2010–2019
Kuweka Maagano Hutulinda, Hutuandaa, na Hutupa Nguvu
Aprili 2014


Kuweka Maagano Hutulinda, Hutuandaa, na Hutupa Nguvu

Sisi ni mwanawake wa kuweka maagano katika vizazi vyote tukitembea katika mapito ya maisha ya muda tukirudi tena katika uwepo Wake.

Eh, kina dada, sisi tunawapenda ninyi. Hivi majuzi nilipokuwa nikizuru Mexico, niliweza kupata tazamo la wakati mfupi la udada tunaouhisi jioni hii. Fikiria maandhari haya: Tukikuwa tu tumemaliza darasa la Msingi Jumapili asubuhi na watoto, walimu, na mimi tulikuwa tumejaa hata katika ukumbi uliokuwa umejaa watu. Punde tu mlango wa darasa la Wasichana ukafunguliwa na niliwaona wasichana na viongozi wao. Sote tulikwenda kuwakumbatia. Kukiwa na watoto wakiwa wameshikilia sketi yangu na wanawake wakiwa wamenizunguka, nilitaka kuwaonyesha hisia nilizokuwa nazo wakati huo.

Sizungumzi Kihispania, hivyo maneno ya kiingereza tu ndio yalikuja akilini mwangu. Nilitazama katika nyuso zao na kusema, “Sisi ni mabinti wa Baba yetu wa Mbinguni, anayetupenda, na tunampenda.” Kila mmoja mara moja akaungana, katika Kihispania. Pale tulikuwepo kwenye ukumbi uliojaa, tukirudia pamoja kauli mbiu ya Wasichana tulipoosema, “Tutasimama kama mashahidi wa Mungu nyakati zote na katika kila kitu, na katika kila mahali.”

Usiku wa leo tunakusanyika duniani kote kama waduasi Wake, tukiwa na hamu ya kutetea na kuidhinisha ufalme wa Mungu. Sisi ni mabinti wa Baba yetu wa Mbinguni. Sisi ni wanawake tunaoweka maagano kwa vipindi vyote tukitembea katika njia hii ya maisha ya muda kurudi katika uwepo Wake. Kuweka maagano hutulinda, hutuandaa, na hutupa nguvu.

Kuna wasichana kati yetu jioni hii ambao wako kwenye umri wa Msingi. Baadhi yenu hivi majuzi mmechukua hatua hiyo ya kwanza katika njia ya uzima wa milele kwa agizo la ubatizo.

Hebu angalia kote. Siku za usoni ni angavu unavyowaona wanawake ambao pia wamefanya maagano na wako tayari kuwaonyesheni njia katika mapito huko mbele.

Kama una miaka 8, 9, 10 au 11, iwe uko katika Kituo cha Mikutano hiki, majumbani mwenu, au katika nyumba za mikutano duniani kote, mnaweza kusimama? Karibuni katika mkutano mkuu wa wanawake. Sasa tafadhali endeleeni kusimama kwa sababutunataka kuwaalika jioni hii mshiriki. Nitaimba bila kutoa sauti wimbo wa watoto wa msingi. Mara tu mnapotambua tuni, anzeni kuimba pamoja na mimi. Sasa, lazima muimbe kwa sauti ili kila mmoja aweze kusikia.

Nifundishe kutembea katika nuru ya upendo wake;

Nifundishe kuomba kwa Baba yangu aliye juu;

Nifundishe kujua kuhusu mambo yaliyo sahihi;

Nifundishe, nifundishe kutembea kwenye nuru.

Bakini mmesimama, wasichana, wakati kila mmoja wenu miaka 12 kwenda juu mnapoimba ubeti wa pili.

Njooni, watoto wadogo, na pamoja tutajifunza

Kuhusu amri zake, ili tuweze kurudi

Nyumbani kwenye uwepo wake, kuishi katika mbele zake---

Daima, daima kutembea katika nuru.1

Hiyo imekuwa maridadi. Mnaweza kuketi chini. Asanteni.

Wanawake wa miaka yote tunapotembea katika nuru Yake. Safari yetu katika njia hii ni ya kibinafsi na imeangazwa vyema na upendo wa Mwokozi.

Tunaingia katika lango kwenye njia ya uzima wa milele na agizo na maagano ya ubatizo, na baadaye tunapokea kipawa cha Roho Mtakatifu. Mzee Robert D. Hales anatuuliza, “[Sisi] Tunaelewa na kufanya watoto [wetu] waelewe kwamba [sisi] tunapobatizwa [sisi] tunabadilishwa milele?”

Pia alielezea kwamba “tunapoelewa maagano yetu ya ubatizo na karama ya Roho Mtakatifu, itabadilisha maisha yetu na kuweka utii wetu kamili kwa ufalme wa Mungu. Pale majaribu yanapotujia, kama tutasikiliza, Roho Mtakatifu atatukumbusha kwamba tumeahidi kumkumbuka Mwokozi na kutii amri za Mungu.”2

Kila wiki tunapokea nembo za sakramenti, tunalifanya upya agano la ubatizo. Mzee David A. Bednar alisema: “Tunaposimama kwenye maji ya ubatizo, tunaliangalia hekalu. Tunapokea sakramenti, tunaelekeza mawazo yetu hekaluni. Tunaahidi kwamba tutamkumbuka Mwokozi daima na kutii amri Zake kama maandalizi ya kushiriki katika maagizo matakatifu ya Hekalu.”3

Maagizo ya hekaluni yanatuongoza kwenye baraka kubwa zilizo katika Upatanisho wa Yesu Kristo. Ndiyo yale maagizo muhimu kwa ajili ya uinuliwaji wetu katika ufalme wa selestia. Tunapojitahidi kuweka maagano yetu, hisia zetu za mapungufu na kutokamilika zinaanza kufifia, hali maagizo na maagano ya hekaluni yanakuwa imara zaidi. Kila mtu anakaribishwa kutembea katika mapito hayo ya uzima wa milele.

Ninashangazwa na nguvu ya mabinti, wasichana, na wanawake niliokutana nao duniani kote ambao wanaishi kulingana na maagano waliyoyaweka. Naomba nishiriki nanyi baadhi ya mifano ya wasichana na wanawake wa maagano niliokutana nao.

Luana alikuwa na umri wa miaka kumi na moja nilipotembelea familia yake huko Buenos Aires, Agentina. Kwa sababu ya matukio ya kutisha katika utoto wake, Luana hakuweza kuzungumza. Alikuwa hajawahi kuzungumza kwa miaka mingi. Alikaa kimya tulivyokuwa tunaongea. Niliendelea kutumaini hata kwa mnong’ono kutoka kwake. Aliniangalia kwa umakini kama vile kutoa maneno kulikuwa si kwa muhimu sana kwa mimi kuelewa moyo wake. Baada ya maombi, tulisimama kuondoka na Luana akanipa mchoro. Alikuwa amemchora Yesu Kristo katika bustani ya Gethsemane. Baadaye niligundua ushuhuda wake kwa sauti sahihi ingawa hakusema kitu. Luana alikuwa amefanya maagano wakati wa ubatizo wake kusimama kama shahidi wa Mungu “kwa nyakati zote na kwa kila kitu na kila mahali.”4 Alielewa Upatanisho wa Yesu Kristo akaushuhudia kupitia mchoro wake. Angelijua hilo, kupitia kuimarishwa na nguvu ya uwezeshwaji ya Upatanisho, angeponywa na kuzungumza tena? Tokea kipindi hicho miaka mitatu iliyopita, Luana amepiga hatua katika juhudi zake za kuzungumza. Sasa anashiriki katika mipango ya wasichana pamoja na marafiki zake. Akiwa na imani katika maagano yake aliyoyafanya wakati wa ubatizo, anaendelea kushirikiana kwenye ushuhuda wake wa Mwokozi.

Vijana duniani kote wanavutiwa na mahekalu. Kule Lima, Peru, nilikutana na baba na binti zake watatu nje ya lango la hekalu. Niliona ni jinsi gani walivyokuwa wamejawa na furaha. Wawili kati ya binti hao walikuwa na ulemavu mkubwa na walikuwa wamekaa katika viti vya magurudumu. Binti wa tatu, wakati akisaidia mahitaji ya dada yake, alielezea kwamba alikuwa na dada wawili nyumbani. Na hao pia walikuwa katika viti vya magurudumu. Hawakuwa na uwezo wa kusafiri kwa masaa 14 kuja hekaluni. Na hekalu lilimaanisha kitu kikubwa kwa baba huyu na binti hawa kwamba wote wanne walikuwa wamekuja hekaluni siku hiyo—wawili wao kuangalia tu yule ambaye anaweza kubatizwa kwa ajili ya wafu na kufanya agizo takatifu. Kama Nefi, “wanafurahia katika maagano ya Bwana.”5

Mwanamke ambaye hajaolewa ninayemfahamu anathamini agizo la kila wiki la sakramenti na ahadi zake takatifu “ili daima Roho wake apate kuwa pamoja [naye].”6 Huo uenzi daima ni ahadi ambayo inalainisha mawimbi ya upweke wake. Unampa nguvu ya kujihusisha katika kukuza vipaji na hamu ya kumtumikia Bwana. Amegundua furaha kubwa katika kuonyesha upendo katika watoto wote katika maisha yake, na anapotafuta amani tulivu, utamkuta hekaluni.

Mwisho, mwanamke mzee akiwa katika miaka ya 90 amewaona watoto wake na wajukuu wakikua na vitukuu wakija duniani. Kama wengi wetu, amekuwa na maisha yaliyojawa huzuni, mateso, na furaha isiyofikirika. Anakiri kwamba kama angekuwa anaandika historia yake ya maisha tena, asingechagua kujumuisha baadhi ya sura ambazo zimeandikwa. Bado, kwa tabasamu, anasema, “Lazima nikae angalau kidogo tena kuona jinsi itakavyokuwa!” Anaendeleakushikilia kwa nguvu maagano katika mapito haya.

Nefi alifundisha:

“Baada ya kuingia katika njia hii nyembamba iliyosonga, nauliza je yote yamekamilishwa? Tazama nawaambia, Hapana. …

“Kwa hivyo, Lazima msonge mbele mkiwa na imani imara katika Kristo, mkiwa na mng’aro mkamilifu wa tumaini, na upendo kwa Mungu na wanadamu wote. Kwa hivyo, kama mtasonga mbele, mkila na kusherehekea neno la Kristo, na mvumilie hadi mwisho, tazama, hivi ndivyo asema Baba: Mtapokea uzima wa milele.” 7

Kila mmoja wetu yuko kwenye mapito hayo. Jioni hii, tumeimba kuhusu kuitembea njia ya nuru. Kama watu binafsi, tuna nguvu. Pamoja na Mungu, sisi hatuzuiliki.

Bwana akamwambia Emma Smith, “Inua moyo wako na ufurahie, na yashikilie maagano ambayo umeyafanya.”8

Tunafurahia kwamba kupitia kuweka maagano yetu tunaweza kuhisi upendo wa Baba yetu wa Mbinguni na Mwokozi wetu, Yesu Kristo. Nashuhudia kwamba Wao wanaishi. Katika jina la Yesu Kristo, amina.