2010–2019
Yeye Kweli Anatupenda
Aprili 2012


Yeye Kweli Anatupenda

Kwa sababu ya mpangilio uliopangwa kitakatifu wa familia, tunaelewa kikamilifu jinsi Baba yetu wa Mbinguni anatupenda kikweli kila mmoja wetu sawa sawa na kikamilifu.

Napendelea kuwa pamoja na wamisionari wa muda. Wamejawa na imani, matumaini na ukarimu wa kweli. Uzoefu wa umisionari wao ni kama maisha madogo kwenye pakiti ya miezi 18 hadi 24. Wanawasili kama watoto wachanga kiroho wakiwa na hamu kali ya kujifunza na kuondoka kama watu wazima, wakionekana tayari kushinda changamoto yoyote na kila moja inayokuja mbele zao. Pia nawapenda wamisionari wazee waliyojitolea, ambao wamejawa na subira, hekima na uhakikisho tuli. Wanaleta kipawa cha uthabiti na upendo kwa nishati ya ujana unaowazunguka. Pamoja wamisionari vijana na wenzi wazee ni kikosi cha nguvu na ulinzi kwa wema, ambacho kina athira kuu katika maisha yao na juu ya wale wanaguswa na huduma yao.

Majuzi niliwasikiliza wawili wa hawa wamisionari hodari vijana walipokuwa wakieleza uzoefu wao na juhudi zao. Katika wakati huu wa tafakari walikuwa wanafikiria watu waliokutana nao siku hiyo, wengine wa hao walikuwa wanavutiwa kuliko wengine. Wanapofikiria juu ya hizi hali, wanaliuliza, “Je! Tunaweza vipi kusaidia kila mtu kukuza hamu ya kujua zaidi kuhusu Baba wa Mbinguni? Je! Tunaweza vipi kuwasaidia wao kuhisi Roho Wake? Je! Tunaweza vipi kuwasaidia wao kujua kwamba tunawapenda?”

Katika jicho la akili yangu ningewaona hawa vijana wawili miaka mitatu au minne baada ya kumaliza misheni zao. Nilipiga twasira kichwani ya wao kama wamepata wenzi wao wa milele na wakihudumu katika jamii za wazee au wakifunza kundi la vijana. Sasa, badala ya kufikiria juu ya wachunguzi wao, walikuwa wanauliza maswali hayo hayo kuhusu washiriki wa jamii yao au vijana waliopatiwa jukumu la kutunza. Ninaona jinsi uzoefu wao wa umisionari unaweza kutumika kama kigezo cha kutunza wengine maishani mwao mwote. Kama jeshi la wafuasi wema hurudi kutoka kwenye misheni zao katika nchi nyingi kote ulimwenguni, wanakuwa wachangiaji wakuu katika kazi ya kuendeleza Kanisa.

Lehi nabii wa Kitabu cha Mormoni inawezekana kwamba alikuwa anatafakari maswali hayo hayo kama hawa wamisionari wakati aliposikiliza majibu ya wanawe kwa maelekezo na maono aliyokuwa amepatiwa:“Lamani na Lemueli, wakiwa wakubwa, walivyonung’unika dhidi ya baba yao. Na walinung’unika kwa sababu hawakujua matendo ya yule Mungu aliyewaumba (1 Nefi 2:12).

Labda kila mmoja wetu amepata kuhisi mfadhaiko aliopata Lehi na wanawe wakubwa wawili. Kama tunavyokabiliana na mtoto mpotevu, mchunguzi asiye na sharti, mzee mtarajiwa asiyejishughulisha, mioyo yetu huvimba kama vile Lehi na tunauliza, “Je! Nawezaje kuwasaidia kuhisi na kusikiliza Roho ili waziweze kukamatwa na vivutio vya dunia?” Maandiko mawili yanatokeza katika akili yangu ambayo yanaweza kutusaidia kupata njia yetu kavuka hivi vivutio na kuhisi uwezo wa upendo wa Mungu.

Nefi alipeana funguo ya mlango wa kujifunza kupitia uzoefu wake binafsi: “Mimi, Nefi, .... pia nikiwa na hamu ya kujua siri za Mungu, kwa hivyo, nikamlilia Bwana; na tazama akanijia mimi, na akanigusa moyo wangu kwamba nikaamini maneno yote ambayo baba yangu alikuwa amezungumza; kwa hivyo, mimi sikumwasi kama kaka zangu. ” (1 Nefi 2:16).

Kuamsha hamu ya kujua huwezesha uwezo wetu wa kiroho kusikia sauti ya mbinguni. Kupata njia ya kuamsha na kulea hio hamu ni utafutaji na jukumu wa kila mmoja wetu---wamisionari, wazazi, waalimu, viongozi, na washiriki. Tunapohisi hiyo hamu ikifanyika ndani ya mioyo yetu, tunakuwa tayari kunufaika kutokana na kujifunza juu ya andiko la pili ambalo nataka kulitaja.

Mnamo Juni 1831, wito ulipokuwa ukipatianwa kwa viongozi wa Kanisa wa mapema, Joseph Smith aliambiwa kwamba “Shetani amezagaa katika nchi, na anaenda akiwadanganya mataifa.” Ili kupambana na huu ushawishi wenye mvuto, Bwana alisema kwamba “nitatoa kwenu utaratibu katika mambo yote, ili msidanganyike”(M&M 52:14).

Mipangilio ni vigezo, miongozo, mfululizo wa hatua, au mapito afuatayo mtu ili kukaa katika ulinganifu na madhumuni ya Mungu. Kama yakifuatiwa, tutakuwa wanyenyekevu, macho, na kuwa na uwezo wa kutambua sauti ya Roho Mtakatifu kutokana na zile sauti ambazo zinavuta na kutupotosha. Bwana basi anatuelekeza, “Yule atetemekaye chini ya uwezo wangu atafanywa kuwa imara, naye atazaa matunda ya sifa na hekima, sawa sawa na kweli na mafunuo ambayo nimewapa ninyi.” (D&C 52:17).

Baraka za ombi nyenyekevu, linalotolewa kwa nia halisi, huwezesha Roho Mtakatifu kugusa mioyo yetu na kutusaidia kukumbuka kile tulichojua mapema kabla ya kuzaliwa katika uzoefu wa duniani. Tunapofahamu wazi zaidi mpango wa Baba wa Mbinguni kwetu, tutaanza kutambua majukumu yetu ya kuwasaidia wengine kujifunza na kuufahamu mpango Wake. Kukaribiana na kuhusiana na kuwasaidia wengine kumbukeni ni njia ya kibinafsi tunayoishi na kutumia injili katika maisha yetu wenyewe. Tunapoishi injili kihalisi katika mpangilio uliofunzwa na Bwana Yesu Kristo, uwezo wetu wa kuwasaidia wengine unaongezeka. Ufuatayo ni uzoefu wa mfano wa jinsi hii kanuni inavyoweza kufanya kazi.

Wamisionari wawili waligonga mlango, wakitarajia kupata mtu atakaye pokea ujumbe wao. Mlango ulifunguliwa, na mtu mkubwa aliwasalimu kwa sauti isiyokuwa ya kirafiki: “Nafikiria nilikwambia usigonge mlango wangu tena. Naliwaonya hapo mbeleni kama mtaweza kurudi tena, haitakuwa uzoefu mzuri. Sasa achaneni nami.” Yeye alifunga mlango upesi.

Wazee walipokuwa wakiondoka, mmisionari aliyekuwa mzee kidogo, mwenye uzoefu alimwekelea mkono mabegani yule mdogo ili kumfariji na kumtia moyo. Bila wao kujua, yule mtu aliwatazama wao dirishani kuhakikisha walielewa ujumbe wake. Alitarajia kuwaona wakicheka na kudhihaki makaribisho yao ya ukali kwa majaribio ya matembezi yao. Hata hivyo, kama alivyoshuhudia onyesho la ukarimu kati ya wamisionari wawili, moyo wake ulilainika ghafula. Akawafungulia mlango na kuwauliza warudi na washiriki ujumbe wao naye.

Ni wakati tunapokubali mapenzi Mungu na kuishi mpangilio Wake kwamba Roho Wake anahisiwa. Mwokozi alifunza, “Hivyo watu wote watatambua ya kuwa ninyi mmekuwa wanafunzi wangu, mkiwa na upendo ninyi kwa ninyi.” (Yohana 13:35). Hii kanuni ya kuwa na upendo wa mmoja na mwengine na kukuza uwezo wetu wa kulenga Kristo katika jinsi tunavyofikiria, tunavyosema, na tunavyotenda ni msingi katika kuwa wanafunzi wa Kristo na waalimu wa injili Yake.

Kuamsha hii hamu hututayarisha kutafuta mipangilio iiliyoahidiwa. Kutafuta mipangilio hutuelekeza sisi kwenye mafundisho ya Kristo kama alivyofunza Mwokozi na viongozi- manabii Wake. Mpangilio wa haya mafundisho ni kuvumilia hadi mwisho: “Heri wale ambao watatafuta kujenga Sayuni yangu katika siku ile, kwani watapata karama na nguvu za Roho Mtakatifu; na wakivumilia hadi siku ya mwisho watainuliwa katika siku ya mwisho, na wataokolewa katika ufalme usio na mwisho wa Mwanakondoo; na yeyote atakayetangaza amani, ndio, habari za shangwe, jinsi gani watakavyokuwa warembo milimani. (1 Nefi 13:37).

Ni njia gani kuu ambayo kwayo tunaweza kufurahia kipawa na uwezo wa Roho Mtakatifu? Ni uwezo ambao huja kwa kuwa wafuasi waaminifu wa Yesu Kristo. Ni upendo wetu kwake Yeye na kwa watu wenzetu. Ni Mwokozi ambaye anayeelezea mpangilio wa upendo alipotufunza. “Amri mpya nawapa, Mpendane. Kama vile nilivyowapenda ninyi, nanyi mpendane vivyo hivyo(Yohana 13:34).

Rais Gordon B. Hinckley alithibitisha kanuni hii aliposema: “Kumpenda Bwana sio tu ushauri; sio pia upendeleo. Ni amri … Upendo wa Mungu ni mzizi wa wema wote, wa uzuri wote, wa nguvu zote za silka, wa uaminifu wote wa kufanya mema” (“Words of the Living Prophet,” Liahona, Dec. 1996, 8; “Dondoo kutoka kwa hotuba za majuzi za Rais Gordon B. Hinckely,” Ensign, Apr. 1996, 73).

Mpango wa Baba uliweka mpangilio wa familia ili kutusaidia kujifunza, kutumia, na kufahamu uwezo wa upendo. Siku ile familia yangu mwenye ilitengenezwa, mpendwa wangu Ann nami tulienda kwenye Hekalu na kuingia katika agano la ndoa. Vyovyote nilivyompenda siku hiyo, ndio nilianza kuona ono la upendo. Kila mmoja wa watoto wetu na wajukuu wetu alipoingia katika maisha yetu, upendo wetu umeweza kupanuliwa kuwapenda kila mmoja wao sawa sawa na kikamilifu. Inaonekana kuwa hakuna mwisho wa mpanuko wa uwezo wa upendo.

Hisia za upendo kutoka kwa Baba yetu wa Mbinguni ni kama mvuto wa mvutano kutoka mbinguni. Tunapoondoa vivutio ambavyo vinavyotuvuta kuelekea duniani na kutumia wakala wetu wa kumtafuta Yeye, tunafungua mioyo yetu kwa nguvu za selestia ambazo zinatuvuta kumwelekea Yeye. Nefi alielezea athira zake kama “hata kwa kumaliza mwili wangu” (2 Nefi 4:21). Uwezo huu huu wa upendo ulimfanya Alma kuimba “wimbo wa upendo wa ukombozi” (Alma 5:26; ona pia mstari 9).. Ulimgusa Mormoni katika njia kwamba alitushauri “ombeni ... kwa nguvu zote za moyo,” kwamba tujazwe na upendo Wake (Moroni 7:48).

Maandiko ya kisasa na ya kale yamejaa kumbusho za upendo wa milele wa Baba wa Mbinguni kwa watoto Wake. Nina imani kwamba mkono wa Baba yetu wa Mbinguni daima umenyoshwa, tayari kumkumbatia kila mmoja wetu na kusema kwa kila mmoja kwa sauti, tulivu, ichomayo, “Nakupenda.”

Kwa sababu ya mpangilio huu wa familia uliundwa kimbinguni, sisi tunafahamu kabisa jinsi Baba yetu wa Mbinguni anavyompenda kila mmoja wetu sawa sawa na kikamilifu. Nashuhudia kwamba hii ni kweli. Mungu anatujua na kutupenda. Yeye ametupatia ono la mahali Pake patakatifu na amewaita manabii na mitume kufunza kanuni na mipangilio ambayo itatuleta tena Kwake. Tunapojitahidi kuamsha hamu za kujua sisi wenyewe na wale wengine na tunavyoishi mpangilio tunagundua tutavutwa Kwake. Nashuhudia kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu, Mfano wetu, na Mkombozi wetu mpendwa, ndivyo ninasema katika jina la Yesu Kristo, amina.