2010–2019
Shahidi
Aprili 2014


Shahidi

Ningependa kushiriki nanyi zile kweli ambazo ni za thamani sana kuzijua.

Nyakati za vita au utovu wa hakika zina njia ya kunoa msisitizo wetu kwenye vitu ambavyo vina maana kihalisi.

Vita vya Dunia vya Pili ilikuwa ni wakati wa msukosuko mkubwa wa kiroho kwangu. Nilikuwa nimeondoka nyumbani kwetu Mjini Brigham, Utah, nikiwa na kijinga cha moto cha ushuhuda na nilihisi haja ya kitu fulani zaidi. Karibu darasa kuu lote katika kipindi cha majumaa likikuwa njiani kwenda kwenye eneo la vita. Nilipokuwa katika kisiwa cha Ie Shima, kaskazini tu mwa Okinawa, Japani, nilisumbuliwa na shaka na utovu wa hakika. Nilikuwa nikitaka ushuhuda wa kibinasfi wa injili. Nilitaka kujua!

Wakati wa usiku mmoja nikikosa usingizi, niliondoka kutoka kwa hema letu na kuingia katika handaki ambalo lilitengenezwa kwa madramu ya galani 50 za mafuta zilizojazwa na changarawe na kuweka moja juu ya ingine kujenga boma. Halikuwa na paa, na kwa hivyo nilitambaa ndani, likatazama juu kwenye anga iliyojaa nyota, na nikapiga magoti kusali.

Karibu tu katikati ya sentensi kitu kikatoa. Mimi siwezi kuelezea kwenu kile kilichotokea kama ningeamua kufanya hivyo. Ilikuwa ni zaidi ya nguvu zangu za kuelezea, lakini ni wazi leo kama ilivyokuwa usiku huo zaidi ya miaka 65 iliyopita. Nilijua ilikuwa ni maonyesho ya kisiri sana na kibinafsi sana. Basi nilijijulia mwenyewe. Nilijua kwa uhakika, kuwa imetolewa kwangu. Baada ya muda fulani, nilitambaa kutoka kwenye handaki na kutembea, au kuelea, kurudi kitandani kwangu. Mimi nilitumia salio la usiku katika hisia ya furaha na mshangao.

Kando na kufikiria mimi nilikuwa mtu maalum, nilifikiria kwamba kama kitu kama hicho kilikuja kwangu, basi kingekuja kwa mtu yeyote. Mimi bado naamini hivyo. Katika miaka ambayo iliyofuata, nimekuja kuelewa kwamba uzoefu kama huo ni mara moja nuru ya kufuata na mzigo wa kubeba.

Mimi natamani kushiriki nanyi kweli hizo ambazo ni za thamani sana kujua, vitu ambavyo mimi nimejifunza na kupata uzoefu navyo katika karibu miaka 90 ya maisha na zaidi ya miaka 50 kama Kiongozi mwenye Mamlaka. Mengi ya yale nimekuja kujua inakuwa katika aina ya vitu ambavyo haviwezi kufunzwa lakini vinaweza kujifunzwa.

Kama vile katika vitu vya thamani kuu, ufahamu ambao ni wa thamani ya milele huja tu kupitia kwa maombi ya kibinafsi na kutafakari. Hayo, yakiunganishwa na kufunga na kujifunza maandiko, yataalika maonyesho na mafunuo na minong’ono ya Roho Mtakatifu. Hii inatupatia sisi maelekezo kutoka juu tunapojifunza fundisho juu ya fundisho.

Mafunuo yanaahidi kwamba “Kanuni yoyote ya akili tuipatayo katika maisha haya, itafufuka pamoja nasi katika ufufuko” na kwamba “maarifa na akili katika maisha haya kwa njia … juhudi yake na utii” (M&M 130:18–19).

Ukweli mmoja wa milele ambao mimi nimekuja kujua ni kwamba Mungu yu hai. Yeye ni Baba yetu. Sisi ni watoto Wake. “Tunaamini katika Mungu, Baba wa Milele, na katika Mwanawe, Yesu Kristo, na katika Roho Mtakatifu” (Makala ya Imani 1:1).

Kati ya majina mengine yote ambayo Yeye angeweza kutumia, Yeye alichagua kuitwa “Baba.” Mwokozi aliamuru, “Basi ninyi salini hivi; Baba yetu uliye mbinguni” (3 Nefi 13:9; ona pia Mathayo 6:9). Matumizi Yake ya jina “Baba” ni somo kwa wote tunapokuja kuelewa kile kilicho na maana sana katika maisha haya.

Uzazi ni fursa takatifu, na kutegemea juu ya uaminifu, inaweza kuwa baraka ya milele. Hatima ya mwisho wa shughuli zote katika Kanisa ni kwamba mtu na mkewe na watoto wao wanaweza kuwa na furaha nyumbani.

Wale waiooa au wale ambao hawawezi kupata watoto hawajaondolewa kutoka kwa baraka za milele wanazotafuta lakini ambazo, kwa sasa, zinabakia kuwa mbali na mfikio wao. Sisi daima hatujui jinsi au wakati baraka zitajiwasilisha zenyewe, lakini ahadi ya mazalisho ya milele haitazuiwa kwa mtu yeyote ambaye hufanya na huweka maagano matakatifu.

Tamaa za kisiri na kusihi kwa majonzi kutagusa moyo wa wote Baba na Mwana. Utapatiwa uhakikisho wa kibinafsi kutoka Kwao kwamba maisha yako yatajaa na kwamba hakuna baraka ambayo ni muhimu itakayopotea.

Kama mtumishi wa Bwana, nikitenda katika ofisi ambayo mimi nimetawazwa, ninatoa kwa wale walio katika hali kama hizo ahadi kwamba hakuna chochote muhimu kwa wokovu wako na kuinuliwa kwako ambacho hakitakuja juu yako. Mikono ambayo sasa ni mitupu itajazwa, na mioyo sasa inayoumia kutoka kwa ndoto zilizovunjika na kutamani zitaponywa.

Ukweli mwingine nimekuja kujua ni kwamba Roho Mtakatifu ni halisi. Yeye ni mshiriki wa tatu wa Uungu. Kazi yake ni kushuhudia ukweli na wema. Yeye hujionyesha Mwenyewe katika njia nyingi, ikijumuisha hisia za amani na hakikisho. Yeye pia anaweza kuleta faraja, mwongozo, na marekebisho yanayohitajika. Uenzi wa Roho Mtakatifu unadumuishwa kote katika maisha yetu kwa kuishi kwa haki.

Kipawa cha Roho Mtakatifu hutolewa kupitia kwa ibada za injili. Mtu mwenye mamlaka huwekelea mikono yake juu ya kichwa cha mshiriki mpya wa Kanisa na kusema maneno kama haya: “Pokea Roho Mtakatifu.”

Ibada hii peke yake haitubadilishi sisi kwa njia inayoweza kuonekana, lakini kama sisi tutasikiliza na kufuata minong’ono, tutapokea baraka za Roho Mtakatifu. Kila mwana au binti wa Baba yetu wa Mbinguni anaweza kuja kujua uhalisi wa ahadi ya Moroni: “Na kwa uwezo wa Roho Mtakatifu mtajua ukweli wa vitu vyote” (Moroni 10:5;mkazo umeongezewa).

Ukweli kutoka juu ambao mimi nimeupokea katika maisha yangu ni ushuhuda wa Bwana Yesu Kristo.

Kikuu na kinachotegemeza yale yote sisi tunafanya, kimejikita kote kwenye mafunuo, ni jina la Bwana, ambalo ndiyo mamlaka ambayo kwayo sisi tunatenda katika Kanisa. Kila sala inayotolewa, hata na watoto wadogo, inaishia katika jina la Yesu Kristo. Kila baraka, kila agizo, kila utawazo, kila kitendo rasmi kinafanywa katika jina la Yesu Kristo. Hili ni Kanisa Lake, na limeitwa kwa jina Lake---Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho (ona M&M 115:4).

Kuna lile tukio kuu katika Kitabu cha Mormoni ambapo Wanefi “walikuwa wakiomba kwa Baba katika jina la [Bwana]. Bwana alitokezea na kuuliza:

“Ni kitu gani mnachohitaji kwamba niwapatie?

“Na wakamwambia: Bwana tunataka kwamba utuambie jina ambalo tutaita hili kanisa; kwani kuna ugomvi miongoni mwa watu kuhusu hili jambo.

“Na Bwana akawaambia: Amin, amin, nawaambia, kwa nini watu wananung’unika na kubishana kwa sababu ya kitu hiki?

“Je, hawajasoma maandiko, ambayo yanasema, lazima mjivike juu yenu jina la Kristo, ambalo ni jina langu? Kwani, kwa jina hili ndilo mtaitwa nalo katika siku ya mwisho;

“Na yeyote atakayechukua jina langu na kuvumilia hadi mwisho, huyo huyo ndiye atakayeokolewa. …

“Kwa hivyo chochote mtakachofanya, mfanye katika jina langu; kwa hivyo mtaliita kanisa katika jina langu; na mtalingana Baba katika jina langu ili aweze kubariki kanisa kwa ajili yangu” (3 Nefi 27:2–7).

Ndiyo jina Lake, Yesu Kristo, “kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo” (Matendo ya Mitume 4:12).

Katika Kanisa sisi tunajua Yeye ni nani: Yesu Kristo, Mwana wa Mungu. Yeye ndiye Mzaliwa wa Pekee wa Baba. Yeye ndiye ambaye aliuawa na Yeye ndiye anayeishi leo. Yeye ndiye Mtetezi wetu kwa Baba. “Kumbukeni kwamba ni juu ya mwamba wa Mkombozi wetu, ambaye ni Kristo, Mwana wa Mungu, kwamba lazima [sisi] tujenge msingi [wetu]” (Helamani 5:12). Yeye ndiye nanga ambayo inatushikilia na kutulinda sisi na familia zetu kuptitia dhoruba za maisha.

Kila Jumapili kote ulimwenguni ambako mikusanyiko hukutana ya taifa lolote au ndimi, sakramenti inabarikiwa kwa maneno sawa. Sisi tunajichukulia juu yetu wenyewe jina la Kristo na daima kumkumbuka Yeye. Hiyo imepigwa chapa juu yetu.

Nabii Nefi alitangaza, “Na tunazungumza kuhusu Kristo, tunafurahia katika Kristo, tunahubiri kuhusu Kristo, tunatoa unabii kumhusu Kristo, na tunaandika kulingana na unabii wetu, ili watoto wetu wajue asili ya kutegemea msamaha wa dhambi zao” (2 Nefi 25:26).

Kila mmoja wetu sharti apate ushuhuda wake wa kibinafsi wa Bwana Yesu Kristo. Sisi basi lazima tushiriki ushuhuda huo na familia zetu na wengine.

Katika haya yote, acha tukumbuke kwamba kuna adui ambaye kibinafsi anataka kuvuruga kazi ya Bwana. Sisi sharti tuchague ni nani tutamfuata. Ulinzi wetu ni rahisi kama kuamua kibinafsi kumfuata Mwokozi, tukihakikisha kwamba sisi tutabakia waaminifu kwenye upande Wake.

Katika Agano Jipya, Yohana aliandika kwamba kulikuwa na wengine ambao hawakuweza kujiweka sharti kwa Mwokozi na mafundisho Yake, na “kwa ajili ya hayo wengi miongoni mwa wanafunzi wake wakarejea nyuma, wasiandamane naye tena.

“Basi Yesu akawaambia wale Thenashara, Je! Ninyi nanyi mwataka kuondoka?

“Basi Simoni Petro akamjibu, Bwana! Twende kwa nani? Wewe unayo maneno ya uzima wa milele.

“Nasi tumesadiki, tena tumejua, ya kuwa wewe ndiwe Mtakatifu wa Mungu” (Yohana 6:66–69).

Petro alikuwa amepata kile ambacho kinaweza kujifunzwa na kila mfuasi wa Mwokozi. Kujitolea kwa uaminifu kwa Yesu Kristo, sisi tunamkubali Yeye kama Mkombozi wetu na tunafanya yote yaliyo katika uwezo wetu kuishi mafundisho Yake.

Baada ya miaka yote ambayo mimi nimeishi na kufunza na kuhudumu, baada ya mamilioni ya maili ambayo mimi nimesafiri duniani kote, kwa yote yale nimeyapitia, kuna ukweli mmoja mkuu ambao mimi ningependa kushiriki. Nao ni ushahidi wangu wa Mwokozi Yesu Kristo.

Joseph Smith na Sidney Rigdon waliandika yafuatayo baada ya tukio takatifu:

Na sasa, baada ya ushuhuda mwingi uliokwisha kutolewa juu yake, huu ni ushuhuda, wa mwisho wa zote, ambao tunautoa juu yake: Kwamba yu hai!

“Kwani tulimwona” (M&M 76:22–23).

Maneno yao ni maneno yangu.

Mimi ninaamini na Mimi nina hakika kwamba Yesu ndiye Kristo, Mwana wa Mungu, na Yeye yu hai Yeye ndiye Mzaliwa wa Pekee wa Baba, na “kwa yeye, na kwa njia yake, na kutoka kwake, dunia zipo na ziliumbwa, na waliomo ni wana na mabinti wa Mungu” (M&M 76:24).

Mimi natoa ushuhuda wangu kwamba Mwokozi yu hai. Mimi namjua Bwana. Mimi ni shahidi Wake. Mimi najua dhabihu Yake kubwa na upendo Wake wa milele kwa watoto wote wa Baba wa Mbinguni. Mimi natoa ushahidi maalum kwa unyenyekevu lakini kwa uhakika kabisa, katika jina la Yesu Kristo, amina.