Ruka uongozaji mkuu
Aprili 2014 | Ishi Mkweli kwa Imani

Ishi Mkweli kwa Imani

Aprili 2014 Mkutano Mkuu

Kila mmoja wetu atabarikiwa sana kama tutajua hadithi za imani na kujitolea ambazo ziliwaelekeza mababu zetu kujiunga na Kanisa la Bwana.

Mimi naipenda historia ya Kanisa. Labda kama wengi wenu, imani yangu inaimarishwa wakati ninapojifunza kujitolea kwa ajabu kwa mababu zetu ambao walikubali na kuishi kwa ukweli kwa imani.

Mwezi mmoja uliopita, vijana 12,000 wa ajabu kutoka Wilaya ya Hekalu la Gilbert Arizona walisherehekea kumalizika kwa hekalu lao jipya kwa maonyesho yenye maongozi, kuonyesha sharti lao la kuishi kwa wema. Mada ya sherehe zao ilikuwa “Kuishi Mkweli kwa---Imani.”

Kama vile wale vijana waaminifu wa Arizona walivyofanya, kila Mtakatifu wa Siku za Mwisho anapaswa kuweka sharti la “kuishi mkweli kwa imani.”

Maneno ya wimbo yanasema, “Mkweli kwa imani ambayo wazazi wetu wameitunza” (“True to the Faith,” Hymns, no. 254).

Tunaweza kuongeza, “Kweli kwa imani ambayo mababu zetu wameitunza”

Nilishangaa kama kila mmoja wa wale vijana wenye shauku wa Arizona walijua historia yao wenyewe ya Kanisa, kama walijua historia ya jinsi familia zao zilivyokuja kuwa washiriki wa Kanisa. Ingekuwa kitu kizuri sana kama kila Mtakatifu wa Siku za Mwisho angejua hadithi za uongofu wa mababu zao.

Iwe au isiwe kuwa wewe ni uzao wa watangulizi, urithi wa watangulizi Wamormoni wa imani na dhabihu ni urithi wako. Ni urithi mtukufu wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho.

Mojawapo wa sura za ajabu sana katika historia ya Kanisa zilitokea wakati Wilford Woodruff, Mtume wa Bwana, alikuwa anafundisha injili ya urejesho ya Yesu Kristo kote katika uingereza katika mwaka wa 1840---miaka 10 tu baada kuanzishwa kwa Kanisa.

Wilford Woodruff na mitume wengine walizingatia kazi zao katika maeneo ya Liverpool, na Preston ya Uingereza, wakiwa na ufanisi mkubwa. Mzee Woodruff, ambaye baadaye alikuwa Rais wa Kanisa, alikuwa daima anaomba kwa Mungu ili amwongoze katika kazi hii muhimu sana. Maombi yake yalileta maongozi ya kuenda sehemu tofauti kufunza injili.

Rais Monson ametufunza sisi kwamba tunapopata maongozi kutoka mbinguni kufanya kitu---tukifanya sasa---tusihairishe. Hivyo ndivyo Wilford Woodruff alifanya. Kwa mwelekeo wazi kutoka kwa Roho “nenda kusini,” Mzee Woodruff karibu aliondoka mara moja na kusafiri hadi sehemu ya Uingereza iliyoitwa Herefordshire---nchi ya kilimo kusini magharibi mwa Uingereza. Huko alikutana na mkulima mfanisi aliyeitwa John Benhow, ambapo alikaribishwa “kwa mioyo mikunjufu na shukrani” (Wilford Woodruff, in Matthias F. Cowley, Wilford Woodruff: History of His Life and Labors as Recorded in His Daily Journals [1909], 117).

Kundi la zaidi ya watu 600, ambao walijiita United Brethren, walikuwa “wakiomba wapate nuru na ukweli” (Wilford Woodruff, in Teachings of Presidents of the Church: Wilford Woodruff [2004], 91). Bwana alimtuma Wilford Woodruff kama jibu la maombi yao.

Mafundisho ya Mzee Woodruff yalizaa matunda mara moja, na wengi walibatizwa. Brigham na Willard Richards walijiunga naye katika Herefordshire, na hawa Mitume watatu walipata ufanisi wa ajabu.

Katika miezi michache tu, walianzisha matawi 33 kwa washiriki 541 ambao walikuwa wamejiunga na Kanisa. Kazi yao ya ajabu, na mwishowe karibu kila mmoja wa washiriki wa United Brethren alibatizwa katika Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho.

Bibi yangu mkuu, mkuu, Hannah Maria Eagles Harris alikuwa mmoja kati ya wa kwanza kumsikiliza Wilford Woodruff. Alimwambia mmewe, Robert Harris Jr., kwamba alikuwa amesikia neno la Mungu na kwamba alikuwa na nia ya kubatizwa. Robert hakupendezwa na kusikia habari za mke wake. Alimwambia yeye angeambatana naye katika mahubiri yaliyofuata yatayotolewa na mmisionari wa kimormoni, na akamnyoroshe.

Akiketi karibu na mbele ya umati, kwa azimio thabiti la kutoyumba, na labda kumpigia mhubiri mtembezi kelele, Robert mara moja aliguswa na Roho, kama vile mke wake alikuwa ameguswa. Alijua ujumbe wa Urejesho ulikuwa ni kweli, na yeye na mkewe walibatizwa.

Hadithi yao ya imani na kujitolea kwao ni sawa na kwa maelfu ya wengine: waliposikia ujumbe wa injili, walijua ilikuwa ni kweli!

Kama vile Bwana anavyosema, “Kondoo wangu waisikia sauti yangu; nami nawajua, nao wanifuata (Yohana 10:27).

Baada ya kusikia sauti ya Mchungaji, wao kikamilifu walitia sharti maisha yao kuishi injili na kufuata maelekezo ya nabii wa Bwana. Kujibu wito wa “kukusanyika katika Sayuni,” wao waliacha nyuma nyumba zao katika Uingereza, wakavuka Atlantiki, na kukusanyika pamoja na Watakatifu wengine katika Nauvoo, Illinois.

Wao walikumbatia injili kwa mioyo yao yote. Wakati wakijaribu kujiendeleza katika nchi yao mpya, walisaidia katika ujenzi wa Hekalu la Nauvoo kwa kutoa zaka kwa kazi zao---kutumia kila moja kwa kumi ya siku wakifanya katika ujenzi wa hekalu.

Walivunjika moyo kwa habari za kifo cha nabii wao mpendwa, Joseph Smith, na kaka yake Hyrum. Lakini walisonga mbele! Walikaa wakweli kwa imani.

Wakati Watakatifu walipokuwa wanateswa na kufurushwa kutoka Nauvoo, Robert na Maria walihisi kubarikiwa sana kupokea endaumenti zao katika hekalu, muda mfupi kabla ya kuvuka Mto Mississippi na kuelekea magharibi. Ingawa walikuwa hawana uhakika wa siku za usoni, walikuwa na hakika juu ya imani yao na shuhuda zao.

Wakiwa na watoto sita, walitembea kwa bidii katika matope walipokuwa wakivuka Iowa hadi upande wao wa magharibi. Walijijengea mahali pa kukaa katika ukingo wa Mto Missouri ambapo palikuja kujulikana kama Winter Quarters.

Hawa watangulizi wajasiri walikuwa wanangojea kwa maelekezo ya kiutume juu jinsi wangeelekea mbele magharibi. Mipango ya kila mtu iliguezwa wakati Brigham Young, Rais wa Jamii ya Mitume Kumi na Wawili, alitoa wito kwa wanaume na wanawake kuhudumu katika Jeshi la Marekani iliyokuja kujulikana kama Mormon Battalion.

Robert Harris Jr. alikuwa mmoja wa watangulizi Wamormoni 500 ambao waliitika mwito huo kutoka kwa Brigham Young. Alijiunga na jeshi, hata ingawa ilimaanisha angamwacha mkewe mjamzito na watoto sita wadogo.

Kwa nini yeye na wanaume wengine wafanye kitu kama hicho?

Jibu linaweza kutolewa na maneno ya babu yangu mkuu, mkuu. Katika barua ambayo aliandika kwa mkewe wakati batalioni ilisimama ikielekea Santa Fe, aliandika, “Imani yangu imeimarika sana kuliko hapo awali [na wakati mimi ninafikiria vitu Brigham Young alitwambia], mimi naamini kuvihusu kama vile Mungu Mkuu angeniambia mimi.”

Kwa ufupi, alijua yeye alikuwa anasikiliza nabii wa Mungu, kama vile wanaume wengine walivyokuwa wanafanya. Hii ndiyo sababu walifanya hivyo! Walijua wao walikuwa wanaongozwa na nabii wa Mungu.

Katika barua hiyo, alionyesha hisia nyororo kwa mke wake na watoto na kuwaambia juu ya maombi yake ya kila siku kwamba yeye na watoto wangebarikiwa.

Baadaye katika barua alitoa kauli ya nguvu sana: “Sisi ni sharti tusisahau vitu ambayo wewe nami tulivisikia na kuviona katika Hekalu la Bwana.”

Ikijumulishwa na ushuhuda wake wa awali kwamba “walikuwa wanaongozwa na Nabii wa Mungu,” haya maonyo mawili yamekuwa kama maandiko kwangu.”

Miezi kumi na nane baada ya kuondoka na batalioni, Robert Harris aliungana tena salama na mpendwa wake Maria. Wao walikaa wakweli na waaminifu kwa injili iliyorejeshwa katika maisha yao yote. Wao walikuwa na watoto 15, 13 kati yao waliishi hata uzee wao. Bibi yangu Fannye Walker, wa Raymond, Alberta, Kanada, alikuwa mmoja wa wajukuu wao 136.

Bibi Walker alikuwa anajivunia jambo kwamba babu yake alikuwa amehudumu katika Batalioni ya Wamormoni, na alikuwa anataka wajukuu wake wote wajue hivyo. Sasa kwamba mimi ni babu, naelewa kwa nini ilikuwa ni muhimu hivyo kwake. Alitaka kugeuza mioyo ya watoto kwa baba. Alitaka wajukuu wake kujua urithi wao wa haki---kwa sababu alijua itabariki maisha yao.

Jinsi tunavyohisi kuunganishwa sana na mababu zetu wema, ndivyo zaidi tutafanya chaguo za hekima na haki.

Na hivyo ndivyo ilivyo. Kila mmoja wetu atabarikiwa sana kama sisi tunajua hadithi za imani na dhabihu zilizowaelekeza mababu zetu kujiunga na Kanisa la Bwana.

Kutoka wakati wa kwanza Robert na Maria walimsikia Wilford Woodruff akifunza na kushuhudia juu ya Urejesho wa injili, walijua injili ilikuwa kweli.

Wao pia walijua kwamba bila kujali kile majaribio au shida zingekuja kwao, wao wangebarikiwa kwa kuwa wakweli kwa imani. Ilionekana kabisa kwamba walikuwa wamesikia maneno ya nabii wetu leo, ambaye amesema, “Hamna dhabihu iliyo kuu sana … katika kupokea baraka [za hekalu]” (Thomas S. Monson, “The Holy Temple—a Beacon to the World,” Ensign orLiahona, May 2011, 92).

Sarafu ya pauni mbili ya Uingereza imechorwa upande mmoja, “Kusimama juu ya Mabega ya Majitu.” Ninapofikiria juu ya mababu zetu watangulizi wakuu, ninahisi kwamba sisi sote tunasimama juu ya mabega ya majitu.

Ingawa maonyo haya yalikuja kutoka kwa barua ya Robert Harris, mimi naamini kwamba mababu wasiohesabika wangetuma ujumbe huo huo kwa watoto wao na wajukuu wao: Kwanza, sisi sharti tusisahau uzoefu tuliopata katika hekalu, na sisi sharti tusisahau ahadi na baraka ambazo zinakuja kwa kila mmoja wetu kwa sababu ya hekalu. Pili, sisi sharti tusisahau kwamba tunaongozwa na nabii wa Mungu.

Mimi nashuhudia kwamba sisi tunaongozwa na nabii wa Mungu. Bwana alirejesha Kanisa Lake katika siku za mwisho kupitia kwa Nabii Joseph Smith, na sisi sharti tusisahau kwamba tumeongozwa na mnyororo usiovunjika wa manabii wa Mungu kutoka kwa Joseph hadi kwa Brigham na kupitia katika kila Rais wa Kanisa aliyefuata hadi kwa nabii wetu leo---Thomas S. Monson. Mimi namjua yeye, mimi namheshimu yeye, na mimi nampenda yeye. Mimi nashuhudia kwamba yeye ni nabii wa Bwana ulimwenguni leo.

Ni hamu ya moyo wangu kwamba, pamoja na watoto wangu na wajukuu, sisi tutaheshimu urithi wa mababu zetu wema---wale watangulizi Wamormoni waaminifu ambao walikuwa tayari kuweka kila kitu kwenye madhabahu kutoa dhabihu na kutetea Mungu wao na imani yao. Mimi naomba kwamba kila mmoja wetu ataishi mkweli kwa imani ambayo wazazi wetu waliitunza. Katika jina takatifu na tukufu la Yesu Kristo, amina.