2010–2019
Fikiria Baraka
Oktoba 2012


Fikiria Baraka

Baba yetu wa Mbinguni anafahamu mahitaji yetu na atatusaidia sisi tunapomwita Yeye kwa usaidizi.

Akina ndugu na dada zangu wapendwa, mkutano mkuu huu unaashiria miaka 49 tangu nilipoidhinishwa, mnamo Oktoba  4 1963 kama mshiriki wa Jamii ya Mitume Kumi na Wawili. Miaka arobaini na tisa ni muda mrefu. Kwa njia nyingi hata hivyo, muda huonekana kuwa mfupi sana tangu niliposimama katika mimbari katika jumba la Tabernacle na kutoa hotuba yangu ya kwanza ya mkutano mkuu.

Mengi yamebadilika tangu Oktoba 4 1963. Tunaishi katika wakati wa kipekee katika historia ya dunia. Tumebarikiwa na mengi sana. Na hali ni vigumu wakati mwingine kutazama matatizo na uhuru usio na mipaka bila kufa moyo. Nimetambua kuwa badala ya kufikiria sana yaliyo hasi, ikiwa tutachukua hatua na kufikiria baraka katika maisha yetu, pamoja na zile zinazoonekana ndogo, wakati mwingine baraka zilizopuuzwa, tunaweza kupata furaha kuu zaidi.

Nimetathmini miaka 49 iliyopita, na nimepata utambuzi fulani. Mojawapo ni kwamba uzoefu usio na hesabu niliyopata haukuwa yale ambayo mtu angeyafikiria kuwa yasiyo ya kawaida. Kwa hakika, wakati ulipotendeka, kila mara ulionekana kuwa ya kutoshika nadhari na hata kuwa wa kawaida. Na hali, kwa kuangalia nyuma, ilikuza na kubariki maisha, na wala si kwa kiwango kidogo, kwa maisha yangu mimi. Ningependekeza zoezi hili kwenu, yaani, kuwa mtafakari maisha yenu na kuangalia hasa baraka kubwa na ndogo ulizopokea.

Ufahamu wangu daima umeimarisha wakati marejeleo yangu ya miaka mingi kwamba maombi yetu yanasikiwa na hujibiwa. Tunajua kuhusu ukweli unaopatikana katika 2 Nefi katika Kitabu cha Mormoni : “wanadamu wapo, ili wapate shangwe.”1 Ninashuhudia kuwa nyingi ya hiyo shangwe huja tunapotambua kuwa tunaweza kuwasiliana na Baba yetu wa Mbinguni kupitia kwa maombi na kuwa maombi haya yatasikika na kujibiwa- pengine si vile na wakati tulitarajia, lakini yatajibiwa na Baba wa Mbinguni ambaye anatujua na kutupenda kwa ukamilifu na aliye na hamu ya furaha yetu. Je!, Si ametuahidi, “Jinyenyekeze; na Bwana Mungu wako atakuongoza kwa mkono, na kukupa jibu la sala zako”?2

Kwa dakika chache nilizoratibiwa, ningependa kushiriki nanyi sampuli ndogo ya uzoefu niliokuwa nao ambamo maombi yamesikilizwa na kujibiwa na ambayo, kwa kutazama nyuma, umeleta baraka katika maisha yangu na pia maisha ya wengine. Shajara yangu ya kila siku niliyoandika miaka hii yote, imenisaida na mambo fulani maalum ambayo huenda nisingeweza kukumbuka kwa njia nyingine ile.

Mapema mnamo 1965, nilipewa jukumu la kuhudhuria mikutano ya vigingi na kufanya mikutano mingine kote katika eneo la Pacific ya Kusini. Hii ilikuwa mara yangu kwa kwanza kuzuru sehemu hii ya ulimwengu, na ilikuwa wakati usiosahaulika kamwe. Mengi yenye asili ya kiroho yalitendeka wakati wa kutekeleza jukumu hili, nilipokutana na viongozi, washiriki na wamisionari.

Mwishoni wa wiki, Jumamosi na Jumapili Februari 20 na 21, tulikuwa Brisbane, Australia kufanya vikao vya mkutano mkuu wa kawaida wa Kigingi cha Brisbane. Wakati wa mikutano siku ya Jumamosi, nilijulishwa kwa rais wa wilaya kutoka eneo lililokuwa karibu. Nilipomsalimia kwa mkono, nilihisi ushawishi mkubwa kuwa nilihitaji kuzungumza naye na kutoa ushauri kwa hivyo nikamwuliza kama angeandamana nami kwa kikao cha Jumapili asubuhi siku iliyofuata ili hili liweze kutimizwa.

Baada ya kikao cha Jumapili tulipata nafasi ya kukutana. Tulizingumza kuhusu majukumu yake mengi kama rais wa wilaya. Tulipokuwa tunafanya hivyo, nilihisi kushawishiwa kumpa mapendekezo maalum kuhusu kazi ya umisionari na jinsi yeye na washiriki wake wangewasaidia wamisionari wa wakati wote katika kazi zao katika eneo lao. Baadaye nilifahamu kuwa alikuwa ameomba kwa ajili ya mwongozo kuhusiana na jambo hili. Kwake, mkutano wetu pamoja ulikuwa ni ushahidi maalum kuwa maombi yake yalisikilizwa na yalikuwa yamejibiwa. Huu ulikuwa mkutano usioonekana mkubwa lakini mmoja ambao nina hakika uliongozwa na Roho na ambao ulileta tofauti katika maisha ya washiriki wake na katika mafanikio ya wamisionari huko.

Akina ndugu na dada, dhamiri za Bwana mara kwa mara hutimizwa tunapoitikia mwongozo wa Roho. Ninaamini kwa tunapotumia zaidi mwongozo na ushawishi unaotujia, zaidi ndipo Bwana atatukabidhi kazi Zake.

Nimejifunza, kama nilivyotaja katika jumbe za awali, kamwe kutoahirisha ushawishi. Kwa wakati moja nilikuwa ninaogelea katika Deseret Gym nzee huko Salt Lake City nilipohisi mwongozo kwenda katika University Hospital kumtembelea rafiki yangu mwema ambaye alikuwa amepoteza matumizi ya miguu yake kutokana na saratani na upasuaji uliofuatia. Mara niliondoka kidimbwini, nikavaa na punde nilikuwa njiani kumwona mtu huyu mwema.

Nilipofika chumbani mwake, nilipata kuwa kilikuwa tupu. Nilipouliza, nilifahamu kuwa pengine ningempata katika sehemu ya kidimbwi cha hospitali, eneo lililotumika kwa mazoezi ya kimwili. Hivyo ndivyo ilivyokuwa. Alikuwa amejiongoza hadi sehemu ile katika kiti chake cha magurudumu na alikuwa anakaa pekee katika chumba chake. Alikuwa kwenye upande wa mbali wa kidimbwi, karibu na sehemu iliyo ya kina zaidi. Nilimwita, na akaendesha kiti chake cha magurudumu ili kunisalimia. Tulikuwa na wakati mwema pamoja, nikaambatana naye kwenda chumbani mwake ambapo nilimpa baraka.

Nilipata kujua baadaye kuwa rafiki yangu alikuwa amekuwa na huzuni sana siku hiyo hata alikuwa amefikiria kuutoa uhai wake. Alikuwa ameomba usaidizi lakini akaanza kuhisi kuwa maombi yake hayakujibiwa. Alienda kwenye kidimbwi na wazo kuwa hii ingelikuwa njia ya kumaliza matatizo yake—kwa kupeleka kiti chake cha magurudumu kwenye sehemi ya kina zaidi kidimbwini. Niliwasili wakati muhimu sana katika kujibu kile nilijua kuwa mwongozo kutoka juu.

Rafiki yangu aliweza kuishi miaka mingine mingi----miaka iliyojaa furaha na shukrani. Nina furaha jinsi gani kwamba nilikuwa chombo mikononi mwa Bwana katika siku hiyo muhimu katika kidimbwi cha kuogelea.

Wakati mwingine, Dada Monson nami tulikuwa tunarejea nyumbani kwa gari kutoka kuwatembelea marafiki, nilisikia kushawishiwa kuwa twende mjini---umbali wa maili nyingi- kumtembelea, mjane mkongwe ambaye wakati mmoja aliishi katika kata yetu. Jina lake lilikuwa Zella Thomas. Kwa wakati huo alikuwa anaishi katika makao ya wakongwe. Mapema alasiri hiyo tulimpata akiwa mdhaifu sana lakini alikuwa amelala kwa amani kitandani mwake.

Zella alikuwa kipofu kwa muda mrefu, lakini alitambua sauti zetu mara moja. Aliuliza kama ningweza kumpa baraka, akiongeza kuwa alikuwa tayari kufa kama Bwana alitaka arejee nyumbani. Kulikuwa na roho mtamu wa amani chumbani mle, na sote tulijua kuwa alikuwa ameomba kwa dhati kuwa nije kumwona na kumpa baraka. Nilimwambia tulikuja kwa sababu ya mwongozo kutoka kwa Baba wa Mbinguni. Nilibusu utosi wake nikijua kuwa huenda nisingemwona tena katika maisha ya muda. Hivyo ndivyo ilivyokuwa, kwani alifariki siku iliyofuata. Kuweza kuleta faraja fulani na amani kwa mpendwa Zella kulikuwa ni baraka kwake na kwangu.

Nafasi ya kuwa baraka katika maisha ya mwingine mara nyingi huja bila kutarajiwa. Usiku mmoja wenye baridi sana wa Jumamosi katika majira ya baridi ya 1983–84, Dada Monson nami tulikwenda kwa gari maili kadha katika bonde la mlima Midway, Utah ambapo tuna nyumba. Hali ya anga usiku huo ilikuwa nyusi kuondoa 24 vipimo vya Fahrenheit, (-31 vipimo vya Celcius) na tulitaka kuhakikisha kuwa kila kitu kilikuwa sawa nyumbani mwetu huko. Tuliangalia na kupata kuwa ilikuwa sawa kwa hivyo tukaondoka kurejea Salt Lake City. Hatukuwa hata tumeenda maili chache katika barabara kuu, kabla gari letu kusita kufanya kazi. Tulikuwa tumekwama kabisa. Ni nadra, kama hata nimewahi kuhisi baridi kama tulivyohisi usiku huo.

Kwa kusita, tulianza kutembea kuelekea mji uliokuwa karibu, magari yakitupita kwa kasi. Mwishowe, gari moja likasimama, na kijana mmoja katupa usaidizi. Hatimaye tulipata kujua kuwa mafuta ya diesel katika tangi la mafuta yalikuwa yameganda kwa sababu ya baridi na kufanya kuwa vigumu kwetu kuendesha gari. Kijana huyu mwema alituendesha kurudi hadi nyumbani mwetu Midway. Nilijaribu kumlipa kwa huduma yake, lakini kwa wema alikataa. Alidhihirisha kuwa alikuwa Skauti Mvulana na alitaka kutenda kitendo chema. Nilijitambulisha kwake, na akaeleza shukrani yake kwa nafasi ya kipekee ya kuwa wa usaidizi. Kwa kudhani alikuwa wa rika ya misionari, nilimwuliza kama alikuwa na mipango ya kuhudumu misheni. Alionyesha kuwa hakuwa na hakika kile alichotaka kufanya.

Jumatatu iliyofuata asubuhi nilimwandikia barua huyu kijana na kumshukuru kwa ukarimu wake. Ndani ya barua nilimhimiza kuhudumu misheni ya wakati wote. Niliambatisha nakala ya mojawapo ya vitabu vyangu na kualamisha milango iliyozingatia huduma ya umisionari.

Karibu juma moja baadaye, mama wa yule kijana alipiga simu na kueleza kuwa mwanawe alikuwa kijana shupavu, lakini kuwa sababu ya athari fulani katika maisha yake, hamu yake ya muda mrefu ya kuhudumu misheni ilikuwa imedidimia. Alisema kuwa yeye na babake walikuwa wameomba na kufunga kwamba moyo wake ubadilishwe. Walikuwa wamepeleka jina lake katika orodha ya maombi katika Hekalu la Provo. Walitumaini kuwa huenda, kwa njia fulani, moyo wake ungeguswa kwa wema na angerudia hamu yake ya kuhudumu misheni na kumtumikia Bwana kwa uaminifu. Mama yake alitaka nijue kuwa aliona matukio ya jioni hiyo baridi kama jibu kwa maombi yao kwa niaba yake. Nilikubaliana naye.

Baada ya miezi kadha na mawasiliano zaidi na huyu kijana Dada Monson nami tulifurahi sana kuhudhuria karamu ya kumuaga kabla ya kuondoka kwake kwenda misheni katika ya British Columbia Vancouver.

Je! Ilikuwa sadfa kuwa njia zetu zilikutana usiku huo baridi wa desemba? Katu siamini hivyo. Badala yake, ninaamini mkutano wetu ulikuwa jibu kwa maombi ya moyoni ya baba na mama kwa mwana waliyemthamini.

Tena, akina ndugu na dada zangu, Baba yetu wa Mbinguni anafahamu mahitaji yetu na atatusaidia tunapomwita kwa usaidizi. Ninaamini hapa hata haja yetu iliyo ndogo au isiyo muhimu. Bwana ana haja na utondoti wa maisha yetu.

Nikependa kuhitimisha kwa kusimulia uzoefu moja wa hivi majuzi uliyokuwa na athari kwa mamia. Ulitokea katika tamasha za kitamaduni za Hekalu la Kansas City, miezi mitano tu iliyopita. Kama vile mambo mengi hufanyika maishani mwetu, wakati huo ilionekana tu kama uzoefu mwingine ambapo kila kitu kilienda kulingana na mpango. Hata hivyo, nilipofahamu kuhusu hali iliyohusishwa na tamasha za kitamaduni kabla ya kuwekwa wakfu kwa hekalu, nilitambua kuwa tamasha za usiku huo hazikuwa za kawaida. Badala yake, zilikuwa za ajabu.

Kama ilivyo na matukio yote yanayoambatanishwa na kuweka wakfu kwa hekalu, vijana katika wilaya ya Hekalu la Kansas City Missouri walikuwa wamefanyiwa mazoezi ya tamasha katika vikundi tofauti katika maeneo yao. Mpango ulikuwa kwamba wangekutana katika ukumbi mmoja mkubwa wa manispaa uliokuwa umekodishwa siku ya Jumamosi asubuhi ya maonyesho ili kujifunza wapi na wakati gani walipaswa kusimama na kiasi cha nafasi kati yao na mtu aliye karibu nao, na jinsi ya kuondoka jukwaani na kadhalika---mambo mengi ambayo wangepaswa kung’amua katika siku hiyo kwani waliokuwa wakisimamia waliweka sehemu mbalimbali pamoja ili maonyesho ya mwisho yawe yamesawazishwa, na ya kitalaamu.

Kulikwa na tatizo moja siku hiyo, onyesho lote lilikuwa linategemea sehemu zilizorekodiwa awali ambazo zingeonyeshwa kwenye skrini kubwa iitwayo Jumbotron. Sehemu hizi zilizorekodiwa zilikuwa muhimu kwa onyesho zima. Hazikuwa zimeungwa zote pamoja tu bali kila sehemu iliyowekwa kwenye sinema ya televisheni ingatanguliza onyesho lililofuata. Sehemu za video zilitia jukaa ambapo onyesho lote lilitegemea. Na hiyo Jumbotron haikuwa inafanya kazi.

Mafundi walifanya kazi kwa upesi upesi ili kutatua tatizo hilo wakati vijana wakingojea, mamia wao, wakipoteza wakati wao wa thamani wa kufanya mazoezi. Hali ilionekana kuwa ya kutowezekana.

Mwandishi na kiongozi wa tamasha, Susan Cooper, baadaye alieleza, “tuliposonga kutoka mpango A hadi B hadi Z, tulijua haikufua dafu… Tulipokuwa tunaangalia mpango wa ratiba, tulijua ingetushinda lakini tulijua kuwa tulikuwa na mojawapo ya uwezo mkubwa zaidi katika ghorofa ya chini---vijana 3,000. Tulihitaji kwenda chini na kuwaambia [wao] kilichokuwa kinaendelea na kupata nguvu kwa imani yao.”3

Saa moja kabla ya hadhira kuanza kuingia, vijana 3,000 walipiga magoti na kuomba pamoja. Waliomba kwamba wale waliokuwa wakirekebisha Jumbotron wangeongozwa kujua la kufanya ili kuirekebisha; waliuliza Baba wa Mbinguni atengeneze kile wao, hawangeweza kufanya wenyewe, kwa sababu ya ukosefu wa muda.

Akasema mmoja aliyeandika kuihusu baadaye, “ilikuwa ombi ambalo vijana hawatasahau, si kwa sababu sakafu ilikuwa mgumu, lakini kwa sababu Roho aliyeyusha mifupa yao.”4

Haikuwa muda mrefu kabla mmoja wa mafundi alipokuja kuwaambia kuwa tatizo lilikuwa limepatikana na kurekebishwa. Alisema suluhisho lilikuwa kwa ajili ya “bahati,” lakini wale vijana wote walijua vyema zaidi.

Tulipoingia kwenye ukumbi wa manispaa jioni hiyo, hatukuwa na habari yoyote kuhusu matatizo ya siku hiyo. Ni baadaye tu ndipo tulipofahamu kutoka kwao. Tulichoshuhudia, hata hivyo ilikuwa ni onyesho zuri la hali ya juu—mojawapo wa yaliyo bora zaidi niliyowahi kuyaona. Vijana waliangaza roho wa nguvu, tukufu ambayo ilihisiwa na wote waliokuwemo. Walionekana kujua hasa wapi pa kuingia, kusimama na kushirikiana na wachezaji wengine kati yao. Nilipojua kuwa mazoezi yao yalikuwa yamefupisha na kwamba sehemu nyingi hazikuwa zimefanyiwa mazoezi na kikundi kizima, nilishangazwa. Hakuna ambaye angelijua. Bwana kwa hakika alikuwa amefidia upungufu wao.

Kamwe sijaacha kushangazwa na jinsi Bwana anavyoweza kuhamasisha na kuongoza marefu na mapana ya ufalme Wake, na hali kuwa na wakati wa kutoa uongozi kuhusu mtu mmoja--- au tamasha moja ya kitamaduni, au Jumbotron moja. Hakika kwamba Yeye anaweza, na kwamba Yeye huweza, ni ushuhuda kwangu.

Akina ndugu na dada, Bwana yupo ndani ya maisha yetu sote. Anatupenda. Anataka kutubariki. Anataka tutafute usaidizi Wake. Anapotuongoza na kutuelekeza, kama anavyosikiliza na kujibu maombi yetu, tutapata furaha hapa na sasa anayotutakia. Na tuweni na ufahamu wa baraka Zake maishani mwetu, ninaomba, katika jina la Yesu Kristo, Mkombozi wetu, amina

Muhtasari

  1. 2 Nefi 2:25.

  2. Mafundisho na Maagano 112:10.

  3. Susan Cooper, in Maurine Proctor, “Nothing’s Too Hard for the Lord: The Kansas City Cultural Celebration,” Meridian Magazine, May 9, 2012, ldsmag.com.

  4. Proctor, Meridian Magazine, May 9, 2012.