2010–2019
Kuitwa Naye Kutangaza Neno Lake
Oktoba 2013


Kuitwa Naye Kutangaza Neno Lake

Kama wewe ni mnyenyekevu na mtiifu na unasikia sauti ya Roho, wewe utapata furaha kuu katika huduma yako kama mmisionari

Nilipoidhinishwa kama Kiongozi Mkuu Mwenye Mamlaka Aprili iliyopita, Nilikuwa nikihudumu kama Rais wa Misheni kule India. Niliona moja kwa moja kile ambacho rais mwingine mstaafu wa misheni alikuwa ameniambia: “Wamisionari wa Kanisa hili ni wema mno.”1

Mmoja wa wamisionari wengi bora zaidi ambaye Dada Funk nami tulihudumu naye alikuwa Mzee Pokhrel kutoka Nepal. Baada ya kuwa mshiriki wa Kanisa kwa miaka miwili tu, aliitwa kuhudumu katika Misheni ya India Bangalore, Misheni inayotumia kingereza. Angekuambia hakuwa amejitayarisha vizuri. Hiyo ilikuwa ya kueleweka. Hakuwahi kuona mmisionari hadi alipokuwa mmisionari. kwa sababu kulikuwa hakuna wamisionari vijana waliohudumu katika Nepal. Hakusoma Kiingereza vizuri ya kutosha ili kuelewa maelekezo yaliyokuja pamoja na wito wake. Alipowasili katika kituo cha mafunzo yamisionari, badala ya kuleta longi nzuri, mashati meupe, na tai, alibeba, kwa maneno yake, “jozi tano za jinzi za denimu, T-shati kadhaa, na mafuta mengi ya nywele.”2

Hata baada ya kupokea nguo zilizofaa, alisema alihisi mpungufu kwa wiki chache za kwanza. Alieleza wakati huo wa misheni yake: “Siyo tu Kiingereza kilikuwa kigumu, lakini kazi ilikuwa ngumu vile vile ... Juu ya hayo yote nilikuwa na njaa, nimechoka, na kutamani nyumbani. ... Hata ingawa hali ilikuwa ngumu, nilikuwa nimejitahidi. Nilihisi mdhaifu na mpungufu. Ningeomba Baba wa Mbinguni wakati huo anisaidie. Bila shaka, kila wakati niliomba, ningehisi kufarijiwa.”3

Ingawa kazi ya umisionari ilikuwa mpya na ngumu kwa Mzee Pokhrel, alihudumu na imani kubwa na uaminifu, akitafuta kuelewa na kufuata kile alichokuwa akijifunza kutoka maandiko, Hubiri Injili Yangu, na viongozi wake wa misheni. Akawa mwalimu mwenye nguvu wa injili---katika lugha ya Kiingereza---na kiongozi bora. Baada ya misheni yake na muda fulani kule Nepal, alirudi India kuendelea na elimu yake. Tangu Januari amehudumu kama rais wa tawi kule New Delhi. Kwa sababu ya ukuaji wa kweli alioupata kama mmisionari, anaendelea kuchangia ukuaji wa kweli wa Kanisa nchini India.

Kijana ambaye kamwe hakuwai kumwona mmisionari alikuwaje mmoja mwenye nguvu za kiroho hivyo? Utapokeaje nguvu za kiroho kama mmisionari ili kufungua milango, masanduku ya ndani, na mioyo ya wale katika misheni ambapo utakapohudumu? Kama kawaida, majibu yanapatikana katika maandiko na maneno ya manabii walio hai na mitume.

Injili ilipohubiriwa kwa mara ya kwanza mnamo Julai 1837, Bwana alifunua, “Yeyote mtakayemtuma katika jina langu, kwa sauti ya ndugu zenu, hawa Kumi na Wawili, akiwa amependekezwa na kupewa mamlaka kisheria na nyinyi, atakuwa na uwezo wa kufungua mlango wa ufalme wangu kwa taifa lolote ninyi mtawatuma.”4

Popote ambapo umetumwa, kwa misheni yoyote ambayo umeitwa, jua ya kwamba mshiriki wa Wale Kumi na Wawili alipendekeza kwa kihalali wito huo na umeitwa na nabii wa Bwana. Umeitwa kwa “unabii, na kwa kuwekewa mikono.”5

Bwana kisha akatoa masharti ya ahadi hii kutekelezwa. Alisema, “ Alimradi [inayomaanisha ahadi itatekelezwa kama] wao [wamisionari ambao wametumwa] [1] watajinyenyekeza mbele zangu, na [2] kukaa katika neno langu, na [3] kusikia sauti ya Roho wangu.”6

Ahadi za Bwana ni dhahiri. Ili kuwa na nguvu za kiroho zinazohitajika kufungua mlango wa Ufalme wa Mungu katika taifa ambalo umetumwa, lazima uwe mnyenyekevu, na mtiifu, na kuwa na uwezo wa kusikia na kufuata Roho.

Hizi sifa tatu karibu zinahusiana. Ikiwa wewe ni mnyenyekevu, utataka kuwa mtiifu. Ikiwa wewe ni mtiifu, utahisi Roho. Roho ni muhimu; kwa kama Rais Ezra Taft Benson alivyofundisha, “Bila Roho, kamwe hautafanikiwa bila kujali talanta yako na uwezo.”7

Kama Rais wa misheni, mara kwa mara niliwahoji wamisionari ambao walitatizika kwa sababu bado hawakuwa wasafi kikamilifu. Waliishi chini ya uwezo wao wa kiroho. Haijalishi vile walivyofanya kazi kwa bidii ama wema waliofanya, walikuwa hawawezi kuhisi amani na kufurahia kikamilifu uenzi wa Roho Mtakatifu hadi wangejinyenyekeza, watubu kikamilifu, na kupokea rehema na neema ya Mwokozi.

Bwana anawaelekeza watumishi Wake wawe wanyenyekevu, kwa sababu mchakato wa kuwa mzima kiroho huanza na moyo uliovunjika. Fikiria wema ambao huja kutoka kwa vitu vilivyovunjika: Udongo huvunjwa ili kupanda ngano. Ngano huvunjwa ili kutengeneza mkate. Mkate huvunjwa ili kuwa nembo ya sakramenti. Wakati mmoja, yule anayetubu, anapokula sakramenti na moyo uliovunjika na roho iliyopondeka, yeye huwa mkamilifu.8 Tunapotubu na kuwa wakamilifu kupitia Upatanisho wa Yesu Kristo, tuna mengi zaidi kumpa Mwokozi tunapomtumikia. “Ndio, njooni kwake na mmtolee nafsi zenu kama sadaka kwake.”9

Ukiwa unalemewa na dhambi na unahitaji kutubu, tafadhali fanya hivyo mara moja. Mwokozi alipowaponya wale ambao walikuwa wagonjwa, mara nyingi aliwaalika waamke. Maandiko yana rekodi kwamba walifanya hivyo punde au mara moja.10 Ili kuponywa mateso yako ya kiroho, tafadhali kubali aliko lake la kuinuka. Bila kuchelewa, zungumza na Askofu wako, rais wa tawi, au rais wa misheni na uanze mchakato wa toba sasa.

Nguvu ya uponyaji ya Upatanisho italeta amani kwa nafsi yako na kukuwezesha kuhisi Roho Mtakatifu. Dhabihu ya Mwokozi haina kipimo, lakini dhambi zetu, ingawa nyingi na kubwa, zinaweza kuhesabiwa na kukiriwa, kuachwa na kusamehewa. “Ni shangwe kubwa kiasi gani kwake katika nafsi ambayo hutubu!”11

Ahadi hii katika Mafundisho na Maagano ina nguvu: “Na wema uyapambe mawazo yako bila kukoma; ndipo kujiamini kwako kutakuwa imara katika uwepo wa Mungu.”12 Na unapoishi maisha ya wema, utahisi kujiamini kwa amani katika msimamo wako mbele za Mungu na utakuwa na nguvu ya Roho kuwa pamoja nawe.13

Baadhi ya watu ambao ni washiriki wa hivi karibuni wa Kanisa au ambao hivi karibuni wamerejea kwa ushirika kamili huenda wakasema, “Sasa ninastahili na nina hamu ya kuhudumu, lakini sijui kama najua ya kutosha.” Mnamo Aprili, Rais Thomas  S. Monson alitufundisha, “ufahamu wa ukweli na majibu ya maswali yetu makubwa hutukujia tunapotii amri za Mungu.”14 Ni ya kutuliza jinsi gani kujua kwamba kupitia utii wetu sisi hupata maarifa.

Wengine huenda wakahisi wana vipaji vidogo, uwezo, ama uzoefu wa kutoa. Ikiwa una wasiwasi kama huo, kumbuka yale ambayo Mzee Pokhrel alipitia. Jiandae vyema uwezavyo na ujue kwamba Baba yetu aliye Mbinguni atapanua juhudi zako za utiifu na unyenyekevu. Mzee Richard  G. Scott alitoa ushauri huu wa kutia moyo: “Tunapotii amri za Bwana na kuwatumikia watoto Wake bila ubinafsi, matokeo ya asili ni nguvu kutoka kwa Mungu---nguvu ya kufanya zaidi tunavyoweza kufanya wenyewe. Ufahamu wetu, vipawa vyetu, uwezo wetu hupanuliwa kwa sababu tunapokea nguvu na uwezo kutoka kwa Bwana.”15

Unapotumaini katika Bwana na wema Wake, Mwenyezi Mungu atawabariki watoto wake kukupitia kwako.16 Mzee Hollings kutoka Nevada alijifunza hayo mapema katika misheni yake. Siku baada ya kuwasili kwake nchini India, alisafiri na Dada Funk nami hadi Rajahmundry, eneo lake la kwanza. Mchana huo Mzee Hollings na Mzee Ganaparam walienda kumtembelea mshiriki wa Kanisa na mama yake. Mama alitaka kujifunza juu ya Kanisa, kwa sababu alikuwa ameona jinsi injili ilivyobariki maisha ya binti yake. Dada Funk alijiunga nao kutoa ushirika. Kwa sababu somo lingefundishwa kwa Kiingereza na mama alizungumza tu Telugu, ndugu katika tawi alikuwa yupo ili kutafsiri kile kilichofundishwa.

Jukumu la Mzee Hollings katika darasa lake la kwanza la kufundisha lilikuwa kufundisha Ono La Kwanza akitumia maneno ya Nabii Joseph. Katika sehemu hiyo ya somo alimgeukia Dada Funk na kuuliza, “Je, napaswa niliseme neno baada ya lingine?” nikiwa najua kuwa litatafsiriwa.

Alijibu, “Liseme neno baada la lingine ili Roho aweze kushuhudia kile usemacho.”

Wakati misionari huyu mpya alipofundisha kwa dhati Ono la Kwanza, akitumia maneno ya Mtume, uso wa dada huyo mpendwa ulibadilika. Machozi yalionekana. Mzee Hollings alipokamilisha ujumbe huo mtukufu, na kabla ya kile alichosema kitafsiriwe, aliuliza kupitia machozi yake katika lugha yake ya asili, “Naweza kubatizwa? Na utamfundisha mwanangu?”

Watumishi vijana wangu wapendwa, milango na mioyo hufunguliwa kila siku kwa ajili ya ujumbe---ujumbe ambao huleta tumaini na amani na furaha kwa watoto wa Mungu duniani kote. Ikiwa ninyi ni wanyenyekevu, na watiifu, na mnasikiliza sauti ya Roho, mtapata furaha kubwa katika huduma yenu kama wamisionari.17 Nini msimu ajabu kuwa mmisionari---wakati ambapo Bwana anaharakisha kazi yake!

Nashuhudia Mwokozi wetu, Yesu Kristo, na “amri Yake tukufu”18 ya “endeni basi, mkawafundishe mataifa yote.”19 Hili ni kanisa Lake. Analiongoza kupitia manabii walio hai na mitume. Wakati wa saa ijayo, Urais wa Kwanza utatufundisha. Tuweze kuwa “wepesi wa kutazama,”20 kama alivyokuwa Mormoni, ili wakati wito utakuja, tunastahili na tuna uwezo wa kutangaza kwa nguvu ya Roho: “Tazama, mimi ni mwanafunzi wa Yesu Kristo, Mwana wa Mungu. Nimeitwa na yeye kutangaza neno lake miongoni mwa watu wake, ili wawe na maisha ya milele.”21 Katika jina la Yesu Kristo, Amina.

Muhtasari

  1. Personal conversations with Dennis C. Brimhall, president of the Kentucky Louisville Mission, 2005–8.

  2. Ashish Pokhrel, “My Name Is Ashish Pokhrel and This Is My Story” (unpublished personal history, Sept. 2011).

  3. Pokhrel, “My Name Is Ashish Pokhrel.”

  4. Mafundisho na Maagano 112:21.

  5. Makala ya Imani 1:5.

  6. Mafundisho na Maagano 112:22.

  7. Ezra Taft Benson, in Preach My Gospel: A Guide to Missionary Service (2004), 176.

  8. Mawazo kutoka kwa hotuba iliyotolewa na Mzee Jeffrey R. Holland huko Bountiful Utah North Stake conference, June 8–9, 2013.

  9. Omni 1:26.

  10. Ona Marko 5:41–42; Yohana 5:8–9.

  11. Mafundisho na Maagano 18:13.

  12. Mafundisho na Maagano 121:45.

  13. Ona Mafundisho na Maagano 121:46.

  14. Thomas S. Monson, “Obedience Brings Blessings,” Ensign au Liahona, May 2013, 89.

  15. Richard G. Scott, “For Peace at Home,” Ensign au Liahona, May 2013, 30.

  16. Katika kuelezea kile mmisionari mpya atafanya, Mzee Russell M. Nelson alisema: “Wao watafanya kile wamisionari daima wamefanya. Wao huhubiri injili! Wao hubariki watoto wa Mwenyezi Mungu!” (“Catch the Wave,” Ensign au Liahona, May 2013, 45).

  17. Ona Hubiri Injili Yangu, v.

  18. Thomas S. Monson, “Come, All Ye Sons of God,” Ensign au Liahona, May 2013, 66.

  19. Mathayo 28:19.

  20. Mormoni 1:2.

  21. 3 Nefi 5:13.