2010–2019
Wachungaji wa Kweli
Oktoba 2013


Wachungaji wa Kweli

Ualimu wa nyumbani hujibu maombi mengi na kuturuhusu sisi kuona mabadiliko yanayoweza kufanyika katika maisha ya watu.

Usiku wa leo Katika Kituo cha Mkutano katika Mji wa Salt Lake na katika maeneo ya mbali na karibu wamekusanyika wale wanashikilia ukuhani wa Mungu. Kwa kweli ninyi mu “ukuhani wa kifalme”---hata “kizazi teule,” kama vile Mtume Petro alivyotangaza.1 Mimi ninastahi kuwa na nafasi ya kuwahutubia ninyi.

Nilipokuwa ninakua, kila musimu wa joto familia yetu ingesafiri kwa gari hadi Provo Canyon, karibu maili 45 (kilometa 72 ) kusini na mashariki kidogo mwa Mji wa Salt Lake, ambapo tungekaa katika nyumba ya mbao ya familia kwa wiki kadhaa. Sisi wavulana daima tulikuwa na dukuduku kuenda kwenye kijito cha kuvua samaki au katika shimo la kuongelea, na tulisisita sana gari liende kasi. Katika siku hizo, gari aliloendesha baba yangu likuwa Oldmobile ya 1928. Kama yeye angeendesha zaidi ya maili 35 (kilometa 56 ) kwa saa, mama yangu angesema “Punguza kasi! Punguza kasi! Nami ningesema, “Kanyaga kichapuzi! Baba! Kanyaga mafuta!

Baba angeendesha gari karibu maili 35 kwa saa katika safari yote hata Provo Canyon au mpaka tungefikia karibu na kona katika barabara na safari yetu ingesimamishwa na kundi la kondoo. Sisi tungetazama mamia ya kondoo yakipita mbele yetu, yakionekana bila mchungaji, mbwa wachache wakibweka nyumba yetu walipokuwa wakipita. Huko nyuma kabisa tungemuona mlisha kondoo kwenye farasi yake---bila kigwe bali kitanzi tu. Mara kwa mara angekaa kivivu kwenye tandiko la farasi akisinzia, kwa vile farasi alijua njia ya kwenda na mbwa waliokuwa wanabweka ilifanya kazi.

Kinyume cha hayo kwa mandhari ambayo mimi niliona katika Munich, Ujerumani, miaka mingi iliyopita. Ilikuwa Jumapili asubuhi, na tulikuwa tunaenda kwenye mkutano mkuu wa wamisionari. Nilipokuwa nikitazama nje mwa dirisha la gari la rais wa misheni, niliona mchungaji akiwa na fimbo mkononi mwake, akiwaongoza kondoo. Walimfuata popote alipoenda. Kama angeenda kushoto, wao wangemfuata yeye kushoto. Kama angeenda kulia, wao wangemfuata katika upande huo. Mimi nilifanya mfananisho kati ya mchungaji wa kweli ambaye huongoza kondoo wake na mlisha kondoo ambaye huenda kwa farasi nyumba ya kondoo wake,

Yesu alisema, “Mimi ndimi mchungaji mwema, na nawajua kondoo wangu.”2 Yeye anatupatia sisi mfano kamili wa kile mchungaji wa kweli anapaswa kuwa.

Ndugu, kama ukuhani wa Mungu, sisi tuna jukumu la uchungaji. Hekima ya Bwana imetupatia mwongozo ambao kwawo sisi tutaweza kuwa wachungaji kwa familia za Kanisa, ambapo sisi tunaweza kuhudumu, tunaweza kufunza, na tunaweza kushuhudia kwao. Hiyo ndiyo inaitwa ualimu wa nyumbani, na ndiyo kuuhuhusu ndiyo mimi ningependa kuongea nanyi usiku wa leo.

Askofu wa kila kata katika Kanisa husimamia kupangwa kwa wenye ukuhani kama walimu wa nyumbani ili kutembelea nyumba za washiriki kila mwezi. Wanaenda katika majozi. Pale inapowezekana, mvulana ambaye ni kuhani au mwalimu katika Ukuhani wa Haruni huandamana na mtu mzima ambaye ana Ukuhani wa Melkidezeki. Wanapokwenda kwenye nyumba ambazo wana majukumu juu yake, mwenye Ukuhani wa Haruni anapaswa kushiriki katika ufunzaji unaofanyika. Kazi kama hiyo itasaidia kuwatayarisha wavulana kwa misheni, pia kwa maisha ya huduma ya ukuhani.

Mpango wa ualimu nyumbani ni jibu la ufunuo wa kisasa, ukipatia wajibu wale waliotawazwa katika ukuhani “kufundisha, kuelezea, kushawishi, kubatiza … na kutembelea nyumba ya kila muumini, na kuwashawishi kusali kwa sauti na kwa siri na kushiriki kazi zote za familia, ... kuliangalia kanisa daima, na kuwa nalo, na kuwaimarisha; na kuona kwamba hakuna uovu katika kanisa, wala kuzozana baina yao, wala kudanganya, kusengenya, wala kusemana mabaya.”3

Rais David  O McKay alionya: “Ualimu wa nyumbani ni mojawapo wa nafasi zetu muhimu na za kufurahisha za kutunza na kuvuvia, kushauri na kuelekeza watoto wa Baba yetu. … Ni huduma takatifu, wito mtakatifu. Ni wajibu wetu kama Walimu wa Nyumbani kubeba … roho katika kila nyumba na moyo. Kupenda kazi hii na kufanya vyema tuwezavyo kutaleta amani isiyo na kipimo, shangwe, na kuridhika kwa [mwalimu] [mwandilifu], mwenye kujitolewa wa watoto wa Mungu.”4

Kutoka katika Kitabu cha Mormoni tunasoma kwamba Alma “aliwatakasa makuhani wao wote na walimu wao wote; na hakuna yeyote aliyetakaswa ila tu wale wanadamu waliokuwa wenye haki.

“Kwa hivyo waliwalinda watu wao, na kuwalisha vitu vilivyohusu utakatifu.”5

Katika kutekeleza majukumu yetu ya ualimu nyumbani, sisi tunakuwa na hekima kama tunajifunza na kuelewa changamoto za wanafamilia wa kila familia, ili kwamba tuweze kuwa na ufanisi katika ufunzaji na kutoa usaizidi unaohitajika.

Matembezi ya ualimu nyumbani pia yanaweza kuwa na uwezekano wa kufanikiwa kama miadi imefanywa mapema. Ili kuonyesha jambo hili, acha mimi nishiriki nanyi tukio nililokuwa nalo miaka kadhaa iliyopita. Wakati huo Kamati Tendaji ya Umisionari ilikuwa inajumuisha Spencer  W. Kimball, Gordon  B. Hinckley, na Thomas  S. Monson. Jioni moja Ndugu na Dada Hinckley waliandaa chakula cha jioni nyumbani kwao kwa wana kamati na wake zao. Tulikuwa tu tumemaliza mlo mtamu sana wakati kulikuwa na kugongwa mlango. Rais Hinckley alifungua mlango na kumpata mmoja wa walimu wa nyumbani wake amesimama hapo. Mwalimu wa nyumbani akasema, “Najua kuwa sikuwa nimefanya miadi ya kuja, na sijakuja na mwenzi wangu, lakini nilihisi ninafaa kuja kwako usiku wa leo. Mimi sikujua kuwa ungekuwa anaandalia wageni.”

Rais Hinckley kwa upole alimwalika ndani yule mwalimu wa nyumbani na kukaa chini ili awafunze Mitume watatu na wake zao kuhusu wajibu wetu kama washiriki. Kwa uoga na hofu, huyu mwalimu wa nyumbani alifanya vyema awezavyo. Rais Hinckley alimshukuru kwa kuja, na baada ya hapo akaondoka upesi.

Mimi nitataja mfano mmoja zaidi wa njia isiyo sahihi ya kutekeleza ualimu wa nyumbani. Rais Marion  G. Romney, ambaye alikuwa mshauri katika Urais wa Kwanza miaka kadha iliyopita, alikuwa anatuambia kuhusu mwalimu wa nyumbani wake ambaye wakati mmoja alikuja katika nyumba ya Romney usiku wa msimu wa baridi. Alikuwa ameweka kofia yake mikononi na aliyumbayumba kwa wasiwasi alipoalikwa kukaa chini na kutoa ujumbe wake. Alibakia kusimama, akasema, “Vyema, nitakuambia Ndugu Romney, ni baridi sana huko nje, na mimi nimeacha injini ya gari ikiguruma ili isisite. Mimi nimepitia ili niweze kumwambia askofu kwamba mimi nimefanya matembezi yangu.”6

Rais Ezra Taft Benson, baada ya kuelezea juu ya tukio la Rais Romney katika mkutano wa wenye ukuhani, kisha alisema, “Tunaweza kufanya vyema kushinda hivyo---vyema zaidi!”7 Mimi nakumbaliana.

Ualimu wa nyumbani ni zaidi ya matembezi tu ya mara moja kwa mwezi. Letu ni jukumu la kufundisha, kuelezea, kuhamasisha, na pale tunapotembelea wale wasio watendaji kamili, kuleta uhudhuria kamili na hatimaye kuinuliwa kwa wana na mabinti wa Mungu.

Ili kusaidia katika juhudi zetu, mimi nashiriki ushauri huu wenye hekima ambao kwa kweli hunahusika na walimu wa nyumbani. Unatoka kwa Abraham Lincoln, ambaye alisema: “Kama unataka kushawishi mtu katika jambo lako, kwanza mthibitishie yeye kuwa wewe ni rafiki yake wa dhati.”8 Rais Ezra Taft Benson alisema: “Juu ya yote, kuwa rafiki wa kweli kwa watu na familia unazofundisha. … Rafiki hufanya zaidi ya kazi ya matembezi ya kila mwezi. Rafiki anajihusisha zaidi na kuhusu kuwasaidia watu kuliko kupata sifa. Rafiki hujali. Rafiki [huonyesha upendo]. Rafiki husikiliza na rafiki hufikia.”9

Ualimu wa nyumbani hujibu maombi mengi na kuturuhusu sisi kuona mabadiliko ambayo yanaweza kufanyika katika maisha ya watu.

Mfano wa haya unaweza kuwa Dick Hammer, ambaye alikuja Utah pamoja na Jeshi la Kuhifadhi la Raia wakati wa Mdororo mkuu. Yeye alikutana na kuoana na msichana wa Watakatifu wa Siku za Mwisho. Alifungua Dick’s Café katika St. . George, Utah, ambapo palikuwa mahali maarufu pa kukutana.

Aliyekuwa amepangwa kama mwalimu wa nyumbani wa familia ya Hammer alikuwa ni Willard Milne, rafiki yangu. Kwa vile nilikuwa namjua Dick Hammer pia, baada ya kupiga chapa ratiba ya chakula cha mkahawa wake, mimi ningemuuliza rafiki yangu Ndugu Milne nilipotembelea St. George, “Je! Rafiki yetu Dick Hammer anaendelea vipi?”

Jibu kwa kawaida lingekuwa, “Yeye anajaribu, lakini kidogo kidogo.”

Wakati Willard Milne na mwenzi wake walitembelea nyumba ya Hammer kila mwezi, wao daima waliweza kuwasilisha ujumbe wa injili na kushiriki shuhuda zao pamoja na Dick na familia.

Miaka ikapita, na basi siku moja Willard akanipigia simu akiwa na habari njema. Ndugu Monson,” yeye alianza, “Dick Hammer ameongoka na atabatizwa. Alikuwa katika mwaka wake wa 90, na tumekuwa marafiki katika maisha yetu yote ya utu uzima. Maamuzi yake yalitia joto katika moyo wangu. Nilikuwa mwalimu wa nyumbani wake kwa miaka mingi.” Kulikuwa na kitu katika sauti ya Willard alipokuwa anatoa ujumbe wa makaribisho yake.

Ndugu Hammer kwa kweli alibatizwa na mwaka mmoja baadaye akaingia katika Hekalu la St.  George na hapo akapokea endaumenti yake na baraka za kufunganishwa.

Mimi nilimuuliza Willard, “Je! Wewe kamwe ulipata kuvunjika moyo kama mwalimu wa nyumbani wake kwa muda mrefu jinsi hiyo?”

Alijibu, “La, ilikuwa inastahili kila juhudi. Ninaposhuhudia shangwe ambayo imekuja kwa wanafamilia wa familia ya Hammer, moyo wangu anajawa na shukrani kwa ajili ya baraka injili imeleta katika maisha yao na kwa nafasi mimi nimekuwa nayo katika kusaidia kwa njia fulani. Mimi ni mtu aliye na furaha.

Ndugu, ni nafasi yetu katika miaka ya kutembelea na kufunza watu wengi---wale ambao hawashiriki kikamilifu pia wale ambao wameweka sharti kamili. Kama sisi tutakuwa na mzingatio katika wito wetu, tunakuwa na nafasi nyingi za kubariki maisha. Matembezi yetu kwa wale ambao wamejiweka mbali na shughuli za Kanisa yanaweza kuwa funguo ambayo hatimaye itafungua milango ya kurudi kwao.

Tukiwa na hili wazo akilini, acha sisi tuwafikie wale ambao sisi tuna jukumu juu yao na kuwaleta wao katika meza ya Bwana ili washerekee neno Lake na kufurahia uenzi wa Roho Yake, na kuwa “si wageni wala wapitaji, bali ninyi ni wenyeji pamoja na watakatifu, watu wa nyumbani mwake Mungu.”10

Kama yeyote wenu ameteleza katika kuzembea kuhusu matembezi yenu ya ualimu nyumbani, wacha niseme kwamba hamna wakati kama sasa wa kujitolea tena ili kutimiza wajibu wenu wa ualimu wa nyumbani. Amueni sasa kufanya juhudi zozote zile zinazohitajika kuwafikia wale ambao ninyi mmepatiwa jukumu juu yao. Kuna nyakati ambazo kusukuma kidogo zaidi kunaweza kuhitajika, pia, ili kumsaidia mwenzi wako wa ualimu nyumbani apate muda wa kuenda pamoja nawe, lakini kama utasisitiza, mtafanikiwa.

Ndugu, juhudi zetu katika ualimu nyumbani zinaendelea. Kazi hii kamwe haitamalizika mpaka Bwana na Mwokozi wetu atakapo, “Imetosha.” Kuna maisha ya kuangaza. Kuna mioyo ya kugusa. Kuna nafsi za kuokoa. Ni fursa yetu takatifu ya kuangaza, kugusa, na kuokoa zile nafsi zenye thamani tulizothaminiwa nazo kwa utunzaji wetu. Tunapaswa kufanya hivyo kwa uaminifu na kwa mioyo iliyojawa na furaha.

Katika kufunga, nitageuka kwa mfano mmoja mahususi ili kuelezea aina ya walimu wa nyumbani tunaopaswa kuwa. Kuna Mwalimu mmoja ambaye maisha yake yanashinda yale mengine yote. Yeye alifundisha katika maisha na mauti, juu ya wajibu na kudra. Yeye aliishi kuhudumu wala si kutumikiwa, kutoa wala si kupokea, kujitolea maisha yake kwa ajili ya wengine wala si kuokoa maisha yake. Yeye alielezea upendo maridadi zaidi kuliko shauku, umaskini kuwa utajiri kuliko hazina. Ilisemekana juu ya Mwalimu huyu kwamba Yeye alifundisha kwa mamlaka na wala si kama vile waandishi.11. Sheria Zake hazikuandikwa kwenye jiwe bali kwenye mioyo ya wanadamu.

Mimi naongea juu ya Bwana Mwalimu, haya Yesu Kristo, Mwana wa Mungu, Mwokozi na Mkombozi wa wanadamu wote. Taarifa za kibiblia zinasema juu Yake, Yeye “alizunguka huko na huko akitenda kazi njema.”12 Tukiwa na Yeye kama mwongozo wetu usioanguka na mfano, tunaweza kuhitimu kwa usaidizi Wake mtakatifu katika ualimu wa nyumbani wetu. Maisha yatabarikiwa. Mioyo itafarijiwa. Nafsi zitaokolewa. Sisi tutakuwa wachungaji wa kweli. Na hiyo iwe hivyo, mimi naomba katika jina la yule Mchungaji mkuu, Yesu Kristo, amina.