Ruka uongozaji mkuu
Aprili 2014 | Ulinzi kutokana na Ponografia—Nyumba Yenye Kiini cha Kristo

Ulinzi kutokana na Ponografia—Nyumba Yenye Kiini cha Kristo

Aprili 2014 Mkutano Mkuu

Chujio kuu duniani … ni chujio la kibinafsi la undani ambalo hutokana na ushuhuda wa kina na unaodumu.

Wapendwa akina kaka na dada, leo nimebarikiwa kuwa na wajukuu wangu 13 walio wazee zaidi katika mkusanyiko huu. Hii imenifanya niulize “Nataka wajukuu wangu wajue nini?” Asubuhi hii ningependa kuzungumza kwa ukweli na familia yangu na yako.

Sisi kama viongozi tumekuwa na wasiwasi mwingi kuhusu uharibifu ambao ponografia inasababisha katika maisha ya washiriki wa Kanisa na familia zao. Shetani anashambulia kwa hasira isiyo na kifani.

Moja ya sababu tuko hapa duniani, ni kujifunza kudhibiti matamanio na hisia za miili yetu. Hizi hisia tulizopewa na Mungu zinatusaidia kutaka kuoa na kuwa na watoto. Uhusiano wa kimwili wa ndoa kati ya mwanamme na mwanamke ambao huleta watoto katika maisha haya ya duniani unakusudiwa pia kuwa mzuri, tukio la upendo ambalo linafunga pamoja mioyo miwili iliyojitolea, unaunganisha roho na mwili, na kuleta utimilifu wa shangwe na furaha tunapojifunza kufikiria mahitaji ya wenzetu kwanza. Rais Spencer W. Kimball alifundisha kwamba katika ndoa, “mwenza … huwa kipa umbele katika maisha ya mume ama mke, na hakuna pendeleo lingine au mtu au kitu kitawahi kuchukua nafasi ya mbele juu ya mwenza....

“Ndoa husadikisha uadilifu kamili na uaminifu kamili.” 1

Miaka mingi iliyopita mmoja kati ya watoto wetu alikuwa amekumbwa na msongamano wa mawazo. Niliingia kwenye chumba chake, ambapo alifungua roho yake na kunielezea kwamba alikuwa amekwenda kwenye nyumba ya rafiki yake na aliona kwa bahati mbaya picha za kushangaza na zisizo nzuri na matendo katika runinga kati ya mwanamme na mwanamke bila nguo. Alianza kulia na kuelezea jinsi alivyojisikia vibaya kuhusu kile alichokiona na alitamani kuwa angekitoa kwenye mawazo yake. Nilishukuru sana kwamba alikuwa ananiamini, akinipa nafasi ya kutuliza moyo wake safi na uliokuwa unauma na kumsaidia kujua jinsi ya kupata afueni kupitia Upatanisho wa Mwokozi. Nakumbuka hisia takatifu nilizokuwa nazo tulipopiga magoti pamoja, kama mama na binti, na kuomba msaada wa Baba yetu wa Mbinguni.

Wengi wa watoto, vijana, na watu wazima kwa kutokuwa na hatia huhatarishwa na ponografia, lakini idadi kubwa ya wote waume kwa wanawake wanachagua kutazama ponografia na hurudishwa tena na tena mpaka inapokuwa uraibu. Watu hawa binafsi wanaweza kutamania kwa mioyo yao yote kutoka kwenye mtego huu lakini mara nyingi hawawezi kuushinda wenyewe. Tunamshukuru sana Mungu wakati wapendwa wetu hawa wanapochagua kutuamini sisi kama wazazi au kiongozi wa Kanisa. Tungekuwa na burasa kutohamaki kwa mshangao, hasira, au kuwakatalia mbali, jambo ambalo linaweza kuwasabisha wasizungumze nasi tena.

Sisi kama wazazi na viongozi, tunahitaji kushauriana na watoto wetu na vijana kila mara, tukisikiliza kwa upendo na kwa uelewa. Wanapaswa kujua hatari za ponografia na jinsi inavyoweza kuchukua sehemu kubwa ya maisha yetu, ikisababisha kupoteza Roho, ikiharibu mawazo, uwongo, kuharibu uhusiano, kupoteza kujitawala, na karibu upotevu mkubwa wa muda, mawazo, na nguvu.

Ponografia ni haribifu, ovu, na ina picha chafu zaidi kama haijawahi kuwa. Tunaposhauriana na watoto wetu, pamoja tunaweza kutengeneza mpango wa familia wenye kanuni na mipaka, tukiwa waangalifu ili kulinda nyumba zetu kwa chujio na vipimo kwenye vifaa vya kielectroniki. Wazazi, je, tunatambua kwamba vifaa vya mikononi vyenye uwezo wa mtandao, siyo kompyutas, ndivyo tatizo kubwa?2

Vijana na watu wazima, kama mmenaswa katika mtego wa Shetani wa ponografia, kumbuka jinsi Mwokozi wetu mpendwa ana rehema. Je, unatambua ni kwa kina gani Bwana anakupenda na kukuthamini, hata sasa? Mwokozi wetu ana nguvu ya kukusafisha na kutuponya. Anaweza kuondoa maumivu na huzuni unayohisi na kukufanya msafi tena kupitia nguvu ya Upatanisho Wake.

Sisi kama viongozi tunajali sana pia kuhusu wenza na familia ya wale wanaoathirika kwa ajili ya uteja wa ponografia. Mzee Richard G. Scott amesihi: “Kama umekuwa huru kutoka kwenye dhambi mbaya wewe mwenyewe, usitaabike bila sababu madhara ya dhambi za mwingine … Unaweza kuhisi huruma ... Hata hivyo haupaswi kujichukulia hisia ya uwajibikaji kwa ajili ya matendo hayo.” 3 Jua kwamba hauko pekee yako. Kuna msaada. Mikutano ya kushinda uteja ya wenza inapataikana, ikiwemo mikutano ya mawasiliano ya simu, ambayo inawaruhusu wenza kupiga simu katika mikutano na kushiriki kutoka nyumbani kwao.

Akina kaka na dada, tutawalindaje watoto na vijana wetu? Chujio ni vifaa muhimu, lakini chujio kuu zaidi duniani, chujio la pekee linaloweza kufanya kazi, ni chujio la kibinafsi la ndani ambalo linatokana na ushuhuda wa kina na unaodumu wa upendo wa Baba yetu a Mbinguni na dhabihu ya Upatanisho ya Mwokozi wetu kwa kila mmoja wetu.

Tutawaongozaje watoto wetu kwa uongofu wa kina na kupokea Upatanisho wa Mwokozi wetu? Ninapenda tangazo la nabii Nefi la kile watu wake walichofanya ili kuimarisha vijana wa siku zake: “Na tunazungumza kuhusu Kristo, tunafurahia katika Kristo, tunahubiri kuhusu Kristo, [na] tunatoa unabii kumhusu Kristo … ili watoto wetu wajue asili ya kutegemea msamaha wa dhambi zao.”4

Tunawezaje kufanya haya katika nyumba zetu? Baadhi yenu mmenisikia nikizungumza kuhusu jinsi mume wangu, Mel, nami tulihisi kushindwa tulipokuwa wazazi wa watoto wanne wadogo. Tulipokumbana na changamoto za uzazi na kutimiza mahitaji yote ya maisha, tulikuwa na mahitaji makubwa ya usaidizi. Tuliomba na kusihi ili kujua kile cha kufanya. Jibu lililokuja lilikuwa bayana: “Ni SAWA kama nyumba iko bila mpangilio na watoto bado wako kwenye nguo zao za kulala na baadhi ya majukumu yameachwa bado bila kutimizwa. Vitu pekee ambavyo kwa kweli vinahitaji kutimizwa katika nyumba ni kusoma maandiko na kuomba kila siku, na mkutano wa jioni wa familia nyumbani kila wiki.”

Tulikuwa tunajitahidi kufanya mambo haya, lakini mara nyingi hayakuwa ya kipaumbele na, katika mkanganyiko, yalikuwa yakisahaulika saa zingine. Tulibadilisha mtazamo wetu na kujaribu kutojali kuhusu yale yaliyokuwa na umuhimu mdogo. Mkazo wetu ukawa ni kuongea, kufurahia, kutangaza, na kushuhudia juu ya Kristo kwa kujitahidi kwenye maombi ya kila siku na kujifunza maandiko na kuwa na mkutano wa jioni wa familia nyumbani kila wiki.

Rafiki yangu hivi majuzi alionya, “Unapowaaomba kina dada wasome maandiko na waombe zaidi, inawachosha sana. Tayari wanahisi kama wana mengi ya kufanya.”

Kina kaka na dada, kwa sababu najua kutokana na yale niliyopitia, na yale mume wangu alipitia, lazima nishuhudie juu ya baraka za kujifunza maandiko kila siku na maombi na mkutano wa jioni wa familia nyumbani kila wiki. Mazoea haya ndiyo husaidia kuondoa uchovu, kutoa maelekezo kwa maisha yetu, na kuongeza ulinzi zaidi kwenye nyumba zetu. Kisha, kama ponografia ama changamoto zingine zitashambulia familia zetu, tunaweza kumwomba Bwana msaada na kutarajia mwongozo mkubwa kutoka kwa Roho, tukijua kwamba tumefanya kile ambacho Baba yetu ametuuliza tukifanye.

Akina kaka na dada, kama haya hayajakuwa mazoea katika nyumba zenu, sote tunaweza kuanza kufanya hivyo sasa. Kama watoto wetu ni wakubwa na wamekataa kuungana nasi, tunaweza kuanza sisi wenyewe. Tunavyofanya hivyo, ushawishi wa Roho utaanza kuzijaza nyumba zetu na maisha yetu na, baada ya muda, watoto huenda wakaitikia.

Kumbuka kwamba Mitume waliohai pia wameahidi kwamba unapotafuta vizazi vilivyopita na kuandaa majina ya familia zetu kwa ajili ya hekalu, tutalindwa sasa na katika maisha yetu yote tunavyostahiki kupata kibali cha hekalu.5Ahadi kweli!

Vijana, wajibikeni kwa ajili ya ukuaji wenu wenyewe wa kiroho. Zima simu yako kama ni lazima, imba wimbo wa Msingi, omba kwa ajili ya msaada, wazia andiko fulani, ondoka kwenye sinema, wazia Mwokozi, pokea sakrament kwa ustahiki, soma Kwa Nguvu ya Vijana, kuwa mfano kwa marafiki zako, ongea na mzazi, nenda umwone askofu wako, omba msaada, na pata ushauri nasaha wa kitaalam, kama unahitajika.

Je, ninataka wajukuu wangu wajue nini? Nawataka wao na ninyi mjue kwamba ninajua Mwokozi yu hai na anatupenda. Amelipa gharama ya dhambi zetu, lakini sisi sharti tupige magoti mbele ya Baba yetu aliye Mbinguni, kwa unyenyekevu wa kina, tukiungama dhambi zetu, tumsihi Yeye msamaha. Sisi sharti tutake kubadilisha mioyo yetu na hamu zetu na tuwe wanyenyekevu ya kutosha kutafuta msaada na msamaha kwa wale tunaweza kuwa tumewaumiza au kuwatelekeza.

Najua kwamba Joseph Smith alimwona Mungu, Baba yetu wa Mbinguni, na Mwokozi wetu, Yesu Kristo. Mimi nashuhudia kwamba sisi tuna nabii anayeishi ulimwenguni, Rais Thomas S. Monson. Pia nashuhudia kwamba hatutawai potoshwa tukitii ushauri wa nabii wa Mungu. Mimi nashuhudia juu ya nguvu za maagano yetu na baraka za hekalu.

Mimi najua kwamba Kitabu cha Mormoni ni cha kweli! Siwezi kuelezea nguvu ya kitabu hiki kikuu. Ninajua tu kwamba, kikitumiwa pamoja na maombi, Kitabu cha Mormoni kimebeba nguvu za kulinda familia, kuimarisha mahusiano, na kutoa ujasiri wa kibinafsi mbele ya Bwana. Mimi nashuhudia vitu hivi katika jina tukufu la Yesu Kristo, amina.

Onesha KumbukumbuFicha Kumbukumbu

  Muhtasari

  1. Teachings of Presidents of the Church: Spencer W. Kimball (2006), 199–200.

  2. Ona Clay Olsen, “What Teens Wish Parents Knew” (address given at Utah Coalition Against Pornography Conference, Mar. 22, 2014); utahcoalition.org.

  3. Richard G. Scott, “To Be Free of Heavy Burdens,” Ensign au Liahona, Nov. 2002, 88.

  4. 2 Nefi 25:26.

  5. Ona David A. Bednar, “The Hearts of the Children Shall Turn,” Ensign au Liahona, Nov. 2011, 24–27; Richard G. Scott, “The Joy of Redeeming the Dead,” Ensign au Liahona, Nov. 2012, 93–95; Neil L. Andersen, “Find Our Cousins!” (address given at RootsTech 2014 Family History Conference, Feb. 8, 2014); lds.org/prophets-and-apostles/unto-all-the-world/find-our-cousins.