2010–2019
Kuendelea Kushikilia kwa Nguvu
Oktoba 2013


Kuendelea Kushikilia kwa Nguvu

Na tuendelee kushikilia fimbo ya chuma ambayo itatuongoza hata katika uwepo wa Baba yetu wa Mbinguni.

Baba Yangu angeweza kukumbuka siku ile, hata saa ile ambayo familia yao—baba, mama, na watoto wanne—walipoacha Kanisa, wengi wao hawakurudi tena katika maisha haya. Alikuwa na miaka 13, shemasi, na katika siku hizo familia zilihudhuria mafundisho ya Jumapili asubuhi na kisha Sakramenti wakati wa mchana. Katika siku maridani majira ya kuchipua, baada ya kurudi kutoka katika ibada ya kuabudu ya Jumapili asubuhi na kuwa na chakula cha familia kati kati ya siku, mama yake akamgeukia baba yake akamuuliza kirahisi, “Sasa, mpendwa, unafiriki twende kwenye mkutano wa Sakramenti mchana huu au tuipeleke familia kwa safari ya gari hadi mikoani?”

Wazo kwamba kulikuwa na chaguo la mkutano wa sakramenti halijawahi kutokea kwa baba yangu, lakini yeye pamoja na ndugu zake watatu walikaa na kusikiliza kwa umakini mkubwa. Hio safari ya gari ya Jumapili mchana ilikuwa ni ya kufurahiwa sana na familia, lakini uamuzi huo mdogo ukawa ndio mwanzo wa mweleko mpya, ambao baadaye ulielekezea familia mbali kabisa na Kanisa kutoka kwenye usalama, ulinzi na baraka kwenda kwenye njia tofauti.

Kama somo kwa wale wenzetu wa siku za leo ambao wanaweza kuwa wameshawishiwa kuchukua njia tofauti, Nabii wa Kitabu cha Mormoni alishiriki ono hii na familia yake ambapo yeye “aliona umati mkubwa wa watu usio na idadi, wengi wao ambao walikuwa wanasogea mbele, ili wapate kufikia njia ambayo ilielekea kwenye mti ambapo [yeye] alikuwa amesimama.

“Na … walifika hapo mbele, na kuipata njia iliyoelekea kwenye mti.

“Na … kulitokea ukungu wa giza; …  hadi wale ambao walikuwa wametangulia njia walipotea njia, kwamba walizungukazunguka na kupotea.”1

Baadaye Lehi aliona kundi la pili ambalo lilikuwa “wakisonga mbele, na wakafika mbele na wakashika mwisho wa fimbo ya chuma; na wakasonga mbele na kupenya ukungu wa giza, wakishikilia fimbo ya chuma, hadi wakafika na kula matunda ya mti.” Bahati mbaya, “Na baada ya kula matunda ya mtu wakatupa macho yao hapa na pale wakawa kama wanaaibika.” Kwa sababu ya wale waliokuwa katika “jengo kubwa na pana” ambao “waliokuwa wakiwadharau na kuwanyooshea vidole wale walikuwa wamekuja … kula lile tunda.” Watu hawa basi “wakaingia katika njia zilizokataliwa na wakapotea.”2 Hawakuweza, au labda hawakupenda, kuvumilia hadi mwisho.

Na kulikuwa, hata hivyo, kundi la tatu ambalo halikufanikiwa kuufikia mti wa uzima, wao baadaye hawakupotea. Juu ya hawa maandiko yanasema kwamba “na wakasonga mbele, daima wameshikilia ile fimbo ya chuma hadi wakafika na kunama na kula matunda ya ule mti.”3 Fimbo ya chuma iliwakilisha katika kundi hili la watu usalama pekee na ulinzi ambao wangeupata, na walishikilia kwa nguvu mara zote; walikataa kuachilia hata kile kilichorahisi kama vile kwenda safari ya gari Jumapili mchana hata mikoani.

Kuhusu kundi hili la watu, Mzee David  A. Bednar amefundisha: “Kishazi muhimu ni ‘daima kushikilia’ kwenye fimbo ya chuma. …Labda kundi hili la tatu la watu mara yote lilisoma na kujifunza na kuyapekua maneno ya Kristo. …Hili ni kundi ambalo wewe na mimi tunatakiwa tujitahidi kujiunga nalo.”4

Wale wenzetu ambao ni washiriki wa Kanisa la Mungu leo hii wamefanya maagano kumfuata Yesu Kristo na kutii amri za Mungu. Wakati wa ubatizo tuliweka maagano kusimama kama mashahidi wa Mwokozi,5 kuwasaidia walio wadhaifu na wenye mahitaji,6 kuweka amri za Mungu, na kutubu inapohitajika, kama vile Mtume Paulo alivyofundisha, “Wote wametenda dhambi, na wamepungukiwa na utukufu wa Mungu.”7

Kila wiki tuna fursa ya kuhudhuria mkutano wa sakramenti ambapo tunaweza kufanya upya tena maagano haya kwa kupokea mkate na maji ya agizo la sakramenti. Kitendo hiki rahisi kinaturuhusu kwa mara nyingine kujiahidi tena kumfuata Yesu Kristo na kutubu pale tunapopungukiwa. Ahadi ya Mungu kwetu ni kutupa Roho Wake kama muongozo na ulinzi.

Kutoka katika Hubiri Injili Yangu, wamisionari wetu hufundisha kwamba ufunuo na ushuhuda unakuja wakati tunapohudhulia Mikutano yetu ya Kanisa ya Jumapili: “Tunapohudhuria ibada za Kanisa na kuabudu pamoja, tunaimarishana. Tunafanywa upya kwa uhusiano wetu na marafiki zetu na wanafamilia, imani yetu inaimarishwa tunaposoma maandiko na kujifunza zaidi kuhusu injili iliyorejeshwa.”8

Mtu anaweza kuuliza, kwa nini kuna mikutano mitatu tofauti siku ya Jumapili na kuna haja gani ya kila moja? Kwa kifupi na tuangalie mikutano hii mitatu:

  • Mkutano ya Sakramenti hutupatia fursa kushiriki katika maagizo ya sakramenti. Tunayafanya upya maagano yetu, tunapokea na kuongeza kipimo cha Roho, na tunakuwa na baraka za ziada za kufundishwa na kuinuliwa na Roho Mtakatifu.

  • Shule ya Jumapili inaturuhusu “kufundishana mafundisho ya ufalme,”9 ili wote “tuinuliwe na kufurahia pamoja.”10 Nguvu kubwa na amani ya kibinafsi huja tunapoelewa mafundisho ya injili iliyorejeshwa.

  • Mikutano ya Ukuhani ni wakati wa wanaume na vijana “kujifunza wajibu [wao] ”11 na  kufundishwa kwa kina zaidi,”12 na Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama huwapa wanawake wa Kanisa fursa ya “kuongeza imani yao …, kuimarisha familia na nyumba [zao], na kuwasaidia wenye mahitaji.”13

Vivyo hivyo, wasichana na watoto wana mikutano yao na madarasa yao ambapo wanafundishwa injili wanapojiandaa kwa ajili ya majukumu muhimu ambayo yanawaelekea. Katika kila mmoja ya hii mikutano ya kipekee lakini iliyounganika, tunajifunza mafundisho, tunahisi Roho, na tunahudumiana. Ingawa kunaweza kuwa na utofauti kwa sababu za umbali, gharama za usafiri, au afya, inabidi tujitahidi kuhudhuria mikutano yetu yote ya Jumapili. Nawaahidi kwamba baraka za shangwe kuu na amani zitakuja kutoka kwa ibada wakati wa ratiba ya mikutano wa masaa matatu.

Familia zetu zimeahidi mara zote kuhudhuria mikutano yetu yote ya Jumapili. Tumeona kwamba hii huimarisha imani yetu na kuongeza uelewa wetu wa injili. Tumejifunza kwamba tunajisikia vizuri kuhusu maamuzi yetu ya kuhudhuria mikutano ya Kanisa, haswa tunaporudi nyumbani kwetu nakuendelea kuitii Sabato. Vile vile tunahudhuria mikutano yetu yote ya Jumapili wakati tunapokuwa mapumzikoni au tumesafiri. Mmoja wa mabinti wetu hivi karibuni aliandika kusema kwamba alihudhuria kanisa katika mji ambao alikuwa anasafiri na kuongeza, “Ndio, Baba, Nilihudhuria mikutano yote mitatu ya Jumapili.” Tunajua kwamba alibarikiwa kwa maamuzi hayo mema.

Kila mmoja wetu ana maamuzi mengi ya kufanya jinsi ya kuiweka siku ya Sabato. Mara zote kutakuwa na shughuli “nzuri” ambayo inaweza na lazima ifanywe dhabihu kwa ajili ya maamuzi bora ya Mahudhurio ya Mikutano ya Kanisa. Kiukweli hii ni moja ya njia ambayo adui “hudanganya [nafsi zetu], na kutuelekeza [kiumakini] mbali.”14 Yeye hutumia shughuli “nzuri” kama mbadala wa “bora” au hata shughuli “bora sana.15

Kuendelea kushikilia kwa juhudi fimbo ya chuma inaamanisha tuhudhurie katika mikutano yote ya Jumapili: mikutano ya sakramenti, Shule ya Jumapili, na ukuhani au Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama. Watoto wetu na vijana wahudhurie mikutano yao katika Msingi, Wavulana na Wasichana. Hatupaswi kuteua au kuchagua mkutano upi wa kuhudhuria. Kirahisi tu tunashikilia kwa juhudi neno la Mungu kwa kuabudu na kuhudhuria mikutano yetu ya Sabato.

Kuendelea kushikiria fimbo ya chuma inamaanisha kwamba tujitahidi kutii amri zote za Mungu, kuwa na sala na kila siku za kibinafsi na kifamilia, na kusoma maandiko kila siku.

Kuendelea kushikilia ni sehemu ya mafundisho ya Kristo yaliyofundishwa katika Kitabu cha Mormoni. Tunaifanyia kazi Imani katika Yesu Kristo, tunatubu dhambi zetu, na kubadilisha mioyo yetu, na kumfuata Yeye chini katika maji ya ubatizo na kupokea uhakiki wa karama ya Roho Mtakatifu, ambayo inafanya kazi kama mwongozo na mfariji. Na tena, kama Nefi alivyofundisha, “tunasonga mbele tukisheherekea katika maneno ya Kristo” mpaka mwisho wa maisha yetu.16

Ndugu na dada zangu, sisi ni watu wa agano. Kwa utashi wetu tunafanya na kuweka maagano, na baraka zilizoahidiwa ni kwamba tutapokea “Yote yale Baba yetu anayo.”17 Tunapoendelea kushikilia kwenye fimbo ya chuma kwa kutii maagano yetu, tutaimarishwa ili kujikinga na majaribu na hatari za dunia. Tutakuwa na uwezo wa kuendesha maisha yetu ya hapa duniani na changamoto zake mpaka tutakapoufikia mti wenye matunda “kitu kizuri sana na kinachopendwa zaidi ya vitu vingine vyovyote.”18

Baba yangu alikuwa na bahati ya kuoa mwanamke mwema ambaye alimtia moyo wa kurudi kanisani la ujana wake na akaanza tena kuendelea katika njia hiyo. Maisha yao ya uaminifu yamebariki watoto wake wote, kizazi kijacho cha wajukuu, na sasa vitukuu.

Kama ilivyo maamuzi rahisi kuhudhuria au kutohudhuria kwao siku moja ya Sabato katika mikutano ya kuabudu ilifanya tofauti kubwa katika maisha ya familia ya babu yangu, maamuzi yetu ya kila siku yataadhiri maisha yetu katika njia nyingi kubwa. Uamuzi unaoonekana mdogo kama vile kuweza au kutoweza kuhudhuria mkutano wa sakramenti unaweza kuwa na matokeo yenye athari, na hata ya milele.

Na tuchague kuwa na bidii na kupata baraka kubwa na ulinzi ambao huja kutoka katika mikusanyiko ya pamoja na kuweka maagano. Na tuendelee kushikilia fimbo ya chuma ambayo itatuongoza hata katika uwepo wa Baba yetu wa Mbinguni ni maombi yangu katika jina takatifu la Yesu Kristo, amina.