Ruka uongozaji mkuu
Aprili 2014 | Karibuni Kwenye Mkutano Mkuu

Karibuni Kwenye Mkutano Mkuu

Aprili 2014 Mkutano Mkuu

Tumeungana katika imani yetu na matumaini yetu kusikiliza na kujifunaza kutoka jumbe ambazo zitatolewa kwetu.

Ndugu na akina Dada wapendwa, nina furaha jinsi gani kuwakaribisheni kwenye mkutano huu mkuu wa ulimwenguni kote wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho. Tumekusanyika hapa pamoja kama Familia kubwa, zaidi ya washiriki milioni 15, tulioungana katika imani yetu na matumaini yetu kusikiliza na kujifunza kutoka jumbe ambazo zitatolewa kwetu.

Miezi sita iliyopita imesonga mbele haraka sana vivyo hivyo kazi ya Kanisa imeendelea mbele bila pingamizi. Ilikuwa heshima kwangu takribani mwezi mmoja uliopita kuweka wakfu Hekalu la Gilbert Arizona, jengo zuri sana. Jioni kabla ya kuweka wakfu, tukio la kitamaduni lilifanyika katika Discovery Park iliyo jirani. Vijana elfu kumi na mbili walifanya onyesho la dakika 90. Uchezaji, uimbaji, na maonyesho ya muziki yalikuwa ya hali ya juu.

Eneo hili limekuwa linakumbwa hususani na majira ya ukame, na ninaamini maombi mengi yametumwa kuelekea Mbinguni kwa zaidi ya wiki saba zilizotangulia kwa ajili ya mvua inayohitajika sana. Kwa bahati mbaya mvua ilianza muda mfupi kabla ya onyesho na ilinyesha wakati wote wa maonyesho! Licha ya kwamba vijana walilowa chepe chepe katika mvua na walipata mzizimo kutoka na hali ya baridi, sote tulihisi Roho wa Bwana. Mada ya mpango ilikuwa, “Ishi Maisha Yako kwa Kuwa Mwaminifu” fikiria kuhusu mada hiyo: “Ishi Maisha Yako kwa Kuwa Mwaminifu” ilionyeshwa vizuri sana na tabasamu ya wavulana na wasichana wenye shauku kubwa. Licha ya baridi na mvua, hii ilikuwa ni uzoefu uliojaa imani na mwongozo ambao vijana hawa siku zote watauthamini na watawaeleza watoto wao na wajukuu katika miaka ijayo.

Siku uliyofuata, uwekaji Wakfu wa Hekalu la Gilbert Arizona ulifanyika. Likawa hekalu la 142 linalofanya kazi katika Kanisa. Tofauti na jioni iliyopita, siku ilikuwa mzuri na ilijaa mwanga wa jua.Vikao vilikuwa kwa kweli na mwongozo wa kiungu. Waliohudhuria pamoja nami walikuwa Rais Henry  B. Eyring, Mzee na Dada Tad R. Callister, Mzee na Dada William  R. Walker, na Mzee na Dada Kent F. Richards

Katika mwezi wa Mei Hekalu la Fort Lauderdale Florida litawekwa Wakfu. Mahekalu mengine yamepangiwa kumalizika na kuwekwa wakfu baadaye mwaka huu. Katika mwaka 2015 tunatumaini kumaliza na kuweka wakfu Mahekalu mapya katika sehemu nyingi ulimwenguni. Mwenendo huu utaendelea. Wakati Mahekalu yote yaliyotangazwa hapo nyuma yatakapomalizika, tutakuwa na Mahekalu 170 yafanyayo kazi ulimwenguni kote.

Ingawa kwa sasa tunalenga juhudi zetu kwenye kumaliza mahekalu yaliyotangazwa hapo awali na hatutakuwa tukitangaza mahekalu yeyote mapya katika wakati wa hivi karibuni, tutaendelea na mchakato wa kuamua mahitaji na wa kutafuta mahali kwa ajili ya mahekalu yatakayokuja. Kisha matangazo yatafanywa katika mikutano mikuu ijayo. Sisi ni wajenzi wa mahekalu na watu wahudhuriao mahekalu.

Sasa, ndugu na akina daada, tuna dukuduku ya kusikiliza jumbe ambazo zitatolewa kwetu leo na kesho. Wale ambao watazungumza nasi wametafuta msaada wa mbinguni na maelekezo walipokuwa wanatayarisha jumbe zao.

Natumai---sote, tulio hapa na kwingineko---tutajazwa na Roho wa Bwana na kutiwa moyo na kutiwa msukumo tunaposikiliza na kujifunza. Katika jina la Yesu Kristo, Mkombozi wetu, amina.