2010–2019
Vimbunga vya Kiroho
Aprili 2014


Vimbunga vya Kiroho

Msiache vimbunga viwaangushe chini. Hizi ni siku zenu---simameni imara kama wafuasi wa Bwana Yesu Kristo.

Ninawasalimu asubuhi hii—hususani vijana ambao wapo hapa katika Kituo cha Mkutano na duniani kote. Ninyi ni kizazi teule na naongea hususani na ninyi.

Miaka mingi iliyopita tulipokuwa tunatembelea familia yetu kule Florida, kimbunga kilishuka si mbali sana na sisi. Mwanamke mmoja aliyekuwa akiishi katika nyumba ya mbao, alikimbilia chooni mwake kwa ajili ya usalama. Nyumba ya mbao ikaanza kutikisika. Muda mchache ukapita, kisha akasikia sauti ya jirani yake, “Nipo hapa kwenye chumba cha mbele.” Akitokea chooni, kwa mshangao mkubwa, aligundua kwamba kimbunga kilikuwa kimeichukua nyumba yake kwa hewa, ikirushwa angani, na ikatua salama juu ya nyumba ya mbao ya jirani yake.

Rafiki zangu vijana, dunia haitaendelea kwa utulivu kuelekea Ujio wa Pili wa Yesu Kristo. Maandiko yanatangaza kwamba “vitu vyote vitakuwa katika vurugu.”1Brigham Young alisema, “Ilifunuliwa kwangu mwanzoni mwa Kanisa hili, kwamba Kanisa litasambaa, kuimarika, kukua na kuendelea, na hii ni kulingana na kuenea kwa injili miongoni mwa mataifa ya dunia, hivyo na nguvu ya Shetani itaongezeka.”2

Picha
illustration of tornado

Inayotia wasiwasi zaidi kuliko unabii wa matetemeko ya ardhi na vita3 ndiyo vimbunga vikali vya kiroho ambavyo vinaweza kukung’oa wewe toka kwenye misingi ya kiroho na vinaweza kuitupa roho yako katika sehemu ambazo haukutegemea, wakati mwingine bila hata ya kujua kama ulikuwa umesongezwa.

Vimbunga vibaya ni majaribu ya adui. Dhambi daima imekuwa ni sehemu ya dunia, lakini haijawahi kupatikana kwa urahisi, kutoweza kutoshelezwa, na kukubalika sana. Kunayo, hakika, nguvu kubwa ambayo inaweza kushinda vimbunga vya dhambi. Inaitwa toba.

Siyo vimbunga vyote katika maisha ni vya kujitakia. Vingine vinakuja kwa sababu ya chaguzi mbaya za watu wengine na vingine vinakuja kwa sababu haya ni maisha ya kidunia.

Akiwa kijana mdogo, Rais Boyd K. Packer aliugua ugonjwa wa polio. Wakati Mzee Dallin H. Oaks akiwa na miaka saba, baba yake alifariki ghafla. Wakati Dada Carol F. McConkie wa urais mkuu wa Wasichana akiwa binti, wazazi wake walitengana. Majaribu yatakuja, lakini unapomwamini Mungu, yataimarisha imani yako.

Picha
illustration of tree and roots

Kwa kawaida, miti inayokua katika mazingira ya upepo huwa imara zaidi. Upepo unapovuma katika mti mdogo, nguvu ndani ya mti hufanya vitu viwili. Kwanza, huchochea mizizi ikue haraka na kutawanyika mbali. Pili, nguvu katika mti huanza kujenga umbo la seli ambalo hufanya shina na matawi kuwa manene na huru zaidi kwa nguvu ya upepo. Mizizi na matawi haya imara zaidi yanaulinda mti dhidi ya upepo ambao hakika utarudi.4

Ninyi mna thamani kubwa zaidi kwa Mungu kuliko mti. Ninyi ni wana na binti Zake. Ameiumba nafsi yenu kuwa imara na iweze kuhimili upepo wa maisha. Vimbunga katika maisha yenu ya ujana, kama upepo dhidi ya mti mchanga, vinaweza kuongeza nguvu zenu za kiroho, vikiwaandaa kwa ajili ya miaka ijayo.

Mnajiandaa vipi wakati wa vimbunga? Kumbukeni ... ni juu ya mwamba wa Mkombozi, ambaye ni Kristo, Mwana wa Mungu, mnakoweza kujenga msingi wenu; ili ibilisi atumapo upepo wake, … majaribu katika kimbunga, … wakati wa mvua na dhoruba kali ikiwapiga, isiweze kuwa na nguvu … ya kuwaangusheni chini… kwa sababu ya mwamba ambao mmejengwa.”5 Huu ndio usalama wenu katika kimbunga.

Rais Thomas S.Monson alisema: “Ijapokuwa wakati fulani viwango vya Kanisa na viwango vya jamii vililinganishana kwa kiwango kikubwa, sasa kuna mgawanyiko mkubwa sana kati yetu, na unakua hata mkubwa zaidi.”6Mgawanyiko huu, kwa wengine, unaleta kimbunga kikubwa cha kiroho. Acheni nitoe mfano.

Mwezi uliopita Urais wa Kwanza na Jamii ya Mitume Kumi na Wawili uliandika barua kwa viongozi wa Kanisa ulimwenguni kote. Sehemu ya barua inasoma: Mabadiliko katika sheria za nchi hayabadilishi, hakika hayawezi, kubadilisha sheria ya maadili ambayo Mungu ameweka. Mungu anatarajia sisi tuhimili na kuzishika amri Zake bila kujali upinzani au mambo ya kijamii. Sheria yake ya usafi wa mwili ipo wazi: tendo la ndoa ni sahihi tu kwa mwanamume na mwanamke ambao wameoana kihalali na kisheria kama mume na mke. Tunawaombeni mpitie…mafundisho yaliyopo kwenye “Familia: Tangazo kwa Ulimwengu.’”7

Wakati ulimwengu unapoacha kutii sheria ya Bwana ya usafi wa mwili, sisi hatufanyi hivyo. Rais Monson alisema: “Mwokozi wa wanadamu alijielezea Mwenyewe kama aliye duniani lakini si wa duniani. Pia sisi tunaweza kuwa duniani lakini siyo wa duniani pale tunapokataa mafundisho ya uongo na kuendelea kuwa wakweli katika amri za Mungu.”8

Wakati serikali nyingi na watu binafsi wenye nia nzuri wameiundua upya ndoa, Bwana bado hajaiunda upya. Hapo mwanzoni, Mungu alianzisha ndoa kati ya mwanaume na mwanamke —Adamu na Hawa. Aliweka malengo ya ndoa kuwa zaidi ya kujiridhisha na kujitimiza kwa watu wazima kuwa, kwa kikubwa zaidi, kujenga mazingira bora ya watoto kuzaliwa, kulelewa na kutunzwa. Familia ni hazina ya mbinguni.9

Kwa nini tunaendelea kuongea juu ya haya? Kama alivyosema Paulo, “Hatuviangalii vitu vinavyoonekana, bali vitu visivyoonekana.”10Kama Mitume wa Bwana Yesu Kristo, tunalo jukumu la kufundisha mpango wa Muumba wetu kwa ajili ya watoto Wake na kuonya dhidi ya madhara ya kutotii amri Zake.

Hivi karibuni, niliongea na Laurel kutoka Marekani. Nanukuu kutoka kwenye barua pepe yake.

“Mwaka huu uliopita baadhi ya rafiki zangu kwenye Facebook walianza kuweka habari za ndoa. Wengi walikubaliana na ndoa ya jinsia moja, na baadhi ya vijana wa WSM waliashiria kwamba “walipenda” taarifa zile. Mimi sikutoa maoni.

“Niliamua kutangaza imani yangu katika ndoa asili kwa uangalifu zaidi.

Picha
young woman using a mobile telephone

“Kwenye picha yangu, niliongeza kipengele, ‘Ninaamini katika ndoa kati ya mwanamume na mwanamke.’ Ghafla palepale nilianza kupata ujumbe, ‘Wewe unajipenda.’ ‘Unahukumu.’ Mmoja alinilinganisha na mmiliki watumwa. Na nilipokea ujumbe huu kutoka kwa rafiki yangu mkubwa ambaye ni mshiriki imara wa Kanisa, ‘Unatakiwa kwenda na wakati. Mambo yanabadilika na sisi lazima tubadilike.’

“Sikujibu,” alisema, “lakini sikufuta ujumbe wangu.”

Alimalizia: “Wakati mwingine, kama Rais Monson alivyosema, ‘Inakubidi usimame peke yako.’ Natumaini kama vijana, tutasimama pamoja katika kuwa wakweli kwa Mungu na mafundisho ya manabii Wake walio hai.”11

Cha muhimu sana kwetu kinapaswa kuwa wale wanaokabiliana na hisia za mapenzi ya jinsia moja. Ni kimbunga cha nguvu sana. Nataka kuonyesha upendo wangu na tamaa kwa wale ambao wanakabiliana na jaribio hili la imani na bado wanabakia wa kweli kwa amri za Mungu!12Lakini kila mtu kwa huru wa uamuzi wao na imani, anastahili ukarimu na kujali kwetu.13

Mwokozi alitufundisha kuwapenda sio tu marafiki zetu bali pia wale ambao wanatofautiana nasi—na hata wale wanaotupinga. Alisema: “Kwani mkiwapenda wawapendao, ni zawadi gani mtapata? …Na mkiwasalimu ndungu zenu peke, ni nini mnafanya zaidi ya wengine?”14

Nabii Joseph Smith alituonya “kuweni waangalifu na haki binafsi” na kuikuza mioyo yetu dhidi ya wale wanaoiona dunia tofauti na sisi tuionavyo, hata kutamani kuichukua mabegani mwetu.”15 Katika injili ya Yesu Kristo, hakuna nafasi kwa wajinga, kupigana ama kuwakebehi wengine.

Kama una swali kuhusu ushauri toka kwa viongozi wa Kanisa, tafadhali ongea matatizo yako halisi na wazazi na viongozi wako. Unahitaji nguvu ambazo zinakuja toka kwa kuwaamini manabii wa Bwana. Rais Harold B. Lee alisema: “Usalama pekee tulionao kama washiriki wa Kanisa hili ni… kujifunza namna ya kutii maneno na amri ambazo Bwana atazitoa kwa manabii Wake---Kutakuwa na vitu vinavyohitaji uvumilivu na imani. Unaweza usipende kile kinachokuja….kinaweza kupingana na mtazamo wako wa kisiasa---mtazamo wa kijamii---kupingana na maisha yako. Lakini kama unasikiliza mambo haya, kama vile yanatoka mdomoni mwa Bwana Mwenyewe….milango ya kuzimu haitakushinda….na Bwana Mungu wako ataondoa nguvu za giza toka kwako …’ (M&M 21:6).”16

Ulinzi mwingine mkubwa dhidi ya kimbunga cha maisha ni Kitabu cha Mormoni.

Wakati Rais Henry B. Eyring alipokuwa kijana, familia yake ilihamia katika mji mwingine. Yeye aliona uhamisho ule haufai na akawa na marafiki kidogo. Hakuwa karibu na wanafunzi shuleni pake. Kimbunga kilikuwa kinavuma. Alifanya nini? Alitoa nguvu zake katika kusoma hususani Kitabu cha Mormoni, akikisoma mara nyingi.17Miaka kadhaa baadaye, Rais Eyring alishuhudia: “Ninapenda kwenda katika Kitabu cha Mormoni kukisoma kwa kina na mara nyingi.”18[Ni] ushuhuda wa nguvu ulioandikwa ambao tunao kwamba Yesu ni Kristo.”19

Bwana amewapeni njia nyingine ya kusimama imara. Zawadi ya kiroho kubwa sana kuliko kimbunga cha adui! Alisema,“Simama….mahala patakatifu, na msiyumbe.”20

Nilipokuwa kijana, palikuwa na mahekalu 13 tu katika Kanisa. Sasa yapo 142. Asilimia themanini na tano ya washiriki wa Kanisa sasa wanaishi kilomita 320 toka hekaluni. Bwana amewapa vizazi vyenu fursa kubwa ya kwenda kwenye mahekalu Yake takatifu kuliko kizazi kingine katika historia ya ulimwengu wote.

Mmeshawahi kusimama hekaluni, mkivalia nguo nyeupe, kusubiri kufanya ubatizo? Mlijisikiaje? Kuna mawazo yanayoweza kuguswa ya utakatifu katika hekalu. Amani ya Bwana inashinda vimbunga vyote vya ulimwengu.

Jinsi mnavyojisikia hekaluni ni mpangilio wa vile mnavyotaka kujisikia katika maisha yenu.21

Watafuteni babu zenu na bibi zenu na binamu zenu ambao wamefariki bila ya kwenda hekaluni. Pelekeni majina yao hekaluni mnapoenda.22 Mnapojifunza juu wa mababu zenu mtaona mipango ya maisha, ndoa, watoto; mipango ya wema; na mara kadhaa mipango ambayo mtataka kujiepusha.23

Baadaye hekaluni mtajifunza zaidi juu ya Uumbwaji wa ulimwengu, juu ya mipangilio katika maisha ya Adamu na Hawa, na muhimu zaidi, juu ya Mwokozi wetu Yesu Kristo.

Vijana wangu, akina kaka na akina dada, tunawapenda sana, tunapendezwa ninyi, na kuwaombea. Msiache vimbunga viwaangushe chini. Hizi ni siku zenu---simameni imara kama wafuasi wa Bwana Yesu Kristo.24

Jengeni kwa uthabiti zaidi misingi yenu kwenye jiwe la Mkombozi wenu.

Yathaminini maisha na mafundisho yake yasiyolinganishwa na mengine.

Fuateni kwa dhati zaidi mfano wake na Amri Zake.

Ukumbatieni sana upendo wa Mwokozi, neema na rehema zake, na zawadi kubwa ya Upatanisho Wake.

Mnapofanya hivyo, nawaahidi kwamba mtaona dhoruba ya kimbunga kama ilivyo---majaribu, mahangaiko, ama changamoto za kuwasaidia kukua. Na mnapoishi kwa haki mwaka baada ya mwaka, nawahakikishieni kwamba yale mtakayopitia yatawathibitishia tena na tena kwamba Yesu ni Kristo. Mwamba wa kiroho chini ya miguu yenu utakuwa thabiti na imara. Mtafurahia kwamba Mungu amewawekeni hapa kuwa sehemu ya maandalizi ya mwisho kwa ajili ya kurudi kwa Kristo kitukufu.

Mwokozi alisema, “Sitawaacheni peke yenu: Nitarudi kwenu.”25Hii ndio ahadi Yake kwenu. Najua ahadi hii ni ya kweli. Najua kwamba Anaishi, katika jina la Yesu Kristo, amina.

Muhtasari

  1. Mafundisho na Maagano 88:91.

  2. Discourses of Brigham Young, sel. John A. Widtsoe (1954), 72.

  3. Ona Dallin H. Oaks, “Preparation for the Second Coming,” Ensign amaLiahona, Mei 2004, 7–10.

  4. Ona A. Stokes, A. H. Fitter, and M. P. Coutts, “Responses of Young Trees to Wind and Shading: Effects on Root Architecture,” Journal of Experimental Botany, vol. 46, no. 290 (Sept. 1995), 1139–46.

  5. Helamani 5:12.

  6. Thomas S. Monson, “Priesthood Power,” Ensign amaLiahona, Mei 2011, 66.

  7. First Presidency letter, Mar. 6, 2014; ona pia David A. Bednar, “We Believe in Being Chaste,” Ensign ama Liahona, Mei 2013, 41–44; Dallin H. Oaks, “No Other Gods,” Ensign orLiahona, Nov. 2013, 72–75; For the Strength of Youth (booklet, 2011), 35–37.

  8. Thomas S. Monson,Ensign ama Liahona, Mei 2011, 67.

  9. Mzee Russell M. Nelson said: “Marriage is the foundry for social order. … That union is not merely between husband and wife; it embraces a partnership with God” (“Nurturing Marriage,” Ensign amaLiahona, Mei 2006, 36). Ona piaMathayo 19:5–6.

  10. 2 Wakorintho 4:18.

  11. Personal correspondence and conversation, Mar. 17, 2014; ona pia Thomas S. Monson, “Dare to Stand Alone,” Ensign amaLiahona, Nov. 2011, 60–67.

  12. Ona Jeffrey R. Holland, “Helping Those Who Struggle with Same-Gender Attraction,” Ensign, Oct. 2007, 42–45;Liahona, Oct. 2007, 40–43.

  13. Even when the antichrist Korihor sought to destroy the faith of the people, the laws of God protected him against retribution: “There was no law against a man’s belief; for it was strictly contrary to the commands of God that there should be a law which should bring men on to unequal grounds. … If a man desired to serve God, it was his privilege; … but if he did not believe in him there was no law to punish him” (Alma 30:7, 9). The eleventh article of faith reads, “We claim the privilege of worshiping Almighty God according to the dictates of our own conscience, and allow all men the same privilege, let them worship how, where, or what they may.”

  14. Mathayo 5:46–47.

  15. Teachings of Presidents of the Church: Joseph Smith (2007), 427, 429.

  16. Teachings of Presidents of the Church: Harold B. Lee (2000), 84–85; ona pia Robert D. Hales, “General Conference: Strengthening Faith and Testimony,” Ensign orLiahona, Nov. 2013, 6–8.

  17. Ona Robert I. Eaton and Henry J. Eyring, I Will Lead You Along: The Life of Henry B. Eyring (2013), 40.

  18. Henry B. Eyring, Choose Higher Ground (2013), 38.

  19. Henry B. Eyring, To Draw Closer to God (1997), 118.

  20. Mafundisho na Maagano 87:8; ona piaMafundisho na Maagano 45:32.

  21. OnaMafundisho na Maagano52:14.

  22. Ona Neil L. Andersen, “Find Our Cousins!” (address given at RootsTech 2014 Family History Conference, Feb. 8, 2014); lds.org/prophets-and-apostles/unto-all-the-world/find-our-cousins.

  23. Ona David A. Bednar, “The Hearts of the Children Shall Turn,” Ensign ama Liahona, Nov. 2011, 24–27.

  24. OnaHelamani 7:9.

  25. Yohana 14:18.