2010–2019
Usiwe na miungu mingine
Oktoba 2013


Usiwe na Miungu Mingine

Je, tunatumikia vipaumbele ama miungu zaidi ya Mungu tunayekiri kumwabudu?

Amri Kumi ni msingi wa imani ya Wakristo na Wayahudi. Zilitolewa na Mungu kwa wana wa Israeli kupitia nabii Musa, amri mbili za mwanzo zinaongoza kuabudu kwetu na vipaumbele vyetu. Amri ya kwanza, Bwana aliamuru, “Usiwe na miungu mingine zaidi yangu” (Kutoka 20:3). Karne kadhaa baadaye, Yesu alipoulizwa, “Ni amri gani iliyokuu katika sheria?” Yeye alijibu, “Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa nafsi yako yote, na kwa akili zako zote” (Mathayo 22:36–37).

Amri ya pili kati ya Amri Kumi inaelezea mwelekeo wakutokuwa na miungu mingine na inaonyesha nini kiwe kipaumbele muhimu katika maisha yetu kama watoto wa Mungu. “Usijifanyie sanamu ya kuchonga na ukaiabudu, au chochote kifananacho” iwe mbinguni au duniani (Kutoka 20:4). Amri kisha inaongeza, “Usizisujudie sanamu wala kuzitumikia” (Kutoka 20:5). Zaidi ya kuzipinga sanamu za kimwili, hii inaelezea kipaumbele cha msingi kwa muda wote. Yehova alielezea, “Kwani Mimi Bwana Mungu wako ni Mungu wa mwenye wivu, … nikionyesha huruma kwa … wao wenye kunipenda, na kuzitii amri zangu” (Kutoka 20:5–6). Maana ya wivu inafichuliwa. Ina asili ya Kiebrania ikimaanisha, “kuwa na hisia milikishi na kali” (Kutoka 20:5, tanbihi b). Basi tunamchukiza Mungu pale tunapo “tumikia miungu mingine—tunapokuwa na vipaumbele vingine.1

I.

Ni “vipaumbele vingine” vipi vinavyotumikiwa” mbele ya Mungu na watu---hata watu wa dini—katika siku zetu? Fikiria uwezekano huu, ya kawaida yote katika ulimwengu wetu:

  • Utamaduni na mila za familia

  • Usahihi wa Kisiasa

  • Matumainio ya kazi

  • Mali

  • Shughuli za burudani

  • Mamlaka, umaarufu, na ufahari

Kama hakuna hata moja ya mifano hii inayohusika kwa yeyote kati yetu, pengine tunaweza kupendekeza mingine yanaoweza. Kanuni ni muhimu kuliko mifano binafsi. Cha msingi si kama tuna vipaumbele vingine. Swali lililotolewa na amri ya pili ni “Ni nini kipaumbele chetu muhimu ?” Tunavitumikia vipaumbele au miungu zaidi ya Mungu tunayepaswa kumuabudu? Je, tumemsahau kumfuata Mwokozi aliyefundisha kwamba kama tunampenda Yeye, tutazitii amri zake? (ona Yohana 14:15). Kama hivyo ndivyo, vipaumbele vyetu vimegeuzwa juu chini kwa sababu ya haki kukosa maslahi na tabia mbaya inayojulikana katika siku zetu.

II.

Kwa Watakatifu wa Siku za Mwisho, amri za Mungu hazitofautishwi na mpango wa Mungu kwa ajili ya watoto Wake----mpango mkuu wa wokovu. Mpango huu, wakati mwingine unaitwa mpango mkuu wa furaha” (Alma 42:8),, unaelezea asili yetu na kudura yetu kama watoto wa Mungu---tumetoka wapi, kwa nini tupo hapa, na tunakwenda wapi. Unaelezea malengo ya uumbaji na hali ya mwili usiokamili na familia ya milele. Kama sisi Watakatifu wa Siku za Mwisho, ambao tumepewa elimu hii, hatuleti vipaumbele vyetu katika huu mpango, kwani tutakuwa kwenye hatari ya kuwatumikia miungu mingine.

Maarifa ya mpango wa Mungu kwa watoto Wake unawapa Watakatifu wa Siku za Mwisho mtazamo mema katika ndoa na familia. Tunajulikana vizuri kama kanisa linalojali familia. Elimu yetu ya dini inaanzia kwa wazazi wetu wa mbinguni, na matamanio yetu makubwa ni kupata utukufu wa milele, ambao tunajua inawezekana kupitia uhusiano wa kifamilia. Tunajua kwamba ndoa ya mume na mke ni muhimu kwa ajili ya kuukamilisha mpango wa Mungu. Ni ndoa hii pekee ndiyo itakayoleta uhakiki wa mwili wa kufa na kuwaandaa wana familia kwa ajili ya uzima wa milele. Tunafikiria ndoa na uzazi na kuwatunza watoto kama sehemu ya mpango wa Mungu na kazi takatifu ya wale waliopewa fursa ya kushiriki. Tunaamini kwamba hazina kubwa hapa duniani na mbinugni ni watoto wetu na vizazi vyetu.

III.

Kwa sababu ya kile tunachokielewa kuhusu majukumu wa milele ya familia, tunahuzunika kwa kupungua kwa idadi ya kuzaliwa watoto na ndoa katika jamii nyingi za nchi za Magharibi ambao tamaduni zao ni za Kikristo na kiyahudi. Nyenzo zinazohusika zinaripoti hivi:

  • Marekani sasa ina idadi ndogo sana ya vizazi katika historia,2 na katika mataifa mengi ya Umoja wa Ulaya na nchi nyingine zilizoendelea idadi ya vizazi imepungua hata kuhitaji kuendelea kudumumisha idadi ya watu3 ifaayo katika nchi zao. Hii inatishia maisha ya tamaduni na hata wa mataifa.

  • Katika Marekani, asilimia ya vijana wenye umri kati ya miaka 18 na 29 ambao wameoa imepungua toka asilimia 59 katika mwaka wa 1960 hadi asilimia 20 kufikia mwaka 2010.4. Umri wa wastani kwa ndoa ya mara ya kwanza kwa sasa imeongezeka katika historia: 26 kwa wanawake na karibu 29 kwa wanaume.5.

  • Katika nchi na tamaduni(1) nyingi familia ya kawaida ya mke na mume waliooana na watoto inakuwa siyo ya lazima wala sheria, (2) kuhangaikia ajira badala ya ndoa na kuwa na watoto limekuwa jambo lisilo la lazima kwa wasichana wengi na (3) nafasi na umuhimu wa baba unadidimia.

Katikati ya mwelekeo huu unaotusumbua, tunatambua kwamba pia mpango wa Mungu ni kwa ajili ya watoto wake wote na kwamba Mungu anawapenda watoto wake wote, kila mahali.6 Sura ya kwanza ya Kitabu cha Mormoni inaelezea kwamba nguvu za Mungu, na wema yake, na neema ziko juu ya wakazi wote wa dunia”(1 Nefi 1:14)14). Sura ya baadaye inaeleza kwamba “ametoa [wokovu] bure kwa wanadamu wote: na kwamba “wote wana haki sawa, na hakuna yeyote anayekatazwa”(2 Nefi 26:27–28). Hivyo, maandiko yanatufundisha kwamba tunawajibika kuwa wenye huruma na hisani (kupenda) kwa watu wote (ona 1 Wathesalonike 3:12; 1 Yohana 3:17; M&M 121:45).

IV.

Pia tunaheshimu imani za dini za watu wote, hata idadi kubwa ya wale wasiokuwa na imani katika Mungu. Tunajua kwamba kwa kupitia uwezo wa kuchagua tuliopewa na Mungu, wengi watakuwa na imani tofauti na yetu, lakini tunategemea kwamba na wengine nao wataheshimu imani ya dini yetu na kuelewa kwamba imani yetu inatufanya kufanya maamuzi tofauti na kuwa na tabia tofauti na yao. Kwa mfano, tunaamini kwamba, kama sehemu muhimu ya mpango Wake wa wokovu, Mungu ameweka viwango vya milele kwamba mahusiano ya kindoa lazima yawe kati mwanamume na mwanamke waliooana.

Uwezo wa kuumba maisha ni uwezo wa kutukuka ambao Mungu amewapa watoto Wake. Matumizi yake yaliamriwa na amri ya kwanza ya Mungu kwa Adamu na Hawa (ona Mwanzo 1:28), lakini amri nyingine muhimu zilitolewa ili kukataza matumizi mabaya yake (ona Kutoka 20:14; 1 Wathesalonike 4:3). Mkazo tunaouweka katika sheria ya usafi hii imeelezewa kwa uelewa wetu wa umuhimu wa mamlaka ya uumbaji katika kukamilisha mpango wa Mungu. Nje ya uhusiano wa ndoa kati ya mwanamume na mwanamke, matumizi yoyote ya uwezo huu ni dhambi na ni kinyume na mpango wa Mungu kwa ajili ya utukufu wa watoto Wake.

Umuhimu tunaouambatanishana na sheria ya usafi wa mwili hii inaelezea ahadi yetu katika muundo wa ndoa ambayo ilianzia kwa Adam na Hawa na imeendelea kwa miaka mingi kama muundo wa Mungu kwa ajili ya uhusiano wa uumbaji kati ya wana na mabinti Zake na kwa ajili ya kuwastawishi watoto Wake. Kwa bahati nzuri, watu wengi wenye uhusiano na madhehebu mengine au vikundi vingine wanakubaliana na sisi juu ya umuhimu wa ndoa, wengine katika misingi ya dini na wengine katika misingi inayooneka mizuri kwa jamii.

Elimu yetu ya mpango wa Mungu kwa ajili ya watoto Wake7 inaelezea kwa nini tunashida ya kuongezeka kwa watoto wanaozaliwa nje ya ndoa---kwa sasa ni asilimia 41 ya uzazi wote Marekani8—na kwamba idadi ya watu wanaoishi pamoja bila ya ndoa imeongezeka sana katika nusu karne iliyopita. Miongo mitano iliyopita, kulikuwa na asilimia ndogo sana ya wanaume na wanawake walioishi pamoja bila kufunga ndoa. Sasa, kundi hili limefikia asilimia 60 ya wasiofunga ndoa.9 Na ongezeko hili linakubabika, hususani miongoni mwa vijana. Utafiti wa hivi karibuni umegundua asilimia 50 ya vijana wanaeleza kwamba kuto-kuoa na kuzaa watoto ni maisha ya kustahili kwao.”10

V.

Kuna misukumo mingi ya kisiasa na kijamii kwa ajili ya kupitisha sheria na mabadiliko ya sera ambayo yanakinzana na sheria za Mungu kuhusu usafi wa mwili na kinyume na asili ya milele na dhumuni la ndoa na kuzaa watoto. Misukumo hii tayari imeidhinisha ndoa ya jinsia moja katika majimbo na mataifa mengi. Misukumo mingine itachanganya jinsia au kubadilisha zile tofauti kati ya wanaume na wanawake ambayo ni muhimu kutimiza mpango mwema na wa furaha wa Mungu.

Kuelewa kwetu juu ya mpango wa Mungu na mafundisho yake kunatupa matarajio ya milele ambayo hayaturuhusu kuwa na tabia kama hizo au kutafuta haki katika sheria zinazoruhusu hivyo. Na, tofauti na makundi mengine ambayo yanaweza kubadilisha sheria zao na hata mafundisho yao, sheria zetu zinategemea kweli za Mungu zinazotambuliwa kwamaba hazibadiliki.

Makala ya imani ya kumi na mbili yetu inaelezea kuamini kwetu katika kuwatii viongozi wa serikali katika kutii na kuheshimu amri za nchi. Lakini sheria za mwanadamu haziwezi kuweka maadili ya kile Mungu alichokiona hakifai. Dhamira ya kipaumbele chetu---ni kumpenda na kumtumikia Mungu inahitajika kwamba tutegemee sheria Zake kwa tabia zetu. Kwa mfano, tunabaki chini ya amri ya Mungu ya kutofanya uzinzi au uasherati hata kama matendo hayo yamehalalishwa chini ya sheria ya jimbo ama nchi tunazoishi. Vile vile, sheria zinazohalalisha ndoa inayoitwa “ndoa ya jinsia moja.” hazibadilishi sheria ya Mungu ya ndoa ama amri Zake na viwango vyetu kuihusu. Tunabaki chini ya agano kumpenda Mungu na kutii amri Zake na kujiepusha na kutumikia miungu mingine na vipaumbele---hata yale yanakuwa maarufu katika nyakati na sehemu zetu hasa.

Katika jitihada hii tunaweza tusieleweke na wengine, na huenda tukapata shutuma za ulokole, kuteseka kutokana na kutengwa, au kubidi kukumbana na uvamizi wa uhuru wa kidini. Kama ni hivyo, ninafikiria lazima tukumbuke kipaumbele chetu cha kwanza---na kama waanzilishi wetu waliotutangulia, tusukume mikokoteni yetu ya kibinafsi kwa ushupavu ule ule walioonyesha.

Mafundisho ya Rais Thomas  S. Monson, yanatumika katika hali hii. Katika mkutano kuu kama huu miaka 27 iliyopita, kwa ujasiri alisema: “Acheni tuwe na ujasiri dhidi ya chaguzi zijulikanazo, ujasiri wa kusimama kwenye kanuni. Ujasiri, siyo mapatano, huleta tabasamu ya idhinisho la Mungu. Ujasiri unakuwa ni tabia iliyohai na ya kuvutia pale inapoonekana kama kukubali kufa na heshima, lakini kama uamuzi wa kuishi vizuri. Mtenda maovu ni yule anayeogopa kutenda kile anachokiona ni chema eti kwa sababu wengine hawatakubali au watamcheka. Kumbuka kwamba watu wote wana woga wao, lakini wale wanaokabiliana woga wao kwa haki nao wana ijasiri pia. .”11

Ninaomba kwamba hatutaacha changamoto za muda za kimwili zitusababishie sisi kusahau amri kuu na vipaumbele tulivyopewa na Muumba wetu na Mwokozi wetu. Tusiiweke sana mioyo yetu katika mambo ya kidunia na kutamani kuheshimika na watu (ona M&M 121:35) na tukaacha kujaribu kupata kudra yetu ya milele. Sisi tunaojua mpango wa Mungu kwa watoto Wake---sisi tulioweka maagano ili kushiriki kwazo-– tuna majukumu ya wazi. Hatustahili kamwe kuondoka kutoka kwa hamu yetu kuu, ambayo ni kupata uzima wa milele.12 Kamwe sharti tusizimue kipaumbele cha kwanza---cha kutokuwa na miungu mingine na kutokuwa na kipaumbele kingine zaidi ya Mungu Baba na Mwana Wake, Mwokozi wetu, Yesu Kristo.

Mungu atusaidie kuelewa hiki kipaumbele na tueleweke na wengine tunapojaribu kusonga mbele kwa busara na njia ya upendo, ninaomba katika jina la Yesu Kristo, amina.

Muhtasari

  1. Ona, kwa mfano, Mafundisho na Maagano 124:84.

  2. Ona Joyce A. Martin and others, “Births: Final Data for 2011,” National Vital Statistics Reports, vol. 62, no. 1 (June 28, 2013), 4; Gloria Goodale, “Behind a Looming Baby Bust,” Christian Science Monitor Weekly, Feb. 4, 2013, 21, 23.

  3. Ona Population Reference Bureau, “2012 World Population Data Sheet,” www.prb.org/Publications/Datasheets/2012/world-population-data-sheet/data-sheet.aspx.

  4. Ona D’Vera Cohn and others, “Barely Half of U.S. Adults Are Married—a Record Low,” Pew Research Center, Social and Demographic Trends, Dec. 14, 2011, available at www.pewsocialtrends.org/2011/12/14/barely-half-of-u-s-adults-are-married-a-record-low; “Rash Retreat from Marriage,” Christian Science Monitor, Jan. 2 and 9, 2012, 34.

  5. U.S. Census Bureau, “Estimated Median Age at First Marriage, by Sex: 1890 to the Present,” available at www.census.gov/population/socdemo/hh-fam/ms2.xls.

  6. Ona Dallin H. Oaks, “All Men Everywhere,” Ensign au Liahona, May 2006, 77–80.

  7. Ona Dallin H. Oaks, “The Great Plan of Happiness,” Ensign, Nov. 1993, 72–75.

  8. Ona Martin, “Births: Final Data for 2011,” 4.

  9. Ona The State of Our Unions: Marriage in America,2012 (2012), 76.

  10. Ona The State of Our Unions, 101, 102.

  11. Thomas S. Monson, “Courage Counts,” Ensign, Nov. 1986, 41.

  12. Ona Dallin H. Oaks, “Desire,” Ensign au Liahona, May 2011, 42–45.