Ruka uongozaji mkuu
Aprili 2014 | Mizizi na Matawi

Mizizi na Matawi

Aprili 2014 Mkutano Mkuu

Kuharakisha kazi ya historia ya familia na hekalu katika siku zetu ni muhimu kwa wokovu na kuinuliwa kwa familia.

Kabla ya kifo chake kutokana na saratani katika mwaka wa 1981, mwandishi mbishani William Saroyan aliandika kwa vyombo vya habari, “Kila mtu atakufa, lakini mimi kila mara niliamini ruhusa itatolewa kwa ajili yangu. Sasa nini?” 1

“Sasa nini” katika mkabala wa kifo katika maisha haya na “sasa nini” ni taamali ya maisha baada ya kifo iliyo katika kitovu cha maswali ya nafsi kwamba injili iliyorejeshwa ya Yesu Kristo hujibu kimaridadi sana katika mpango wa furaha wa Baba.

Katika maisha haya tunacheka, tunalia, tunafanya kazi, tuncheza, tunaishi, na kisha tunakufa. Ayubu hakauliza swali fupi na dhahiri, “Mtu akifa, je! Atakuwa hai tena? 2 Jibu la mvuvumo ni ndio kwa sababu ya dhabihu ya upatanisho ya Mwokozi. Sehemu Ayubu ya dibaji anuwai ya swali hili ni ya kuvutia sana: “Mwanadamu aliyezaliwa na mwanamke siku zake si nyingi. … Yeye huchanua kama vile ua, kisha hukatwa. … Kwani yako matumaini ya mti, ya kuwa ukikatwa utachipuka tena, Wala machipukizi yake hayatakoma. … na kutoa matawi kama mche.” 3

Mpango wa Baba yetu ni kuhusu familia. Maandiko kadhaa yetu ya kugusa sana moyo ni matumizi ya dhana ya mti pamoja na mizizi na matawi yake kama analogia.

Katika sura ya mwisho ya Agano la Kale, Malaki, katika kuelezea juu ya Ujio wa Pili wa Mwokozi, kwa uwazi hutumia tashbihi hii. Akiongea juu ya wenye kiburi na waovu, anasema kwamba watachomwa kama makapi na “kwamba hata haitawaachia shina wala tawi.” 4 Malaki hufunga sura hii na ahadi ya Bwana ya uhakikisho:

“Angalieni, nitawapelekea Eliya nabii, kabla haijaja siku ile ya Bwana, iliyo kuu na kuogofya:

“Naye ataigeuza mioyo ya baba iwaelekee watoto wao, na mioyo ya watoto iwaelekee baba zao, ili nisije nikaipiga dunia kwa laana.” 5

Katika machweo ya Urejesho, Moroni alisisitiza tena ujumbe huu katika maagizo yake ya mwanzo kwa kijana Joseph Smith mnamo 1823. 6

Wakristo na Wayahudi kote ulimwenguni wanakubali tukio la Agano la Kale la Eliya. 7 Yeye alikuwa nabii wa mwisho kushikilia nguvu za kufunganisha za Ukuhani wa Melkizediki kabla nyakati za Yesu Kristo. 8

Eliya Arejesha Funguo

Kurudi kwa Eliya kulitokea katika Hekalu la Kirtland mmamo Aprili 3, 1836. Alitangaza alikuwa anatimiza ahadi ya Malaki. Alikabidhi funguo za ukuhani za kufunganisha familia katika kipindi hiki. 9 Ujumbe wa Eliya uliletwa kwa kile ambacho mara nyingine huitwa roho ya Eliya, ambayo, kama vile Mzee Russell M. Nelson amefunza, ni “maonyesho ya Roho Mtakatifu akishuhudia asili takatifu ya familia.” 10

Mwokozi alikuwa dhahiri kabisa kuhusu haja ya ubatizo, Yeye alifunza, “Mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuuona ufalme wa Mungu.” 11 Mwokozi yeye wenyewe alibatizwa kuweka mfano. Na itakuwaje kwa wale waliokufa ambao hawakubatizwa?

Fundisho la Hekalu na Kazi ya Historia ya Familia

Mnamo Oktoba 11, 1840, katika Nauvoo, Vilate Kimball aliandika barua kwa mume wake, Mzee Heber C. Kimball, ambaye pamoja na washiriki wengine wa wale Kumi na Wawili walikuwa wanahudumu misheni katika Uingereza. Mkutano mkuu wa Oktoba ulikuwa umefanyika siku chache kabla.

Ninanukuu sehemu za barua ya kibinafsi ya Vilate: “Tumekuwa mkutano mkuu mkubwa na wa kupendeza sana ambao umepata kuwa tangu Kanisa kuanzishwa. … Rais [Joseph] Smith amefungua mada mpya na tukufu. … Ambayo ni ubatizo wa wafu. Paulo anaongea juu yake katika Wakorintho wa Kwanza sura ya 15 aya ya 29. Joseph alipokea maelezo yake kamili kwa ufunuo. Alisema ni fursa kwa washiriki wa Kanisa hili kubatizwa kwa wote wa jamii yao ambao walikufa kabla ya injili hii kuja. … Kwa kufanya hivyo tunatenda kama mawakala wao wenyewe, na kuwapatia nafasi ya kuja mbele katika Ufufuo wa Kwanza. Yeye anasema wao watakuwa na injili kuhuburiwa kwa wao katika gereza.”

Vilate aliongezea: “Mimi ninataka kubatizwa kwa niaba ya mama yangu. … Si hili ni fundisho tukufu?” 12

Fundisho muhimu la kuunganisha familia lilikuja mstari juu ya mstari na fundisho juu ya fundisho. Ibada za uwakilishaji ni kitovu cha kuunganisha familia pamoja milele, kushikanisha mizizi na matawi.

Fundisho la familia kuhusiana na kazi ya historia ya familia na hekalu ni wazi. Bwana katika maagizo ya awali ya ufunuo wa mwanzoni yanalenga “ubatizo wa wafu wenu.”13 Jukumu letu la kimafundisho ni kwa wahenga wetu wenyewe. Hii ni kwa sababu utaratibu wa kiselestia ya mbinguni una msingi katika familia. 14 Urais wa Kwanza umewahimiza washiriki hasa vijana na watu wazima waseja, kusisitizia kazi ya historia ya familia na ibada kwa majina ya familia zao wenyewe au majina ya wahenga wa washiriki wa kata wa kigingi. 15 Tunahitaji kuunganisha yote mizizi na matawi yetu. Dhana ya kuhusishwa na ufalme wa milele ni tukufu kwa kweli.

Mahekalu

Wilford Woodruff alionyesha kwamba Nabii Joseph Smith aliishi muda mrefu wa kutosha kuweka msingi wa kazi ya hekalu. “Wakati wa mwisho kukutana na Jamii ya Mitume Kumi na Wawili ilikuwa ni wakati aliwapatia wao endaumenti zao.” 16

Baada ya kifo cha kishahidi cha Nabii, watakatifu walikamilisha Hekalu ya Nauvoo, na nguvu za kufunganisha zilitumika kwa maelfu ya washiriki waaminifu kabla ya kutoka kwenda Mountain West. Miaka thelathini baadaye, katika kukamilika kwa Hekalu la St. George, Rais Brigham Young alisema umuhimu wa milele wa ibada za kuokoa hatimaye zinapatikana kwa wote wanaoishi na wafu. 17

Hii kwa urahisi ilisemwa na Rais Wilford Woodruff: “Hamna kabisa kanuni yoyote ambayo Bwana amefunua ninayofurahia zaidi kuliko ukombozi wa wafu wetu; kwamba tutakuwa na baba zetu, mama zetu, wake zetu, na watoto wetu kuwa pamoja nasi katika kundi la familia, katika ile asubuhi ya ufufuo wa kwanza na katika Ufalme wa Selestia. Hizi ni kanuni kuu sana. Zinafaa kila dhabihu.” 18

Ni wakati mzuri jinsi gani kuwa hai. Hiki ndio kipindi cha mwisho, na sisi tunaweza kuhisi kuharakishwa kwa kazi ya wokovu katika kila eneo ambapo maagizo ya kuokoa yanahusishwa. 19 Sasa tuna mahekalu karibu kote ulimwenguni ya kutoa maagizo haya ya kuokoa. Kuudhuria hekalu kwa kufanywa upya kiroho, amani, usalama, na maelekezo katika maisha yetu pia baraka kuu. 20

Chini ya mwaka mmoja baada ya Rais Thomas S. Monson kuitwa kama Mtume, aliweka wakfu Maktaba ya Nasaba ya Hekalu la Los Angeles. Aliongea juu ya wahenga waliokufa “wakingojea ile siku ambayo wewe na mimi tutafanya utafiti ambao unafaa kufungua njia, … [na] vile vile kwenda katika nyumba ya Mungu na kufanya kazi hiyo… [ambayo wao] … hawawezi kufanya.” 21

Aliyekuwa wakati huo Mzee Monson alitoa hayo maneno ya kuweka wakfu mnamo Juni 20,1964, kulikuwa tu mahekalu 12 yanayofanya kazi. Wakati wa kipindi Rais Monson alihudumu katika mabaraza makuu ya Kanisa, 130 kati ya mahekalu 142 yanayofanya kazi yalikuwa yamewekwa wakfu. Ni kitu cha miujiza kuona kuharakisha kwa kazi ya wokovu katika siku yetu. Mahekalu ishirini na nane zaidi yalitangazwa na yako katika hali tofauti za kukamilika. Asilia mia themanini na nane zaidi ya washiriki wa Kanisa sasa wanaishi chini ya maili 200 (320 kilometa) ya hekalu.

Tekinolojia ya Historia ya Familia

Tekinolojia ya historia ya familia pia imepanuka kiajabu. Rais Howard W. Hunter alitangaza katika Novemba 1994: “Tumeanza kutumia tekinolojia ya habari kuharakisha kazi takatifu ya kutoa ibada kwa wafu. Kazi ya tekinolojia … umetiwa kasi na Bwana mwenyewe. … Hata hivyo, tunasimama tu kwenye kilele cha kile tunachoweza kufanya na vyombo hivi.” 22

Katika miaka 19 tangu kauli hii ya kinabii, kitiwa kasi kwa tekinolojia ni karibu isiaminike. Mama wa miaka 36 wa watoto wadogo majuzi alitamka kwangu, “Fikiria tu---tumetoka kwa visoma microfilamu katika vituo vya historia ya familia vilivyopangiwa hadi kukaa katika meza za jikoni na kompyuta yangu nikifanya historia ya familia baada ya watoto wangu kulala.”Ndungu na dada, vituo vyetu vya historia ya familia sasa viko nyumbani kwetu.

Kazi ya hekalu na historia ya familia si tu kutuhusu sisi. Fikiria wale walio katika upande mwengine wa pazia wakingojea ibada za kuokoa ambazo zingewaweka huru kutoka na kifungo cha gereza ya roho. Prison inaelezwa kama “hali ya kuzuizini au kifungoni.” 23 Wale walio katika kifungoni wanaweza kuuliza swali la Saroyan: “Sasa nini?”

Dada mmoja mwaminifu alishiriki uzoefu wa kiroho maalumu katika Hekalu Salt Lake. Hali katika chumba cha uthibitisho, baada ya uthibitisho wa uwakilishi wa agizo kutangazwa, alisikia, “Na wafungwa watakuwa huru!” Alihisi hali ya haraka kuu kwa wale ambao wanangojea kazi ya ubatizo na uthibitisho. Aliporudi nyumbani, alipekua maandiko kwa kishazi alichosikia. Alipata tamko la Joseph Smith katika sehemu ya 128 ya Mafundisho na Maagano: “Acheni mioyo yenu ifurahi, na kuwa na furaha kupita kiasi. Acheni nchi ipasuke kwa kuimba. Acheni wafu waimbe nyimbo za sifa ya milele kwa Mfalme Imanueli, aliyeagiza, kabla ya ulimwengu kuwepo, kile ambacho kingetuwezesha sisi kuwakomboa kutoka kifungoni mwao; kwani wafungwa watawekwa huru.” 24

Swali ni, tunahitaji kufanya nini? Ushauri wa Nabii Joseph ulikuwa ni kuwasilisha katika hekalu “kumbukumbu za wafu wetu, ambayo itastahili makubalio yote.” 25

Uongozi wa Kanisa ulitoa wito ulio wazi kwa kizazi chipukizi kuongoza njia katika matumizi ya tekinolojia ili kupata uzoefu wa roho ya Eliya, kuwatafuta wahenga wao, na kufanya maagizo ya hekalu kwa ajili yao. 26 Wingi wa kuinua uzito katika kuharakisha kazi ya wokovu utafanya na ninyi vijana.27

Kama kila kijana katika kata hataenda tu hekaluni na kufanya ubatizo wa wafu wao bali pia atafanya kazi na familia zao na washiriki wengine wa kata ili kutoa majina ya familia ili ibada zifanywe, wote wao na Kanisa litabarikiwa sana. Usipuuze ushawishi wa wafu katika kusaidia juhudi zako na furaha ya hatimaye kukutana na wale uliowahudumia. Baraka muhimu milele za kuunganisha familia ni karibu zaidi ya kuaeleweka. 28

Katika ushiriki wa Kanisa duniani kote, asilimia hamsini na moja ya watu wazima kwa sasa hawana wazazi wao katika sehemu ya Family Tree ya tovuti ya Intaneti ya FamilySearch ya Kanisa. Asilimia sitini na tano ya watu wazima hawana mababu wote wanne walioorodheshwa. 29 Kumbuka, sisi bila mizizi na matawi yetu hatuwezi kuokolewa. Washiriki wa Kanisa wanahitaji kupata na kutia habari hizi muhimu.

Sisi hatimaye tuna mafundisho, mahekalu, na tekinolojia kwa familia kutumiza kazi hii tukufu ya wokovu. Mimi napendekeza njia moja ambayo haya yanaweza kufanywa. Familia zinaweza kuwa na “Mkusanyiko wa Family Tree.” Hii inapaswa kuwa juhudi ya kila mara. Kila mmoja angeweza kuleta historia zilizopo, hadithi, na picha, ikijumuisha mali ya thamani ya kina babu na wazazi. Vijana wetu wamesisimka kujifunza kuhusu maisha ya wana familia---kule walitoka na jinsi walivyoishi. Wengi wameshapata mioyo kugeukia baba zao. Wanapenda hadithi na picha, wana ujuzi wa tekinolojia wa kuskani na kupakia hadithi hizi na picha kwa Family Tree na kuunganisha hati za vyanzo za wahenga ili kuhifadhi hizi kwa wakati wote. Kwa hakika, lengo muhimu ni kuamua ni maagizo gani bado yanahitaji kufanywa na kupangia kwa kazi muhimu ya hekalu. Kijitabu cha My Family kinaweza kutumika ili kusaidia kuandika habari za familia, hadithi, na picha ambazo zinaweza kisha kupakiwa kwenye Famliy Tree.

Masharti na matarajio ya familia yanafaa kuwa kipa umbele cha juu ili kulinda kudra yetu ya kiungu. Kwa wale ambao wanatafuta kuwa na mazao zaidi ya kutumia siku ya Sabato kwa familia nzima, kuharakisha kazi hii ni mchanga ulio na rutuba. Mama mmoja aliongea kwa uchangamfu jinsi mwanawe wa miaka 17 huenda kwenye kompyuta baada ya kanisa siku ya Jumapili kufanya kazi ya historia ya familia na mwanawe wa miaka 10 anayependa kusikiliza hadithi na kuona picha za wahenga wake. Hii imebariki familia nzima kuhisi roho ya Eliya. Mizizi na matawi yetu yenye thamani sharti yaishamirishwe.

Yesu Kristo alitoa maisha Yake kama upatanisho wa uwakilishi. Yeye alisuluhisha swali la msingi lililoulizwa na Ayubu. Yeye alishinda kifo kwa ajili ya wanadamu wote, ambavyo hatungeweza kujifanyia wenyewe. Sisi tunaweza, hata hivyo, kufanya ibada za uwakilishi na kwa kweli kuwa waokozi kwenye Mlima Sayuni30 kwa familia zetu wenyewe ili kwamba sisi, na wao, tuweze kuinuliwa pamoja na kuokolewa.

Mimi nashuhudia juu ya dhabihu ya upatanisho ya Mwokozi na kwa hakika mpango wa Baba kwa ajili yetu na familia zetu. Katika jina la Yesu Kristo, amina.

Onesha KumbukumbuFicha Kumbukumbu

  Muhtasari

  1. William Saroyan, in Henry Allen, “Raging against Aging,” Wall Street Journal, Dec. 31, 2011–Jan. 1, 2012, C9.

  2. Ayubu 14:14.

  3. Ayubu 14:1, 2, 7, 9.

  4. Malaki 4:1. Hivi majuzi makala kadha yakiandikwa juu ongezeko la idadi kubwa sana ya watu wanaochagua kutokuwa na watoto ili waboreshe kiwango chao cha maisha (ona Abby Ellin, “The Childless Plan for Their Fading Days,” New York Times, Feb. 15, 2014, B4). Nchi nyingi zimepungukiwa na idadi ya watu kama matokeo ya chaguo za watu hawa. Wakati mwengine hii inaitwa (ona The New Economic Reality: Demographic Winter [documentary], byutv.org/shows).

  5. Malaki 4:5–6.

  6. Ona Historia ya Kanisa, 1:12; Mafundisho na Maagano 2.

  7. Wayahudi wamekuwa wakingojea kurudi kwa Eliya kwa miaka 2,400. Kufikia siku ya leo, katika Sedasi au mlo mkuu wa kila mwaka, wao umwandali sehemu kwa ajili yake na kwenda mlangoni kwa matumaini yeye atawasili kuashiria ujio wa Masiya.

  8. Ona Bible Dictionary, “Elijah.”

  9. Ona Mafundisho na Maagano 110:14–16; pia onaMafundisho na Maagano 2.

  10. Russell M. Nelson, “A New Harvest Time,” Ensign, May 1998, 34.

  11. Yohana 3:5.

  12. Vilate M. Kimball to Heber C. Kimball, Oct. 11, 1840, Vilate M. Kimball letters, Church History Library; tahajia na herufi kubwa zimesanifishwa.

  13. Mafundisho na Maagano 127:5; mkazo umeongezewa.

  14. Ona Teachings of Presidents of the Church: Joseph Fielding Smith (2013), 68.

  15. Ona Barua ya Urahisi wa Kwanza, Oct. 8, 2012.

  16. Ona The Discourses of Wilford Woodruff, sel. G. Homer Durham (1946), 147.

  17. Brigham Young alisema, “Yote ninayotaka ni kuona watu hawa wakijitolea mali yao na faida yao kujenga ufalme wa Mungu, kujenga mahekalu, na ndani yao wakisimamia kwa walio hai na wafu … kwamba waweza kuvishwa taji la wana na mabinti wa Mwenyezi” (Deseret News, Sept. 6, 1876, 498). Ubatizo wa wafu ulianza mnamo Januari 9, 1877, na endaumenti za wafu zilifanywa siku mbili baadaye. Furaha ya haya ilionyeshwa na Lucy B. Young ambaye alisema “moyo wake ulijaa katika uwezekano wa kupokelewa na [jamii zake waliokufa] kwa mikono wazi, kama wote wangekuwa na wale ambao hawangweza kujifanyia kazi wenyewe” (katika Richard E. Bennett, “‘Which Is the Wisest Course?’ The Transformation in Mormon Temple Consciousness, 1870–1898,” BYU Studies Quarterly, vol. 52, no. 2 [2013], 22).

  18. Teachings of Presidents of the Church: Wilford Woodruff (2004), 192–93.

  19. Rais Wilford Woodruff, (ambaye anajulikana kama mmoja wa wamisionari wakuu wa nyakati zote hadi walio hai), kuongea juu ya kazi ya wafu alisema: “Mimi nilichukua sehemu hii ya huduma yetu kama misheni ya umuhimu mwingi kama vile kuhubiri kwa walio hai; wafu watasikia sauti ya watumishi wa Mungu katika ulimwengu wa roho, na hawawezi kuja asubuhi ya kwanza ya ufufuo, isipokuwa maagizo fulani yafanywe, kwa niaba [yao]. … Inachukua juhudi sawa kuokoa mtu mfu … kama mtu aliye hai” (Teachings of Presidents of the Church: Wilford Woodruff, 188).

  20. Rais Howard W. Hunter aliwaalika washiriki wa Kanisa kwenda kwenye hekalu kila mara “kwa baraka za kibinafsi za kuabudu hekaluni, kwa utakatifu na usalama ambao unapatikana ndani ya kuta takatifu wa wakfu. … Ni takatifu kwa Bwana. Inapaswa kuwa takatifu kwetu” (“The Great Symbol of Our Membership,”Ensign, Oct. 1994, 5;Tambuli, Nov. 1994, 6).

  21. “Messages of Inspiration from President Thomas S. Monson,” Church News, Dec. 29, 2013, 2.

  22. Howard W. Hunter, “We Have a Work to Do,” Ensign, Mar. 1995, 65.

  23. Merriam-Webster’s Collegiate Dictionary, 11th ed. (2003), “prison.”

  24. Mafundisho na Maagano 128:22; ona pia Mafundisho na Maagano 138:42. “Kabla ya ulimwengu kuwepo, Bwana alitawaza kile ambacho huwezesha roho zilizopo katika [gereza] kukombolewa” (kiambaisho cha utatu wa maandiko, “Gereza”).

  25. Mafundisho na Maagano 128:24.

  26. Ona barua ya Urais wa Kwanza, Oct. 8, 2012; ona pia David A. Bednar, “The Hearts of the Children Shall Turn,”Ensign orLiahona, Nov. 2011, 24–27; R. Scott Lloyd, “‘Find Our Cousins’: Apostle [Neil L. Andersen] Counsels LDS Youth at RootsTech Conference,” Church News, Feb. 16, 2014, 8–9.

  27. Utafiti mmoja wa majuizi unaonyesha kwamba mzingatio mkubwa wa kizazi hiki ni kuishi maisha mazyri ambapo wao “wanawapatia wengine, na kujifahamisha madhumuni makuu” (Emily Esfahani Smith and Jennifer L. Aaker, “Millennial Searchers,” New York Times Sunday Review, Dec. 1, 2013, 6).

  28. Ona Howard W. Hunter, “A Temple-Motivated People,”Ensign, Feb. 1995, 2–5;Liahona, May 1995, 2–7.

  29. Takwimu zimetolewa na Family History Department.

  30. Ona Obadia 1:21.