2010–2019
Nguvu katika Ukuhani
Oktoba 2013


Nguvu katika Ukuhani

Mtu anaweza kufungua pazia ili mwanga mtamu uweze kuingia chumbani, lakini mtu yule hamiliki jua ama mwanga wala joto litokanalo na jua.

Baraka za Ukuhani ni kwa Wote

Watoto wanapoimba kwenye mkutano wa sakramenti kwa furaha wimbo wa Msingi “Upendo Unasemwa Hapa,” kila mtu alitabasamu kwa kuwakubali. Mama jasiri aliyekuwa anawalea watoto watano alikuwa akisikiliza kwa makini ubeti wa pili: “Familia yangu mara zote imekuwa ikibarikiwa kwa kuwa na [nguvu] za ukuhani nyumbani].”1 Kwa masikitiko alifikiria, “Watoto wangu kamwe hawajawai jua nyumba kama hiyo.”2

Ujumbe wangu kwa mama huyu mwaminifu na kila mtu ni kwamba tunaweza kuishi kila wakati “tukibarikiwa kwa nguvu za ukuhani,” licha ya hali zetu.

Wakati mwingine sisi hushiriki sana nguvu ya ukuhani na wanaume Kanisani. Ukuhani ni nguvu na mamlaka ya Mungu yaliyotolewa kwa ajili ya wokovu na baraka kwa wote---waume, wake, na watoto.

Mtu anaweza kufungua pazia ili mwanga mtamu uweze kuingia chumbani, lakini mtu yule hamiliki jua ama mwanga wala joto litokanalo na jua. Baraka za ukuhani ni kubwa kuliko mtu yule anayeulizwa kuhudumia hicho kipawa.

Ili kupokea baraka, uwezo, na ahadi za ukuhani katika maisha haya na yajayo ni moja ya fursa kubwa na majukumu ya maisha haya ya duniani. Tunapostahili, ibada za ukuhani zinarutubisha maisha yetu hapa duniani na kutuandaa kwa ajili ya maisha yajayo. Bwana alisema, “Katika ibada---uwezo wa uungu hutambulika.”3

Kuna baraka maalum zitokazo kwa Mungu kwa ajili ya kila mtu anayestahili anayebatizwa, anapokea Roho Mtakatifu, na kula sakramenti kila mara. Hekalu huleta mwanga wa ziada na nguvu, pamoja na ahadi ya uzima wa milele.4

Ibada zote zinatualika sisi kuongeza imani yetu katika Yesu Kristo na kufanya na kuwekaa maagano na Mungu. Tunapoyaweka haya maagano matakatifu, tunapokea nguvu na baraka za ukuhani.

Je, hatuzihisi nguvu hizi za ukuhani katika maisha yetu na kuziona miongoni mwa washiriki wa Kanisa wanaoweka maagano? Tunaziona kwa washiriki wapya pale wanapotoka kwenye maji ya ubatizo wakijiona wamesamehewa na kuwa safi. Tunawaona watoto na vijana wetu wakiwa makini katika ushawishi na uongozi wa Roho Mtakatifu. Tunaona ibada za hekalu zikiwa chanzo cha nguvu na mwanga kwa ajili ya wanaume na wanawake wema ulimwenguni kote.

Mwezi uliopita niliwaona wanandoa vijana wakipata nguvu nyingi toka kwa ahadi za kuunganishwa hekaluni wakati mtoto wao wa kiume alipozaliwa lakini akaishi wiki moja tu. Kupitia ibada za ukuhani, tunapata faraja, nguvu, ulinzi, amani, na ahadi za milele.5

Ni nini Tunachojua kuhusu Ukuhani

Wengine wanaweza kuuliza swali la dhati, “Kama uwezo na baraka za ukuhani zinapatikana kwa wote, kwa nini ibada za ukuhani zinatolewa na wanaume?

Wakati malaika alipomwuliza Nefi, “Hujui uradhi wa Mungu?” Nefi alijibu kwa ukweli, “Ninajua kwamba anawapenda watoto wake, hata hivyo, mimi sijui maana ya vitu vyote.”6

Tunapozungumzia ukuhani, kuna mambo mengi tunayoyajua.

Sisi Sote Tuko Sawa

Tunajua kwamba Mungu anawapenda watoto Wake wote na hana mapendeleo kwa watu. “Hamkatai yeyote anayekuja kwake… . mwanamume [au] mwanamke; ….na wote ni sawa mbele za Mungu.”7

Kama tunajua kwamba upendo wa Mungu ni sawa kwa wana na mabinti Zake, pia tunajua kwamba hakuwaumba wanaume na wanawake sawa. Tunajua kwamba jinsia ni sifa muhimu kwa maisha haya na utambulisho wa milele na malengo. Majukumu matakatifu yanapewa kila jinsia.8

Kutoka Mwanzoni

Tunajua kwamba kutoka mwanzoni Bwana alipanga jinsi ukuhani wake utakavyosimamiwa. “Ukuhani kwanza ulitolewa kwa Adamu.”9 Nuhu, Ibrahimu, na Musa wote walisimamia ibada za ukuhani. Yesu Kristo alikuwa na ni Kuhani Mkuu. Aliwaita Mitume. “Ninyi hamkunichagua mimi, Alisema, bali nimewachagua Mimi, na kuwatawaza ninyi.”10 Katika siku zetu, Yohana Mbatizaji, Petro, Yakobo, na Yohana walirejesha ukuhani hapa duniani kupitia Nabii Joseph Smith.11 Hii ndiyo njia ambayo Baba wa Mbinguni anavyosimamia ukuhani Wake.12

Vipawa Vingi kutoka kwa Mungu

Tunajua kuwa nguvu ya ukuhani mtukufu hazifanyi kazi bila ya imani, Roho Mtakatifu, na karama za kiroho. Maandiko yanaonya: “Usikatae karama za Mungu, kwani zipo nyingi, ... Na kuna njia nyingi ambazo karama hizi zinatumika; lakini ni Mungu yule yule anayewezesha zifanye kazi.”13

Ustahiki

Tunajua kwamba ustahiki ni chanzo cha kutenda na kupokea ibada za ukuhani. Dada Linda K. Burton, alisema, “Haki inahitajika …. ili kuzialika nguvu za ukuhani katika maisha yetu.”14

Kwa mfano, zingatia pigo la ponografia linavyo enea kwa kasi ulimwenguni kote. Kiwango cha Bwana cha haki hakitoi nafasi kwa ponografia miongoni mwa wale wanaotumikia ibada za ukuhani. Bwana alisema:

“Mtubu kutoka matendo yenu ... makundi yenu ya machukizo na ya siri.”15

“Taa ya mwili ni jicho. … Lakini jicho lako likiwa bovu, mwili wako wote utakuwa na giza..”16

“[Kwani] kila mtu atazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake.”17

Kuhudumu bila kustahiki au kupitisha sakramenti, kuwaombea wagonjwa, au kushiriki katika ibada nyingine za ukuhani, kama vile Mzee David  A. Bednar amesema, ni kulitaja bure jina la Mungu.18Kama mtu hastahili, lazima ajiondoe kwenye utumishi wa ibada za ukuhani na kwa maombi aende kwa askofu wake kama hatua ya kwanza ya kutubu na kuzirudia amri.

Unyenyekevu

Kitu kingine tunachojua ni kwamba baraka za ukuhani ni nyingi katika familia ambazo mama na baba wema wameungana katika kuwaongoza watoto. Lakini pia tunajua kwamba Mungu hutoa baraka za zizi hizi kwa wale walio kwenye hali nyingi nyingine.19

Mama, akiwa amebeba mzigo wa kuitumikia familia yake kiroho na kimwili, kwa umakini alieleza kwamba kuwasiliana na walimu wa nyumbani kuja kumbariki mmoja wa mtoto wake kunahitaji unyenyekevu wake. Lakini aliongeza kwa maarifa kwamba hakuhitaji kuwa na unyenyekevu zaidi ya ule wa walimu wa nyumbani pale walipokuwa wakijiandaa kumbariki mtoto wake.20

Funguo za Ukuhani

Tunajua kuwa funguo za ukuhani, walizonazo washiriki wa Urais wa Kwanza na Jamii ya Mitume Kumi na Wawili, zinaongoza kazi ya Bwana duniani. Funguo maalum hupewa marais wa vigingi na maaskofu kwa ajili ya majukumu ya maeneo yao. Wao huita wanaume na wanawake kwa ufunuo ambao huidhinishwa na kutengwa ili kuyatumia mamlaka hayo katika kufundisha na kutumikia.21

Huku tukijua mengi juu ya ukuhani, kuuona kupitia lensi ya mwili huu mara nyingi hakuwezi kutoa ufahamu wa kutosha jinsi Mungu anavyofanya kazi.  Lakini anatukumbuka kwa upole, “Maana mawazo yangu si mawazo yenu, wala njia zenu si njia zangu; asema Bwana.,”22 inatuhakikishia kwamba na mtazamo wa milele tutaona vitu “vile vitu vilivyo” ”23 na kuelewa upendo Wake mkamilifu

Sisi sote hutumika kwa hiari. Wakati mwingine tunajihisi kutumika kidogo kwa wito wetu, na kutamani kuulizwa kufanya zaidi. Mara nyingine tunashukuru inapofikia wakati wa kuachiliwa kwetu. Hatuamui kwa wito tunaopokea.24 Nilijifunza somo hili mapema katika ndoa yangu. Kama wanandoa, mke wangu Kathy nami tulikuwa tunaiishi Florida. Jumapili moja msaidizi katika urais wa kigingi alinielezea kwamba walikuwa wameona vyema kumwita Kathy kuwa mwalimu wa seminari ya asubuhi mapema.

“Tutaifanyaje?” Niliuliza. “Tuna watoto wadogo, darasa la seminari linaanza saa 11:00 asubuhi, na mimi ni rais wa Wavulana wa kata.”

Yule mshauri alitabasamu na kusema, “Itakuwa sawa, Ndugu Andersen. Tutamwita, na tutakuachiliwa wewe.”

Na hivyo ndivyo ilivyofanyika.

Mchango wa Wanawake

Kuuliza kwa uaminifu na kusikiliza kwa dhati mawazo na matatizo yanayowakabili akina mama ni muhimu katika maisha, ndoa, na katika kuujenga ufalme wa Mungu.

Miaka ishirini iliyopita katika mkutano mkuu, Mzee  M. Russell Ballard alielezea maongezi aliyokuwa nayo na rais mkuu wa Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama. Kulikuwa na swali ambalo liliulizwa juu ya kuuimarisha ustahiki wa vijana wanaojianda kwenda kutumikia misheni. Dada Elaine Jack alisema kwa kutabasamu, “Unajua, Mzee Ballard, wanawake wa Kanisa wanaweza kuwa na mapendekezo mazuri … kama wakiulizwa. Zaidi ya yote, … sisini akina mama zao!”25

Rais Thomas  S. Monson ana historia ya miaka mingi ya kusikiliza matatizo ya wanawake. Mwanamke ambaye amemshawaishi zaidi ya wote ni Dada Frances Monson. Sote tunamkosa sana. Pia, hii Alihamisi iliyopita, Rais Monson pia hivi karibuni aliwakumbusha Viongozi wenye Mamlaka mengi aliyojifunza kama askofu kutoka kwa wajane 84 wa kata yake. Hakika waliushawishi utumishi wake na maisha yake yote.

Bila mshangao, kabla ya uamuzi wa maombi ya Rais Monson kuhusu mabadiliko ya umri wa kutumikia misheni, kulikuwa na mijadala mingi pamoja na urais Mkuu wa Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama, Wasichana, na Msingi.

Maaskofu, mnapofuata mfano wa Rais Monson, mtahisi kwa wingi kabisa mkono wa mwongozo wa Bwana ukibariki kazi zenu takatifu.

Tuliishi Brazil kwa miaka kadhaa. Mara tu baada ya kuwasili nilikutana na Adelson Parrella, aliyekuwa akihudumu kama mmoja wa Wale Sabiini, na kaka yake Adilson, aliyekuwa akihudumu katika urais wa kigingi. Baadaye nikakutana na kaka yao Adalton, akihudumu kama Rais wa kigingi huko Florianopolis na kaka mwingine Adelmo, akihudumu kama askofu. Nilifurahishwa sana na imani ya Ndugu hawa, na nikauliza kuhusu wazazi wao.

Familia ilibatizwa huko Santos, Brazil, miaka 42 iliyopita. Adelson Parrella alisema, “Mara ya kwanza baba alionekana kuwa na furaha kuhusu kujiunga na Kanisa. Hata hivyo, yeye [punde] hakuwa anahudhuria na kumwambia mama yetu naye asihudhurie kanisa.”

Adelson aliniambia kwamba mama yake alikuwa akishona nguo za majirani ili kulipa nauli ya basi ya watoto wake kwenda kanisani. Vijana hao wanne wadogo walitembea pamoja kwa zaidi ya maili moja kwenda mji mwingine, kupanda basi na kusafiri kwa dakika 45, na baadaye kutembea tena kwa dakika 20 kwenda kanisani.

Ijapokuwa hakuweza kwenda kanisani na watoto wake, Dada Parrella alisoma maandiko pamoja na vijana na mabinti zake, aliwafundisha injili, na aliomba pamoja nao. Nyumba yao yenye unyenyekevu ilijaa wingi wa baraka za nguvu ya ukuhani. Vijana wale wadogo walikua, wakahudumu misheni, wakasoma, na wakaoa hekaluni. Baraka za ukuhani zilijaza nyumbani mwao.

Miaka kadhaa baadaye, kama dada mjane, Vany de Parrella aliingia hekaluni kwa ajili ya endaumenti yake mwenyewe na, baadaye, alihudumu misheni tatu huko Brazil. Sasa ana miaka 84, imani yake inaendelea kuvibariki vizazi vilivyomfuata.

Ushuhuda na Ahadi

Nguvu ya ukuhani mtukufu wa Mungu inapatikana katika Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho. Nashuhudia kwamba mnaposhiriki kwa ustahiki katika ibada za ukuhani, Bwana atawapeeni nguvu kubwa, amani, na mtazamo wa milele. Bila kujali hali yako, nyumba yako itabarikiwa kwa nguvu za uwezo wa ukuhani na wale walio karibu yako nao watataka kikamilifu zaidi baraka hizi kwa ajili yao wenyewe.

Kama wanaume na wanawake, dada na kaka, vijana na mabinti wa Mungu, tunasonga mbele pamoja. Hii ndiyo fursa yetu, jukumu letu, na baraka zetu. Hii ndiyo hatima yetu--- kuuandaa ufalme wa Mungu kwa ajili ya kurudi kwa Mwokozi. Katika jina la Yesu Kristo, amina.

Muhtasari

  1. “Love Is Spoken Here,” Children’s Songbook, 190–91.

  2. Barua pepe ya kibinafsi, Aug. 5, 2013.

  3. Mafundisho na Maagano 84:20.

  4. Ona Mafundisho na Maagano 138:37, 51.

  5. Ona Mafundisho na Maagano 84:35; 109:22.

  6. 1 Nefi 11:16–17.

  7. 2 Nefi 26:33.

  8. Ona “Familia: Tangazo kwa Ulimwengu,” Ensign au Liahona, Nov. 2010, 129.

  9. Teachings of Presidents of the Church: Joseph Smith (2007), 104; ona pia Mafundisho na Maagano 84:16; 107:40–53; 128:18, 21; Russell M. Nelson, “Lessons from Eve,” Ensign, Nov. 1987, 86–89.

  10. Yohana 15:16.

  11. Ona Joseph Smith—History 1:72; ona pia Mafundisho na Maagano 13; 27.

  12. Ona M. Russell Ballard, “Let Us Think Straight,” BYU Campus Education Week devotional, Aug. 20, 2013); speeches.byu.edu. Mzee Ballard alisema: “Kwa nini wanaume hutakaswa kwa ofisi za ukuhani na si wanawake? Rais Gordon  B. Hinckley alieleza kwamba ilikuwa ni Bwana, si mwanadamu, ‘aliyeamurisha kwamba wanaume katika Kanisa Lake wagepaswa kuwa na ukuhani,’ na kwamba ilikuwa pia ni Bwana aliyewapa wanawake na ‘uwezo wa kukamilisha muungano huu mkuu na waajabu, ambao ni Kanisa na ufalme wa Mungu’(“Women of the Church,” Ensign, Nov. 1996, 70). Yote yakinenwa na kutendeka, Bwana hajafunua ni kwa nini amepanga Kanisa kama alivyolipanga.”

  13. Moroni 10:8.

  14. Linda  K. Burton, “Priesthood: A Sacred Trust to Be Used for the Benefit of Men, Women, and Children” (Brigham Young University Women’s Conference address, Mei 3, 2013); ce.byu.edu/cw/womensconference/pdf/archive/2013/lindaBurtonTalk.pdf.

  15. 3 Nefi 30:2.

  16. Mathayo 6:22–23.

  17. Mathayo 5:28; ona pia Alma 39:9. President Thomas S. Monson said: Ponografia hasa ni hatari na ina tawala. Kutazama ponografia kwa kutaka kuona ni nini kunaweza kuwa tabia ya kukudhibiti, kuelekeza kwa mengine machafu zaidi na kwa dhambi ya usafi wa mwili. Epuka ponografia uwezavyo” (“Preparation Brings Blessings,” Ensign or Liahona, May 2010, 65).Mathayo 5:28; ona pia Alma 39:9. Rais Thomas S. Monson alisema: Ya kustusha sana---ni ripoti ya idadi ya watu wanaotumia tovuti kwa ajili ya uovu na malengo ya kudhoofisha, kutazama ponografia ikiwa lengo linaloenea zaidi ya zote. Akina ndugu na dada zangu, kujishughulisha katika hayo kutaangamiza roho kwa kweli. Kuwa mwenye nguvu. Kuwa msafi. Epuka aina ya mambo hayo ya kudhoofisha na kuangamiza uwezavyo-popote huenda yapo! Ninatoa onyo hili kwa wote, kwote” (“Until We Meet Again,” Ensign or Liahona, May 2009, 113).Epuka aina yoyote ya ponografia. Itapuuza roho na kuvuta dhamira. Tunaambiwa katika Mafundisho na Maagano, “Na kile kisichojenga siyo cha Mungu, nacho ni giza” [Mafundisho na Maagano 50:23]” (“True to the Faith,” Ensign or Liahona, May 2006, 18–19).

  18. Ona David A. Bednar, Act in Doctrine (2012), 53.

  19. Ona Dallin H. Oaks, “Priesthood Authority in the Family and the Church,” Ensign or Liahona, Nov. 2005, 24–27.

  20. Barua ya kibinafsi, Aug. 5, 2013; onaYakobo 5:14.

  21. Ona Waebrania 5:4.

  22. Isaya 55:8.

  23. Yakobo 4:13.

  24. Ona Mafundisho na Maagano 81:4–5. President Gordon B. Hinckley alisema: “Sharti lenu ni muhimu sana katika eneo lenu la majukumu kama lilivyo sharti langu katika eneo langu. Hamna wito katika kanisa ili ambao ni mdogo au ulio na maana kidogo” (“This Is the Work of the Master,” Ensign, May 1995, 71).

  25. M. Russell Ballard, “Strength in Counsel,” Ensign, Nov. 1993, 76.