2010–2019
Funguo na Mamlaka ya Ukuhani
Aprili 2014


Funguo na Mamlaka ya Ukuhani

Funguo za ukuhani zinawaelekeza wanawake na wanaume vile vile, na maagizo ya ukuhani na mamlaka ya ukuhani yanafungamana na wanawake na wanaume vile vile.

I.

Katika mkutano huu tumeona kupumzishwa kwa ndugu wapendwa, na tumewaidhinisha wale walioitwa. Katika mzingo huu—ambao ni wa kawaida katika Kanisa—hatushuki daraja pale tunapo pumzishwa, na hatupandi daraja pale tunapoitwa kutumikia. Hakuna kupanda wala kushuka katika utumishi wa Bwana. Kuna tu “kusonga mbele au kurudi nyuma,” na tofauti hiyo inategemea jinsi tunavyopokea na kulifanyia kazi tendo la kupumzishwa na kuitwa katika wito. Wakati mmoja nilihudhuria kupumzishwa kwa Rais wa vijana wa kigingi ambaye alihudumu vizuri sana kwa miaka tisa na sasa alikuwa na furaha ya kupumzishwa na katika wito mwingine ambao yeye na mke wake walipokea. Waliitwa kuwa viongozi wa watoto wadogo katika kata yao. Ni katika Kanisa hili pekee ndipo jambo hili linaweza kuwa la kawaida na la heshima!

II.

Akihutubia mkutano mkuu wa wanawake, rais mkuu wa Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama, Linda K. Burton alisema, “Tunatumaini kuzalisha kati yetu wenyewe hamu kubwa ya uelewa wa ukuhani.”1 Haja hiyo inatuhusu sisi wote, na nitaifuatilia kwa kuongea juu ya funguo na mamlaka ya ukuhani. Kwa sababu ya umuhimu wa mada hii kwa wanaume na wanawake, nimefurahi kwamba matangazo haya yanatangazwa na kuchapishwa kwa ajili ya waumini wote wa Kanisa. Nguvu za ukuhani zinatubariki sisi sote. Funguo za ukuhani zinawaongoza wanawake na pia wanaume.

III.

Rais Joseph F. Smith alielezea ukuhani kama “nguvu za Mungu alizopewa mwanadamu ambazo mwanadamu anaweza kufanyia kazi hapa duniani kwa ajili ya wokovu wa familia ya mwanadamu.” 2 Viongozi wengine wamefundisha kwamba ukuhani “ni uwezo wa juu katika dunia hii. Ni uwezo ambao kwao dunia iliumbwa.”3 Maandiko yanafundisha kwamba “ukuhani huu huu, ambao ulikuwepo hapo mwanzo, utakuwepo hata mwisho wa dunia pia” (Musa 6:7). Hivyo, ukuhani ni uwezo ambao kwao tutafufuka na kuendelea katika uzima wa milele.

Uelewa tunaouhitaji unaanza na uelewa wa funguo za ukuhani. “Funguo za ukuhani ni mamlaka ya Mungu ambayo ameyatoa kwa wenye ukuhani ili kuongoza, kuamuru, na kutawala matumizi ya ukuhani hapa duniani.” 4 Kila jambo au ibada inayofanyika Kanisani inafanyika chini ya mwongozo wa moja kwa moja au usio wa moja kwa moja wa ruhusa ya mtu mwenye kushikilia funguo kwa ajili ya kazi hiyo. Kama Mzee M. . Russell Ballard alivyoelezea, “Wale wenye funguo za ukuhani … hakika wanafanya iwezekane kwa wote wanaohudumu kwa haki chini ya mwongozo wao ili kutumia mamlaka ya ukuhani na kuwa na nafasi ya uwezo wa ukuhani.”5

Katika kudhibiti matumizi ya mamlaka ya ukuhani, kazi za funguo za ukuhani ni mbili kukuza na kuzuia. Inakuza kwa kuwezesha mamlaka na baraka za ukuhani kuweza kupatikana kwa watoto wote wa Mungu. Inazuia kwa kuelekeza kuwa ni nani atakayepewa mamlaka ya ukuhani, nani atashikilia ofisi zake, na jinsi gani mamlaka na uwezo utakavyotolewa. Kwa mfano, mtu mwenye ukuhani hawezi kutoa ofisi au mamlaka yake kwa mtu mwingine, isipokuwa awe ameruhusiwa na mtu mwenye funguo. Bila ya ruhusa hiyo, utawazo hautakuwa na maana yoyote. Hii inaeleza kwa nini mwenye ukuhani—bila kujali ofisi—hawezi kumtawaza muumini wa familia yake au kusimamia sakramenti katika nyumba yake mwenyewe bila ya ruhusa kutoka kwa yule anayeshikilia funguo halali.

Isipokuwa kazi takatifu ambazo akina dada wanazifanya hekaluni chini ya funguo alizonazo rais wa hekalu, ambazo nitazizungumzia baadaye, ni yule tu mwenye ofisi ya ukuhani anaweza kusimamia katika ibada za ukuhani. Na ibada zote za ukuhani zilizoruhusiwa zinaandikwa katika kumbukumbu za Kanisa.

Hatimaye, funguo zote za ukuhani zinashikiliwa na Bwana Yesu Kristo, ambaye Yeye ndiye mwenye ukuhani. Yeye ndiye anayeamua ni funguo gani zinatolewa kwa wanadamu na ni jinsi gani hizo funguo zitatumika. Tumezoea kufikiria kwamba funguo zote za ukuhani zilitolewa kwa Joseph Smith katika Hekalu la Kirtland, lakini maandiko yanasema kwamba kile kilichotolewa kilikuwa ni “funguo za kipindi hiki cha nyakati” (M&M 110:16). Kwenye mkutano mkuu miaka mingi iliyopita Rais Spencer W. Kimball alitukumbusha kwamba kuna funguo zingine ambazo hazijatolewa kwa mwanandamu duniani, zikiwemo funguo za uumbaji na ufufuko.6

Asili ya kiungu ya udhibiti unafanya utumiaji wa funguo za ukuhani kuelezea tofauti muhimu kati ya maamuzi juu ya mambo ya utawala wa Kanisa na maamuzi yahusuyo ukuhani. Urais wa Kwanza na Baraza la Urais wa Kwanza na Jamii ya Kumi na Wawili, wanaosimamia katika Kanisa, wameruhusiwa kufanya maamuzi mengi yahusuyo sheria na taratibu za Kanisa—mambo kama vile sehemu za majengo ya Kanisa na umri kwa ajili ya utumishi wa umisionari. Lakini hata hivyo hawa viongozi wasimamizi wana na wanatumia funguo zote ambazo zimetolewa kwa wanaume katika kipindi hiki, hawapo huru kutangaza mpango mtukufu kwamba wanaume tu ndiyowatakuwa wanashikilia ofisi katika ukuhani.

IV.

Sasa naja kwenye mada ya mamlaka ya ukuhani. Ninaanza na kanuni tatu ambazo zimejadiliwa: (1) ukuhani ni uwezo wa Mungu aliopewa mwanandamu kutenda kwa ajili ya wokovu wa familia ya mwanadamu, (2)  mamlaka ya ukuhani yanasimamiwa na wale wenye ukuhani ambao wana funguo za ukuhani, na (3) kwa sababu maandiko yanasema kwamba “mamlaka mengine yote [na] ofisi katika kanisa ni kiambatisho katika ukuhani huu wa [Melkizedeki]” (M&M 107:5), yale yote yanayofanyika chini ya usimamizi wa funguo hizo za ukuhani yanafanyika kwa mamlaka ya ukuhani.

Hii inahusiana vipi kwa wanawake? Katika hotuba ya Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama, Rais Joseph Fielding Smith, wakati huo akiwa Rais wa Jamii ya Mitume Kumi na Wawili, alisema haya: “Wakati kina dada hawajapewa Ukuhani, haujatolewa kwao, hiyo haimaanishi kwamba Bwana hajawapa mamlaka…. Mtu anaweza kuwa na mamlaka aliyopewa, au kupewa kwa dada, ili afanye mambo fulani katika Kanisa ambayo ni muhimu kwa ajili ya wokovu wetu, kama vile kazi ambazo dada zetu wanazifanya katika nyumba ya Bwana. Wana mamlaka waliyopewa ili kufanya mambo makubwa na ya ajabu, matakatifu kwa Bwana, na kuunganisha kama vile baraka zinazotolewa kwa wanaume wenye Ukuhani.”7

Katika hotuba hiyo nzuri, Rais Smith alisema tena na tena kwamba wanawake wamepewa mamlaka. Kwa wanawake alisema, “Mnaweza kuzungumza kwa mamlaka, kwa sababu Bwana ameweka mamlaka juu yenu.” Pia Alisema kwamba Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama “umepewa uwezo na mamlaka ya kutenda mambo mengi makubwa. Kazi wanayoifanya inafanywa kwa mamlaka matakatifu. Na kwa hakika, kazi ya Kanisa inafanywa na wanawake na wanaume, iwe hekaluni au katika kata au matawi, inafanywa chini ya mwongozo wa wale wenye funguo za ukuhani. Hivyo, tukizungumzia Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama, Rais Smith alielezea, [Bwana] amewapa wao kundi hili kuu ambapo wana mamlaka ya kuhudumu chini ya mwongozo wa maaskofu wa kata … , wakiangalia maslahi ya watu wetu yote kiroho na kimwili.”8

Hivyo, imesemwa kweli kwamba kwa Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama siyo darasa la wanawake tu balini sehemu wanayostahili kuwepo—iliyoanzishwa kiroho kama kiambatisho cha ukuhani.9

Hatuna mazoea ya kuzungumza juu ya wanawake kuwa na mamlaka ya ukuhani katika miito yao ya Kanisani, lakini yanaweza kuwa mamlaka gani mengine? Wakati mwanamke—kijana au mzee—anaposimikwa kufundisha injili kama mmisionari, anapewa mamlaka ya ukuhani kufanya kazi za ukuhani. Hiyo ni kweli wakati mwanamke anaposimikwa kufanya kazi kama afisa au mwalimu katika utaratibu wa Kanisa chini ya usimamizi wa yule anayeshikilia funguo za ukuhani. Yeyote anayefanya kazi katika ofisi au wito uliotoka kwa mtu mwenye funguo za ukuhani anatumia mamlaka ya ukuhani katika kutenda kazi yake aliyopangiwa.

Yeyote anayetumia mamlaka ya ukuhani wanapaswa kusahau kuhusu haki zao na wazingatie zaidi majukumu yao. Hiyo ndiyo kanuni inayohitajika katika jamii kiujumla. Mwandishi wa Mrusi anayejulikana sasa Aleksandr Solzhenitsyn alinukuliwa akisema, “Huu ni wakati … wa kujilinda dhidi ya haki nyingi za binadamu kama ilivyo wajibu wa mwanadamu.”10 Watakatifu wa Siku za Mwisho hakika wanatambua kwamba ili kuweza kutukuka si jambo la kudai haki lakini ni jambo la kutimiza majukumu.

V.

Bwana ametoa mwongozo kwamba ni wanaume pekee ambao watatawazwa katika ofisi ya ukuhani. Lakini kama baadhi ya viongozi wa Makanisa mengine walivyosisitiza, wanaume sio “ukuhani.” 11 Wanaume wanashikilia ukuhani, pamoja na wajibu mtakatifu wa kuutumia kwa ajili ya baraka kwa watoto wote wa Mungu.

Uwezo mkubwa zaidi ambao Mungu amewapa wanawe hauwezi kutendewa kazi bila ya ushirikiano na mmoja wa mabinti Zake, kwa sababu ni kwa kupitia mabinti Zake pekee Mungu ametoa uwezo “wa kuwa waumbaji wa miili … ili kusudi la Mungu na Mpango Mkuu uweze kuleta matunda.”12 Hayo ni maneno ya Rais J. Reuben Clark.

Aliendelea: “Hapa ni mahali pa wake zetu na mahali pa mama zetu katika Mpango wa Milele. Wao hawana Ukuhani; hawapewi wajibu wa kutenda kazi na majukumu ya Ukuhani, wala hawapewi mzigo wa majukumu yake; wao ni wajenzi na wapangaji chini ya nguvu zake, na wapokeaji wa baraka zake, wakiwa na msaada wa nguvu za ukuhani na wakiwa na majukumu kama vile yaitwavyo kiungu, kama ilivyo muhimu katika nafasi yake ya umilele kama ulivyo Ukuhani wenyewe.”13

Katika maneno yale mazuri, Rais Clark alikuwa anazungumza juu ya familia. Kama ilivyoelezwa katika tangazo la familia, baba ni msimamizi wa familia, na yeye na mama wana majukumu tofauti, lakini “wanawajibika kusaidiana kama wenza sawa.”14 Miaka kadhaa kabla ya tangazo kwa familia, Rais Spencer W. Kimball alitoa ufafanuzi wenye maongozi: “Tunapozungumzia ndoa kama uhusiano wa pamoja, acheni sisi tuzungumzie ndoa kama uhusiano ulio kamili. Hatutaki wanawake wetu wa WSM wawe wenzi baridi au wenzi wenye mapungufu katika majukumu ya milele! Tafadhali kuweni wenzi wenye kuchangia na wenzi kamili.”15

Machoni pa Mungu, iwe Kanisani au katika familia, wanawake na wanaume wako sawa, na wana majukumu tofauti.

Ninafunga kwa baadhi ya kweli kuhusu baraka za ukuhani. Tofauti na funguo za ukuhani na ibada za ukuhani, baraka za ukuhani zinapatikana kwa wanawake na kwa wanaume kwa njia moja. Kipawa cha Roho Mtakatifu na baraka za hekalu ni mfano halisi wa ukweli huu.

Kwenye maongezi yake mazuri katika Wiki ya Elimu ya BYU, Mzee . M. Russell Ballard alitoa mafundisho haya:

“Mafundisho ya Kanisa letu yanawaweka wanawake sawa na, na hali tofauti na wanaume. Mungu hajaifanya jinsia moja kuwa ni nzuri au muhimu kuliko ingine. …

“Wakati wanaume na wanawake wanapokwenda hekaluni, wote wanawekwa wakfu kwa nguvu sawa, ambayo ni nguvu za ukuhani. … Fursa ya nguvu na baraka za ukuhani inapatikana kwa watoto wote wa Mungu.”16

Ninashuhudia juu ya nguvu na baraka za ukuhani wa Mungu, zipatikanazo kwa wana na binti Zake pia. Ninashuhudia juu ya mamlaka ya ukuhani, ambayo yanafanya kazi kupitia kwa ofisi na kazi zote za Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho. Ninashuhudia juu ya mwongozo wa kazi tukufu za funguo za ukuhani, zinazoshikiliwa na kutendewa kazi kwa ukamilifu wake na nabii/rais wetu, Thomas S. Monson. Mwisho na muhimu zaidi, ninashuhudia juu ya Bwana na Mwokozi wetu, Yesu Kristo, ambaye huu ndio ukuhani wake na sisi ndiyo watumishi wake, katika jina la Yesu kristo, amina.

Muhktasari

  1. Linda K. Burton, “Priesthood: ‘A Sacred Trust to Be Used for the Benefit of Men, Women, and Children’” (Brigham Young University Women’s Conference address, May 3, 2013), 1; ce.byu.edu/cw/womensconference/transcripts.php.

  2. Joseph F. Smith, Gospel Doctrine, 5th ed. (1939), 139.

  3. Boyd K. Packer, “Priesthood Power in the Home” (worldwide leadership training meeting, Feb. 2012); lds.org/broadcasts; see also James E. Faust, “Power of the Priesthood,” Ensign, May 1997, 41–43.

  4. Handbook 2: Administering the Church (2010), 2.1.1.

  5. M. Russell Ballard, “Men and Women in the Work of the Lord,” New Era, Apr. 2014, 4;Liahona, Apr. 2014, 48; ona pia Daughters in My Kingdom: The History and Work of Relief Society (2011), 138.

  6. Ona Spencer W. Kimball, “Our Great Potential,” Ensign, May 1977, 49.

  7. Joseph Fielding Smith, “Relief Society—an Aid to the Priesthood,” Relief Society Magazine, Jan. 1959, 4.

  8. Joseph Fielding Smith, “Relief Society—an Aid to the Priesthood,” 4, 5; ona pia Teachings of Presidents of the Church: Joseph Fielding Smith (2013), 302.

  9. Ona Boyd K. Packer, “The Relief Society,” Ensign, May 1998, 72; ona pia Daughters in My Kingdom, 138.

  10. Aleksandr Solzhenitsyn, “A World Split Apart” (commencement address delivered at Harvard University, June 8, 1978); ona pia Patricia T. Holland, “A Woman’s Perspective on the Priesthood,” Ensign, July 1980, 25; Tambuli, June 1982, 23; Dallin H. Oaks, “Rights and Responsibilities,” Mercer Law Review, vol. 36, no. 2 (winter 1985), 427–42.

  11. Ona James E. Faust, “You Are All Heaven Sent,” Ensign au Liahona, Nov. 2002, 113; M. Russell Ballard, “This Is My Work and Glory,” Ensign auLiahona, May 2013, 19; Dallin H. Oaks, “Priesthood Authority in the Family and the Church,” Ensign auLiahona, Nov. 2005, 26. Sisi wakati mwengine tunasema kwamba Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama ni “mwenzi wa ukuhani.”It kuwa sahihi sana kusema kwamba katika kazi ya Bwana Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama na wanawake wa Kanisa ni wenzi na wenye ukuhani.”

  12. J. Reuben Clark Jr., “Our Wives and Our Mothers in the Eternal Plan,” Relief Society Magazine, Dec. 1946, 800.

  13. J. Reuben Clark Jr., “Our Wives and Our Mothers,” 801.

  14. “Familia: Tangazo kwa Ulimwengu,” Ensign au Liahona, Nov. 2010, 129.

  15. Spencer W. Kimball, “Privileges and Responsibilities of Sisters,” Ensign, Nov. 1978, 106.

  16. M. Russell Ballard, New Era, Apr. 2014, 4;Liahona, Apr. 2014, 48; ona pia Sheri L. Dew, Women and the Priesthood (2013), especially chapter 6, for a valuable elaboration of the doctrines stated here.