2010–2019
Utiifu kupitia Uaminifu Wetu
Aprili 2014


Utiifu kupitia Uaminifu Wetu

Utiifu ni nembo ya imani yetu katika hekima na nguvu za mamlaka kuu kabisa, hata Mungu

Mikutano ya jioni ya familia nyumbani ambayo Dada Perry nami tumekuwa tukifanya kila usiku wa Jumatatu ghafla imeongezeka kwa ukubwa. Kaka yangu, binti yake, kaka wa Barbara, na mpwa na mume wake wamehamia katika jumba la majumui letu. Ndiyo wakati wa pekee nimebarikiwa kuwa na familia kuishi karibu nami tangu nilipokuwa mvulana. Wakati huo, familia yangu iliishi kwenye kipande cha ardhi pamoja na wana familia kadhaa wa familia kuu ya mama yangu. Nyumba ya babu yangu Sonne ilikuwa karibu nasi upande wa kaskazini, nyumba ya Shangazi Emma ilikuwa karibu kusini mwa nyumba yetu. Upande wa kusini wa kipande cha ardhi aliishi Shangazi Josephine, na upande wa mashariki ndipo alipoishi Mjomba Alma.

Wakati wa uvulana wangu tuliingiliana na wanafamilia wa familia kuu kila siku na kushiriki nyakati za kufanya kazi, kucheza, na kutembeleana. Hatungeweza kujiingiza katika jambo baya lolote bila ripoti kuwafikia mama zetu upesi sana. Dunia ni tofauti sasa---wanafamilia wamesambaa sana. Hata kama wanaishi karibu sana na mmoja na mwengine, huwa hawaishi mlango wa pili. Bado, ninaamini kwamba uvulana wangu na mazingira yangu ya sasa ni kidogo kama mbinguni, nikiwa na wanafamilia wapendwa wakiishi karibu mmoja na mwengine. Inakuwa kama ukumbusho wa kila mara kwangu wa asili ya milele ya kitengo cha familia.

Nilipokuwa ninakua, nilikuwa na uhusiano maalum na babu yangu. Nilikuwa mwana mkubwa katika familia hii, mimi niliondoa theluji katika njia msimu wa baridi na kutunza uwanja wa nyasi katika msimu wa joto katika nyumba yetu, nyumba ya babu na nyumba za mashangazi zangu wawili. Babu kwa kawaida alikuwa anakaa hapo mbele barazani nilipokuwa nikikata nyasi za uwanja wa nyasi. Nikimaliza, ningekaa katika ngazi ya mbele na kuzungumza naye. Nyakati hizi ni kumbukumbu za thamani sana kwangu.

Siku moja nilimuuliza baba yangu ningejuaje kama daima ninafanya kitu kilicho sahihi, kwa kuwa maisha huwa na chaguo nyingi sana. Kama vile babu yangu alivyofanya kawaida, yeye alinijibu kwa kile alilopitia kutoka kwa maisha ya shamba.

Alinifunza kuhusu kuwaadilisha kundi la farasi ili waweze kufanya kazi pamoja. Alielezea kwamba kundi la farasi daima lazima lijue ni nani ndiye kiongozi. Kitu muhimu cha kuonyesha uthibiti na kumwelekeza farasi ni lijamu na kigwe. Kama mshiriki wa kundi atawahi kuamini kwamba hana haja ya kutii maelekezo ya msimamizi, kundi kamwe halitavuruta na kufanya kazi pamoja kwa uwezo wao wote.

Sasa acha tutazame somo babu yangu alinifunza mimi kwa kutumia mfano huu. Ni nani ndiye msimamizi wa kundi la farasi? Baba yangu aliamini ni Bwana. Yeye ndiye aliye na madhumuni na mpango. Yeye ndiye mfunzaji na mjenzi wa kundi la farasi, na vivyo hivyo kwa kila farasi binafsi. Msimamizi anajua vyema, na njia ya pekee kwa farasi kujua yeye daima anafanya kile kilicho sahihi ni kwa kuwa mtiifu na kufuata maelekezo ya msimamizi..

Ni nini kile babu yangu alikuwa anafananisha na lijamu na kigwe? Niliamini wakati huo, kama ninvyoamini sasa, kwamba babu yangu alikuwa ananifundisha mimi kufuata ushawishi wa Roho Mtakatifu. Akilini mwake, lijamu na kigwe ilikuwa ya kiroho. Farasi mtiifu, ambaye alikuwa sehemu ya kundi la farasi walioadilishwa, anahitaji zaidi kidogo kuliko kuvutwa tu kutoka kwa msimamizi ili afanye kwa usahihi kile yeye anataka afanye. Huu mvuto wa pole unalingana na sauti, ndogo, tulivu ambayo kwayo Bwana huongea nasi. Kutokana na heshima kwa wakala wetu, kamwe si mvuto wa thabiti, wa nguvu sana

Wanaume na wanawake ambao wanapuuza ushawishi tulivu wa Roho mara nyingi wanajifunza, kama mwana mpotevu alivyojifunza, kupitia matokeo ya maisha yake ya kutotii na anasa. Ilikuwa tu baada ya matokeo ya asili kumnyenyekeza mwana mpotevu ndipo “alipozingatia moyoni mwake” na kusikia minong’ono ya Roho ikimwambia arudi kwa nyumba ya baba yake (ona Luka 15:11–32).

Kwa hivyo somo babu yangu alinifunza mimi lilikuwa daima kuwa tayari kupokea mvuto wa upole wa Roho. Alinifunza mimi kwamba ningeweza daima kupokea ushawishi kama huo kama ningepotoka kutoka kwenye njia. Na singekuwa na hatia ya makosa mazito sana kama ningeruhusu Roho aniongoze katika maamuzi yangu.

Kama Yakobo 3:3 inavyosema, “Angalieni, twatia lijamu katika vinywa vya farasi, ili wamtii, hivi twageuza mwili wao wote.”

Sisi sharti tuwe na usikivu kwa lijamu yetu ya kiroho. Hata kwa mvuto kidogo kutoka kwa Bwana, sisi sharti tuwe na hiari ya kubadili kabisa mwenendo wetu. Ili kufanikiwa katika maisha, sisi sharti tufunze roho na mwili mwetu kushirikiana katika utiifu wa amri za Mungu. Tukitii ushawishi wa upole wa Roho Mtakatifu, unaweza kuunganisha roho na miili yetu katika madhumuni ambayo yatatuelekeza sisi kurudi kwa nyumba yetu ya milele ili kuishi na Baba yetu wa milele aliye Mbinguni.

Makala ya imani yetu ya tatu, hutufunza umuhimu wa utiifu: “Tunaamini kwamba kwa njia ya Upatanisho wa Kristo, wanadamu wote wanaweza kuokolewa, kwa kutii sheria na ibada za Injili.”

Aina ya utiifu babu yangu alielezea katika mfano wake wa kundi la farasi pia huhitaji imani maalum---yaani, imani kamili kabisa katika msimamizi wa kundi. Somo babu yangu alinifunza mimi, kwa hivyo, pia lilidokezea kanuni ya kwanza ya injili---imani katika Yesu Kristo.

Mtume Paulo alifunza: “Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana” (Waebrania 11:1). Kisha Paulo akatumia mifano ya Abili, Enoki, Nuhu, na Ibarhimu kufunza kuhusu imani. Alizingatia hadithi ya Ibrahimu, kwani Ibarhimu ndiye baba ya waaminifu. Paulo aliandika:

“Kwa imani Ibrahimu alipoitwa aliitika, atoke aende mahali pale atakapopapata kuwa urithi; akatoka asijue aendako.

“Kwa imani alikaa ugenini katika ile nchi ya ahadi, kama katika nchi isiyo yake. …

“Kwa imani hata Sera mwenyewe alipokea uwezo wa kuwa na mimba; alipokuwa amepita wakati wake; kwa kuwa alimhesabu yeye aliyeahidi kuwa mwaminifu” (Waebrania 11:8–9, 11).

Tunajua kwamba kupitia Isaka, mwana wa Ibrahimu na Sera, ahadi ilitolewa kwa Ibrahimu---na Sera ahadi za uzao “watu wengi kama nyota za mbinguni wingi wao, na kama mchanga ulio ufuoni, usioweza kuhesabika” ” (ona aya ya 12; ona pia Mwanzo 17:15–16). Na kisha, imani ya Ibrahimu ilijaribiwa kwa njia ambayo wengi wetu wangefikiria kuwa mbaya sana .

Nimetafakari mara nyingi juu ya hadithi ya Ibrahimu na Isaka, na mimi bado sijaamini kama ninaelewa kikamilifu uaminifu na utiifu wa Ibarhimu. Labda ninaweza kumfikiria yeye kwa uaminifu akitayarisha mikoba kuondoka asubuhi moja mapema, lakini ni kwa jinsi gani alichukua hizo hatua zote pamoja na mwanawe Isaka, kwa zaidi ya safari ya siku tatu hadi Mlima Moria? Ni kwa jinsi gani walibeba kuni za moto huko mlimani? Ni kwa njia gani alijenga madhabahu? Ni kwa jinsi gani alimfunga Isaka na kumweka juu ya madhabahu, alimwelezea vipi yeye angekuwa dhabihu? Na ni kwa jinsi gani alikuwa na nguvu za kuinua kisu ili kumchinja mwanawe? Imani ya Ibrahimu ilimpatia nguvu za kufuata maelekezo ya Mungu kwa usahihi mpaka wakati wa ajabu ambapo malaika alipomwita yeye kutoka mbinguni na kutangaza kwa Ibrahimu kwamba alikuwa amefaulu mtihani wa kufadhaisha. Na kisha malaika wa Bwana alirudia ahadi za agano la Ibrahimu.

Mimi natambua kwamba changamoto zinazohusiana na kuwa na imani katika Yesu Kristo na utiifu zitakuwa ngumu zaidi kwa watu fulani kuliko wengine. Nina miaka ya kutosha ya uzoefu wa kujua kwamba tabia za farasi zinaweza kuwa tofauti sana, na kwa hivyo, inaweza kuwa rahisi au vigumu sana kuadilisha, na kwamba baadhi ya watu tofauti ni vigumu sana. Kila mmoja wetu ni mwana na binti wa Mungu, na tuna hadithi ya kipekee ya maisha kabla ya kuzaliwa na ya maisha duniani. Kulingana na hayo, kuna masuluhisho machache ya saizi moja ya kuwatosha wote. Na kwa hivyo mimi natambua kikamilifu asili ya maisha ya bahati nasibu na, cha muhimu sana, haja ya daima ya kanuni ya pili ya injili, hata toba.

Pia ni kweli kwamba nyakati ambazo babu yangu aliishi ulikuwa wakati rahisi, hasa kuhusu chaguo katika ya haki na kosa. Ilhali baadhi ya watu wenye akili sana na umaizi wanaweza kuamini nyakati zetu ngumu zinahitaji hata masuluhisho tata sana zaidi, mimi niko mbali na kushawishiwa kuwa wao ni sahihi. Badala yake, mimi nina msimamo wa kwamba utata unahitaji urahisi mkubwa, kama jibu la babu yangu alilonipatia kwa swali langu la uaminifu kuhusu jinsi ya kujua haki na kosa. Mimi najua kile ninachofaa kutoa leo ni fomyula rahisi, lakini mimi ninaweza kushuhudia kuhusu jinsi inavyofanya vyema kwangu. Mimi naipendekeza kwenu na hata kuwapatia changamoto ya kujaribu maneno yangu, na ikiwa mtafanya hivyo, ninawaahidi yatawaelekeza kwa uwazi wa chaguo mnapokabiliwa na chaguo na kwamba yataweza kuwaelekeza kwenye majibu rahisi kwa maswali ambayo yanawakanganya wasomi na wale wanaofikiria wana hekima.

Mara nyingi sisi hufikiria juu ya utiifu kama kufuata amri au kanuni za mamlaka kuu kwa ubaridi bila kutumia akili. Ukweli, kwa ubora wote, utiifu ni nembo ya imani yetu katika hekima na nguvu za mamlaka kuu, hata Mungu. Wakati Ibrahimu alionyesha uaminifu usio wa kuyumbayumba na utiifu kwa Mungu, hata wakati aliamuriwa kumtuoa mwanawe dhabihu, Mungu alimnusuru yeye. Vivyo hivyo, tunapoonyesha uaminifu wetu kupitia utiifu, Mungu hatimaye atatuokoa sisi.

Wale ambao wanajitegemea tu wenyewew na kufuata tu hamu zao wenyewe na matakwa ya ubinafsi wana mapungufu wanapolinganishwa na wale ambao wanamfuata Mungu na kupata umaizi Wake, nguvu, na vipawa. Imeshasemekana, “kwamba mtu ambaye amejifunganisha mwenyewe hutengeneza kifurishi kidogo sana.” Utiifu wa nguvu na hai ni chochote kile ila unyonge au kukosa upinzani. Ndiyo njia ambayo kwayo tunatangaza imani yetu katika Mungu na kujihitimisha wenyewe kupokea nguvu za mbinguni. Utiifu ni chaguo. Ni chaguo kati ya elimu na nguvu zetu ndogo na hekima ya Mungu isiyo na kipimo na uenyezi. Kilingana na somo babu yangu alilonipatia, ni chaguo kuhisi lijamu ya kiroho katika midomo yetu na kufuata uongozi wa msimamizi.

Tuweni warithi wa agano na mbegu ya Ibrahimu kupitia uaminifu wetu na kwa kupokea maagizo ya injili iliyorejeshwa. Mimi nawaahidi ninyi kwamba baraka za uzima wa milele zinapatikana kwa kila mtu aliye mwaminifu na mtiifu. Katika jina la Yesu Kristo, amina.