2010–2019
Karibuni kwenye Mkutano Mkuu
Aprili 2013


Karibuni kwenye Mkutano Mkuu

Nawahimiza ninyi muwe na wasikivu na wenye kupokea jumbe ambazo sisi tutasikia. Kwamba tuweze kufanya hivyo ni maombi yangu.

Ndugu na dada zangu wapendwa, nina furaha jinsi gani kuwakaribisha ninyi kwenye Mkutano Mkuu wa Kanisa wa 183 wa Kila Mwaka.

Katika miezi sita tangu tulipokutana, imekuwa nafasi yangu kusafiri kidogo na kukutana na baadhi yenu katika maeneo yenu. Baada ya mkutano mkuu mwezi wa Oktoba, nilitembelea Ujerumani, ambapo ilikuwa fursa yangu kukutana na washiriki wetu katika sehemu kadhaa katika nchi hiyo, pamoja na sehemu za Austria.

Mwishoni mwa mwezi wa Oktoba, niliweka wakfu Hekalu la Calgary Alberta katika Kanada, kwa usaidizi wa Mzee na Dada M. Russell Ballard, Mzee na Dada Craig C. Christensen, Mzee na Dada William R. Walker. Katika mwezi wa Novemba, niliweka upya Hekalu la Boise Idaho. Pia waliosafiri nami na kushiriki katika kuweka wakfu huku walikuwa ni Mzee na Dada David A. Bednar, na Mzee na Dada William R. Walker.

Sherehe za kitamaduni zilizofanywa kuandamana na kuwekwa wakfu zilikuwa za kufana sana. Mimi sikuhudhuria sherehe za kitamaduni katika Calgary kwa vile ilikuwa ni maadhimisho ya miaka 85 ya kuzaliwa kwa Dada Monson na niliona inafaa niwe karibu naye. Hata hivyo, yeye nami tulikuwa na fursa ya kutazama hizo sherehe katika sebule yetu kwa kutimia televisheni ya muunganisho, na kisha tulisafiri kwa ndege hadi Calgary asubuhi iliyofuata kwa kuweka wakfu. Katika Boise zaidi ya vijana 9,000 kutoka wilaya ya hekalu walishiriki katika sherehe za kitamaduni. Walikuwepo vijana wengi mno waliojumuika hata kwamba hapakuwa na nafasi kwa wana familia kuhudhuria katika uwanja ambao walipokuwa wanafanya maonyesho.

Ni mwezi uliopita tu Mzee Dieter F. Uchtdorf, akiandamana na Dada Uchtdorf na Mzee na Dada Jeffrey R. Holland, na Mzee na Dada Gregory A. Schwitzer, walisafiri hadi Tegucigalpa, Hondoras, kuweka wakfu hekalu jipya lililomalizika huko. Sherehe za kitamaduni za kufana zilizoandaliwa na vijana zilifanyika jioni kabla ya kuwekwa wakfu.

Kuna mahekalu mengine ambayo yalitangazwa na ambayo yako katika wendo tofauti katika mfanyiko wa matayarisho au ambayo yako katika ujenzi.

Ni fursa yangu asubuhi ya leo kutangaza mahekalu wawili zaidi, ambayo katika miezi na miaka inayokuja yatajengwa katika maeneo yafuatayo: Cedar City, Utah, na Rio de Janerio, Brazil. Ndugu na kina dada, ujenzi wa mahekalu unaendelea bila kusita.

Kama mnavyojua, katika Mkutano Mkuu wa Oktoba nilitangaza mabadiliko katika umri ambao wavulana na wasichana wanaweza kuhudumu kama wamisionari wa muda, wavulana sasa wanaweza kuhudumu wakiwa umri wa miaka 18 na wasichana wakiwa umri wa miaka 19.

Kujibu kwa vijana wetu kumekuwa kwa ajabu sana na kuvutia sana. Kufikia tarehe 4 Aprili—siku mbili zilizopita—tuna wamisionari wa muda 65,634 wanaohudumu, tukiwa na zaidi ya 20,000 ambao wamepokea wito lakini bado hawajaingia katika kituo cha ummisionari na 6,000 zaidi katika mfanyiko wa mahojiano na maaskofu na marais wao wa vigingi. Imetubidi sisi kuunda misheni 58 mpya ili kutoa nafasi kwa ongezeko la idadi la wamisionari.

Ili kusaidia kukidhi mahitaji ya hili jeshi la wamisionari, na kwa sababu wengi wa wamsionari wetu wanatoka katika hali ya wastani, tunawaalika ninyi, kama vile mnavyoweza, kuchangia kwa moyo mkujufu kwenye Hazina Kuu ya Ummisionari ya Kanisa.

Sasa, ndugu na kina dada, tutasikia jumbe zenye maongozi leo na kesho. Wale ambao watatuhutubia sisi wametafuta kwa maombi kujua kile ambacho Bwana angependa sisi tusikie wakati huu.

Nawahimiza ninyi muwe na wasikivu na wenye kupokea jumbe ambazo sisi tutasikia. Kwamba tuweze kufanya hivyo ni maombi yangu katika jina la Yesu Kristo, Bwana, amina.