2010–2019
Unaweza Kufanya Hivyo Sasa!
Oktoba 2013


Unaweza Kufanya Hivyo Sasa!

Kama tuko tayari kusimama na kuendelea kwenye njia, … tunaweza kujifunza kitu kutokana na kushindwa kwetu na kuwa bora na wenye furaha.

Nilipokuwa kijana, kuanguka na kuinuka kulionekana kuwa kutendo kimoja na sawa sawa. Katika miaka mingi, hata hivyo, mimi nimefikia maamuzi kwamba sheria za fizikia zimebadilika---na si kwa manufaa yangu.

Si kitambo sana mimi nilikuwa niliteleza kwa skii pamoja na mjukuu wa kiume wangu wa miaka 12. Tulikuwa tunafurahia wakati wetu pamoja tulipofika kwenye sehemu ya barafu na kuishia kuanguka kwenye mteremko mkali.

Nilijaribu kila mbinu kusimama lakini nisiweze---nilikuwa nimeanguka, na singeweza kusimama.

Nilihisi vyema kimwili, lakini kujistahi kwangu kulikuwa kumeumizwa. Kwa hivyo nilihakikisha kwamba helmeti na miwani yangu ilikuwa mahali pake kwa vile nilipendelea kwa wale watelezaji wa skii wasinitambue. Ningejifikiria kuketi pale kujihisi bure wakati walivyoweza kuteleza kiajabu, wakisema, “Halo, Ndungu Ucthdorf!”

Nilianza kujiuliza ingehitajika nini kuniokoa. Hapo ndipo mjukuu wangu mvulana alipokuja kando yangu. Nilimwambia kile kilichokuwa kimetokea, lakini alionekana kutoshughulika sana na maelezo yangu ya kwa nini singeweza kuinuka. Yeye aliniangalia mimi katika macho, akininyoshea mkono, na kuchukua mkono wangu, na sauti thabiti akasema, “Babu, wewe unaweza kufanya hivyo sasa!”

Mara moja, nikasimama.

Nilikuwa bado ninatingisa kichwa juu ya haya. Kile kilichokuwa kinaonekana kutowezekana tu muda mchache mapema ghafula kikawa uhalisi, kwa sababu mvulana wa miaka 12 alininyooshea mkono na kusema, “Wewe unaweza kufanya hivyo!” Kwangu mimi, ilikuwa ni mchanganyiko wa kujiamini, mhemuko, na nguvu.

Ndungu, kunaweza kuwa na wakati katika maisha yetu ambapo kuinuka na kuendelea mbele inaonekana kuwa vigumu zaidi ya uwezo wetu. Siku hiyo kwenye mteremko uliofunikwa na theluji nilijifunza kitu. Hata wakati tunafikiria hatuwezi kuinuka---bado kuna tumaini. Na wakati mwingine tunahitaji tu mtu kututazama machoni, kuchukua mkono wetu, na kusema, “Wewe unaweza kufanya hivyo sasa!”

Madanganyo ya Ubabe

Tunaweza kufikiria kwamba wanawake wana shinda wanaume kwa kuwa na hisia za upungufu na maudhiko---kwamba inawaathiri wao sana kuliko sisi. Mimi sina uhakika kwamba hii ni kweli, Wanaume hupitia hisia za kuwa na hatia, kusononeka, na kushindwa. Tunaweza kujifanya hisia hizi hazitusumbui, lakini zinafanya hivyo. Tunaweza kuhisi kulemewa na mzigo wa kushindwa kwetu na mapungufu ambayo yanaanza na kufikiria kamwe hatutaweza kufaulu. Tunaweza hata kudhania kwamba kwa sababu tumeanguka mbeleni, kuanguka ni kudra yetu. Kama mwandishi mmoja alivyosema, “Tunapiga makasia mbele, mashua dhidi ya mkondo, yakisukumwa nyuma bila kusita.”1

Mimi nishaona watu waliojawa na uwezo na neema wakijiondoa kutoka kwa kazi yenye changamoto ya kujenga ufalme wa Mungu kwa sababu wameanguka mara moja au mbili. Hawa walikuwa watu wa ahadi ambao wangekuwa wenye ukuhani hodari na watumishi wa Mungu. Lakini kwa sababu wamejikwaa na kuvunjika moyo, wanajiondoa kutoka kwa wajibu wao wa ukuhani na kutafuta shughuli rahisi lakini zisizo za kustahili.

Na hivyo, wanaendelea, kuishi wakitimiza tu sehemu ndogo ya maisha ambayo wangetimiza, kamwe wasiinuke hata kwenye uwezo ambao ni haki yao ya kuzaliwa. Kama vile mshairi alivyoonyesha huzuni, hawa ni miongoni mwa zile nafsi zenye bahati mbaya ambazo “hufa pamoja na muziki wao [mwingi] ukiwa [bado] ndani yao.”2

Hakuna mtu yeyote anayependa kushindwa. Na hasa hatupendi wakati wengine---hasa wale tunaowapenda ---wakituona sisi tukishindwa. Sisi sote tunataka kuheshimika, na kuthaminiwa,. Tunataka kuwa washindi. Lakini sisi wanadamu hatuwezi kuwa washindi bila juhudi na nidhamu au bila kufanya makosa.

Ndugu, kudra yetu haithibitshwi na idadi ya mara tunayojikwaa bali na idadi ya mara tunazoinuka, kujipangusa wenyewe, na kusonga mbele.

Huzuni Iliyo kwa jinsi ya Mungu

Tunajua haya maisha ya duniani ni mtihani. Lakini kwa sababu Baba yetu wa Mbinguni anatupenda kwa upendo kamili, Yeye hutuonyesha mahali pa kupata majibu. Yeye ametupatia ramani ambayo inaturuhusu kupitia katika maeneo kanganyishi na majaribu yasiyotarajiwa ambayo kila mmoja wetu anakabiliana nayo. Maneno ya manabii ni sehemu ya ramani hiyo.

Tunapopotea---tunapoanguka au kuondoka kutoka kwenye njia ya Baba yetu wa Mbinguni---maneno ya manabii yanatuambia sisi jinsi ya kuinuka tena na kurudi kwenye mkondo.

Kati ya kanuni zote zilizofunzwa na manabii kote katika karne nyingi, moja ambayo imesisitizwa mara na mara tena ni ujumbe wa matumaini na kuinua ambao wanadamu wanaweza kutubu, kubadilisha njia, na kurudi tena kwenye mapito ya kweli ya uanafunzi.

Hii haimaanishi kwamba sisi tunapaswa kukubaliana na udhaifu wetu, makosa, au dhambi. Na kuna tofauti muhimu kati ya huzuni wa dhambi ambao huelekeza hata kwenye toba na huzuni ambayo hulekeza hadi kukata tama.

Mtume Paulo alifunza kwamba “ huzuni iliyo kwa jinsi ya mungu huleta toba iletayo wokovu … lakini huzuni ya ulimwengu hufanya mauti.”3 huzuni iliyo kwa jinsi ya mungu huvuvia mabadiliko na matumaini kupitia Upatanisho wa Yesu Kristo. Huzuni ya dunia hutuangusha chini, huzima tumaini, na kutushauri kuingia katika majaribu zaidi.

Huzuni iliyo kwa jinsi ya mungu hupelekea hata uongofu4 na mabadiliko ya moyo.5 Hutufanya sisi kuchukia dhambi na kupenda wema.6 Hutuhimiza kusimama na kutembea katika nuru ya upendo wa Kristo. Toba ya kweli ni kuhusu mabadiliko, wala si mateso, au usumbufu. Ndio, majuto ya kuhisi moyoni na toba kweli kwa utovu mara nyingi ni uchungu na hatua muhimu katika mchakato mtakatifu wa toba. Lakini wakati hatia inapopelekea kujichukia au kutuzuia sisi kutokana na kuinuka tena, ni kikwazo badala kudumumisha toba.

Akina ndugu, kuna njia bora. Acha tuinuke na kuwa wanaume wa Mungu. Sisi tuna mshindi, Mwokozi, ambaye alitembea kupitia bonde la kivuli cha mauti kwa niaba yetu. Yeye alijipatiana Mwenyewe kama fidia ya dhambi zetu. Hakuna yeyote ambaye ameshakuwa na upendo mkuu huu kuliko huyu---Yesu Kristo, Mwanakondoo asiye na mawaa, kwa hiari alijileta Mwenyewe kwenye madhabahu ya dhabihu na kulipa bei ya dhambi zetu kwa “bure ghali sana.”7 Yeye alijichukulia juu Yake Mwenyewe mateso yetu. Yeye alichukua mizigo yetu, hatia zetu juu ya mabega Yake. Wapendwa marafiki zangu, tunapoamua kuja Kwake, tunapojichukulia juu yetu wenyewe jina Lake, na kutembea kwa ujasiri katika njia ya uanafunzi, basi kupitia Upatanisho sisi tumeahidiwa si tu furaha na “amani katika ulimwengu huu” bali pia “uzima wa milele katika ulimwengu ujao.”8

Tunapofanya makosa, tunapotenda dhambi na kuanguka, acha sisi tufikirie kuhusu kile kinachomaanisha na kutubu kikweli. Inamaanisha kugeuza moyo wetu na upendeleo kwa Mungu na kuachana na dhambi. Toba ya kweli ya moyo huleta pamoja nayo hakikisho la mbinguni kwamba sisi tunaweza “kufanya hivyo sasa.”

Wewe Ni Nani?

Mojawapo wa mbinu za adui za kutuzuia sisi kutokuendelea ni kutukanganya kuhusu sisi ni kina nani na tunatamani nini hasa.

Tunataka kutumia wakati na watoto wetu, lakini pia tunataka kujumuika katika uraibu wetu wa kiume tuupendao. Tunataka kupunguza uzito, lakini pia tunataka kufurahia chakula tunachotamani. Tunataka kuwa kama Kristo, lakini pia tunataka kumkemea mtu yule anayeruka foleni barabarani.

Madhumuni ya Shetani ni kutujaribu kubadilisha lulu zenye thamani kuu za furaha ya kweli na thamani tukufu kwa kishaufu ambacho ni kijonzi tu cha furaha na shangwe ghusi.

Mbinu nyingine ambayo adui hutumia ni kutuvunja moyo tusiinuke ni kutufanya sisi kuona amri kama vitu ambavyo vimelazimishwa juu yetu. Nachukulia ni asili ya binadamu kukataa chochote ambacho hakionekana kuwa ni wazo letu wenyewe hapo kwanza.

Kama tunaona kula lishe ya afya na kufanya mazoezi kama kitu tu ambacho daktari wetu anatarajia kutoka kwetu, pengine tutaweza kushindwa. Tukiona chaguzi hizi kama sisi ni kina nani na nani tunataka kuwa, tuna nafasi kuu ya kukaa kwenye njia na kufaulu.

Kama tunaona ualimu wa nyumbani kama tu lengo la rais wa kigingi, tunaweza kuweka thamani ya chini ya kuitenda. Kama tukiiona kama ni lengo letu---kitu tunachotamani kufanya ili tuwe zaidi kama Kristo na kuwahudumia wengine---hatutatimiza tu sharti letu bali kulitimiza katika njia ambayo kwa kweli hubariki familia tunazotembelea na familia zetu wenyewe pia.

Mara nyingi, sisi ndio husaidiwa na marafiki au familia. Lakini tukiangalia kote kwa macho makini na lengo la moyo wa kujali, tutambua fursa ambazo Bwana hutoa ili kusaidia wengine kuinuka tena na kuelekea kwa uwezo wao wa kweli. Maandiko yanaonyesha, “Lolote mfanyalo, lifanyeni kwa moyo, kama kwa Bwana na si kwa wanadamu.”9

Inakuwa ni nyenzo kuu ya nguvu za kiroho kuishi maisha ya uaminifu na wema na kuweka macho yetu kwenye mahali tunakotaka kuwa milele. Hata kama tunaona mwisho wa safari takatifu tu kwa jicho la imani, itatusaidia kukaa katika njia hii.

Wakati usikivu wetu unazingatia zaidi kwenye ufanisi wetu au kufeli kwetu kila siku, tunaweza kupotea njia, kutangatanga, na kuanguka. Kwa kuweka macho yetu kwenye malengo ya juu, kutatusaidia kuwa wana bora, na ndugu, kina baba wakarimu, na mabwana wenye upendo.

Hata wale ambao wanaweka mioyo yao juu ya malengo ya milele wanaweza kujikwaa mara kwa mara, lakini hawatashindwa. Wanaamini na kutegemea juu ya ahadi za Mungu. Watainuka tena kwa tumaini angavu katika Mungu mwema na ono la kudra kuu. Wanajua wanaweza kutenda hivyo sasa.

Unaweza Kutenda Hivyo Sasa

Kila mtu, kijana na mzee, ameshapata kuwa na uzoefu wake mwenyewe wa kibinafsi wa kuanguka. Kuanguka ndio kile watu hufanya. Lakini almradi tu tayari kuinuka tena na kuendelea kwenye njia kuelekea malengo ya kiroho ambayo Mungu ametupatia, tunaweza kujifunza kitu kutokana na kushindwa na kuwa bora na kufurahia kama matokeo.

Ndugu zangu wapendwa, marafiki zangu wapendwa, kutakuwa na nyakati ambapo unafikiria huwezi kusimama au kuendelea. Tafadhali amini Mwokozi na upendo Wake. Kwa imani katika Bwana Yesu Kristo, uwezo na matumaini ya injili ya urejesho, utaweza kutembea vima na kuendelea mbele.

Ndugu, tunawapenda. Sisi tunawaombea. Mimi natamani ninyi mngemsikia Rais Monson akiwaombea ninyi. Hata kama wewe ni baba kijana, mwenye ukuhani mkongwe, au shemasi aliyetawazwa majuzi, sisi tunawajali nyinyi. Bwana anawajali ninyi!

Tunatambua kwamba njia yenu nyakati zingine itakuwa na ugumu. Lakini mimi nitawapatia ahadi hii katika jina la Bwana: inuka na ufuate hatua za Mkombozi na Mwokozi wetu, na siku moja tutatazama nyumba na kujawa na shukrani za milele kwamba ulichagua kutumainia Upatanisho na nguvu zake za kukuinua na kukupatia nguvu.

Rafiki na ndugu zangu wapendwa, bila kujali mara ngapi mmeteleza au kuanguka, “Inuka! Kudra yenu ni tukufu! Simama vima na utembee katika nuru ya injili ya urejesho ya Yesu Kristo! Ninyi mna nguvu sana kuliko mnavyojua. Ninyi mna uwezo kuliko mnavyofikira. Mnaweza kutenda hivyo sasa! Juu ya haya mimi nashuhudia katika jina takatifu la Bwana na Mkombozi wetu,Yesu Kristo, amina.