2010–2019
Dakika Zako Nne
Aprili 2014


Dakika Zako Nne

Muujiza wa Upatanisho unaweza kuziba mapungufu katika utendaji wetu.

Michezo ya hivi majuzi ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ulivutia dunia wakati wanariadha waliowakilisha nchi 89 wakishiriki katika michezo 98 tofauti. Cha kushangaza, 10 wa wanariadha hawa walikuwa washiriki wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho, 3 ambao walishinda medali majuzi waliangaziwa katikaChurch News: : Christopher Fogt, Noelle Pikus - Pace, na Torah Bright.1 Tunatoa pongezi zetu kwao na kwa wanariadha wote walioshiriki. Pongezi sana!

Nazungumzia michezo hii asubuhi hii nikielekeza mawazo yangu kwa wavulana, wasichana, na vijana watu wazima wasseja---- ninyiambo mko katika miaka yenu muhimu ambayo inalenga mkondoi kwa maisha yenu. Ninahisi kiasi kikubwa cha dharura katika kuwazungumzia.

Ili muweze kuhisi dharura hii, kwanza nashiriki hadithi ya Noelle Pikus-Pace, mmoja wa hawa wanariadha wa Watakatifu wa Siku za Mwisho. Katika mchezo wa Noelle, wanariadha wembamba, wanavuta kasi wanapokimbia na kisha kuruka kichwa mbele kwenye sledi ndogo. Wakiwa nyuso zikiwa nchi kidogo juu ya ardhi, wanakimbia chini kwenye njia yenye mipindo, ya barafu katika kasi ambayo inapita maili 90 (kilometa 145) kwa saa.

Cha ajabu, miaka mingiya matayarisho yatazingatiwa kama mafanikio ama masikitiko kulingana na kile kilichotokea katika nafasi ya vipindi vinne vya sekunde 60- vya mbio.

Ndoto ya awali ya Noelle ya Olimpiki ya 2006 ilikatishwa wakati ajali mbaya ilipomwacha na mguu uliovunjika, kutoweza kushindana. Katika Olimpiki ya 2010 ndoto yake ilikatizwa tena wakati alipopungukiwa tu na chini ya moja kwa kumi ya sekunde kusimama kwenye jukwaa la medal.2

Je! Unaweza kufikiria wasiwasi aliokuwa nao aliposubiri kuanza mbio yake ya kwanza katika michezo wa Olimpiki wa 2014? Miaka ya maandalizi yangefikia kilele chake katika muda mfupi wa wakati. Dakika nne kwa jumla. Alitumia miaka akijitayarisha kwa hizo dakika nne na angetumia maisha yake yote akizifikiria.

Mikimbio ya Noelle za fainali ilikuwa karibu haina makosa hata kidogo, hatutawahi kusahau mruko wake kwenye jukwaa ili kukumbatia familia yake baada ya kuvuka kwenye leni ya kumaliza, akisema, “Tumeweza!” Miaka ya maandalizi imelipa. Tuliona medali yake ya Wasichana kwenye shingo lake, medali yake ya fedha iliwekwa pale kando yake.3

Inaweza kuonekana kuwa si haki kwamba ndoto nzima ya Noelle ya Olimpiki ilitegemea kile alifanya wakati wa tu dakika nne fupi. Lakini alijua, na ndio sababu alijiandaa kwa bidii. Alihisi ukubwa, umuhimu wa dakika zake nne, na kile zingemaanisha kwa maisha yake yote.

Pia tunakumbuka Christopher Fogt, mshiriki wa timu ilioshinda medali ya shaba katika mbio za bobsledi ya watu wane. Ingawa angejiondoa baada ya ajali ya 2010 ya Olimpiki, aliamua kuvumilia. Baada ya mbio bora ya ukombozi, alishinda thamana aliotafuta kwa dhati..4

Sasa, fikiria jinsi njia yako kuelekea uzima wa milele ni sawa na matokeo ya “dakika nne za hawa wanariadha.” Wewe ni kiumbe cha milele. Kabla hujazaliwa, ulikuwepo kama roho. Katika uwepo wa Baba wa Mbinguni, ulijifunza na kujiandaa kuja duniani kwa muda mfupi, na, hasa, kutenda. Maisha haya dakika zako nne. Wakati uko hapa, vitendo vyako vitaamua kama utashinda tuzo ya uzima wa milele. Nabii Amuleki alielezea, “maisha haya ndiyo wakati …kujitayarisha kukutana na Mungu; ndio, tazama, wakati wa maisha haya ndiyo siku … kufanya kazi [ zako ] .”5

Kwa njia moja, dakika zako nne tayari zimeanza. Mda unayoyoma. Maneno ya Mtume Paulo yanaonekana kufaa: “Pigeni mbio namna hiyo, ili mpate tuzo.” 6

Kama njia hio hiyo hatua fulani ni muhimu katika utendaji mfupi sana wa mwanariadha wa Olimpiki, miruko ama vitendo angani kwa watelezaji barafuni na watelezaji waubao wa thelujini, kupiga kona za mkimbio wa bobsledi, au kupiga milazo kupitia milango ya mteremko ya kozi ya slalom, hivyo ndivyo ilivyo maishani mwetu ambapo mambo fulani ni muhimu kabisa---vituo vya ukaguzi ambavyo hutusongeza mbele katika utendaji wetu wa kiroho duniani. Hizi alama za kiroho ni maagizo ya injili muhimu yaliyotolewa na Mungu: Ubatizo, kupokea karama ya Roho Mtakatifu, kuteuliwa katika ukuhani, maagizo ya hekalu, na kushiriki sakramenti kila wiki.

“Katika ibada hizo… , nguvu za uchamungu hujidhihirisha.”7

Na kwa njia hiyo hiyo ambayo nidhamu ya mazoezi humuandaa na kumfanya mwanariadha kufanya mambo katika mchezo wake kwa ustadi wa juu kabisa, kutii amri kutakufanya ustahili kufanya ibada hizi uokozi.

Je! Unahisi dharura hii?

Marafiki wangu vijana, popote mlipo katika “utendaji wenu wa dakika nne,” nawasihi mtafakari, “Je, Ninahitaji kufanya nini baada ya hapa ili kuhakikisha medali yangu?” Pengine wakati wa mkutano huu, Roho atakuzungumzia kile ambacho ndicho: kujiandaa kimakusudi zaidi kwa ibada katika maisha yako ya baadaye ama kupokea ibada ambayo ulipaswa kupokea muda mrefu uliopita. Chochote kitakachohitajika, ichukue hatua hiyo. Ifanye saa hizi. Usisubiri. Dakika zako nne zitaisha haraka, na utakuwa na maisha ya milele kufikiri juu ya kile ulichofanya katika maisha haya.8

Nidhamu ya kibinafsi inahitajika. Maombi ya kila siku, kujifunza maandiko, na mahudhurio ya kanisa lazima yawe msingi wa mazoezi yako. Mfano thabiti ya kutii amri, kuweka maagano ambayo tayari umefanya, na kufuata kiwango cha Bwana kinachopatikana katika Kwa Nguvu za Vijana inahitajika.

Pengine unajua kuhusu mambo katika maisha yako ambayo yanatishia kupunguza ama kusimamisha maendeleo yako ya kiroho . Kama ni hivyo, fuata ushauri huu wa kiroho: “Tuweke kando kila mzigo mzito, na dhambi ile ituzingayo kwa upesi; na tupige mbio kwa saburi katika yale mashindano yaliyowekwa mbele yetu.”9

Bado hujachelewa kutubu. Lakini huenda hivi karibuni ukawa umechelewa, kwa sababu hakuna anayejua wakati dakika zako nne zitaisha.

Sasa, huenda unafikiria kwako mwenyewe, “Tayari nimeharibu dakika zangu. Dakika zangu tatu tayari zimeharibika. Naweza pia kuachana nayo.” Kama ni hivyo, wacha kufikiria hayo, na kamwe usifikirie hayo tena. Muujiza wa Upatanisho unaweza kusimamia kasoro katika utendaji wetu. Kama vile Mzee Jeffrey R. Holland amefundisha:

“Kwa wale miongoni mwenu … ambao bado huenda mnasita, … Ninashuhudia uwezo wa kufanyiza upya wa upendo wa Mungu na muujiza wa neema Yake. …

“...Kamwe haujachelewa ilimradi Bwana … amesema kuna wakati. … usichelewe.”10

Kumbuka, hauko peke yako. Mwokozi ameahidi kwamba hatakuwacha bila faraja.11 Pia una familia, marafiki, na viongozi ambao wanakutakia mema.

Ingawa hotuba yangu imeelekezwa kwa vijana wa Kanisa, kwa wazazi na mababu, ninatoa yafuatayo:

Hivi majuzi, Mzee David A. Bednar alieleza njia rahisi ya kufanya tathmini ya familia ili kukagua maendeleo juu ya njia ya agano na ibada muhimu. Yote yanayohitajika ni kipande cha karatasi iliyo na sehemu mbili: “jina” na “mpango wa agizo lifuatalo ama linalohitajika.” Nilifanya hivyo hivi majuzi, nikiorodhesha kila mwanafamilia. Miongoni mwao, niligundua mjukuu mchanga, ambaye angebarikiwa hivi karibuni. Mjukuu mwenye umri wa miaka sita, ambaye maandalizi yake kwa ajili ya ubatizo yalikuwa muhimu; na mwana ambaye angefika umri wa miaka 18, ambaye maandalizi yake kwa ajili ya ukuhani na endaumenti ya hekalu ilikuwa karibu ifanyike. Kila mtu katika orodha alihitaji ibada ya sakramenti. Zoezi hili rahisi lilimsaidia Lesa pamoja nami katika kutimiza wajibu wetu wa kusaidia kila mwana familia wetu kwenye njia ya agano, nikiwa na mpango wa utekelezaji kwa kila mmoja wao. Pengine hili ni wazo kwenu, ambalo litasababisha majadiliano ya familia, masomo ya jioni ya familia nyumbani, maandalizi, na hata mialiko kwa ajili ya maagizo muhimu katika familia yako.12

Kama mtelezaji wa ski na mtelezaji wa ubao mwenyewe, nilifurahishwa sana na matokeo ya “dakika nne” ya medali ya shaba ya mwanariadha MSM wa Australia wa, Mtelezaji wa ubao Torah Bright katika mashindano ya nusu paipu. Alishangaza dunia alipomaliza mbio bila dosari akimalizia kwa mbio ya makalio ya rodeo 720. Ingawa, hata cha kuvutia sana na kustajaabisha kwa ulimwengu ilikuwa ni vile alionyesha upendo wa Kristo kwa washindani wake. Aligundua kwamba Mtumiaji wa ubao wa kuteleza Mmerikani Kelly Clark, ambaye alikuwa na jaribio mbaya la kwanza katika raundi yake ya mwisho, alionekana kuwa na wasiwasi kuhusu jaribio lake la pili. “Alinikumbatia,” Clark alikumbuka. “Alinishika tu hadi kweli nikatulia ya kutosha na nikapunguza kupumua kwangu. Ilikuwa vizuri kupata kumbatio kutoka kwa rafiki.” Kelly Clark baadaye angejiunga na Torah kwenye jukwaa kama mshindi wa medali ya shaba.

Alipoulizwa kuhusu tendo hili lisilo la kawaida la wema kwa mpinzani wake, ambayo ingeweza kuweka medali yake ya fedha hatarini, Torah alisema tu, “Mimi ni mshindani---Ninataka kufanya vyema niwezavyo---lakini ninataka washindani wenzangu wafanye vyema wawezavyo, pia.”13

Ukikumbuka haya, je,kuna mtu ambaye anahitaji himizo lako? mwanafamilia ? rafiki ? mwanafunzi mwenzako shuleni ama mshiriki mwenzako katika jamii? Unaweza kuwasaidiaje na dakika zao nne ?

Marafiki wapendwa, mko katikati mwa safari ya kusisimua. Kwa njia fulani, mnashindana chini ya nusu---bomba au mkondo wa sledi, na inaweza kuwa na changamoto kufanya kila kitu au kupiga kila kona katika mkondo. Lakini kumbukeni, mmefanya matayarisho kwa ajili ya miaka hii. Huu ni wakati wenu kutenda . Hizi ni dakika zenu nne ! Wakati ni sasa !

Ninatoa imani yangu kamilifu katika uwezo wenu. Mnaye Mwokozi wa ulimwengu kwa upande wenu. Mkitafuta usaidizi Wake na kufuata maelekezo Yake, mnaweza kushindwa vipi?

Ninahitimisha kwa ushuhuda wangu wa baraka tulizonazo katika nabii aliye hai, Rais Thomas S. Monson, na juu ya Yesu Kristo na nafasi Yake kama Mwokozi na Mkombozi wetu, katika jina Lake takatifu, Yesu Kristo, amina.

Muhtasari

  1. Ona Christine Rappleye, “Mormons in the Olympics: 3 Medals for LDS Athletes at the Winter Games,” deseretnews.com/article/865597546/Mormons-in-the-Olympics-3-medals-for-LDS-athletes-at-the-Winter-Games.html.

  2. Ona Christine Rappleye, “Mormons in the Olympics.”

  3. Ona Sarah Petersen, “Noelle Pikus-Pace Wears LDS Young Women Necklace throughout Olympics,” deseretnews.com/article/865596771/Noelle-Pikus-Pace-wears-LDS-Young-Women-necklace-throughout-Olympics.html.

  4. Ona Amy Donaldson, “Army, Faith Helped Push Mormon Bobsledder Chris Fogt to Olympic Success,” deseretnews.com/article/865597390/Army-faith-helped-push-Mormon-bobsledder-Chris-Fogt-to-Olympic-success.html.

  5. Alma 34:32.

  6. Ona 1 Wakorintho 9:24.

  7. Mafundisho na Maagano 84:20.

  8. Ona Alma 34:31–33.

  9. Waebrania 12:1.

  10. Jeffrey R. Holland, “The Laborers in the Vineyard,” Ensign au Liahona, May 2012, 33.

  11. Ona Yohana 14:18.

  12. David A. Bednar, mzungumzo na mwandishi.

  13. Vidya Rao, “Snowboarder Kelly Clark: Hug from Competitor Helped Me Win Bronze,” today.com/sochi/snowboarder-kelly-clark-hug-competitor-helped-me-win-bronze-2D12108132.