2010–2019
Karibuni kwenye Mkutano Mkuu
Oktoba 2013


Karibuni kwenye Mkutano Mkuu

Ni maombi yangu kwamba sisi tutaweza kujazwa na Roho wa Mungu tunaposikiliza na kujifunza.

Ni vyema jinsi gani, ndugu na dada zangu wapendwa, kukutana pamoja mara ingine tena. Imekuwa tu zaidi ya miaka 183 tangu Kanisa lianzishe na Nabii Joseph Smith, chini ya maelekezo ya Bwana. Katika mkutano huo hapo Aprili  6, 1830, kulikuwa na washiriki sita wa Kanisa waliohunduria.

Mimi nina furaha kutangaza kwamba wiki mbili, zilizopita washiriki wa Kanisa walifika milioni 15. Kanisa linaendelea kukua bila kukoma na kubadilisha maisha ya watu wengi na wengi sana kila mwaka. Linaenea kote ulimwenguni jeshi letu la wamisionari linapotafuta wale ambao wanatafuta ukweli.

Imekuwa tu karibu mwaka mmoja tangu mimi nitangaze kushushwa kwa umri wa huduma ya umisionari. Tangu wakati huo, idadi ya wamisionari wa muda wanaohudumu imeongezeka kutoka 58,500 katika Oktoba 2012 hadi 80,333 leo. Ni tukio la ajabu na maongozi jinsi gani sisi ambalo tumelishuhudia!

Maandiko matakatifu hayana tamko linalolingana zaidi, hamna jukumu la kifungo zaidi, hamna maelekezo yaliyo wazi zaidi kushinda amri iliyotolewa na Bwana aliyefufuka Yeye alipotokea katika Galilaya kwa wafuasi kumi na moja. Yeye alisema, “Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu.”1 Nabii Joseph Smith alitangaza, “Baada ya yote ambayo yamesemwa, wajibu mkuu na muhimu sana ni kuhubiri injili.”2 Wengine wenu hapa leo bado mtakumbuka maneno ya Rais David  O. McKay, ambaye alitoa msemo unajulikana “Kila mshiriki ni mmisionari!”3

Kwa maneno yao mimi ninaongeza yangu mwenyewe. Sasa ni wakati wa washiriki na wamisionari kuja pamoja, kufanya kazi pamoja, kutumika katika shamba la mzeituni la Bwana ili kuleta nafsi Kwake. Yeye ametayarisha njia za sisi kushiriki injili katika njia nyingi sana, na Yeye atatusaidia sisi katika kutumika kwetu ikiwa sisi tutatenda kwa imani ili kutimiza kazi Yake.

Ili kukimu jeshi letu linaloongezeka kila dakika, mimi nimewauliza washiriki wetu wakati uliopita wachange, kama wanavyoweza, kwenye hazina ya kata ya misionari au kwa Hazina Kuu ya Misionari ya Kanisa. Jibu la mwito huo limekuwa la kuridhisha na limesaidia kukimu maelfu ya wamisionari ambao hali yao haiwaruhusu wao kujikimu wenyewe. Nawashukuru ninyi kwa mchango wenu kwa moyo mkujufu. Haja ya msaada inaendelea, kwamba tuweze kuendelea kuwasaidia wale ambao hamu ya kuhudumu ni kubwa lakini hawana hela za kufanya hivyo wenyewe.

Sasa, ndugu na kina dada, tumekuja hapa ili tuelekezwe na kupatiwa maongozi. Jumbe nyingi ambazo zinahusisha mada za injili tofauti, zitatolewa katika siku mbili zifuatazo. Wanaume na wanawake ambao wataongea nanyi wametafuta usaidizi wa mbinguni kuhusu jumbe watakazotoa.

Ni maombi yangu kwamba tuweze kujazwa na Roho wa Bwana tunaposikiliza na kujifunza. Katika jina la Mwokozi wetu, Yesu Kristo, amina.

Muhtasari

  1. Mathayo 28:19.

  2. Teachings of Presidents of the Church: Joseph Smith (2007), 330.

  3. David O. McKay, in Conference Report, Apr. 1959, 122.