2010–2019
Unafikiria Nini?
Aprili 2014


Unafikiria Nini?

Nawasihi ninyi mfanyie mazoezi kuuliza swali hili, kwa fikra ororo kwa uzoefu wa wengine: “Unafikiria nini?”

Miaka arubaini na moja iliyopita nilipanda kwenye kiti cha dereva cha lori lenye miguu kumi na minane nikiwa na mke wangu mrembo, Jan, na mwana wetu mchanga Scotty. Tulikuwa tunabeba mzigo mzito wa vifaa vya ujenzi kupitia majimbo kadhaa.

Katika siku hizo hakukuwa na sheria juu ya matumizi ya mishipi ya gari ama viti vya watoto. Mke wangu alimbeba mtoto wetu mwenye thamani katika mikono yake. Maneno yake, “Kweli tuko juu sana na ardhi,” yangenipa dokezo kuhusu hisia zake za wasiwasi.

Tulipokuwa tunateremka katika Donner Pass ya kihistoria, sehemu iliyoinuka ghafla ya barabara kuu, chumba cha mwendeshi cha lori mara moja na bila kutarajiwa kilijaa moshi mzito. Ikawa vigumu kuona na sisi hatungeweza kupumua vyema.

Kwa gari zito kubwa, breki pekee zake hazitoshi kupunguza kasi kwa haraka. Nikutumia breki za injini na kupunguza gia, nilijaribu kwa hangaiko kusimama.

Mara tu nilivyokuwa ninaenda kusimama kando ya barabara, lakini kabla tusimame kabisa, mke wangu alifungua mlango wa chumba cha mwendeshi lori na kuruka nje akiwa na mtoto wetu mkononi mwake. Nilitazama bila uwezo wa kufanya lolote wakiporomoka mchangani.

Punde niliposimamisha lori, nilikimbia kutoka kwa chumba cha mwendeshi kilichokuwa kimejaa moshi. Na adrenalini ikipigwa mwilini, nilikimbia kupitia mawe na magugu na kuwakumbatia mikononi mwangu. Mikono wa viwiko vya Jan vilikuwa vimeumia na kutoka damu, lakini kwa bahati mzuri yeye na mwana wetu walikuwa wanapumua. Niliwakumbatia tu karibu kivumbi kilipokuwa kinatulia hapo kando ya barabara kuu.

Pigo la moyo wangu lilipokuwa linakaribia kupiga kama kawaida na nikashika pumzi, niliropokwa, “Jameni, ni nini ulikuwa unafikiria? Unajua hiyo ilikuwa hatari jinsi gani? Ungeuwawa!”

Aliniangalia, na machozi yakimwagika chini ya mashavu yaliyochafuliwa kwa moshi, na kusema kitu kilichochoma moyo wangu na bado kinapiga mwangwi katika masikio yangu: “Nilikuwa najaribu tu kumwokoa mwana wetu.”

Niligundua katika wakati huo alifikiria injini ilikuwa imeshika moto, akiwa na hofu lori lingelipuka, na tungekufa. Mimi, hata hivyo, nilijua kwamba ilikuwa hitilafu ya umeme---hatari lakini isiyoua. Nilimuangalia mke wangu wa thamani, akipapasa polepole kichwa cha mwana wetu mchanga, na nikashangaa ni aina gani ya mwanamke angefanya jambo la ujasiri hivi---na lisilo na mantiki kamwe.

Hali hii ingekuwa ya hatari kihisia kama vile hitilafu ya kweli ya injini yetu. Kwa shukrani, baada ya kuvumulia kunyamaziwa kwa muda ya kutosha, kila mmoja wetu akiamini yule mwingine alikuwa na hatia, hatimaye tulishiriki hisia zilizokuwa zinachemka chini ya milipuko yetu ya hasira. Hisia za upendo na hofu zilizoshirikishwa kwa ajili ya usalama wa yule mwingine zilizuia tukio la hatari kuwa la uangamizi kwa ndoa yetu bora kabisa.

Paulo alionya, “Neno lolote lilio ovu lisitoke vinywani mwenu, bali lililo jema la kumfaa mwenye kuhitaji, ili liwape neema wanaosikia” (Waefeso 4:29). Maneno yake yanavuma na kiasi fulani cha usafi.

Kishazi “neno lolote lililo ovu” kinamaanisha nini kwako? Sisi sote hupitia mara kwa mara hisia kali za hasira---zetu wenyewe na za wengine. Tumeona hasira isiyozuiwa ikilipuka hadharani. Tumeipitia kama aina ya “hitilafu ya umeme” ya kihisia katika michezo, uwanja wa kisiasa, na hata katika nyumba zetu wenyewe.

Watoto wakati mwingine huwazungumuzia wazazi wapendwa kwa ulimi mkali kama wembe. Wapenzi, ambao wameshiriki baadhi ya matukio mazuri na yakugusa ya maisha, hupoteza muono na subira na mmoja na mwengine na kuinua sauti zao. Sisi sote, ingawa ni watoto wa agano wa Baba mpendwa wa Mbinguni, tumejuta kufanya hukumu ya haraka na tumezungumza na maneno ya kuchukiza kabla kuelewa hali kutoka kwa muono mwingine. Sote tumekuwa na fursa ya kujifunza jinsi maneno ya hatari yanaweza kuchukua hali kutoka kwa hali hatari hadi hali angamizi.

Barua ya hivi majuzi kutoka kwa Urais wa Kwanza inasema wazi, “Injili ya Yesu Kristo inatufunza kuwapenda na kuwatendea watu wote kwa ukarimu na utu---hata wakati sisi hatukubaliani” (Barua ya Urais wa Kwanza, Jan. 10, 2014). Ni mawaidha gani ya ustadi ambayo tunaweza na tunapaswa kushiriki katika majadiliano yanayoendelea ya umma, hasa tunapotazama ulimwengu kutoka kwa mitazamo inayotofautiana.

Mwandishi wa Mithali anashauri, “Jawabu la upole hugeuza hasira; bali neno liumizalo huchochea ghadhabu (Mithali 15:1). “Jawabu la upole” linajumuisha jibu lililowaziwa---maneno ya adhabu kutoka kwa moyo mnyenyekevu. Haimaanishi kamwe hatuzungumzi moja kwa moja ama kwamba tunatatanisha ukweli wa kimafundisho. Maneno ambayo huenda yakawa thabiti katika taarifa yanaweza kuwa ya upole katika roho.

Kitabu cha Mormoni kina mfano mzuri wa lugha ya kudhibitisha pia iliyotolewa katika mazingira ya kutokubaliana katika ndoa. Wana wa Saria na Lehi walikuwa wametumwa warudi Yerusalemu kuchukua mabamba ya shaba na hawakuwa wamerejea. Saria aliamini wanawe walikuwa hatarini. Alijawa na hasira na alihitaji mtu wa kulaumu.

Sikilizeni hadithi kupitia macho ya mwanawe Nefi: “ Kwani [mamangu] alikuwa amedhani kwamba tulikuwa tumeangamia nyikani; na pia alikuwa amemlalamikia baba yangu, akimwambia kwamba yeye ni mtu wa maono; na kusema: Tazama wewe umetuongoza kutoka nchi yetu ya urithi, na wana wangu hawapo tena, na tunaangamia nyikani” (1 Nefi 5:2).

Sasa, tuzingatie kile Saria huenda alikuwa anafikiria. Alikuwa amejawa na wasiwasi kuhusu kurudi kwa wanawe ambao walikuwa wenye ugomvi mahali ambapo maisha ya mumewe yalikuwa yametishwa. Na alikuwa amebadilisha nyumba yake mzuri na marafiki na hema katika jangwa lililotengwa akiwa bado katika miaka yake ya kuzaa. Akiwa amesukumwa hadi katika kiwango cha kuvunjika cha hofu yake, inaonekana kama Saria aliruka kishujaa, ikiwa si kimantiki, kutoka juu ya lori lililoenda kwa kasi kwa jitihada ya kulinda familia yake. Alielezea wasiwasi halali kwa mumewe katika lugha ya hasira na shaka na lawama---lugha ambayo wanadamu wote wanaonekana kuwa na umaarufu.

Nabii Lehi alisikiliza hofu iliyosababisha hasira ya mkewe. Kisha akatoa jibu la adhabu katika lugha ya upendo. Kwanza, alikubali ukweli wa jinsi vitu vilivyoonekana kutoka kwa mtazamo wake: “Na ... baba yangu akamzungumzia, na kusema: Najua kwamba mimi ni mtu wa maono; ... lakini [kama] ningekaa huko Yerusalemu, [tungeangamia] na ndugu zangu.” (1 Nefi 5:4).

Kisha mumewe akashughulikia hofu zake juu ya maslahi ya wana wao, kama vile Roho Mtakatifu bila shaka alimshuhudia, akisema:

“Lakini tazama, nimepokea uthibitisho wa nchi ya ahadi, vitu ambavyo kwavyo ninafurahia; ndio, na ninajua kwamba Bwana atawakomboa wana wangu kutoka mikononi mwa Labani...

“Na kwa lugha ya aina hii baba yangu … alimfariji mama yangu, … kutuhusu.” (1 Nefi 5:5–6).

Kunayo leo haja kuu ya wanaume na wanawake kukuza heshima kwa kila mmoja na mwingine katika tofauti kubwa ya imani na tabia na katika matofautiano ya kina ya ajenda zinazopingana. Haiwezekani kujua yote yanayoarifu akili zetu na mioyo ama hata kuelewa kabisa mazingira ya majaribio na chaguo tunazokumbana nazo kila mmoja wetu.

Hata hivyo, nini huenda kikatendekea “neno lolote lililo ovu” Paulo alizumgunza kuhusu ikiwa msimamo wetu wenyewe ungejumuisha huruma kwa ajili ya yale wengine wamepitia kwanza? Nikiwa ninakubali viwango vya upungufu wangu wenyewe na kasoro, Ninawasihi mzoee kuuliza, swali hili, kwa kuthamini yale wengine wamepitia: “Je, Unafikiria nini?”

Unakumbuka wakati Bwana aliwashangaza Samweli na Sauli kwa kumchagua mvulana mdogo mchungaji, Daudi wa Bethlehemu, kama mfalme wa Israeli? Bwana alimwambia nabii, “Bwana haangalii kama binadamu aangaliavyo; maana wanadamu huitazama sura ya nje, bali Bwana huutazama moyo” (1 Samweli 16:7).

Wakati chumba cha mwendeshaji lori letu kilijaa moshi, mke wangu alitenda kwa ushujaa vile angefikiri kumlinda mwana wetu. Mimi pia nilitenda kama mlinzi nilipohoji uchaguzi wake. Cha kuchangaza, haikujalisha aliyesawa zaidi. Kile kilichojalisha kilikuwa kusikiliza kila mmoja na kuelewa mtazamo wa yule mwingine.

Nia ya kuona kupitia macho ya kila mmoja na mwengine itabadilisha “neno lolote lililo ovu” kuwa “neema ya ihudumiayo” Mtume Paulo alielewa hili, na kwa kiwango fulani kila mmoja wetu anaweza kulipitia pia. Huenda haitabadilisha au kutatua tatizo, lakini uwezekano muhimu zaidi huenda ukawa kama neema inaweza kutubadilisha.

Mimi ninatoa ushahidi kwa unyenyekevu kwamba tunaweza “kutoa neema” kupitia lugha ya faraja wakati kipawa kilichokuzwa cha Roho Mtakatifu kitachoma mioyo yetu na huruma kwa ajili ya hisia na mazingira ya wengine. Hutuwezesha kubadilisha hali hatari kuwa mahali patakatifu. Mimi nashuhudia juu ya Mwokozi mwenye upendo ambaye “huutazama moyo [wetu]” na hujali kile sisi tunafikiria. Katika jina la Yesu Kristo, amina.