2010–2019
Kuweka Takatifu
Aprili 2012


Kuweka Takatifu

Vitu takatifu vinapaswa kuchukuliwa kwa makini sana, kupewa heshima kubwa, na kuangaliwa kwa uchaji mkuu.

Miaka mengine 1,500 kabla ya Kristo, mchungaji alivutiwa na kichaka kilichoungua kwenye mteremko wa Mlima Horeb. Tukio hilo takatifu Lilianzisha mabadiliko ya Musa kutoka kwa mchungaji mpaka kwa nabii na kazi yake kutoka kwa uchungaji wa kondoo mpaka ukusanyaji Waisraeli. Miaka elfu moja na mia tatu baadaye, kuhani mwenye fadhila katika ukumbi wa mfalme alivutiwa kwa ushahidi wa nabii aliyehukumiwa. Tukio hilo lilianzisha mabadiliko ya Alma kutoka kwa mtumishi wa umma mpaka kwa mtumishi wa Mungu. Karibu miaka 2,000 baadaye, kijana wa miaka 14 aliingia mitini akitafuta majibu kwa swali aminifu. Tukio la Joseph Smith kwenye kijisitu lilimweka katika njia ya unabii na urejesho.

Maisha ya Musa, Alma, na Joseph Smith yote yalibadilishwa kwa kukutana na Uungu. Uzoefu huu uliwaimarisha wao ili wabakie watakatifu kwa Bwana na kazi Yake maishani mwao mwote licha ya upinzani mkuu na majaribio yaliofuatia.

Uzoefu wetu na Uungu hauwezi kuwa wa moja kwa moja au wakuvutia ama changamoto zetu kuogofya. Ingawa, kama vile manabii, uthabiti wetu wa kuvumilia kwa haki unategemea kutambua, kukumbuka, na kushikilia kwa utakatifu kile tunachopokea kutoka mbinguni.

Leo mamlaka, funguo, na maagizo yamerejeshwa duniani. Kuna pia maandiko na mashahidi maalum. Wanaomtafuta Mungu wanaweza kupokea ubatizo kwa ondoleo wa dhambi na udhibitisho “kwa kuwawekea mikono kwa ajili ya ubatizo wa moto na Roho Mtakatifu” (D&C 20:41) Kwa hivi vipawa vya thamani vilivorejeshwa, uwiano wetu wa kiuungu hakika utajumuhisha mshiriki wa tatu wa Uungu, Roho Mtakatifu.

Kupitia kwa sauti ndogo tulivu, Roho hunisemeza

Kuniongoza, kuniokoa.

(“The Still Small Voice,” Children’s Songbook, 106)

Acha Roho Mtakatifu aongoze;

Acha atufunze kilicho kweli.

Atashuhudia kuhusu Kristo,

Huangazaakili zetu kwa ono la mbinguni.

(“Let the Holy Spirit Guide,” Hymns, no. 143)

Tunapotafuta majibu kutoka kwa Mungu, tunahisi sauti ndogo tulivu ukinong’onezea roho zetu. Hizi hisia—hivi vishawishi—ni kawaida sana na vyenye kutatiza kiasi kwamba tunaweza kutovitilia maanani au kuviona kuwa mawazo au uelewa. Hizi jumbe za kibinafsi hushuhudia juu ya upendo wa Mungu wa kibinafsi na kujali kwake kwa kila mtoto Wake na misheni za kibinafsi za maisha yao ya muda. Kutafakari kila siku juu ya na kuandika mawazo yanayotoka kwa Roho hutimiza malengo mawili ya kutusaidia sisi(1) kutambua uwiano wetu wa binafsi na Uungu na (2) kuuhifadhi kwa ajili yetu na uzao wetu. Kuyaandika ni utambuzi na kukiri rasmi shukrani zetu kwa Mungu, kwani “katika lolote mwanadamu hamkosei Mungu, au ghadhabu ya Mungu haiwaki kwa yeyote, isipokuwa wale tu wasiokiri mkono wake katika mambo yote” (D&C 59:21).

Kwa kuhusu kile tunachopokea kwa Roho, Bwana alisema, “Kumbukeni kwamba kile ambacho huja kutoka juu ni kitakatifu(D&C 63:64). Taarifa yake ni zaidi ya ukumbusho; pia ni ufafanuzi na maelezo. Nuru na ujuzi kutoka mbinguni ni takatifu. Ni takatifu kwa sababu mbinguni ndio chimbuko lake.

Takatifu humaanisha kustahili uchaji na heshima. Kwa kutambua kitu kama kitakatifu, Bwana anaonyesha kwamba ni cha thamani ya juu na muhimu kuliko vitu vingine. Vitu takatifu vinapaswa kuchukuliwa kwa makini sana, kupewa heshima kubwa, na kuangaliwa kwa uchaji mkuu. Utakatifu ni wa thamani sana katika uongozi wa maadili ya mbinguni.

Kile ambacho ni kitakatifu kwa Mungu kinakuwa kitakatifu kwetu tu kwa njia ya matumizi ya wakala; kila mmoja lazima achague kukubali na kushikilia kitakatifu kile ambacho Mungu amefafanua kama kitakatifu. Anatuma nuru na ujuzi kutoka mbinguni. Anatualika kukubali na kuiweka kama takatifu.

Lakini “kuna upinzani katika vitu vyote” (2 Nephi 2:11). Kinyume cha utakatifu ni upujufu au kidunia—kile ambacho ni cha muda au kidunia. Kilicho kidunia daima hushindana na utakatifu kwa ajili ya usikivu wetu na vipaumbele vyetu. Maarifa ya kidunia ni muhimu kwa maisha yetu ya kila siku. Aidha, Bwana anatuekeleza kutafuta elimu na hekima, kusoma na kujifunza kutoka vitabu bora, na kujifahamisha na lugha, ndimi, na watu (ona M&M 88:118; 90:15). Kwa hivyo, chaguzi za kuweka matakatifu juu ya kidunia ni mojawapo wa chaguzi za kipaumbele husika, sio tegemezi; “kuelimika ni vyemaikiwa [sisi] tutatii mawaidha ya Mungu” (2 Nephi 9:29; umetiliwa mkazo).

Vita kwa ajili ya kipaumbele kati ya matakatifu na ya kidunia katika kila moyo wa mwanadamu inaweza kuonekana kwa uzoefu wa Musa kwenye kichaka kinachoungua. Pale Musa alipokea wito wake mtakatifu kutoka kwa Yehova kuokoa wana wa Israeli kutoka utumwa. Hata hivyo, maarifa yake ya kidunia kuhusu nguvu za Misri na Firauni ilimfanya kuwa shaka. Hatimaye, Musa alifanya imani katika maneno ya Bwana, kukomesha ujuzi wake wa kidunia na kuamini katika yale matakatifu. Uaminifu huo ulimpatia uwezo wa kushinda majaribu ya muda na kuongoza Israeli kutoka Misri.

Baada ya kukimbia kutoka kwa jeshi la Noah kisha tena kuanguka katika utumwa katika mikono ya Amuloni, Alma angeweza kuwa na shaka na ushahidi wa kiroho aliyoupokea wakati wa kumsikiliza Abinadi. Hata hivyo, aliamini yale matakatifu na kupewa nguvu za kustahimili na kuepuka majaribio yake ya muda.

Joseph Smith alikabiliana mtanziko kama huo katika siku za mapema za kutafsiri Kitabu cha Mormoni. Alijua hali takatifu ya mabamba na kazi ya utafsiri. Hata hivyo Martin Harris alimsihi kupatia kipaumbele kwa masuala ya kidunia ya urafiki na fedha, kinyume na maelekezo matakatifu. Matokeo yake, mswada wa tafsiri ulipotea. Bwana alimshutumu Joseph kwa kutoa “yaliyokuwa matakatifu, kwa waovu” (M&M 10:9)na kumnyima fursa ya mabamba na kipawa cha utafsiri. Wakati vipaumbele vya Joseph vilipoundwa upya vizuri, mambo matakatifu yalirudishwa na kazi iliendelea.

Kitabu cha Mormoni kinapeana mifano mengine ya mapambano ya kupatia kipaumbele yale matakatifu. Kinaongea kuhusu waaminio ambao imani yao iliwaelekeza kwa mti wa uzima ili kushiriki tunda lake, upendo wa Mungu. Kisha udhihaki wa wale waliokuwa katika jumba kuu na lenye nafasi kubwa waliwafanya waaminio kubadili mwelekeo wao kutoka kwa utakatifu hadi kwa kidunia. (Ona 1 Nefi 8:11, 24–28.) Baadaye, Wanefi walichagua kiburi na kukana roho ya unabii na ya ufunuo, “wakifanyia mzaha yale yaliyo takatifu” (Helamani 4:12). Hata baadhi ya mashahidi wa ishara na miujiza kuhusishwa na kuzaliwa kwa Bwana walichagua kukataa vipaji takatifu kutoka mbinguni kwa upendeleo wa maelezo ya kidunia (ona 3 Nefi 2:1–3).

Leo mapambano yanaendelea. Sauti ya kidunia inaongezeka kwa wingi na nguvu. Ulimwengu unazidi kudhihaki na kuhimiza waaminio kuachana imani ambazo ulimwengu hunaziona kuwa hazina mantiki na zisizo busara. Kwa sababu “tunaona kwa kioo kwa jinsi ya fumbo” (1 Wakorintho 13:12) na “sijui maana ya vitu vyote” (1 Nefi 11:17), nyakati zingine tunaweza kuhisi kuathiriwa kwa urahisi na kuwa mahitaji makubwa ya hakikisho la kiroho. Bwana alimwambia Oliver Cowdery:

“kama wataka ushahidi zaidi, rejesha mawazo yako juu ya usiku ule uliponililia katika moyo wako, kwamba uweze kujua ukweli wa mambo haya.

“Sikusema amani akilini mwako kuhusiana na jambo hili? Ni ushahidi gani mkubwa zaidi unaoweza kupata kuliko kutoka kwa Mungu?” (M&M 6:22–23).

Bwana alimkumbusha Oliver na sisi kutegemea na kushikilia ushahidi mtakatifu wa kibinafsi aliokuwa tayari ameupokea wakati imani yake ilikumbwa na changamoto. Kama vile Musa, Alma, na Joseph mapema, haya matukio ya kiuungu yalikuwa kama nanga ya kutuweka salama na kwenye mkondo nyakati za majaribu.

Yale matakatifu hayawezi kusalimishwa kwa uteuzi. Wale ambao watakaochagua kuachana na hata jambo moja takatifu watatiwa giza akilini mwao (ona M&M 84:54), na isipokuwa watubu, nuru waliyonayo itachukuliwa kutoka kwao (ona M&M 1:33). Bila nanga ya utakatifu, watajipata wakielea katika bahari ya kidunia. Kinyume chake, wale hushikilia mambo matakatifu hupokea ahadi takatifu: “Kile kilicho cha Mungu ni nuru; na yule ambaye huipokea nuru, na kukaa ndani ya Mungu, hupokea nuru zaidi na nuru hiyo huzidi kung’ara hata mchana mkamilifu” (M&M 50:24).

Bwana aweze kutabariki ili daima na kila mara kutambua, kukumbuka, na kushikilia kile ambacho tumepokea kutoka juu. Nashuhudia kwamba tunapofanya hivi, tutakuwa na uwezo wa kuvumilia majaribio na kushinda changamoto za siku zetu. Katika jina la Yesu Kristo, amina.