2010–2019
Nguvu za Kibinafsi kupitia Upatanisho wa Yesu Kristo
Oktoba 2013


Nguvu za Kibinafsi kupitia Upatanisho wa Yesu Kristo.

Kupitia Upatanisho wa Yesu Kristo, kila mmoja wetu anaweza kuwa msafi na mzigo wetu wa uasi kuondolewa.

Hivi majuzi, nilibarikiwa kukutanana kikundi cha kuvutia sana kutoka jimbo la Idaho. Msichana mmoja mwadilifu aliniuliza ninachohisi kuwa ni kitu cha muhimu sana wanachotakiwa kufanya katika maisha yao wakati huu. Nilipendekeza wajifunze kutambua nguvu ya Upatanisho wa Yesu Kristo katika maisha yao. Leo ninafafanua wazi kipengele kimoja cha nguvu ile, ambacho ni nguvu ya kibinafsi tunazoweza kupokea kupitia Upatanisho wa Yesu Kristo.

Katika Kitabu cha Mormoni tunasoma kuhusu Amonina na nduguze wakifundisha injili ya Yesu Kristo kwa watu ambao walikuwa “wakorofi na wagumu na wakatili.”1 Watu wengi waliongolewa na walichagua kuacha tabia zao za dhambi. Kuongolewa kwao kulikuwa kikamilifu hivi kwamba walizika silaha zao na wakafanya maagano na Mungu kwamba hawatazitumia tena.2

Baadaye,wengi wa ndugu zao ambao hawakuongolewa waliwajia na wakaanza kuwauwa. Na sasa watu waaminifu walichagua kuangamia kwa upanga kuliko kuhatarisha maisha yao ya kiroho kwa kuchukua silaha. Mfano wao wa haki uliwasaidia watu zaidi kuongolewa na kuweka chini silaha zao za uasi.3

Kupitia kwa Amoni, Bwana aliwaongoza kuwa wakimbizi miongoni mwa Wanefi, na walikuja kujulikana kama watu wa Amoni.4 Wanefi waliwalinda kwa miaka mingi, lakini hatimaye jeshi la Wanefi lilianza kupungua nguvu, na wanajeshi zaidi walihitajika haraka.5

Watu wa Amoni walikuwa kwenye wakati mgumu wa maisha yao ya kiroho.Walikuwa wamekuwa wakweli kwa maagano yao ya kutochukua silaha tena. Lakini walijua kwamba kina baba wanajukumu la kutoa ulinzi kwa familia zao.6 Haja hili ilionekana kubwa ya kutosha kustahili kufikiria kuvunja agano lao.7

Kiongozi wao wa ukuhani mwenye busara, Helamani, alijua kwamba kuvunja agano na Bwana si halali. Alitoa mwongozo mwingine. Aliwakumbusha kwamba vijana wao hawakuwa na kosa la dhambi zilezile na kwa hiyo hawakuwa na haja ya kufanya agano hilo hilo.8 Ingawa vijana walikuwa wadogo sana,walikuwa wenye nguvu kimwili na muhimu zaidi walikuwa waadilifu na wakamilifu.Vijana walikuwa wameimarishwa na imani ya mama zao.9 Chini ya maelekezo ya nabii---kiongozi wao, vijana hawa walichukua nafasi za baba zao kwenye ulinzi wa familia zao na makazi yao.10

Matukio yaliyokuwepo wakati huu wa maamuzi muhimu yalionyesha jinsi Upatanisho wa Yesu Kristo unaleta nguvu za kibinafsi kwa maisha ya watoto wa Mungu. Fikiria hisia ororo za baba zao. Jinsi gani waliweza kuhisi walipojua kwamba vitendo vyao vya uasi vilivyopita viliwazuia kulinda wake zao na watoto wakati walipohitajika.Wakijua binafsi uovu ambao watoto wao sasa wanakabiliana nao ni lazima walilia kwa siri. Kina baba, sio watoto, wanatakiwa kulinda familia zao! 11 Huzuni yao lazima ilikuwa nzito.

Kwa nini kiongozi wao wa ukuhani mwenye fikira elekezi aogope fikira zao za kutwaa silaha zao, “Kwa kuogopa—watapoteza roho zao”?12 Bwana ametangaza, “Tazama, yule ambaye ametubu dhambi zake, huyu anasamehewa, na Mimi, Bwana, sizikumbuki tena.”13 ‎Hawa kina baba waaminifu wametubu dhambi zao muda mrefu na wamekuwa wasafi kupitia Upatanisho wa Yesu Kristo, kwa hiyo kwa nini walishauriwa wasilinde familia zao?

Ni ukweli wa kimsingi kwamba kupitia kwa Upatanisho wa Yesu Kristo, tunaweza kusafishwa. Tunaweza kuwa wasafi na wakamilifu. Hata hivyo,wakati mwingine chaguo zetu zisizo na maana zinatuacha na matokeo ya muda mrefu. Mojawapo wa hatua muhimu kukamilisha toba ni kuchukua matokeo ya muda mfupi na mrefu wa dhambi zetu zilizopita. Chaguoi zao zilizopita zimefunua hawa akina baba wa Kiamoni kwa tamaa za kimwili ambazo tena zinaweza kuwa sehemu zinazoweza kudhuriwa na kwamba Shetani angeweza kujaribu kuzitumia.

Shetani atajaribu kutumia mawazo yetu ya hatia zilizopita kutuvutia turudi katika himaya yake. Lazima tuwe waangalifu kuepuka vishawishi vyake. Hicho ndicho kilichokuwa kisa cha akina baba waaminifu wa Kiamoni. Hata baada ya miaka yao mingi ya maisha ya uamnifu, ilikuwa ni muhimu kwao kujilinda wenyewe kiroho kutoka mvuto wowote kwa mawazo ya dhambi zilizopita.

Kati ya vita vingi, Kapteni Moroni alielekeza kuimarishwa kwa miji isiyo na nguvu. “Alisababisha kwamba itabidi wajenge ulingo wa mbao ndani ya handaki;na waliutupa nje uchafu uliokuwa ndani ya shimo mkabala na ulingo wa mbao… mpaka walipouzunguka mji na ukuta imara wa mbao na udongo, kwa urefu mkubwa.”14. Kapteni Moroni alielewa umuhimu wa kuimarisha sehemu legevu na kuujenga imara.15

Hawa akina baba wa Kiamoni walikuwa karibu sawa.Walihitaji ngome ndefu na pana katikati ya maisha yao ya uaminifu na tabia isiyo ya haki ya maisha yao yaliyopita.Waliweza kulinda familia zao kwa uaminifu bila kuhatarisha siha yao ya kiroho.

Habari za kufurahisha kwa yeyote anayetamani kuondolewa matokeo ya chaguo hafifu za zamani ni kwamba Bwana anaona udhaifu kitofauti na aonavyo uasi.Na Bwana anapoonya kwamba uasi usio na toba utaleta adhabu,16 wakati Bwana anapozungumzia udhaifu, ni wakati wote kwa rehema.17

Bila wasiwasi, kuna baadhi ya ruhusa ambazo Akina baba wa Kiamoni walifundishwa mila za uongo za wazazi wao, lakini watoto wote wa Baba huko mbinguni huja kwenye maisha ya duniani na Nuru ya Kristo. Bila kujali matendo yao ya dhambi, matokeo yalikuwa ukuaji hatari kwamba Shetani atajaribu kutumia.

Kwa rehema walifunzwa injili,wakatubu,na kupitia Upatanisho wa Yesu Kristo kwa sababu kiroho una nguvu zaidi ya vishawishi vya Shetani. Inawezekana hawakuhisi majaribu ya kurudi kwenye ukatili wao wa zamani, hata hivyo kwa kumfuata nabii---kiongozi wao, hawakumpa Shetani nafasi ya “[kudanganya] roho zao,na [kuwaongoza] mbali kwa uangalifu chini kwenye jehanum.”18 Upatanisho wa Mwokozi sio tuu uliwasafisha kutoka kwenye dhambi, lakini kwa sababu ya utiifu wao kwa ushauri wa kiongozi wao wa ukuhani,mwokozi aliweza kuwalinda kutoka kwenye unyonge wao na kuwaimarisha.Unyenyekevu wao,uamuzi wa maisha kuacha dhambi zaoilifanya zaidi kulinda familia zao kuliko chochote wangeweza kufanya kwenye uwanja wa vita.Kukubali kwao hakukuwanyima Baraka. Kuliwaimarisha na kuwabariki wao na kubariki vizazi vya baadaye.

Mwisho wa hadithi unapamba jinsi rehema ya Bwana inafanya “vitu dhaifu vinakuwa vyenye nguvu.”19 Wale akina Baba waaminifu waliwatuma vijana wao chini ya uangalizi wa Helamani. Ingawa vijana walipigana vita vikali ambako karibu wote walipata majeraha kiasi, hakuna hata mmoja aliyepoteza maisha.20 Wavulana walithibitisha kuwa ni muhimu kuongeza nguvu jeshi lililochoka.Walikuwa waaminifu na wenye nguvu zaidi kiroho waliporudi nyumbani. Familia zao zilibarikiwa, zililindwa, na kuimarishwa.21 Katika siku yetu, wanafunzi wasio hesabika wa Kitabu cha Mormoni wameelimika zaidi kwa mfano wa hawa wana halisi na wenye haki.

Kila mmoja wetu tumekuwa na muda katika maisha yetu ambapo tumefanya maamuzi yasiyo na maana. Sisi sote tupo katika hekaheka ya kutaka nguvu ya wokovu ya Upatanisho wa Yesu Kristo. Kila mmoja wetu lazima tutubu kila aina ya uasi. “Kwani Mimi Bwana siwezi kuiangalia dhambi na kuivumilia hata kidogo.”22 Hawezi kwa sababu anajua nini kinatakiwa kuwa kama Yeye.

Wengi wetu tumeruhusu unyonge kujengeka katika tabia zetu. Kupitia kwa Upatanisho wa Yesu Kristo, sisi, kama Waamoni, tunaweza kujenga ngome za kiroho kati yetu na makosa yeyote yaliyopita ambayo Shetani anajaribu kuyatumia. Ulinzi wa kiroho uliojengwa kuwazunguka kina Baba wa Kiamoni walibarikiwa na kuimarishwa wenyewe, familia zao, nchi yao, na vizazi vijavyo. Hali kama hii inaweza kuwa kweli kwetu sisi.

Sasa tunawezaje kujenga ngome hizi za milele? Hatua ya kwanza ni lazima tuwe wakweli, tulioimarika na tuliotubu kikamilifu. Kupitia Upatanisho wa Yesu Kristo, kila mmoja wetu anaweza kuwa msafi na mzigo wa uasi wetu utaondolewa. Kumbuka, toba siyo adhabu. Ni njia iliyojaa matumaini kwenda kwenye utukufu mkubwa baadaye.

Baba aliye Mbinguni ametupatia vifaa ambavyo vinasaidia kujenga ngome kati ya kuweza kwetu kudhurika na uaminifu wetu. Fikiria mapendekezo yafuatayo:

  • Fanya maagano na hupokea maagizo kwa ajili kwako mwenyewe. Kisha kwa uangalifu na bila mabadiliko fanya kazi ya kutoa ibada hekaluni kwa ajili ya wahenga wako.

  • Shiriki injili pamoja na wasio washiriki au wanafamilia wasio shiriki kikamilifu au marafiki. Kushiriki kweli hizi kunaweza kuleta upya wa furaha maishani mwako.

  • Hudumu kwa uaminifu katika wito wote wa Kanisa, hasa mipango ya ualimu wa nyumbani na mwalimu mtembelezi. Usiwe tu mwalimu wa nyumbani au mtembelezi wa dakika 15---kwa mwezi. Bali, wafikie kila mwanafamilia kipekee. Uwajue kibinafsi. Uwe rafiki wa kweli. Kupitia kwa vitendo vyako vya huruma, waoneshe jinsi unavyowajali kila mmoja wao.

  • Cha muhimu,wahudumie wanafamilia yako mwenyewe. Fanya maendeleo ya kiroho kwa mchumba wako na watoto kuwa kipaumbele cha juu. Uwe msikivu kwa vitu unavyoweza kufanya kusaidia kila mmoja wao. Toa kwa uhuru muda wako na usikivu.

Katika kila moja ya mapendekezo haya, kuna msimamo wa sawia, jaza maisha yako na huduma kwa wengine. Na unapopoteza maisha yako katika huduma ya watoto wa Baba wa Mbinguni,23 majaribu ya Shetani yanapoteza nguvu katika maisha yako.

Kwa sababu Baba yako aliye mbinguni anakupenda sana, Upatanisho wa Yesu Kristo unafanya nguvu ile kuwezekana. Je, haya sio maajabu? Wengi kati yenu mmeuona mzigo wa chaguo zisisizo faa, na kila mmoja wenu anaweza kuona mwongezeko wa Msamaha wa Bwana, rehema, na nguvu. Mimi nimeihisi, na nina shuhudia kwamba inapatikana kwa kila mmoja wenu, katika jina la Yesu Kristo, amina.