2010–2019
Kufundisha kwa Nguvu na Mamlaka ya Mungu
Oktoba 2013


Kufundisha kwa Uwezo na Mamlaka ya Mungu

Bwana ametoa njia kwa kila Mtakatifu wa Siku za Mwisho anayestahili kufundisha kwa njia ya Bwana.

Tuna shukrani kupindukia kwa walimu kote katika Kanisa. Tunawapenda ninyi na tuna imani kubwa kwenu. Ninyi ni mojawapo wa miujiza mikubwa ya urejesho wa injili.

Hakika kuna siri ya kuwa mwalimu wa injili mwenye ufanisi, katika kufunza kwa uwezo na mamlaka ya Mungu. Ninatumia neno siri kwa sababu kanuni ambazo kwazo ufanisi wa mwalimu hutegemea zinaweza kueleweka tu kwa wale ambao wana ushuhuda wa kile kilichotendeka katika asubuhi njema, siku angavu, mapema katika msimu wa kuchipua wa mwaka 1820.

Katika jibu kwa maombi ya unyenyekevu ya mvulana wa miaka 14, mbingu zilifunguka. Mungu Baba wa Milele, na Mwanawe, Yesu Kristo, walitokea na kuzungumza na Nabii Joseph Smith. Fidia ya iliyokuwa inangojewa ya vitu vyote ilikuwa imeanza na kanuni ya ufunuo ilianzishwa milele katika kipindi chetu. Ujumbe wa Joseph, ujumbe wetu kwa ulimwengu, unaweza kufupishwa katika maneno mawili: “Mungu husema.” Yeye alinena hapo kale, Yeye alinena na Joseph, na Yeye atanena nawe. Hii ndiyo inakutenga kutokana na walimu wote wengine duniani. Hii ndiyo kwa nini huwezi kushindwa.

Umeitwa kwa roho ya unabii na ufunuo na kutengwa kwa mamlaka ya ukuhani. Hii inamaanisha nini?

Kwanza, inamaanisha kwamba wewe uko katika kazi ya Bwana. Wewe ni wakala Wake, na umepewa mamlaka na kutawazwa kumwakilisha Yeye na kutenda kwa niaba Yake. Kama wakala Wake, wewe una haki ya kuwa na usaidizi Wake. Ni sharti ujiulize, “Mwokozi angesema nini kama Yeye angekuwa anafundisha katika darasa langu leo, na Yeye angesema vipi?” Kisha sharti uendelee kufanya vivyo.

Jukumu hili linaweza kusababisha wengine kuhisi kupungukiwa au hata pengine kuogopa. Njia hii si ngumu. Bwana ametoa njia kwa kila Mtakatifu wa Siku za Mwisho mstahiki kufunza katika njia ya Mwokozi.

Pili, wewe umeitwa kuhubiri injili ya Yesu Kristo. Kamwe usifunze dhana zako au falsafa, hata zilizochanganywa na maandiko. Injili ni “uwezo wa Mungu hata kwa wokovu,”1 na ni kupitia tu kwa injili ambapo tunaokolewa.

La tatu, umeamriwa kufunza kanuni za injili kama zilivyo katika maandiko ya Kanisa, kutoka kwa maneno ya mitume na manabii wa siku hizi, na kufundisha kile unachofunzwa na Roho Mtakatifu.

Basi tutaanzia wapi?

Jukumu letu la kwanza na kuu ni kuishi ili kwamba tuweze kuwa na Roho Mtakatifu kama kiongozi na mwenzi wetu. Wakati Hyrum Smith alipotaka kujihusisha katika kazi hii ya siku za mwisho, Bwana alisema: ”Tazama, hii ndiyo kazi yako, kuzishika amri zangu, ndiyo, kwa nguvu zako zote, akili na uwezo.”2 Hiki ndiyo kizio cha kuanzia. Ushauri, uliotolewa na Bwana kwa Hyrum, ni ushauri sawa na ule Yeye ametoa kwa Watakatifu wote katika kila kipindi.

Ukisema na walimu leo, Urais wa Kwanza alisema hivi: “Sehemu muhimu sana ya huduma yenu itakuwa matayarisho ya kibinafsi ya kila siku yenu wenyewe, ikijumuisha maombi, kujifunza maandiko, na utiifu kwa amri. Tunawahimiza mjitolee wenyewe kuishi injili kwa madhumuni makuu kuliko hapo awali.”3

Ni muhimu kwamba Urais wa Kwanza haukusema kwamba sehemu muhimu sana ya huduma yako ni kutayarisha somo lako vyema au kuwa na umahiri wa mbinu tofauti za kufunza. Bila shaka, ni lazima mtayarishe kila somo kwa bidii na kujitahidi kujifunza jinsi unaweza kufunza ili kuwasaidia wanafunzi wako kutumia wakala wao na kuruhusu injili iingie ndani ya mioyo yao, lakini sehemu ya kwanza na muhimu ya huduma yako ni matayarisho yako ya kibinafsi na kiroho. Mnapofuata ushauri huu Urais wa Kwanza umeahidi; “Roho Mtakatifu atawasaidia ninyi kujua kile cha kufanya.Ushuhuda wenu wenyewe utakua, uongofu wenu utapata kina, na mtaimarishwa ili kukabiliana na changamoto za maisha.”4

Ni baraka kuu gani ambazo mwalimu angetamani?

Kisha, Bwana ameamuru kwamba kabla sisi tutafute kutangaza neno Lake, sisi lazima tutafute kulipokea.5 Ninyi sharti muwe wanaume na wanawake wenye ufahamu makini kwa kupekua maandiko kwa bidii, na kwa kuyahifadhi ndani ya mioyo yenu. Kisha muulize usaidizi wa Bwana, Yeye atawabariki na Roho Yake na neno Lake. Ninyi mtakuwa na uwezo wa Mungu hata kuwashwishi wanadamu.

Paulo anatuambia kwamba injili huja kwa wanadamu kwa njia mbili, katika neno na katika uwezo.6 Neno la injili limeandikwa katika maandiko, na tunaweza kupokea neno kwa kupekua kwa bidii. Uwezo wa injili huja katika maisha ya wale ambao wanaoishi kwa njia ambayo Roho Mtakatifu ni mwenzi wao na wale hufuata msukumo wanaopokea. Baadhi hulenga usikivu wao tu kwenye kupokea neno na wanakuwa weledi katika kutoa habari. Wengine wanapuuza matayarisho yao na kutumainia kwamba Bwana kwa njia moja au nyingine atawasaidia kupitishwa muda wa darasa. Huwezi kutarajia Roho kukusaidia wewe kukumbuka maandiko na kanuni ambazo wewe hujajifunza au kufikiria. Ili kufanikiwa kufunza injili, ni sharti muwe na yote neno na uwezo wa injili katika maisha yenu.

Alma alielewa kanuni hizi alipokuwa anawaelezea wana wa Mosia na jinsi walifunza kwa uwezo na mamlaka ya Mungu. Tunasoma:

“Walikuwa watu ambao wana ufahamu mwema na walikuwa wameyapekua maandiko kwa bidii, ili wajue neno la Mungu.

“Lakini haya sio yote; kwani walikuwa wamejitoa kwa sala, na kufunga; kwa hivyo walikuwa na roho ya … ufunuo.”7

Kisha lazima ujifunze kusikiliza. Mzee Jeffrey R. Holland alifundisha kanuni hii kwa wamisionari. Kile alichosema kinafaa kwa walimu wote. Nitanukuu kutoka kwa hotuba ya Mzee Holland lakini nitachukua uhuru wa kubadili maneno wamisionari na wachunguzi na maneno walimu na wanafunzi mtawalia: La pili tu kwa jukumu [walimu] walililonalo la kusikiliza Roho, ni jukumu walilonalo la kumsikiliza [mwanafunzi]. … Kama tutasikiliza kwa masikio ya kiroho, … [wanafunzi wetu] watatuambia sisi ni masomo gani wanahitaji kusikia!”

Mzee Holland aliendelea: “Jambo ni la kweli kwamba [walimu] bado wanalenga sana katika kuwasilisha maudhui ya somo wanayoona kuwa rahisi, ya kurejelewarejelewa badala ya kulenga juu ya [wanafunzi] wao kama watu binafsi.”8

Baada kujitayarisha mwenyewe na somo lako kwa ubora kabisa wa uwezo wako, ni sharti uwe tayari kuachilia. Wakati ule msukumo tulivu wawa Roho Mtakatifu unapokuja, wewe sharti uwe na ujasiri wa kuweka mbali umbo na muhtasari wako na kuenda pale msukumo wa Roho unakupeleka. Unapofanya hivyo, somo unalowasilisha si somo lako tena, bali linakuwa somo la Mwokozi.

Unapojitolea mwenyewe kuishi injili kwa kusudi kuu kuliko hapo awali na kupekua maandiko, kuyahifadhi katika moyo wako, Roho Mtakatifu yule yule, ambaye alifunua maneno haya kwa mitume na manbii hapo kale, atakushuhudia ukweli wake. Kimsingi, Roho Mtakatifu atayafunua upya kwako.Wakati haya yanapotokea, maneno ambayo unasoma si tu maneno ya Nefi, au Paulo, au Alma, bali yanakuwa maneno yako. Kisha, unapofunza, Roho Mtakatifu ataweza kukufunza vitu vyote na kuvileta vitu vyote katika ukumbusho wako. Hakika, “kwani mtapewa katika saa ile ile, ndiyo, katika wakati ule ule, kile mtakachosema.”9 Wakati hiki kitatokea, utajipata mwenyewe ukisema kitu ambacho wewe hukuwa umepanga kukisema. Kisha, ikiwa utakuwa msikivu, utajifunza kitu fulani kutokana na vitu ambavyo unasema. Rais Marion  G.Romney alisema, “Mimi daima najua wakati ninaposema chini maongozi ya Roho Mtakatifu kwa sababu daima mimi hujifunza kitu kutokana na kile nimesema.”10Kumbuka, mwalimu pia ni mwanafunzi.

Mwisho, wewe sharti usimame kama shahidi huru kutokana na vitu ambavyo wewe hufunza na si tu kupiga mwangwi maneno yaliyopo ndani ya kitabu cha kiada au mawazo ya wengine. Unaposherekea ya maneno ya Kristo na kujitahidi kuishi kusudi kuu kuliko hapo awali. Roho Mtakatifu atakufunulia kuwa vitu unavyofundisha ni kweli. Hii ni roho ya ufunuo na roho yuyu huyu atapeleka ujumbe wako katika mioyo ya wale wanaotamani na wana hiari kupokea.

Hebu sasa tuhitimishe pale tulipoanza---katika Bustani Takatifu. Kwa sababu ya kilichotokea katika asubuhi hiyo njema ya msimu wa mchipuko, muda usio kitambo sana, una haki ya kufundisha kwa nguvu na mamlaka ya Mungu.{nb Juu ya haya mimi natoa ushuhuda wangu katika jina la Yesu Kristo, amina.