Ruka uongozaji mkuu
Aprili 2014 | Udada: Ee, Ni kwa Jinsi Gani Tunahitajiana

Udada: Ee, Ni kwa Jinsi Gani Tunahitajiana

Aprili 2014 Mkutano Mkuu

Sisi sharti tusisite kuzingatia juu ya tofauti zetu na tutafaute kile tulichonacho sote.

Katika video ile, tuliziona nchi nane na kusikia lugha nane tofauti. Ona jinsi lugha zilivyo nyingi zilizongezwa katika mstari ule wa mwisho. Inatia moyo kujua kwamba kama kidada wa ulimwengu tuliweza kupaza sauti zetu katika ushuhuda wa ukweli wa milele kwamba sisi ni mabinti wa Baba yetu wa Mbinguni mwenye upendo.

Ni nafasi nzuri kiasi gani kuwa hapa katika kipindi hiki cha kihistoria na kuwahutubia wanawake wote wa Kanisa wenye umri wa miaka minane na zaidi. Kuna uhusiano mzuri katika muungano wetu jioni hii ya leo. Kama ninavyoona sisi sote tumekusanyika pamoja katika Ukumbi wa Mikutano na tukiwafikiria maelfu ya wengine wanatazama matangazo haya katika maeneno mengine duniani kote, muunganisho wa shuhuda zetu na imani katika Yesu Kristo hakika unajumuisha mojawapo ya mikutano iliyojaa imani na wenye nguvu wa wanawake katika historia ya Kanisa, kama siyo ya ulimwengu.

Usiku wa leo tunafurahia katika majukumu mbali mbali kama wanawake wa Kanisa. Japokuwa kwa njia nyingi tupo tofauti na wakipekee, pia tunatambua kwamba sisi sote ni mabinti wa yule yule Baba wa Mbinguni na hivyo kutufanya sisi tuwe madada. Tumeunganishwa katika lengo la kuujenga ufalme wa Mungu na katika maagano tuliyoyaweka, bila kujali matatizo yetu. Muungano huu, bila shaka, ni udada mtakatifu zaidi katika uso wa dunia!1

Kuwa madada hunamaanisha kwamba kuna mfungo usioweza kuvunjika kati yetu. Madada hujaliana, wanalindana, wanafarijiana, na wapo pale kwa ajili yao wenyewe kwa shida na raha. Bwana amesema, “Ninawaambia, muwe na umoja; na kama hamna umoja ninyi siyo wangu.”2

Adui angependa sisi tukosoane au tuhukumiane sisi kwa sisi. Anataka tuzingatie tofauti zetu na kujilinganisha na mwingine. Unaweza kupenda kufanya mazoezi ya nguvu sana kwa saa moja kila siku kwa sababu inakusaidia kuhisi vizuri, wakati ninafikiria kuwa ni moja ya mafanikio kama ninatembea kupanda ngazi badala ya kupanda lifti. Bado tunaweza kuwa marafiki, ndivyo siyo?

Sisi kama wanawake tunaweza kuwa makini kwetu wenyewe. Tunapojilinganisha sisi kwa sisi mara zote tutajisikia vibaya juu ya wengine. Dada Patricia T. Holland aliwahi kusema, “Lengo ni, hatuwezi kujiita Wakristo na kuendelea kuwahukumu wengine—au kujihukumu sisi wenyewe—vibaya sana.”3 Aliendelea kusema kwamba hakuna kitu kibaya kwetu kama kupoteza huruma zetu na udada. Tunatakiwa kutulia na kufurahia tofauti zetu takatifu. Tunatakiwa kujua kwamba sote tunatamani kuhudumu katika ufalme kwa kutumia vipaji vyetu vya kipekee kwa njia zetu wenyewe. Ndipo tunapoweza kufurahia udada wetu, mahusiano yetu, na kuanza kuhudumu.

Ukweli ni kwamba kwa hakika na kwa kweli tunahitajiana. Wanawake kwa kawaida hutafuta urafiki, kusaidiana, na uenza. Tuna mengi ya kujifunza toka kwetu wenyewe, na mara nyingi tunaacha vizuizi tulivyovijenga wenyewe kutufanya tusifurahie uhusiano ambao unaweza kuwa wa baraka kubwa katika maisha yetu. Kwa mfano, sisi wanawake ambao kidogo ni wazee tunahitaji ambacho ninyi wasichana wenye umri wa darasa la msingi mnachoweza kutoa. Tunaweza kujifunza zaidi kutoka kwenu juu ya utumishi na upendo kama wa Yesu.

Hivi majuzi nilisikia hadithi nzuri juu ya msichana mdogo aitwaye Sarah, ambaye mama yake alipata nafasi ya kumsaidia mwanamke mwingine aitwaye Brenda katika kata yake, aliyekuwa na ugonjwa wa seli. Sarah alipenda kwenda na mama yake kumsaidia Brenda. Alimpaka mafuta Brenda kwenye kiganja na kuanza kumkanda vidole vyake na mikono yake kwa sababu mara nyingi alikuwa na maumivu. Sarah baadaye akajifunza kunyoosha mikono ya Brenda juu ya kichwa chake ili kuipa misuli mazoezi. Sarah alichana nywele za Brenda na kuongea naye wakati mama yake akimsaidia vitu vingine. Sarah alijufunza umuhimu wa furaha ya kumtumikia mtu mwingine na akaja kuelewa kwamba hata mtoto anaweza kuleta tofauti kubwa katika maisha ya mtu mwingine.

Ninaupenda mfano tulionao katika sura ya kwanza ya Luka ambao unaelezea uhusiano mzuri kati ya Mariamu, mama wa Yesu, na binamu yake Elizabeti. Mariamu alikuwa msichana wakati alipojulishwa juu ya wajibu wake mkubwa wa kuwa mama wa Mwana wa Mungu. Mwanzoni, inaweza kuonekana kama ni wajibu mkubwa wa kuubeba peke yake. Alikuwa Bwana Mwenyewe ambaye alimpa Mariamu mtu wa kumsaidia kuubeba mzigo wake. Kupitia kwa ujumbe wa malaika Gabrieli, Mariamu alipewa jina la mwanamka anayeaminika na mwenye huruma ambaye angemgeukia kwa ajili ya msaada—binamu yake Elizabeti.

Huyu binti na binamu yake ambaye “alikuwa na umri wa miaka mingi,”4 walikuwa na urafiki mkubwa katika wakati wa ujauzito wao wa kimiujiza, na naweza kufikiria umuhimu wa miezi mitatu waliyokuwa pamoja wakiweza kuongea, kuoneana huruma, na kusaidiana katika miito yao ya kipekee. Ni mfano mzuri kiasi gani kwa wanawake wa vizazi tofauti walivyoshirikiana.

Wale kati yetu ambao ni wakubwa wanaweza wakawa kichocheo kwa kizazi kichanga. Wakati mama yangu alipokuwa msichana mdogo, hakuna kati ya wazazi wake aliyekuwa mshiriki mkamilifu Kanisani. Japokuwa alikuwa na umri mdogo wa miaka mitano, alitembea peke yake kwenda kanisani na kuhudhuria mikutano ya—Msingi—Shule ya Jumapili, na sakramenti—yote kwa nyakati tofauti.

Hivi karibuni nilimwuliza mama yangu kwa nini aliweza kufanya hivyo wiki hadi wiki wakati akiwa hana msaada au kutiwa moyo nyumbani. Jibu lake lilikuwa, “Nilikuwa na walimu wa msingi walionipenda.” Walimu hawa walimjali na kumfundisha injili. Walimfundisha kwamba alikuwa na Baba wa Mbinguni aliyempenda na ulikuwa ni upendo ambao ulimfanya aje wiki baada ya wiki. Mama yangu aliniambia, “Huu ndiyo mmojawapo wa ushawishi muhimu sana katika maisha yangu ya mapema.” Natumaini naweza kuwashukuru kina dada hao siku moja. Hakuna mipaka ya umri inapokuja kwenye utumishi kama wa Yesu.

Wiki kadhaa zilizopita nilikutana na rais wa Wasichana wa kigingi huko California aliyeniambia kwamba mama yake mzee wa umri wa miaka 81 alikuwa ameitwa kuwa mshauri wa Mia Maid. Nilishangazwa, hivyo nikampigia simu mama yake. Wakati askofu wa Dada Val Baker alipomuomba akutane naye, alikuwa anatarajiwa aitwe kuwa mtunza maktaba au mtu wa historia. Alipomwomba kutumikia kama mshauri wa Mia Maid wa wasichana, jibu lake lilikuwa, “Unahakika?”

Askofu wake kwa uhakika alijibu, “Dada Baker, bila shaka; wito huu unatoka kwa Bwana.”

Alisema hakuwa na jibu lingine kwa hayo ila, “Bila shaka.”

Napenda mwongozo aliokuwa nao askofu huyu kwamba wasichana wane wa Mia Maid aliokuwa nao katika kata yake wana mengi ya kujifunza kutoka kwa busara, uzoefu, na mfano wa kudumu wa huyu dada mzee. Na wajua ni wapi Dada Baker atakwenda pale atakapohitaji msaada wa kufungua ukurasa wake wa facebook?

Ninafikiria msaada mkubwa ambao akina dada wa Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama wanaoweza kuwa katika kuwakaribisha wasichana ambao hivi karibuni wamekuwa katika mpango wa Wasichana. Kina dada zetu wadogo mara nyingi wanafikiri kama hawana nafasi sawa na wale wa Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama. Kabla hawajatimiza miaka 18, wanahitaji viongozi wa Wasichana na akina mama ambao kwa furaha watashuhudia juu ya baraka kubwa za Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama. Wanatakiwa wawe na shauku kuwa sehemu ya kundi tukufu. Wakati wasichana wanapoanza kuhudhuria Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama, wanachohitaji zaidi ni rafiki wa kukaa karibu nao, mkono wa kuwakumbatia mabega yao, na nafasi ya kufundisha na kutumikia. Naomba sote tutoke na tusaidiane katika kipindi cha mpito wa maisha yetu.

Asante sana ninyi nyote wanawake wa Kanisa ambao mnasaidia kwa kuvuka mipaka ya umri na tamaduni ili kubariki na kuwatumikia wengine. Wasichana wanatumikia katika madarasa ya watoto ya Msingi na wazee. Kina dada waseja wa marika yote wanatumia masaa mengi wakiwatunza wenye dhiki ambao wapo karibu nao. Tunawatambua maelfu ya wasichana ambao wanatumikia kwa miezi 18 ya maisha yao ili kushiriki injili na ulimwengu. Mambo haya yote ni ushahidi kwamba, kama wimbo wetu unaoenziwa unavyosema, “jukumu la malaika limepwea wanawake.”5

Kama kuna vizuizi, ni kwa sababu sisi wenyewe tumevitengeneza. Lazima tuache kuangalia zaidi tofauti zetu na tuangalie yale tunayofanana kwazo; ndipo tunapoweza kuanza kugundua uwezo wetu mkubwa na kufanikisha mazuri katika ulimwengu huu. Dada Marjorie P. Hinckley aliwahi kusema, ”Ee, ni jinsi gani kila mmoja anamhitaji mwenziwe. Wengi wetu tulio wazee tunawahitaji ninyi vijana. Na natumaini, ninyi mlio vijana mnatuhitaji sisi wazee. Huu ni ukweli wa kijamii kwamba wanawake wanawahitaji wanawake. Tunahitaji kuridhika na urafiki wa kweli na kila mmoja.”6 Dada Hinckley alikuwa sahihi; ee, ni kwa jinsi gani kila mtu anamuhitaji mwenzake!

Akina dada, hakuna kundi lingine la wanawake hapa duniani lenye uwezo kupata baraka nyingi kuliko sisi wanawake wa Watakatifu wa Siku za Mwisho. Sisi ni washiriki wa Kanisa la Bwana, na bila kujali matatizo ya kibinafsi, wote tunaweza kufurahia baraka nyingi za nguvu za ukuhani kwa kutunza maagano tuliyoweka wakati wa ubatizo na katika hekalu. Tuna nabii aliye hai ili kutuongoza na kutufundisha, na tunafaidi zawadi kubwa ya Roho Mtakatifu, ambaye anatumika kama mfariji na kiongozi wa maisha yetu. Tumebarikiwa kufanya kazi bega kwa bega na ndugu wema tunapoziimarisha nyumba na familia zetu. Tuna nafasi ya uwezona nguvu za ibada za hekalu na nyingine zaidi.

Kwa nyongeza ya kufurahia baraka zote hizi, tupo pamoja—akina dada katika injili ya Yesu Kristo. Tumebarikiwa na asili za kusaidia ambazo zinatuwezesha kuonyesha upendo na huduma kama ya Kristo kwa kila aliye karibu nasi. Tunapotazama mbele ya tofauti zetu za umri, tamaduni, na tofauti za kawaida na kutumikiana, tutajazwa na upendo wa Kristo na mwongozo ambao unatuongoza sisi kujua lini na nani wa kumtumikia.

Ninatoa mwaliko kwenu ambao uliwahi kutolewa huko nyuma, na rais wa Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama ambaye alisema, “Ninawalikeni siyo tu mpendane zaidi lakini mpendane vizuri zaidi.7Nategemea kuwa tutagundua ni jinsi gani kila mtu anamhitaji mwingine, naomba tupendane vizuri zaidi, hii ni sala yangu, katika jina la Yesu Kristo, amina.

Onesha KumbukumbuFicha Kumbukumbu

  Muhtasari

  1. Ona Barbara B. Smith, “The Bonds of Sisterhood,” Ensign, Mar. 1983, 20–23.

  2. Mafundisho na Maagano 38:27.

  3. Patricia T. Holland, “‘One Thing Needful’: Becoming Women of Greater Faith in Christ,” Ensign, Oct. 1987, 29.

  4. Luka 1:7.

  5. “As Sisters in Zion,” Hymns, no. 309.

  6. Glimpses into the Life and Heart of Marjorie Pay Hinckley, ed. Virginia H. Pearce (1999), 254–55.

  7. Bonnie D. Parkin, “Choosing Charity: That Good Part,”Ensign or Liahona, Nov. 2003, 106.