Ruka uongozaji mkuu
Aprili 2014 | Kufuatilia

Kufuatilia

Aprili 2014 Mkutano Mkuu

Tunaweza sote kuwa na uthabiti zaidi katika kujuhusisha na kazi ya umisionari kuwa kubadilisha uoga wetu na imani ya kweli

Miaka sitini na nne iliyopita Septemba hii nilirudi nyumbani kutoka kwenye huduma ya umisheni Uingereza. Siku tatu baada ya kurudi nilihudhuria densi ya Hello Day katika Chuo Kikuu cha Utah na rafiki yangu. Aliniambia kuhusu msichana mrembo wa mwaka wa pili chuoni aliyeitwa Barbara Bowen ambaye alifikiria ni lazima nikutane naye. Alimleta kwangu na kututambulisha, na tukaanza kucheza densi.

Kwa bahati mbaya, hii ndio tuliyozoea kuiita “kucheza kwa kidali,” inayomaanisha kwamba ulipata nafasi ya kucheza na msichana mpaka mtu akuguse begani na kucheza na msichana uliyekuwa unacheza naye. Barbara alikuwa mcheshi na anayejulikana, hivyo niliweza kucheza naye chini ya dakika moja kabla ya kijana mwingine aliponigusa begani na kunitoa.

Hiyo ilikuwa inakubalika kwangu. Nikiwa nimejifunza somo la kufuatilia katika misheni, Nilichukua namba yake ya simu na nikampigia simu siku iliyofuata kumuomba kwenda katika miadi nami, lakini alikuwa na majukumu mengine shuleni pamoja na marafiki zake. Cha kushukuru misheni yangu ilinifundisha kutokata tamaa hata katika nyakati za kukata tamaa, mwishowe nilipata nafasi kupata miadi naye. Mazungumzo hayo yalielekezea kwenye mazungumzo mengine. Kwa kiasi fulani wakati wa mazungumzo hayo niliweza kumshawishi kwamba nilikuwa ndio mmisionari aliyerejea wa pekee wa ukweli na anayeishi—angalau, kwa mtazamo wake. Sasa hivi, miaka 64 baadaye, kuna watoto saba, na wajukuu na vitukuu wengi ambao wanasimama kama ushahidi wa ukweli muhimu kwamba haijalishi ujumbe wako ni mzuri kiasi gani, huwezi kupata nafasi ya kuugeuza bila msimamo, kufuatilia kwa kung’ang’aniza.

Hii inaweza kuwa ndiyo sababu nimepata msukumo wa kufuatilia leo kwenye mbili kati jumbe zangu za mikutano mikuu wa awali.

Katika Mkutano wa Oktoba 2011, Niliomba kwamba tukumbuke maneno haya muhimu ya Bwana: “Kwani hivyo ndivyo kanisa langu litakavyoitwa katika siku za mwisho, hata Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho.”1

Kwa maneno haya, Bwana anafanya bayana kwamba hii siyo tu kichwa cha habari cha kawaida lakini pia jina ambalo Kanisa Lake litajulikana. Kwa sababu ya tamko Lake la wazi, tusiliite kanisa kwa majina mengine, kama vile “Kanisa la Mormon” au “Kanisa la LDS.”

Neno Mormoni linaweza kutumiwa kiusahihi katika muktadha kuwaita washiriki wa Kanisa, kama vile waanzilishi wa Mormoni, au kwenye asasi kama vile Kwaya ya Mormon Tabernacle. Washiriki wa kanisa wanajulikana sana kama Wamormoni na katika mabadilishano na wale wasio wa imani yetu tunaweza kiusahihi kujitambulisha kama Wamormoni mradi kwamba tunaunganisha hili na jina kamili la kanisa.

Kama washiriki watajifunza kutumia jina sahihi la Kanisa katika muunganiko wa neno Mormoni, itasisitiza kuwa sisi ni wakiristo, washiriki wa Kanisa la Mwokozi.

Ndugu na kina dada, na tufuatilie na kukuza tabia ya kuweka bayana kwamba sisi ni washiriki wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho.

Ujumbe wa pili ambao nahisi lazima niufuatilie ulitolewa katika mkutano mkuu uliopita nilipowapa moyo washiriki kuomba ili waweze kuongozwa kwa angalau mtu mmoja ambaye watamualika kujifunza kuhusu injili iliyorejeshwa kabla ya Krisimas. Washiriki wengi wa Kanisa wameshirikiana nami ujuzi maalumu ambalo limetokana na kuomba kwao kwa Bwana kwa ajili ya fursa za Umisionari.

Mmoja kati ya wamisionari waliorejea, kwa mfano, alisali kwa makusudi kuongozwa kwa mtu ambaye anaweza kumfikia. Jina la mmoja wa wanafunzi wenzake waliyeenda naye chuo lilimjia akilini. Aliwasiliana naye kupitia Facebook, na akagundua kwamba alikuwa akiomba kwa madhumuni na maana katika maisha yake. Alimfuatilia kwa wakati alipokuwa akitafuta ukweli, na mnamo Desemba alibatizwa.

Mialiko mingi ya aina hii iliripotiwa kwangu, lakini michache tu ndio imefuatiliwa kama vile huyu ndugu alivyofuatilia.

Naamini sana katika kanuni ya kufuatilia. Kama inavyosema kwenye mwongozo wa umisionari Hubiri Injili Yangu,, “kutoa mwaliko bila kufuatilia ni kama kuanza safari bila kumalizia au kununua tiketi kwenda kwenye tamasha bila kwenda kwenye ukumbi. Bila kumalizia tendo, ahadi inakuwa haina maana.”2

Hubiri Injili Yangu inamfundisha kila mtu siyo tu jinsi ya kutoalika pekee lakini pia jinsi ya kufuatilia katika mialiko yetu. Dhumuni la kazi ya umisionari inaelezewa kama kualika “wengine kuja kwa Kristo kwa kuwasaidia wengine kupokea injili iliyorejeshwa kupitia imani katika Yesu Kristo na Upatanisho Wake, toba, ubatizo, kupokea karama ya Roho Mtakatifu, na kuvumilia hadi mwisho.”3

Kualika hakika ni sehemu ya mchakato. Lakini gundua kwamba kuna zaidi ya kazi ya umisionari kwa washiriki zaidi ya kutoa mialiko tu kwa watu kuwasikiliza wamisionari. Inajumuisha pia kufuatilia na wamisionari katika kupalilia imani, kutoa motisha katika toba, maandalizi kwa ajili ya kufanya maagano na kuvumilia hadi mwisho.

Kanuni ya kufuatilia imeonyeshwa katika kitabu cha Matendo ya Mitume:

“Basi Petro na Yohana walikuwa wakikwea pamoja kwenda hakaluni. …

“Na mtu mmoja aliyekuwa kiwete toka tumboni mwa mamaye alichukuliwa na watu, ambaye walimweka kila siku katika mlango wa hekalu uitwao Mzuri, ili aombe sadaka kwa watu waingiao ndani ya hekalu;

“Mtu huyo akiwaona Petro na Yohana wakiingia hekaluni aliomba apewe sadaka.

“Na Petro, akimkazia macho, pamoja na Yohana, akasema, Tutazame sisi.

“Akawaangalia, akitarajia kupata kitu kwao.

“Lakini Petro akasema, Mimi sina fedha, wala dhahabu, lakini nilicho nacho ndicho nikupacho: Kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareti, simama uende.”

Huo ni mwaliko wenye nguvu sana kutoka kwa mtumishi wa Bwana, sivyo? Lakini Petro hakusita kualika. Ufafanuzi wa maandiko baadaye unatuambia kwamba “alimchukua kwa mkono wake wa kulia, na kumuinua: na mara mara nyayo zake na vifundo vya miguu yake vikatiwa nguvu.

“Akaondoka upesi akasimama, akaanza kwenda, akaingia ndani ya hekalu pamoja nao, akienda, akiruka ruka, na kumsifu Mungu.”4

Kwa maneno mengine, Petro hakutumia tu mamlaka ya ukuhani wake na kumwalika mtu huyu kuamka na kutembea. Vile vile alifuatilia kwenye mwaliko wake kwa kumwendea mwanaume, akimchukua kwa mkono wake wa kuume, akamwinua, na kisha kutembea naye kwenda hekaluni.

Katika roho ya mfano wa Petro, napendekeza kwamba wote tunaweza kuhusika kila mara katika kazi ya umisionari kwa kubadilisha woga na imani halisi, kumwalika mtu angalu mara moja katika miezi mitatu –-mara nne kila mwaka –kufundishwa na wamisionari. Wako tayari kuwafundisha kwa Roho na kwa mwongozo wa kiungu kutoka kwa Bwana. Kwa pamoja tunaweza kufuatilia mialiko yetu kuwashika wengine mkono, kuwainua na kutembea nao katika safari ya kiroho.

Ili kuwasaidia katika mchakato huu, nawaalika washiriki wote, bila kujali miito yenu ya sasa au kiwango cha shughuli katika Kanisa, kupata nakala ya Hubiri Injili Yangu. Inapatika kwenye vituo vya huduma na pia kwenye mtandao. Toleo la mtandao linaweza kusomwa au kupakuliwa bila kulipa. Ni mwongozo kwa kazi ya umisionari –ambayo humaanisha ni mwongozo kwetu sisi wote. Kisome, jifunze, na baadaye kufanyia kazi yale uliyojifunza kukusaidia kuelewa jinsi ya kuleta roho kwa Kristo kupitia mwaliko na kufuatilia. Kama Rais Thomas S. Monson alivyosema, “Sasa ni wakati wa washiriki na wamisionari kuja pamoja, kufanya kazi pamoja, kufanya kazi katika shamba la Mzabibu la Bwana kuleta roho kwake.”5

Yesu Kristo alifundisha wafuasi Wake:

“Mavuno kweli ni mengi, lakini wafanyakazi ni wachache;

“Salini basi Bwana wa mavuno, ili atume wafanyakazi katika mavuno yake.”6

Bwana amejibu maombi ya sala hiyo katika siku hizi kwa idadi kubwa ya wamisionari katika historia ya dunia. Katika mwongezeko huu wa wafanyakazi waadilifu, Bwana ametupa fursa nyingine kumsaidia katika haya mavuno makuu ya nafasi.

Kuna njia kwa washiriki kusaidia na kuunga mkono wamisionari wetu wachapakazi. Kwa mfano, unaweza kuwambia wamisionari kwamba unajifunza Hubiri Injili Yangu na kuwauliza kukuonyesha kile wanachojifunza katika kujifunza kwao. Unaposhirikiana nao, ujasiri ulioongezeka kati ya washiriki na wamisionari utakua, kama Bwana alivyoamuru:

“Bali kwamba kila mwanadamu aweze kuongea katika jina la Mungu Bwana, hata Mwokozi wa ulimwengu.”7

Na “Tazama, nimewatuma ninyi kwenda kushuhudia na kuwaonya watu, na ni wajibu wa kila mtu ambayo ameonywa amwonye jirani yake.”8

Ndugu na kina dada, unaweza kufikiria matokeo kama familia na marafiki watajumuisha vitu wanavyojifunza kutoka katika kujifunza kibinafsi katika Hubiri Injili Yangukatika barua na barua pepe za wamisionari? Unaweza kupata taswira ya baraka ambazo huja kutoka kwa familia wanapojua na kuelewa vizuri kwamba watoto wao wa kike kwa wa kiume watajifunza na kufundisha wakiwa kwenye misheni? Na unaweza kufikira baraka za ajabu kwenye rehema ya upatanisho ambayo itakuwa yetu, binafsi na kama kundi, kulingana na ahadi ya Mwokozi kwa wote wanaoshuhudia katika mchakato wa kualika nafsi kuja Kwake—na baadaye kufuatilia kwenye mialiko hiyo.

“Mmebarikiwa ninyi,” Bwana alisema kupitia Nabii Joseph Smith, “ kwani shuhuda zenu mlizozitoa zimeandikwa mbinguni ili malaika wazione; nao hufurahia juu yenu, na dhambi zenu zimesamehewa.”9

“Kwani nitawasamehe dhambi zenu kwa mara hii –kwamba ninyi muendelee kuwa thabiti …katika kutoa ushuhuda kwa walimwengu wote kwa yale mambo yote ambayo yamejulishwa kwenu.”10

Kama tukifuatilia, Bwana hatatuacha. Nimeona furaha ambayo ni kubwa sana kuielezea ambayo inajumuisha mwaliko unaosukumwa na ushuhuda na kufuatilia kiuaminifu miongoni mwa washiriki wa Kanisa duniani kote. Nikiwa Argentina hivi karibuni, niliwatia moyo washiriki kumwalika mtu mmoja kanisani kabla ya mkutano mkuu huu. Mtoto wa miaka minane anayeitwa Joshua alinisikiliza na akamwalika rafiki yake mpendwa na familia yake kwenye ufunguzi wa jumba katika kata yao pale Buenos Aires. Niruhusu nisome kutoka kwenye barua niliyoipokea punde ambayo inaelezea mwaliko wa Joshua na ufuatiliaji wake wa kiaminifu:

“Kila baada ya dakika chache [Joshua] alikimbia nje na kuona kama kuna mtu alikuwa anakuja. Alisema kwamba alijua kwamba wangekuja.

Jioni iliendelea kupita na rafiki ya Joshua hakuja, lakini Joshua hakukata tamaa. Kwa imani akaangalia mlango wa mbele kila dakika. Ilikuwa ni wakati wa kuanza kuweka kando wakati Josuha alipoanza kuruka ruka na kusema, ‘ Wamefika, Wamefika! Niliangalia na kuona familia nzima wakitembea kuelekea kanisani. Joshua alikimbia kwenda kuwalaki na kumkumbatia rafiki yake. Wote waliingia ndani na wakaonekana kufurahia sana ufunguzi wa jumba. Wakachukua vipeperushi na wakatumia mda mwingi wakisalimiana na kujuana na watu wengine na marafiki wapya. Ilikuwa ni vizuri kuona imani ya kijana huyu na kujua kwamba Watoto wa Msingi wanaweza kuwa Wamisionari pia.”11

Ni ushuhuda wangu kwamba tupojitahidi kutenda upande wetu, tukimtafuta mtu wa kushiriki naye injili, kuwaalika, na kufuatilia kwa imani, Bwana atatufurahia sisi na mamia ya maelfu ya watoto wa Mungu wataona maana na amani katika Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho. Na Mungu atubariki sote katika juhudi za kuharakisha kazi hii ya wokovu, ninaomba kwa unyenyekevu, katika Jina la Yesu Kristo, amina.

Onesha KumbukumbuFicha Kumbukumbu