2010–2019
Kuharakisha Mpango wa Bwana
Oktoba 2013


Kuharakisha Mpango wa Bwana!

Lazima sote tutengeneze na tutekeleze mpango wetu wenyewe wa kibinafsi na shauku ya kuhudumu pamoja na wamisionari wa muda.

Miaka michache iliyopita nilihitaji kuzungumza na mke wa mmoja wa askofu katika kigingi chetu, hivyo basi nikapiga simu nyumbani kwao. Mwana mdogo akashika simu. Nikasema, Habari, mamako yupo?”

Jibu lake, “Ndio, yupo. Nitamwita. Je, huyu ni nani?”

Jibu langu: “ Mweleze ni Rais Nielsen.”

Kulikuwa na kimya kifuupi, na kisha, katika sauti ya kusisimua sana, nikasikia, “Ee!, Mama, Rais Hinckley yuko kwenye simu!”

Siwezi kufikiria kile huenda alikuwa akifikiria. Lazima iwe ilikuwa safari ndefu kabisa ambayo aliwahi kuwa nayo kuelekea kwa simu. Wazo lilinijia: “Je, nimhadae? Sikumhadaa lakini tulicheka kweli kweli. Sasa ninavyofikiria kuhusu hayo, lazima iwe alikuwa amevujwa moyo kuzungumza nami tu [na si Rais Hinckley].

Je, ungefanya nini kama nabii wa Bwana angekupigia simu kwa kweli? Amekupigia! Rais Thomas  S.Monson, kama yeye alivyofanya tena asubuhi ameita kila mmoja wetu kwa kazi muhimu sana. Alisema, “Sasa ni wakati wa washiriki na wamisionari kuja pamoja, kufanya kazi pamoja, kufanya kazi katika shamba la Bwana ili kuleta nafsi Kwake” (“Faith in the Work of Salvation” [worldwide leadership training broadcast, June 2013]; lds.org/broadcasts).

Je, tumekuwa tukisikiliza?

Kote duniani, vikingi, wilaya na misheni zinaona kiwango kipya cha bidii, tangazo la Mwokozi kwa Joseph Smith mnamo 1832 linapotekelezwa: “Tazama nitaharakisha kazi yangu katika wakati wake.” (M&M 88:73).

Akina ndugu na dada, wakati huo ni sasa! Ninauhisi, na nina uhakika ninyi pia mnauhisi

Nilitaka kuweka furaha yangu na imani yangu katika Yesu Kristo katika matendo. Nilipokuwa nikicheza mchezo wa mpira, nilifikiria kulingana na mipango ya mchezo. Hakukuwa na shaka kwenda katika mashindano ikiwa timu yetu ilikuwa tayari na wachezaji waliofaa, tungepata mafanikio. Hata hivyo, hivi karibuni nilizungumza na kocha anaye aminika wa BYU, LaVell Edwards juu ya mpango wetu wa mchezo, na akasema, Sijali ni mpango gani utachagua ila tu tufunge bao!” Kama mmoja wa mchezaji mkuu wake, nilifikiri ilikuwa vigumu zaidi kuliko hiyo, lakini pengine falsafa yake rahisi ndiyo sababu ana uwanja ulioitwa jina lake.

Kwa vile sote tuko katika timu ya Bwana, je, sote tunao mpango wetu wenyewe wa kushinda? Je, tuko tayari kucheza? Ikiwa sisi, kama washiriki, kwa kweli tulipenda familia zetu, marafiki, na washiriki, je, si tutataka kushiriki ushuhuda wetu wa injili rejesho nao?

Katika warsha ya marais wapya wa misheni iliyokuwa mnamo Juni, marais wapatao 173 na wake zao walipokea maelekezo ya mwisho kabla ya kuanza huduma yao. Washiriki wote 15 wa Urais wa kwanza na Jamii ya Mitume Kumi na Wawili walihutubia kundi hili maalum.

Mzee L. Tom Perry aliongeza maoni ya kuhitimisha “Huu ni wakati wa ajabu zaidi katika historia ya Kanisa. Hili ni jambo ambalo linalingana na matukio makubwa yaliyotokea katika historia ya nyuma, kama vile Ono la Kwanza, kama vile karama ya Kitabu cha Mormoni, kama vile Urejesho wa injili, kama vile vitu vyote vilivyojenga huo msingi kwa ajili yetu kuendelea mbele na kufundisha katika ufalme wa Baba yetu wa Mbinguni” (“Concluding Remarks” [hotuba iliyotolewa katika warsha ya marais wapya wa misheni, June 26, 2013], 1, Church History Library, Salt Lake City).

Tunahitaji kushughulika kama vile hatujawahi tena ili kulingana na msisimko wa viongozi wetu na dhamira ya wamisionari wetu wa muda. Kazi hii haitasonga mbele kama vile Bwana alivyokusudia bila sisi! Kama vile Rais Henry  B. Eyring amesema, “Bila kujali umri wetu, uwezo, wito Kanisani, au eneo, sisi ni kitu kimoja tumeitwa kwa kazi ili kumsaidia Yeye katika mavuno Yake ya nafsi” (“We Are One,” Ensign or Liahona, May 2013, 62).

Naomba nikaweze kushiriki mpango maalum ambao nimehisi kuvutiwa kutekeleza baada kuomba, na kusoma sura ya 13 ya Hubiri Injili Yangu, ya kutafakari matukio yaliyopita, Nawaalika mzingatie pointi hizi tatu mnapofikiria juu ya mipango yenu wenyewe.

Kwanza, omba hasa kuleta mtu karibu na Mwokozi na injili Yake kila siku. Unaweza kufanya hivyo kwa kuona watu wote kama wana na mabinti za Mungu tukisaidiana kwenye safari yao kurudi nyumbani. Fikiria juu ya marafiki wapya utakaopata.

Pili, waombee wamisionari wanaohudumu katika eneo lako na wachunguzu wao kwa majina yao kila siku. Njia ya pekee ya kufanya hivyo ni kuwasalimia, angalia beji yao, waite kwa majina yao, na waulize wanawafundisha kina nani. Mzee Russell  M. Nelson hivi karibuni alieleza, “Hadi ujue jina la mtu na sura, Bwana hawezi kusaidia kujua moyo wake.”

Nilihudhuria ubatizo wa dada mzuri aliyeshiriki ushuhuda wake. Milele nitakumbuka akisema, “Sijawahi kuwa na watu wengi hivi wakiniombea na kuhisi upendo mwingi sana! Mimi najua kuwa kazi hii ni ya kweli!“

Tatu, alika rafiki kwa shughuli ndani au nje ya nyumba yako. Popote mwendapo au chochote mfanyacho, tafakari ni nani angefurahia tukio hilo na kisha msikilize Roho anavyokuongoza.

Mwokozi amenifundisha somo lililo wazi katika kujifunza kwangu injili ambalo, naamini, linatumika vizuri kwa “kuharakisha”. Wakati nina hisia zito kuhusu jambo fulani, huonekana katika maandishi yangu na mara nyingi huishia katika alama ya mshangao ambayo maana inaonyesha “hisia kali [au] ama ishara ya umuhimu mkubwa” (Merriam-Webster’s Collegiate Dictionary, 11th ed. [2003], “exclamation point”).

Nilifurahishwa vile maandiko kuhusu “mkusanyiko ambaouliyoishia na alama hii ya kituo, yalianza kuonekana, kama vile ombi la dhati la Alma: “Ee vile natamani ningekuwa malaika, na ningekuwa na matarajio ya moyo wangu, kwamba ningeenda mbele na kuhutubia watu na parapanda ya Mungu, na sauti ya kutingisha ulimwengu, na kuhubiri toba kwa watu wote!” (Alma 29:1).

Utafiti unapendekeza kuna vifungu 65 vinavyoonyesha hisia za nguvu za kimisionari, ikijumuisha hivi.

“Ni shangwe kubwa kiasi gani kwake katika nafsi ambayo hutubu! …

“Na kama itakuwa kwamba utafanya kazi siku zako zote katika kutangaza toba kwa watu hawa, na kuleta, japo iwe nafsi moja kwangu, shangwe yako itakuwa kubwa jinsi gani pamoja naye katika ufalme wa Baba yangu!

“Na sasa, kama shangwe yako itakuwa kubwa kwa hiyo nafsi moja ambayo umeileta kwangu katika ufalme wa Baba yangu, itakuwa shangwe kubwa namna gani kwako kama utazileta nafsi nyingi kwangu!” (M&M 18:13, 15–16).

Ufahamu wangu wa mistari hii ya kipekee ulitenda jukumu muhimu katika zoezi langu la kwanza kama Sabini wa Eneo. Nilikuwa na wasiwasi kidogo kuwa mwenzi wa Mtume, Mzee Quentin  L. Cook, katika mkutano mkuu wa kigingi. Nilipotembea katika ofisi ya rais wa kigingi mwishoni mwa wiki hiyo, niliona jozi la viatu vilivyokuwa vinaonekana vimechakaa juu ya kredenza nyuma ya dawati lake na ikiwa pamoja na andiko linaloishia na alama ya mshangao. Nilipokuwa nikilisoma, nilihisi Bwana alikuwa na ufahamu juu ya masomo yangu na alikuwa amejibu maombi yangu na kwamba alijua ni nini hasa nilihitaji ili kutuliza moyo wangu.

Nilimwuliza rais wa kigingi aniambie hadithi ya viatu hivyo.

Alisema:

“Hivi ni viatu vya kijana mpya Kanisani ambaye hali ya familia yake ilikuwa ngumu, lakini bado alikuwa na nia ya kuhudumu misheni ya kufuzu na alifanya hivyo kule Guatemala. Aliporejea nilikutana naye kumuachisha kwa heshima na nikaona kuwa viatu vyake vilikuwa vimechakaa. Kijana huyu alikuwa ametoa yote kwake Bwana bila msaada mkubwa, ikiwapo wowote, kutoka kwa familia.

“Aligundua nilikuwa nikitazama viatu vyake na akaniuliza, ‘Rais kuna chochote kibaya?”

“Nilijibu, Hapana, Mzee, kila kitu kiko sawa! Je, ninaweza kuchukua viatu hivyo?”

Rais wa kigingi akaendelea: Heshima yangu na upendo kwake huyu mmisionari aliyerejea nyumbani ulipita kifani! Nilitaka kukumbuka tukio hilo, hivyo basi nikavibadilisha rangi viatu vyake. Ni kumbusho kwangu ninapotembea kuingia katika ofisini kwa juhudi ambayo lazima sote tutoe licha ya hali zetu. Mstari ulikuwa kutoka kwa Isaya: “Jinsi ilivyo mizuri juu ya milima Miguu yake aletaye habari njema, Yeye aitangazaye amani, Aletaye habari njema ya mambo mema, Yeye autangazaye wokovu, Auambiaye Sayuni, Mungu wako anamiliki!’ (Isaya 52:7).”

Akina ndugu na dada wapendwa, mke mwema wa askofu angekuwa akishangaa ni kwa nini nabii alikuwa akimpigia simu. Ninashuhudia kuwa yeye na sisi hatuhitaji kushangaa tena---ALAMA YA MSHANGAO!

Najua ni lazima kila mmoja wetu akuze na kutekeleza mpango wetu mwenyewe wa kuhudumu na shauku pamoja na wamisionari---ALAMA YA MSHANGAO!

Naongeza ushuhuda wangu kwa ule wa Nabii Joseph Smith: “Na sasa, baada ya ushuhuda uliokwisha kutolewa juu yake, huu ni ushuhuda, wa mwisho wa zote, ambao ninatoa juu yake: Kwamba yu hai!” (M&M 76:22). Katika jina takatifu la Yesu Kristo, amina.