2010–2019
Weka Imani Yako katika Bwana
Oktoba 2013


Weka Imani Yako katika Bwana

Jihusishe katika kufanya kile unaweza katika kushiriki ujumbe mkuu huu wa Urejesho wa injili ya Yesu Kristo.

Dada Ballard nami hivi majuzi tulirudi kutoka kwa kazi katika nchi tano za Ulaya. Huko tulikuwa na fursa ya kukutana na wamisionari wetu wengi, labda wana na binti zenu. Tangu matangazo ya Rais Thomas S. Monson ya kushushwa kwa umri wa kuhudumu kwa wavulana na wasichana wetu, mimi nimekuwa na fursa ya kukutana na zaidi ya 3,000 kati yao. Nuru ya Kristo inang’aa katika nyuso zao na wako tayari kupeleka kazi hii mbele---kutafuta na kufunza, kubatiza, na kurudisha tena, na kuimarisha na kujenga ufalme wa Mungu. Kukutana nao, mtu mara moja anajua, hata hivyo, kwamba hawawezi kufanya kazi hii peke yao. Leo ninataka kuzungumza na washiriki wote wa Kanisa kwa sababu kuna umuhimu wa kujihusisha katika kushiriki injili.

Kama inavyodondolewa mara nyingi, Nabii Joseph Smith alitangaza kwamba “baada ya yote ambayo yamesemwa, wajibu mkuu na muhimu ni kuhubiri injili” (Teachings of Presidents of the Church: Joseph Smith [2007], 330).

Katika mwaka wa 1974 Rais Spencer  W. Kimball alisema hivi: “Labda sababu kuu sana ya kazi ya umisionari ni kuupa ulimwengu nafasi ya kusikia na kukubali injili. Maandiko yamejaa amri na ahadi na wito na zawadi kwa kufunza injili. Natumia neno amri kwa makusudi kwani linaonekana kuwa maelekezo yanayoendelea kutoka kwayo sisi, peke yetu na kwa pamoja hatuwezi kuepuka” (“When the World Will Be Converted,” Ensign, Oct. 1974, 4).

Katika Julai ya mwaka huo huo, Dada Ballard nami tuliondoka pamoja wa watoto wetu na kwenda kusimamia Misheni ya Canada Toronto. Maneno ya Rais Kimball yalikuwa yanavuma katika masikio yangu, haswa wakati yeye alisema, “Ndugu zangu, mimi nashangaa kama tunafanya yote yale tunayoweza. Kwani sisi tunazembea katika mbinu yetu ya kuufunza ulimwengu wote? Tumekuwa tukihamasisha watu sasa kwa miaka 144. Je! Tu Tayari kurefusha misamba yetu? Kupanua ono letu?” ?” (Ensign, Oct. 1974, 5).

Yeye pia anatuuliza sisi tuongezee kasi yetu, tukifanya kazi pamoja kujenga Kanisa na ufalme wa Mungu.

Juni iliyopita Rais Thomas  Monson alipia mwagwi wito huo huo kwa washiriki wa Kanisa. Rais alisema: Sasa ndiyo wakati wa washiriki na wamisionari kuja pamoja … [na] kufanya kazi katika shamba za mzeituni la Bwana ili kuleta nafsi Kwake. Yeye ameyatarisha mbinu kwa ajili yetu za kushiriki injili katika njia nyingi, na Yeye atatusaidia katika kazi zetu kama tutatenda kwa imani kutimiza kazi Yake” (“Imani katika Kazi ya Wokovu” [hotuba iliyotolewa katika matangazo maalum, June  23, 2013]; lds.org/broadcasts).

Ni vyema, ndugu na kina dada, kutafakari juu ya mafundisho ya manabii kutoka nyakati za Joseph Smith hadi leo. Yametuhimiza na kuuita uongozi na washiriki wa Kanisa kuwa wanashughulika kwa bidii katika kuleta ujumbe wa Urejesho wa injili kwa watoto wote wa Baba yetu wa Mbinguni katika ulimwengu wote.

Ujumbe wangu alasiri ya leo ni kwamba Bwana anaharakisha kazi Yake. Katika siku yetu hii inaweza tu kufanyika wakati kila mshiriki wa Kanisa akifikia kwa upendo ili kushiriki kweli za injili ya Urejesho ya Yesu Kristo. Sisi tunahitaji kufanya kazi tukishirikiana na wamisionari 80,000 wetu wanaohudumu sasa. Habari kuhusu kazi kubwa hii, hasa kazi kwa viongozi wa kigingi na kata, kwa uwazi imeandaliwa kwenye tovuti ya LDS.org inayoitwa “Kuharakisha Kazi ya Wokovu.”

Sisi tunajua kutokana na utafiti wetu kwamba wanaoshiriki sana Kanisani wanataka baraka za injili kuwa sehemu ya maisha ya wengine ambao wanawapenda, hata wale ambao wao kamwe hawajakutana nao. Bali sisi pia tunajua kwamba washiriki wengi wanasita kufanya kazi ya umisionari na kushiriki injili kwa sababu mbili za kimsingi.

  • Ya kwanza ni hofu. Washiriki wengi hata hawaombi nafasi za kushiriki injili, wakihofia kwamba wao wanaweza kupokea msukumo mtukufu wa kufanya kitu wanachofikiria wao hawana uwezo wa kufanya hivyo.

  • Sababu ya pili ni kutoelewa kazi ya umisionari ni nini.

Sisi tunajua kwamba wakati mtu anaamka na kutoa hotuba katika mkutano wa sakramenti na kusema, “Leo, nitaongea kuhusu kazi ya umisionari,” au labda hata wakati Mzee Ballard husimama katika mkutano mkuu na kusema kitu hicho hicho, wengine wenu wanaweza kufikiria, “Ee hapana, hapana tena; tumesikia haya hapo awali.”

Sasa, tunajua kwamba hakuna mtu anayependelea kuhisi hatia. Labda unaweza kuhisi unaweza kuulizwa kufanya vitu ambavyo haviwezekani katika uhusiano wa marafiki au majirani. Kwa usaidizi wa Bwana, acha mimi niondoe uoga wowote ambao wewe au wamisionari wa muda wetu wanaweza kuwa nao katika kushiriki injili na wengine.

Fanya uamuzi wa kufanya kile Yesu Kristo ametuuliza kufanya. Mwokozi alisema:

“Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa;

“Kwa maana kila aombaye hupokea; naye atafutaye huona; naye abishaye atafunguliwa.

“Au kuna mtu yupi kwenu, ambaye, mwanawe akimwomba mkate, atampa jiwe?

“Au akiomba samaki, atampa nyoka?

“Basi ikiwa …mnajua kuwapa watoto wenu vipawa vyema, je! Si zaidi sana Baba yenu aliye mbinguni atawapa mema wao wamwombao?”(Mathayo 7:7–11).

Ndugu na kina dada, uoga utakubadilishwa na imani na tumaini wakati washiriki na wamisionari wa muda wanapiga magoti katika maombi na kumuomba Bwana awabariki wao na nafasi za umisionari. Kisha, sharti tuonyeshe imani yetu na kutafuta nafasi za kutanguliza injili ya Yesu Kristo kwa watoto wa Baba yetu wa mbinguni na bila shaka, nafasi zitakuja. Hizi nafasi kamwe hazitahitaji jibu la kushurutishwa au kulazimishwa. Zitatiririka kama matokeo asili ya upendo wetu kwa ndugu na dada zetu. Kuwa tu na msimamo wa kutegemea mema, na wale ambao unaozungumza nao watahisi upendo wako. Kamwe hawatasahau hio hisia hata kama wakati unapoweza kuwa si sawa kwao kukubali injili. Hiyo pia inaweza kubadilika katika siku za usoni wakati hali zao zitabadilika.

Haiwezekani kwetu kushindwa tunapofanya vyema tuwezavyo katika kazi ya Bwana. Hali matokeo ya jawabu la kutumia wakala wa mtu, kushiriki injili ni jukumu letu.

Mtumainie Bwana. Yeye ni Mchungani Mwema. Yeye anawajua kondoo Wake, na kondoo Wake wanajua sauti Yake, na leo, sauti ya Mchungaji Mwema ni sauti yako na sauti yangu. Na ikiwa sisi hatutajihusisha, wengi ambao wangesikia ujumbe wa Urejesho watapitwa. Kusema wazi, ni jambo la imani na matendo katika sehemu yetu. Kanuni ni rahisi kabisa---omba, kibinafsi, na katika familia yako, na kwa nafasi ya umisionari. Bwana amesema katika Mafundisho na Maagano kwamba watu wengi wazuiwa kutoka kwa ukweli “kwa sababu tu hawajui mahali pa kuupata” (M&M 123:12).

Huhitajiki kuwa mtu mnenaji sana au mtu bora kwa kuzungumza au mwalimu mwenye ushawishi. Ukiwa na upendo wa kudumu na tumaini lililo ndani yako, Bwana ameahidi kwamba kama ‘”mtazapa sauti zenu kwa watu hawa; [na] myaseme mawazo nitakayoyaweka mioyoni mwenu, … na ninyi hamtashindwa mbele za watu;

“[Na] kwani mtapewa … katika wakati ule ule, kile mtakachosema” (M&M 100:5–6).

Hubiri Injili Yangu hutukumbusha sisi sote kwamba “hakuna chochote kinachotendeka katika kazi ya umisionari hadi pale [sisi] tunapopata mtu wa kufunza. Zungumza na watu wengi kama unavyoweza kila siku. Ni kawaida kuwa na wasi wasi kidogo kuhusu kuzungumza na watu, lakini unaweza kuomba upate imani na nguvu za kuwa jasiri zaidi katika kufungua kinywa chako na kuhubiri injili iliyorejeshwa” ([2004], 156–57). Ninyi wamisionari wa muda, kama mnataka kufunza zaidi sharti msungumze na watu zaidi kila siku. Hii daima imekuwa kile ambacho Bwana ametuma wamisionari kuenenda mbele kufanya.

Bwana anatujua sisi. Yeye anajua changamoto zetu. Nafahamu kwamba baadhi yenu mnahisi kubebeshwa mzigo mzito, lakini mimi naomba kwamba hakuna kati yenu hatahisi kwamba katika kuwafikia wengine kwa njia ya kawaida na ya kupendeza ili kushiriki injili kutaweza kuwa mzigo. Badala yake, ni nafasi maalum! Hamna shangwe kuu katika maisha kushinda kujihusisha katika huduma ya Bwana.

Muhimu ni kwamba wewe upate mvuvio wa Mungu, kwamba wewe umuombe Yeye maelekezo, na kisha uende na kufanya kama Roho anavyokusukuma wewe. Wakati washiriki wanaona kazi ya wokovu kama jukumu lao peke yao, inaweza kuongofya. Wakati wanaiona kama mwaliko wa kumfuata Bwana katika kuleta nafsi kwake kufunzwa na wazee na kina dada wa muda, inakuwa ya maongozi, kusisimua, na kuinua.

Hatuulizi kila mtu kufanya kila kitu. Kwa kawaida tunauliza washiriki wote waombe tukijua kwamba kama kila mshiriki, vijana na wazee, watafikia tu “mmoja” kati ya sasa na Krismasi, mamilioni watahisi upendo wa Bwana Yesu Kristo. Ni zawadi ya jinsi gani kwa Mwokozi.

Majuma mawili yaliyopita nilipokea barua kutoka familia ya mshiriki mmisionari yenye ufanisi sana, familia ya Munns kutoka Florida. Waliandika:

“Mpendwa Mzee Ballard, dakika 30 baada ya matangazo ya duniani kote juu ya kaharakisha kasi ya wokovu, sisi tilifanya baraza la misionari la familia yetu wenyewe. Tulisisimka kupata kwamba wajukuu wetu vijana walitaka kujumuishwa. Tunafurahia kuripoti kwamba tangu mkutano wa baraza letu, tumeongezea sehemu yetu ya watu wa kufunzwa kwa asilmia 200.

“Tumepata kuwa wajukuu wetu wameleta rafiki zao kanisani, tumefurahia mikutano ya sakramenti na baadhi ya rafiki zetu wasiohudhuria kikamilifu, na tumepata kuwa na wachunguzi wapya kuweka sharti la kuchukua mazungumzo ya misionari. Mmojawapo wa dada zetu wasiohudhuria kikamilifu si tu alirudi kanisani bali pia alileta wachunguzi wapya pamoja naye.

“Hakuna aliyekataa mwaliko wa kuchukua mazungumzo ya misionari. Ni wakati wa msisimko jinsi gani wa kuwa mshiriki katika Kanisa hili”(barua ya kibinafsi, Agosti. 15, 2013).

Sikiliza misukumo ya Roho. Fanya maombi ya kusihi kwa Bwana katika sala kuu. Jihusishe katika kufanya kile unaweza katika kushiriki ujumbe mkuu huu wa Urejesho wa injili ya Yesu Kristo.

Nitanukuu kutoka kwa mshiriki misionari mwenye ufanisi mwengine Clayton Christensen: “Kila mara unapouchukua mkono wa mtu kitamthali kwa mkono wako na kumjulisha yeye kwa Yesu Kristo, wewe utahisi jinsi kwa kina Mwokozi wetu hukupenda na humpenda mtu ambaye mkono wake u mkononi mwako” (The Power of Everyday Missionaries: The What and How of Sharing the Gospel [2013], 1).

Mungu na awabariki ninyi, ndugu na dada, mpate shangwe kuu ambayo huja kutokana kupata miujiza kupitia imani yenu. Kama tunavyofunzwa katika Moroni mlango wa 7:

“Kristo amesema: Ikiwa mtakuwa na imani ndani yangu mtakuwa na uwezo wa kufanya kitu chochote ambacho ni cha kufaa kwangu. …

“ … kwani ni kwa imani kwamba miujiza hufanyika; na ni kwa imani kwamba malaika huonekana na kuhudumia watu; kwa hivyo, kama vitu hivi vimekoma msiba uwe kwa watoto wa watu, kwani ni kwa sababu ya kutoamini, na yote ni bure.” (Moroni 7:33, 37).

Kutoka kwa uzoefu wangu, ninashuhudia kwenu kwamba Bwana atayasikia maombi yenu na mtakuwa na nafasi sasa na miaka ijayo za kutanguliza injili ya Yesu Kristo kwa watoto wenye thamani wa Baba yetu wa Mbinguni. Ninaomba sisi zote tuweze kuhisi furaha nyingi inayokuja na huduma ya umisionari, katika jina la Yesu Kristo, amina.