2010–2019
Tayari na Mstahiki Kuhudumu
Aprili 2012


Tayari na Mstahiki Kuhudumu

Miujiza iko kila mahali inapoweza kupatikana wakati ukuhani unaeleweka, uwezo wake unaheshimiwa na kutumiwa vyema, na imani inatumika.

Ndugu zangu wapendwa, ni vyema jinsi gani kukutana nanyi tena. Tunapohudhuria mkutano mkuu wa ukuhani, mimi hutafakari juu ya mafundisho ya kati wa viongozi wenye hekima wa Mungu ambao wamenena katika mikutano mikuu ya ukuhani ya Kanisa. Wengi wameshaenda kwenye matuzo yao ya milele, na bado kutoka kwa ung’avu wa akili zao, na kina cha nafsi zao, na kutoka kwa joto la mioyo yao, wametupatia sisi mwelekeo wa maongozi. Nitashiriki nanyi usiku wa leo kati ya mafundisho yao kuhusu ukuhani.

Kutoka kwa Nabii Joseph Smith: “Ukuhani ni kanuni ya milele, na ulikuwepo na Mungu kutoka milele, na utakuwa milele, bila mwanzo wa siku au mwisho wa miaka.”1

Kutoka kwa maneno ya Rais Wilford Woodruff, tunajifunza: “Ukuhani Mtakatifu ni mkondo ambao kwao Mungu huwasiliana na ushiriki na mwanadamu hapa ulimwenguni; na wajumbe wa mbinguni ambao wamewahi tembelea ulimwengu kuwasiliana na wanadamu ni watu ambao walishikilia na kuheshimu ukuhani walipokuwa hapa duniani; na kila kitu ambacho Mungu amefanya kitendeke kwa ajili ya wokovu wa mwanadamu kutoka kuja kwa mwanadamu hapa ulimwenguni hata ukombozi wa dunia, kimekuwa na kitakuwa kwa uwezo wa ukuhani wa milele.” 2

Rais Joseph F. Smith alifafanua: “Ukuhani… ni … uwezo wa Mungu aliokabidhiwa kwa mtu ambao kwao mtu anaweza kutenda hapa ulimwenguni kwa wokovu wa familia ya mwanadamu, katika jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu, na kutenda ki haki; bila ya kujipatia haya mamlaka, na wala kuhazima kutoka kwa vizazi ambavyo vimekufa na kwenda, bali kwa mamlaka ambayo yamepeanwa katika siku hii ambayo tunaishi na malaika wahudumu na roho kutoka juu,” moja kwa moja kutoka uwepo wa Mwenyezi Mungu.”3

Na mwisho basi kutoka kwa Rais John Taylor: Ukuhani ni nini? …. Ni serikali ya Mungu, ikiwa ni hapa ulimwenguni au mbinguni, kwani ni kwa nguvu, wakala, au kanuni ambayo vitu vyote vinatawaliwa katika ulimwengu na mbinguni, na kwa uwezo ambao vitu vyote vinathibitishwa na kuhimiliwa. Unatawala vitu vyote---unaelekeza vitu vyote---unahimili vitu vyote---na ndio unashughulikia vitu vyote ambavyo Mungu na kweli zinazohusika nao.” 4

Tumebarikiwa jinsi gani kuwa hapa katika hizi siku za mwisho, wakati ukuhani wa Mungu upo hapa ulimwenguni. Tumejaliwa jinsi gani kuwa na ukuhani huu. Ukuhani si tu kipawa kama ulivyo amri ya kuhudumu, nafasi ya kuinua, na nafasi ya kubariki maisha ya wengine.

Kwa hizi nafasi huja na majukumu na wajibu. Nalipenda na kulitukuza neno tukufu wajibu na kile chote linalosimamia.

Kwa nafasi moja au ingine, katika mazingira aina moja ua ingine, nimekuwa nikihudhuria mikutano ya ukuhani kwa zaidi ya miaka 72---tangu nilipotawazwa kama shemasi katika umri wa miaka 12. Nyakati kwa kweli zinasonga mbele. Wajibu huenda sambamba na mwendo. Wajibu hauzimi au haufifii. Balaa za ugomvi huja na kupita, lakini vita vinavyopigwa nafsi za wanadamu vinaendelea bila kukoma. Kama mwito huja neno la Bwana kwenu, kwangu, na kwa wenye ukuhani kila mahali: “Kwa sababu hiyo, sasa acha kila mtu na ajifunze wajibu wake, na kutenda kazi katika ofisi ambayo ameteuliwa, kwa bidii yote.” 5

Mwito wa wajibu ulikuja kwa Adamu, hadi kwa Nuhu, kwa Ibrahimu, kwa Musa, kwa Samweli, kwa Daudi. Ulikuja kwa Nabii Joseph Smith na kwa kila mrithi wake. Mwito wa wajibu ulikuja kwa kijana Nefi alipokuwa ameelekezwa na Bwana, kupitia baba yake Lehi, kurudi Yerusalemu na kaka zake kuchukua mabamba kutoka kwa Labani. Ndugu za Nefi walinung’unika, wakisema ilikuwa ni kitu kigumu ambacho kilitakiwa kutoka kwao. Jibu la Nefi lilikuwa nini? Alisema, “Nitaenda na kutenda vitu ambavyo Bwana ameamuru, kwani ninajua kwamba Bwana hatoi amri kwa watoto wa watu, isipokua awatayarishie njia ya kutimiza kitu ambacho amewaamuru.” 6

Wakati mwito huu unakuja kwako na kwangu, jibu letu litakuwa nini? Je! Tutanung’unika, kama vile Lamani na Lemueli na kusema, “Hiki kitu kigumu kinachohitajiwa kutoka kwetu”? 7 Au tutafanya, kama Nefi, kibinafsi kutangaza, “Nitaenda na kutenda”? Je! Tutapendelea kuhudumu na kutii?

Nyakati zingine hekima ya Mungu inaweza kuonekana kama upumbavu au tu kuwa kitu kigumu, lakini mojawapo wa masomo makuu na yenye thamani tunayoweza kujifunza katika maisha haya ya muda ni kwamba wakati Mungu anaongea na mtu atii, huyo mtu daima atakuwa sahihi.

Ninapofikiria juu ya neno wajibu na jinsi kutenda wajibu wetu kunaweza kurutubisha maisha yetu na maisha ya wengine, nakumbuka maneno yaliyoandikwa na mshairi na mtunzi mashuhuri:

Nililala na kuota.

Kwamba maisha ni shangwe

Niliamuka na kuona

Kwamba maisha ni wajibu

Nikatenda na kutazama

Wajibu ni shangwe. 8

Robert Louis Stevenson alisema kwa njia nyingine. Alisema, “Najua kwamba furaha ni nini, kwani nimefanya kazi nzuri.” 9

Tunapotenda wajibu wetu na kutumia ukuhani wetu, tutapata shangwe ya kweli. Tutapata uzoefu wa uridhisho wa kutumiza kazi zetu.

Tumefunzwa wajibu mahususi wa ukuhani ambao tunashikilia, kama ni Ukuhani wa Haruni au wa Melkidezeki. Nawahimiza mtafakari juu ya huu wajibu na kisha kutenda kwa uwezo wenu kuutimiza. Ili tuweza kutenda hivyo, kila mmoja sharti awe mstahiki. Na tuwe na mikono tayari, mikono safi, na mikono ya upendeleo kwamba tuweze kushiriki katika kutoa kile Baba yetu wa Mbinguni angependa wengine wapokee kutoka Kwake. Kama hatustahiki, inawezekana tupoteze uwezo wa ukuhani, na kama tunaupoteza, tunapoteza kiini cha kuinuliwa. Na tuwe wastahiki kuhudumu.

Rasi Harold B. Lee, mmoja wa waalimu wakuu katika Kanisa, alisema: “Mtu anapokuwa mwenye ukuhani, anakuwa wakala wa Bwana. Anafaa kufikiria wito wake kama vile yupo kwenye shughuli za Bwana.” 10

Wakati wa Vita vya Dunia vya II, katika sehemu ya mapema ya 1944, uzoefu unaohusisha ukuhani ulifanyika wakati Marini wa Marekani walikuwa wanavamia Kwajalein Atoll, sehemu ya Visiwa vya Marshall na viliopo katika Bahari Pacific karibu katikaki ya Australia na Hawaii. Kilichotokea wakati huu kilielezwa na mwandishi --- sio mshiriki wa Kanisa---ambaye alifanya kazi kwa gazeti katika Hawaii. Mnamo 1944 makala ya gazeti aliandika uzoefu ufuatao, alielezea kwamba yeye na wale waandishi walikuwa katika kundi la pili nyuma ya Marini huko Kwajalein Atoll. Walipokuwa wakisonga mbele, waliona kijana marini akielea kwenye maji kifudifudi, hasa akiwa amejeruhiwa vibaya. Maji ya kina kifupi yaliyomzunguka yalikuwa mekundu kwa damu yake. Na wakamwona marini mwengine akimwendea yule mweziwe aliyekuwa amejeruhiwa. Huyu wa pili alikuwa pia amejeruhiwa, mkono wake ulikuwa unaning’nia kwa upande wake. Akainua kichwa cha yule aliyekuwa anaelea majini ili hasizame. Kwa sauti ya kushituka aliita usaidizi. Waandishi walimtazama tena yule mvulana ambaye alikuwa anamsaidia mweziwe na kusema, “ Mwanangu, hakuna chochote tunachoweza kumfanyia huyu kijana.”

“Kisha,” mwandishi aliandika, “Niliona kitu ambacho nilikuwa sijawahi kuona hapo awali. Huyu kijana, aliyekuwa amejeruhiwa vibaya mwenyewe, alienda ufuoni pamoja na mwili ulionekana kama hauna uzima wa marini mwenziwe. Akiweka kichwa cha mwenziwe kwenye goti lake. Yalikuwa madhari ya aina gani hayo---vijana wawili waliojeruhiwa vibaya sana---wasafi, vjiana wa sura nzuri –wa ajabu, hata katika dhiki yao. Na yule kijana mmoja akainamisha kichwa chake juu ya yule wengine na kusema “Nakuamuru wewe, katika jina la Yesu Kristo na kwa uwezo wa ukuhani, kwamba ubakie hai mpaka nitakapopata masaada wa tiba.’” Mwandishi alihitimisha makala haya kwa: “Watatu wetu,[marini wawili nami], tukiwa hapa hospitalini. Madaktari hawakujua … [jinsi walibakia hai], lakini mimi najua.” 11

Miujiza iko kila mahali inapoweza kupatikana wakati ukuhani unaeleweka, uwezo wake unaheshimiwa na kutumiwa vyema, na imani inatumika. Wakati imani inakuwepo badala ya hofu, wakati huduma ya kujitolea uondoa choyo inayodumu, uwezo wa Mungu huleta madhumuni Yake kutimizika.

Wito wa wajibu unaweza kuja kimya wakati sisi wenye ukuhani tunapojibu wajibu wetu tunaopokea. Rais George Albert Smith, huyu kiongozi wa staha na mwenye uwezo, alitamka, “Ni wajibu wenu kwanza kabisa kujifunza kile Bwana anataka na kisha, kwa uwezo na nguvu za ukuhani wenu mtakatifu, ili upanue wito wenu mbele za watu wenzenu … kwamba watu waweze kuwa na shukrani kuwafuatia ninyi.”12

Wito kama huo wa wajibu---wito usio wa kidrama bali ambao hata hivyo ulisaidia kuokoa nafsi---ulinijia mnamo 1950 wakati niliitwa kama askofu mpya. Majukumu yangu kama askofu yalikuwa mengi na tofauti tofauti, na nilijaribu kwa uwezo wangu wote kufanya kile nilihitajiwa kufanya. Marekani ikuwa inapingana vita vingine wakati huo. Kwa sababu wengi wa washiriki wetu walikuwa wanatumika katika jeshi, wajibu ulikuja kutoka makao makuu ya Kanisa kwa maaskofu wote wampatie kila mwanajeshi na toleo la Church Newsna Improvement Era,magazeti ya Kanisa ya wakati huo. Kwa ziada, kila askofu aliulizwa kuandika barua ya kibinasfi, kila mwezi kwa kila mwanajeshi kutoka kwa kata yake. Kata yetu ilikuwa na wanajeshi 23 rasmi. Jamii za ukuhani, kwa juhudi, zilileta pesa za matoleo ya magazeti. Nikachukua jukumu, hata wajibu, wa kuandika barua 23 za kibinafsi kila mwezi. Baada ya hii miaka yote bado nina nakala za barua zangu na majibu niliyopokea. Majonzi huja kirahisi wakati hizi barua zinasomwa tena. Ni shangwe kujifunza tena kuhusu maombi ya askari ya kuishi injili, uamuzi wa baharia kuweka imani pamoja na familia yake.

Jioni moja nilimpatia dada mmoja katika kata furushi la barua 23 la mwezi huo. Kazi yake ilikuwa ni kushughulikia utumaji barua na kusimamia orodha ya anwani zilizobadilika kila mara. Alitazama mojawapo wa bahasha na, kwa tabasamu, akauliza, “Askofu, Je! Wewe hauvunjiki moyo? Hapa kuna barua ingine kwa Ndugu Bryson. Hii ni barua ya 17 ambayo umemtumia bila yeye kujibu.”

Nilijibu, “Naam, labda itakuwa mwezi huu.” Na kama ilivyotokea, huo ndio ulikuwa mwezi. Kwa mara ya kwanza, alijibu barua yangu. Katika majibu yake ni lulu, ni tunu. Alikuwa anatumika mbali sana kwenye pwani ya mbali, kusikoweza kufikiwa, aliyetamani nyumbani, mpweke. Aliandika, “Askofu Mpendwa, mimi sipendi kuandika barua,”(ningemwambia hayo miezi saba iliyopita) Barua yake iliendelea, “Asante sana kwa Church News na magazeti, lakini cha muhimu sana asante kwa barua za kibinafsi. Nimebadilika. Nilitawazwa kwa Ukuhani wa Haruni. Moyo wangu umejazwa. Mimi ni mtu mwenye furaha.”

Ndugu Bryson hakuwa na furaha zaidi kumshinda askofu wake. Nilikuwa nimejifunza matumizi ya msemo, “Tenda wajibu [wako], hivyi ndio vyema, muachie Bwana hayo mengine.” 13

Miaka baadaye, nikuhudhuria Kigingi cha Salt Lake Cottonwood wakati James E. Faust akihudumu kama rais. Nilielezea hii taarifa katika juhudi za kuwatia moyo wanajeshi wetu. Baada ya mkutano, kijana wenye umbo zuri alikuja kwangu. Alichukua mkono wangu na kuushika na kuuliza, “Askofu Monson, je! Unanikumbuka?”

Ghafula nikatambua yeye ni nani. “Ndugu Bryson!” nilitamka. “Hali yako? Unafanya nini Kanisani?”

Kwa uchangamfu na furaha, alijibu, “Mimi ni sawa. Nahudumu katika urais wa jamii ya wazee. Asante sana tena kwa kunijali na barua zako za kibinafsi ambazo ulinitumia na mimi nazithamini sana.”

Ndugu, dunia ina haja ya usaidizi wenu. Je! Mnafanya yale yote mnayofaa kufanya? Mnakumbuka maneno ya Rais John Taylor: “Kama hautapanua wito wako, Mungu atawawajibisha kwa wale wote ambao mngewaokoa kama mgetenda wajibu wenu.”?14 Kuna miguu ya kuimarisha, kuna mikono ya kukumbatia, akili za kutia moyo, mioyo ya kupatia maongozi, na nafsi za kuokoa. Baraka za milele zinawangojea ninyi. Yenu ni nafasi ya kutokua mtazamaji bali mshiriki katika jukwaa la huduma ya ukuhani. Na tusikie makumbusho yanayopatikana katika Waraka wa Yakobo: “Lakini iweni watendaji wa neno, wala si wasikiaji tu, hali mkijidanganya nafsi zenu.” 15

Na tujifunze na kutafakari juu ya wajibu wetu. Na tuwe tayari na kustahili kuhudumu. Na katika utendaji wa wajibu wetu ufuate hatua za Bwana. Wewe na mimi tunapotembea mapito ambayo Yesu alitembea, tutagundua Yeye ni zaidi ya mtoto mchanga katika Bethlehemu, zaidi ya mwana wa seremala, zaidi ya mwalimu mkuu aliyehishi. Tutakuja kumjua Yeye kama Mwana wa Mungu, Mwokozi wetu na Mkombozi wetu. Wakati wito wa wajibu ulikuja Kwake, Yeye alijibu, “Baba, mapenzi yako na yatimizwe, na utukufu uwe wako milele na milele.”16 Na kila mmoja wetu afanye vivyo hivyo, naomba katika jina Lake takatifu, jina la Yesu Kristo, Bwana, amina.

Muhtasari

  1. Teachings of Presidents of the Church: Joseph Smith (2007), 104.

  2. Teachings of Presidents of the Church: Wilford Woodruff (2004), 38.

  3. Joseph F. Smith, Gospel Doctrine, 5th ed. (1939), 139–40; mkazo umewekwa.

  4. Teachings of Presidents of the Church: John Taylor (2001), 119.

  5. Mafundisho na Maagano 107:99; mkazo umewekwa.

  6. 1 Nefi 3:7; ona pia mstari 1–5.

  7. Ona 1 Nefi 3:5.

  8. Rabindranath Tagore, katika William Jay Jacobs, Mother Teresa: Helping the Poor (1991), 42.

  9. Robert Louis Stevenson, in Elbert Hubbard II, comp., The Note Book of Elbert Hubbard: Mottoes, Epigrams, Short Essays, Passages, Orphic Sayings and Preachments (1927), 55.

  10. Stand Ye in Holy Places: Selected Sermons and Writings of President Harold B. Lee (1976), 255.

  11. Katika Ernest Eberhard Jr., “Giving Our Young Men the Proper Priesthood Perspective,” typescript, July 19, 1971, 4–5, Church History Library.

  12. George Albert Smith, katika Conference Report, Apr. 1942, 14.

  13. Henry Wadsworth Longfellow, “The Legend Beautiful,” katika The Complete Poetical Works of Longfellow (1893), 258.

  14. Teachings: John Taylor, 164.

  15. Yakobo 1:22.

  16. Musa 4:2.