

(“Who’s on the Lord’s Side?” Hymns, no. 260)

Kwa maneno hayo yakiimbwa na takribani watu 2,000 bali ikionekana kama swali kwangu, nilitaka kusimama na kusema, “Mimi!”

Wengine wamekuja kufikiri juu ya shughuli katika Kanisa kama lengo kuu. Hapo pana hatari. Ni rahisi kuwa mtendaji Kanisani na kutokuwa mkamilifu katika injili. Acha nisisitize: shughuli katika Kanisa ni lengo zuri sana; ingawa, haitoshi. Shughuli katika Kanisa ni onyesho la nje la hamu yetu ya kiroho. Kama tutahudhuria mikutano yetu, kushika na kutimiza majukumu ya Kanisa, na kuhudumia wengine, itajulikana wazi wazi.

Kwa kinyume, mambo ya injili kila mara huwa hayaonekani na huwa vigumu kupima, lakini ni ya umuhimu wa milele. Kwa mfano, tuna imani kiasi gani? Tunatubu kiasi gani? Kwa jinsi gani maagizo yana umuhimu maishani mwetu? Tunalengaje maagano yetu?

Narudia: tunahitaji injilinaKanisa. Hakika, dhamira ya Kanisa ni kuweza kutusaidia kuishi injili. Tunashangaa kila mara: jinsi gani mtu anaweza kushiriki kikamilifu Kanisani akiwa kijana na kisha asiweze anapozeeka.? Jinsi gani mtu mzee aliyehudhuria na kuhudumu kila mara anaweza kukoma kuja? Jinsi gani mtu aliyeudhiwa na kiongozi ama mshiriki mwengine kuruhusu hayo kukatiza ushiriki wake wa Kanisa? Pengine sababu ni kuwa hawakuongoka vyema katika injili—mambo ya milele.

Nadokeza njia tatu muhimu za kuwa na injili kama msingi wetu.:

  1. Kupanua uelewa wetu wa Uungu. Ujuzi imara wa na upendo wa washiriki watatu wa Uungu ni wa msingi. Kwa uzingatifu ombeni kwa Baba, katika jina la Mwana, na mtafute mwongozo kutoka kwa Roho Mtakatifu. Pamoja na masomo ya kila mara na kutafakari kwa unyenyekevu, hujenga daima imani isiotingika katika Yesu Kristo, “Kwani ni vipi mtu atamjua yule bwana ambaye hajamtumikia, na aliye mgeni kwake, na yuko mbali katika mawazo na nia za moyo wake?” (Mosia 5:13).

  2. Lenga juu ya maagizo na maagano. Ikiwa kuna mengine ya maagizo muhimu ambayo bado hayajafanywa katika maisha yako, kwa dhamira jitayarishe kuyapokea kila moja. Kisha tunapaswa kuweka mazoea ya kuishi maagano yetu kwa haki, kikamilifu tukitumia toleo la kila wiki la sakramenti. Wengi wetu hawabadilishwi kila mara kwa uwezo wake wa kusafishwa kwa sababu ya ukosefu wetu wa uchaji kwa agizo hili takatifu.

  3. Unganisha injili na Kanisa. Kumakinikia injili, itakuwa baraka zaidi, sio kidogo, maishani mwetu. Tunapokuja katika kila mkutano ulioandaliwa “tafuteni maarifa, hata kwa kujifunza na pia kwa imani.” (M&M 88:118), Roho Mtakatifu atakuwa ndiye kiongozi wetu. Tukija kuburudishwa, kila mara tutaudhika. Rais Spencer  W. Kimball aliwahi kuulizwa, “Utafanya nini unapojipata katika mkutano wa kuchosha wa sakramenti?” Jibu lake: “Sijui. Sijawahi kuwa katika mmoja” (quoted by Gene R. Cook, in Gerry Avant, “Learning Gospel Is Lifetime Pursuit,” Church News, Mar. 24, 1990, 10).

Katika maisha yetu tunapaswa kutamani kilichofanyika baada ya Bwana kuwatembelea watu wa Dunia Mpya na kutengeneza Kanisa Lake. Maandiko yanasema, “Na ikawa kwamba walienda hivyo [kumaanisha Wanafunzi Wake] miongoni mwa watu wote wa Nefi, na walihubiri injili ya Kristo kwa watu wote usoni mwa nchi; na waliomgeukia Bwana, na waliunganishwa kwa kanisa la Kristo, na hivyo ndivyo watu wa kizazi hicho walivyobarikiwa” (3 Nefi 28:23).

Bwana anataka washiriki wa Kanisa kuongoka kikamilifu kwa injili Yake. Hii ndio njia pekee ya kupata usalama wa kiroho sasa na furaha milele.Katika jina la Yesu Kristo, amina.