2010–2019
Kuwa Uwiano na Muziki wa Imani
Aprili 2012


Kuwa Uwiano na Muziki wa Imani

Mungu anawapenda watoto Wake wote. Anataka wote warudi Kwake. Anatamani kila mmoja kuwa na uwiano na muziki mtakatifu wa imani.

Viongozi Wakuu wenye Mamlaka wa Kanisa wanavyokutana na washiriki wote ulimwenguni kote, tunaona kibinafsi jinsi Watakatifu wa Siku za Mwisho ni kikosi cha wema. Tunawasifia ninyi kwa yale yote mnayoyafanya kubariki maisha ya watu wote.

Wale kati yetu wenye kazi za uhusiano mwema wa umma wanatambua vyema kwamba viongozi wengi wenye ushawishi mwingi na waandishi katika Marekani na kote duniani wameongezea mazungumzo yao ya umma kuhusu Kanisa na washiriki wake. Kongamano la ajabu la mambo limeinua hadhi ya Kanisa sana. 1

Wengi wanaoandika juu ya Kanisa wamefanya juhudi za uaminifu kuelewa watu wetu na mafundisho yetu. Wamekuwa wastaraabu na wamejabiru kuwa busara, kwa hayo tunashukuru.

Pia tunatambua kwamba watu wengi hawana uwiano na mambo matakatifu. Rabi Mkuu Lord Sacks wa Uingereza, akiongea na viongozi wa Katoliki ya Kirumi Desemba iliyopita katika Chuo Kikuu cha Pontifical Gregorian, aliona jinsi sehemu zingine za dunia zimekuwa za malimwengu. Alisema kwamba mkosefu mmoja ni “wakanaji Mungu wa hima wa kisayansi walio viziwi kwa muziki wa imani.”2

Ono kuu la utangulizi katika Kitabu cha Mormoni ni ndoto ya Lehi ya kinabii ya mti wa uzima.3 Hili ono linaelezea wazi changamoto kwa imani ambazo zilizopo katika siku zetu na utengamano mkuu uliyopo kati ya wale wanaompenda, wanaomwabudu, na wanaohisi kuwajibika kwa Mungu na wale ambao hawafanyi hivi. Lehi anaeleza tabia fulani ambazo zinaangamiza imani. Wengine wana kiburi, majisifu, na upumbavu. Wanapendelea tu hekima za ulimwengu.4 Wengine wanapendelea Mungu lakini wamepotelea katika ukungu wa giza wa kilimwengu na dhambi.5 Wengine wameonja upendo wa Mungu na neno Lake lakini wanahisi aibu kwa sababu ya wale wanawadhiaki na wanaanguka katika “mapito yaliyokatazwa.”6

Mwisho, kuna wale ambao wana uwiano na muziki wa imani. Mnajua ninyi ni kina nani. Mnampenda Bwana na injili Yake na daima mnajaribu kuishi na kushiriki ujumbe Wake, hasa na familia zenu.7 Mna upatanifu na uswawishi wa Roho, unaoamshwa na ngvuvu za neno la Mungu, mna ushikaji dini katika nyumba zenu, na kwa bidii mnajaribu kuishi maisha kama Kristo kama wafuasi Wake.

Tunatambua jinsi mlivyo na shughuli. Bila wahudumu wa kulipwa, jukumu la kusimamia Kanisa linawategemea ninyi washiriki mliojiweka wakfu. Tunajua ni kawaida kwa washiriki wa uaskofu na urais wa vigingi na wengine kutoa huduma ya uaminifu kwa masaa mengi. Urais wa vikundi saidizi na jamii ni mfano katika huduma yao ya kujitolea. Hii huduma na kujitolea kumesambaa kote katika ushiriki, kwa wale wanaoweka rekodi za kikarani, waalimu wa nyumbani na watembelezi, na wale wanaofunza madarasa. Tunashukrani kwa wale wanaohudumu kwa ujasiri kama viongozi wa Maskauti au chekechea. Ninyi nyote tunawapenda na tunawathamini kwa yale mnayofanya na kile mlicho!

Tunatambua kwamba kuna washiriki walio na upendeleo mdogo na uaminifu mdogo kwa kati ya mafundisho ya Mwokozi. Hamu yetu ni kwa wale washiriki walioamka kikamilifu kwa imani na kuongeza ushiriki wao na masharti yao. Mungu anawapenda watoto Wake wote. Anataka wote warudi Kwake. Anatamani kila mmoja kuwa na uwiano na muziki mtakatifu wa imani. Upatanisho wa Mwokozi ni kipawa kwa kila mmoja.

Inahitajika kufunzwa na kueleweka kwamba tunawapenda na kuwaheshimu watu wote ambao Lehi alielezea.8 Kumbukeni, siyo juu yetu kuhukumu. Hukumu ni ya Bwana.9 Rais Thomas S. Monson ametuuliza dhahiri kuwa na “kwa ujasiri kuepukana na kuhukumu wengine.”10 Pia amemuuliza kila mshiriki mwaminifu kuokoa wale ambao wameonja tunda la injili na kisha kuna wale walioanguka pia wale ambao hawajapata njia nyembamba na iliyosonga. Tunaomba kwamba watashikilia fimbo na kushiriki upendo wa Mungu, ambayo itajaza “nafsi kwa shangwe kuu zaidi.”11

Hali ono la Lehi linajumuisha watu wote, wazo la fundisho muhimu ni la maana kwa umilele wa familia. “Familia imetawazwa na Mungu.” Ni kitengo muhimu sana katika wakati na umilele.”12 Lehi alipokula tunda la mti wa uzima (upendo wa Mungu), alitamani kwamba familia ilile pia.”13

Hamu yetu kuu ni kulea watoto wetu katika kweli na haki. Kanuni moja ambayo itatusaidia kutimiza hayo ni kuepuka kuwa wa kuhukumu sana juu ya tabia za zile za kupumbavu au zisizo na hekima lakini si za dhambi. Miaka mingi iliyopita, wakati mke wangu nami tulipokuwa na watoto nyumbani, Mzee Dallin H. Oaks alifunza kwamba ilikuwa muhimu kutofautisha kati ya makosa ya ujana ambayo yalihitaji kukosolewa na dhambi ambazo zinahitaji kurudiwa na toba.14 Pale ambapo kuna ukosefu wa hekima, watoto wetu wanahitaji kufunzwa. Pale kuna dhambi, toba inahitajika. 15 Tulipata hii kuwa na usaidizi kwetu katika familia yetu wenyewe.

Ushikaji wa kidini katika nyumba hubariki familia zetu. Mfano hasa ni muhimu. Kiletulicho kinasema kwa sauti sana kwamba watoto wetu wasiweze kusikia kile tunachosema. Nilipokuwa karibu umri wa miaka mitano, mama yangu akipokea habari kwamba kaka yangu mkubwa ameuawa wakati meli ya vita ambayo alikuwa akitumika ilipigwa bomu baharini katika pwani ya Japani karibu na mwisho wa Vita vya Dunia vya II.16 Hizi habari zilikuwa pigo kubwa kwake. Alikuwa na mhemko na kuenda katika chumba cha kulala. Baada ya muda mchache nilichungulia katika chumba ili kuona kama yuko SAWA. Alikuwa amepiga magoti karibu na kitanda akiomba. Amani kuu ilinijia kwa sababu alikuwa amenifunza kuomba na kumpenda Mwokozi. Huu ulikuwa ni mfano kawaida aliyotoa kwangu. Kina mama na baba wanaoomba na watoto kunaweza kuwa muhimu sana kuliko mfano mwingine wowote.

Ujumbe, huduma, na Upatanisho wa Yesu Kristo, Mwokozi wetu, ni mtalaa muhimu wa familia. Hakuna maandiko yanaonyesha imani yetu vyema kuliko 2 Nefi 25:26: “Na tunazungumza kuhusu Kristo, tunafurahia katika Kristo, tunahubiri kuhusu Kristo, tunatoa unabii kumhusu Kristo, na tunaandika kulingana na unabii wetu, ili watoto wetu wajue asili ya kutegemea msamaha wa dhambi zao.”

Mojawapo wa kigezo cha kimsingi cha ono la Lehi ni kwamba washiriki waaminifu lazima wakamate kabisa fimbo ya chuma ili kuwaweka katika njia nyembamba na iliyosonga ielekeayo hata kwenye mti wa uzima. Ni muhimu kwa washiriki kusoma, kutafakari, na kujifunza maandiko.17

Kitabu cha Mormoni ni cha umuhimu mkubwa sana.18 Kutakuwa, na, daima wale ambao watapuuza umuhimu wa au hata kashifu hiki kitabu kitakatifu. Wengine wametumia dhiaka. Kabla nihudumu misheni, profesa wa chuo kikuu alidondoa maneno ya Mark Twain ambayo kama ungechukua “Na ikawa kwamba” kutoka kwa Kitabu cha Mormoni “kingekuwa tu kijitabu.”19

Miezi michache, nikihudumu misheni katika London, England, profesa mashuhuri wa Chuo Kikuu cha London aliyeelimika Oxford, Mmisri mtaalam katika lugha za Kisemiti, alisoma Kitabu cha Mormoni, akawasiliana na Rais David O. Mckay, na akakutana na wamisionari. Aliwataarifu kwamba alikuwa ameshawishika Kitabu cha Mormoni kwa kweli ni tafsiri ya elimu ya Kiyahudi na lugha ya Wamisri ya vipindi vilivyoelezewa katika Kitabu cha Mormoni.20 Mfano mmoja miongoni mwa mingi alitumia ilikuwa ni kiunganishi cha fungu la maneno “Na ikawa kwamba,” ambacho alisema kilifanana jinsi angetafsiri fungu la maneno katika maandishi ya Kisemiti cha kale.21 Profesa alielezwa kwamba hali mtazamo wake ukifuatia utaalam wake ulikuwa umemsaidia, ilikuwa bado ni muhimu kuwa na ushuhuda wa kiroho. Kupitia kujifunza na maombi alipata ushahidi wa kiroho na kubatizwa. Kwa hivyo kile mchekeshaji maarufu alichokiona kama kitu cha mzaa, msomi alikitambua kama ushahidi wa kina wa kweli za Kitabu cha Mormoni, ambao uthibitishwa kwake na Roho.

Mafundisho muhimu ya wakala yanahitaji ushuhuda wa injili rejesho sharti ufuatilie imani badala ya ushahidi wa nje au sayansi. Kusisitiza kwa shauku juu ya mambo ambayo bado hayajafunuliwa kikamilifu kama vile jinsi bikira kuzaa au Ufufuko wa Mwokozi kuna uwezekano kulikuweko au hasa jinsi Joseph Smith alitafsiri maandiko yetu hakutafaa au hakutazaa maendeleo ya kiroho. Haya ni mambo ya imani. Cha misngi, ushauri wa Moroni wa kusoma na kutafakari na kisha kumuuliza Mungu kwa imani yote ya moyo, kwa nia halisi, ili kuthibitisha kweli za kimaandiko kwa ushuhuda wa Roho ndiyo jibu.22 Kwa ziada, tunapokazia mawazo katika maisha yetu ni lazima kiroho na kuishi injili, tunabarikiwa kwa Roho na kuhonja uzuri Wake kwa hisia ya shangwe, furaha na hasa amani.23

Kwa uwazi, mstari wa kugawa kati ya wale wanaosikia muziki wa imani na wale walioviziwi wa -toni au kuchepuka ndiyo kujifunza hai kwa maandiko. Niliguswa kwa kina miaka iliyopita kwamba nabii mpendwa, Spencer W. Kimball, alisisitiza haja ya kusoma na kujifunza maandiko daima. Alisema: “Nimepata kwamba uhusiano wangu na uungu unapokuwa wa kijuujuu na inapoonekana kwamba hamna sikio la kiungu linalosikiliza na hamna sauti ya kiungu inayoongea, kwamba niko mbali, mbali sana. Kama nikijizamisha katika maandiko umbali unapunguka na roho urejea.”24

Natumaini tunasoma Kitabu cha Mormoni pamoja na watoto wetu kila mara. Nimezungumza haya na watoto wangu. Wameshiriki nami mawazo mawili. Kwanza, kushikilia kusoma maandiko kila siku kama familia ndio njia. Binti anaelezea kwa njia ya uchangamfu juhudi zao za asubuhi mapema pamoja na watoto wao vijana za kusoma maandiko kila mara. Yeye na mumewe wanaamka mapema asubuhi, wanatembea ukungu wa kiza kushika paipu za chumba ambazo zimewekwa gazini hadi pale familia ukusanyika kusoma neno la Mungu. Kushikilia ndio jibu, na hali ya uchesi usaidia. Inahitaji juhudi nyingi kutoka kwa kila mwanafamilia kila siku, lakini ni juhudi za kustahili. Vipingamizi vya muda vinashindwa na kushikilia.

Pili ni jinsi wana wetu mdogo na mkewe wanasoma maaadiko pamoja na familia yao dogo. Wawili kati ya watoto wanne hawajakua kiasi cha kusoma. Kwa mtoto wa miaka mitano wana siginali ya vidole vitano ambayo yeye hujibu ili aweze kushiriki kikamilifu katika kusoma kwa maandiko kwa familia. Siginali ya kidole 1 ni yeye arudie, “Na ikawa kwamba” inapotokea katika Kitabu cha Mormoni. Wacha niseme napenda kwamba maneno hayo yanatokea mara nyingi sana. Kwa kawaida, kwa upendeleo wa familia za vijana, kidole 2 ni “Na kwa hivyo tunaona”; vidole 3, 4 na 5 huchaguliwa na wazazi kulingana na maneno yaliyopo katika sura wanayosoma.

Tunajua kwamba kujifunza maandiko kwa familia na jioni ya familia nyumbani kila mara si kamili. Pasipo kutia maanani changamoto tunazokumbana nazo, msivunjike moyo.

Tafadhali elewa kwamba imani katika Bwana Yesu Kristo na kuziweka amri Zake ni na daima itakuwa jaribio kuu la maisha ya muda. Juu ya yote mengine, kila mmoja wetu sharti atambue kwamba mtu anapokuwa kiziwi kwa toni za muziki wa imani, yeye hayupo kwenye uwiano na Roho. Kama nabii Nefi alivyofunza, “Mmesikia sauti yake … ; na amewazungumzia kwa sauti ndogo tulivu, lakini mlikuwa mmekufa ganzi, kwamba hamkupata yale maneno yake.”25

Mafundisho yetu ni wazi; tunafaa kuwa halisi na wenye furaha. Tunasisitiza imani yetu, wala si hofu yetu. Tunafurahia katika hakikisho la Bwana kwamba Yeye atasimama nasi na kutupatia sisi mwaongozo na maelekezo.26 Roho Mtakatifu ushuhudia kwa mioyo yetu kwamba tuna Baba wa Mbinguni wenye upendo, ambaye mpango Wake wa ukombozi wetu utatimizwa katika kila njia kwa sababu ya dhabihu ya upatanishi ya Yesu Kristo.

Kama Naomi W. Randall, mwandishi wa “I Am a Child of God,” alivyoandika, Roho Wake huongoza; upendo wake huhakikisha kwamba hofu huondoka imani inapodumu.”27

Acha sisi, kwa hivyo, popote tulipo katika mapito ya ufuasi katika ono la Lehi, tuamue kuamsha ndani yetu na familia hamu kuu ya kudai kipawa cha uzima wa milele kisichofahamika cha Mwokozi. Naomba kwamba tukae katika toni na muziki wa imani. Nashuhudia uungu wa Yesu Kristo na uhalisi wa Upatanisho Wake katika jina la Yesu Kristo, amina.

Muhtasari

  1. Ona Mafundisho na Maagano 1:30.

  2. Jonathan Sacks, “Has Europe Lost Its Soul?” (address delivered on Dec. 12, 2011, at the Pontifical Gregorian University), chiefrabbi.org/ReadArtical.aspx?id=1843.

  3. Ona 1 Nefi 8.

  4. Ona 1 Nefi 8:27; 11:35.

  5. Ona 1 Nefi 8:23; 12:17.

  6. 1 Nefi 8:28.

  7. Ona 1 Nefi 8:12.

  8. Maelekezo ya Mwokozi ni kumtafuta mwanakondoo aliyepotea; Ona Matthew 18:12–14.

  9. Ona Yohana 5:22; Ona pia Matthew 7:1–2.

  10. Thomas S. Monson, “May You Have Courage,” Liahona na Ensign, May 2009, 124.

  11. 1 Nefi 8:12.

  12. Handbook 2: Administering the Church (2010), 1.1.1.

  13. 1 Nefi 8:12.

  14. Ona Dallin H. Oaks, “Sins and Mistakes,” Ensign, Oct. 1996, 62. Mzee Oaks alifunza wazo hili alipokuwa rais wa chuo cha Brigham Young karibu na mwaka wa 1980.

  15. Ona Mafundisho na Maagano 1:25–27.

  16. Ona Marva Jeanne Kimball Pedersen, Vaughn Roberts Kimball: A Memorial (1995). Vaughn alicheza mpira wa miguu kama mlinzi katika chuo cha Brigham Young majira ya kuchipua mnamo 1941. Baada ya mashambulizi ya bandari ya Pearl Harbor, mnamo Desemba 8, 1941, alijiunga na jeshi la wanamaji la Marekani. Aliuawa mnamoMei 11, 1945, na mashambulizi ya mabomu ya adui dhidi ya USS Bunker Hill na kuzikwa baharini.

  17. Ona Yohana 5:39.

  18. Ona Ezra Taft Benson, “The Book of Mormon—Keystone of Our Religion,” Ensign, Nov. 1986, 4; or Liahona na Ensign, Oct. 2011, 52.

  19. Mark Twain, Roughing It (1891), 127–28. Kila kizazi kipya kiliwasilisha taarifa za Twain kama vile zilikuwa ugunduzi mpya. Kwa kawaida kuna rejeleo dogo kwamba Mark Twain hanapuuza Ukristo na dini kwa kawaida.

  20. Ona 1 Nefi 1:2.

  21. Nilikutana na Dkt. Ebeid Sarofim huko London wakati wazee walikuwa wanamfundisha.. Ona pia N. Eldon Tanner, katika Conference Report, Apr. 1962, 53. Wasomi wengi wa maandishi ya Kisemeti na Kimisri wamesema kwamba mrudio wa maneno ya kiunganishi ”Na ikawa kwamba”katika mwanzo wa kila sentensi; Ona Hugh Nibley, Since Cumorah, 2nd ed. (1988), 150.

  22. Ona Moroni 10:3–4; wahakiki wachache kwa uaminifu wametahini haya kwa dhamira halisi.

  23. Ona Mafundisho na Maagano 59:23.

  24. Teachings of Presidents of the Church: Spencer W. Kimball (2006), 67.

  25. 1 Nefi 17:45; Ona pia Ezra Taft Benson, “Seek the Spirit of the Lord,” Tambuli, Sept. 1988, 5; Ensign, Apr. 1988, 4: “Tutasikia maneno ya Bwana mara nyingi kwa hisia. Kama sisi ni wanyenyekevu na wasikivu, Bwana atatupatia ushawishi kupitia hisia zetu.

  26. Ona Mafundisho na Maagano 68:6.

  27. “When Faith Endures,” Hymns, no. 128.