2010–2019
Huru Milele, Kujitendea Wenyewe
Oktoba 2014


Huru Milele, Kujitendea Wenyewe

Ni mapenzi ya Mungu kwamba sisi tuwe wanaume na wanawake huru waliowezeshwa kuinuka hata kwa uwezo wao kamili yote kimwili na kiroho.

Maigizo ya William Shakespear ya The Life of King Henry V yanajumuisha mchezo wa usiku kwenye kambi ya wanajeshi wa Kiingereza huko Agincourt kabla ya vita vyao na jeshi la Ufaransa. Katika mwanga mdogo na kuficha kidogo, Mfalme Henry anazurura bila kujulikana miongoni mwa wanajeshi wake. Anaongea nao, akijaribu kutathimini kujiamini kwa majeshi yake ambayo yalikuwa yamezidiwa kwa wingi, na kwa sababu hawakumgundua yeye ni nani, ni wakweli katika maongezi yao. Wakati wa maongezi yao pamoja na Mfalme, waliongelea juu ya nani anastahili kuchukua jukumu kwa ajili ya yanayotokea vitani---ni mfalme au kila askari mwenyewe.

Ikafika wakati fulani Mfalme Henry alitangaza, “Nafikiri mimi singekufa popote nimetosheleka sana kama vile katika jeshi la mfalme, kwa sababu malengo yake ni ya haki.”

Michael William anajibu, “Hiyo ni zaidi ya tunayoyajua.”

Askari mwingine aliunga mkono, “Ndiyo, ni zaidi ya kutaka kujua, kwa sababu ni vyema kwetu kujua kwamba sisi ni raia wa mfalme: kama kazi yake si sahihi, utii wetu kwa mfalme unatuondolea hatia yake kwetu.”

Williams aliongeza, “Kama kazi yake si njema, mfalme mwenyewe anawajibika sana.”

Haishangazi, Mfalme Henry hakubaliani, “Kila kazi ya utii ni ya mfalme, lakini kila nafsi ya raia ni yake mwenyewe.”1

Shakespeare hajaribu kutatua malumbano haya katika mchezo, na kwa njia moja au nyingine ni mjadala unaoendelea hadi sasa---swali ni nani anayebeba majukumu kwa yale yanayotokea katika maisha yetu?

Wakati mambo yanapokuwa mabaya, kuna tabia ya kulaumu wengine hata Mungu. Wakati mwingine watu huanza kujiona kama wanastahili, na mtu binafsi au kikundi hujaribu kuwekelea majukumu ya ustawi wao kwa wengine au kwa serikali. Katika hali ya kiroho wengine huona kwamba wanaume na wanawake hawahitaji kujaribu kuwa wema kibinafsi---kwa sababu Mungu anatupenda na kutuokoa “vile tulivyo.”

Lakini Mungu anataka kwamba watoto Wake watende kulingana uhuru aliowapa, “ili kila mtu aweze kuhukumiwa kutokana na dhambi zake katika siku ya hukumu.”2 Ni mpango Wake na mapenzi Yake kwamba tuna wajibu mkubwa wa kufanya maamuzi katika drama ya maisha yetu wenyewe. Mungu ataishi maisha yetu kwa niaba yetu wala kututhibiti kana vile sisi ni vibaraka Wake, jinsi Lusiferi alipendekeza wakati mmoja. Wala manabii Wake kukubali kuwa “wathibiti vibaraka” katika mahali pa Mungu. Brigham Young alisema: “Mimi singependa Mtakatifu wa Siku za Mwisho katika dunia hii, au mbinguni, ili kutoshelezwa na chochote kinachonitosheleza, pasipo Roho ya Bwana Yesu Kristo,---roho ya ufunuo, huwafanya kutosheleka. Ningependa wao wajijulie wenyewe na kuelewa wenyewe.”3

Kwa hivyo Mungu hatuokoi “kama tulivyo,” kwanza, kwa sababu “kama tulivyo” sisi tu wachafu, na “hakuna kitu kichafu kinachoweza kukaa … katika uwepo wake; kwani, katika lugha ya Adamu, Mtu wa Utakatifu ni jina lake, na jina la Mwanawe wa pekee ni Mwana wa Mtu wa [Utakatifu].”4 Na pili, Mungu hatatenda kutufanya kitu ambacho sisi hatujachagua kuwa kwa vitendo vyetu. Kwa kweli Yeye anatupenda, na kwa sababu Yeye anatupenda, Yeye wala hatatulazimisha au kututekeleza. Badala yake Yeye hutusaidia na hutuongoza. Kwa kweli, maonyesho ya kweli ya upendo wa Mungu ni amri Zake.

Tunatakiwa (na inabidi) kufurahi katika mpango wa Mungu ambao unaturuhusu sisi kufanya chaguo kujitendea wenyewe na kupata matokeo, au kama maandiko yanavyoonyesha, kuonja machungu, ili kwamba tuweze kujua zawadi ya mema.”5 Tunashukuru daima kwamba Upatanisho wa Mwokozi umeishinda dhambi ya asili ili kwamba tuweze kuzaliwa katika ulimwengu huu na tusiadhibiwe kwa makosa ya Adamu.6 Tukiwa tumekombolewa kutoka kwa Kuanguka, tunakuwa hatuna makosa mbele za Mungu na kuwa huru milele, tukijua mema na mabaya, tukitenda wenyewe na siyo kutendewa.”7. Tunaweza kuchagua aina ya mtu ambaye tungependa kuwa, na kwa msaada wa Mungu, tunaweza kuwa kama Yeye alivyo.8

Injili ya Yesu Kristo inafungua njia ya vile tunavyoweza kuwa. Kupitia Upatanisho wa Yesu Kristo na neema Yake, kushindwa kwetu kuishi vizuri sheria ya selestia na mara nyingi katika umauti kunaweza kufutwa na tunawezeshwa kuendeleza tabia za kama Kristo. Haki inahitaji, hata hivyo, hakuna kati ya haya yanawezatokea bila ya makubaliano yetu ya hiari na ushiriki wetu. Mara yote imekuwa hivi. Uwepo wetu duniani kama wanadamu ni matokeo ya uchaguzi ambao kila mmoja wetu aliufanya ili kushiriki katika mpango wa Baba.9 Hivyo, wokovu kwa kweli siyo matokeo ya matakwa ya uungu, bali haitendeki kwa mapenzi ya uungu pekee.10

Haki ni tabia muhimu ya Mungu. Tunaweza kuwa na imani na Mungu kwa sababu Yeye anaaminika. Maandiko yanatufundisha kwamba “Kwani Mungu haenendi katika njia zisizo nyoofu, wala hageuki mkono wa kulia wala wa kushoto, wala habadilishi kauli kutoka ile aliyosema, hivyo njia zake ni nyoofu, na mwelekeo wake ni imara milele”11 “Mungu hana upendeleo.”12 Tunategemea tabia yake ya haki ili kupata imani, kujiamini na tumaini.

Lakini kama matokeo ya kuwa kamili, kuna mambo ambayo Mungu hawezi kuyafanya. Hawezi kuwa mdhalimu katika kuwaokoa baadhi na kuwaangamiza wengine. Hawezi kuiangalia dhambi na kuivumilia hata kidogo.”13 Hawezi kukubali rehema kuibia haki.14

Kuna ushahidi mwingi wa haki Yake kwamba Mungu alianzisha kanuni ya huruma. Ni kwa sababu Yeye ni mwema kwamba alianzisha njia kwa ajili ya rehema kuchukua nafasi yake katika uzima wa milele. Hivyo sasa, “haki hutekeleza madai yake yote, na pia huruma hudai yote yaliyo yake.”15

Tunajua kwamba “mateso na kifo chake yeye ambaye hakutenda dhambi, ambaye ulipendezwa naye; … tazama damu ya mwana [Wake] iliyomwagika”16 ambayo inaridhisha madai ya haki, inaeneza rehema, na hutukomboa sisi.17 Hata hivyo, “kulingana na haki, mpango wa ukombozi haungeletwa tu kwa tabia ya toba.18 Ni mahitaji na nafasi kwa ajili ya toba ambayo inawezesha rehema kufanya kazi yake bila ya kuiangamiza haki.

Kristo hakufa ili kuwaokoa wachache bali kutoa nafasi ya toba. Tunategemea “mkitegemea kabisa ustahili wa yule aliye mkuu kuokoa”19 mfanyiko wa toba, kwa kutenda juu ya toba ni mabadiliko ya hiari. Kwa kufanya toba kuwa kigezo cha kupata kipawa cha neema, Mungu huwezesha kubakiza majukumu yetu wenyewe. Toba, huheshimu na husimamia uhuru wetu wa maadili: “Na hivyo rehema inaridhisha mahitaji ya haki, na kuwazingira kwa mikono ya usalama, wakati yule ambaye hatumii imani kwa kutubu anajiweka wazi kwa sheria yote ya madai ya haki; kwa hivyo ni tu yule ambaye ana imani kwa toba atatimiziwa mpango mkuu wa ukombozi.”20

Kutoelewa haki na rehema za Mungu ni kitu kimoja; kupinga uwepo wa Mungu au utukufu wake ni kitu kingine, lakini aidha kutaleta matokeo katika kupokea kidogo kwetu---wakati mwingine kidogo sana---kuliko uwezo wetu, mtakatifu. Mungu asiyehitaji kitu toka kwa watu wake hufanya kazi sawa na Mungu ambaye hayupo. Ulimwengu bila Mungu, Mungu aliye hai, Mungu ambaye huanzisha sheria ya kimaadili ya kutawala na kukamilisha watoto, pia ni sawa na ulimwengu usio na kweli au haki. Ni katika ulimwengu wote kukubalika kwa yaliyo mema na yaliyo mabaya kunatofautiana kati ya mtu na mtu.

Uhusiano unamaana kila mtu ana mamlaka juu yake mwenyewe. Hakika, siyo tu wote wale wanaomkana Mungu wanaokubali falsafa hii. Baadhi ya wanaoamini Mungu bado wamaamini kwamba wao wenyewe binafsi wanaamua kipi kizuri na kipi kibaya. Kijana mmoja alielezea kwa njia hii: “Sifikiri kama ninaweza kusema kwamba Wahindu si sahihi au Wakatoliki si sahihi au kuwa Mwangalikana si sahihi – nafikiri mtazamo huo unategemea kile unachokiamini… .sifikiri kuna lililo la kweli na la uongo.”21 Mwingine, aliuliza juu ya misingi ya dini anayoiamini, alijibu: “Mimi binafsi---nalifikiria hilo pia. Nina maana inawezekanaje pawepo na mamlaka kwa yale unayoyaamini?”22

Kwa wale wanaoamini kitu chochote au kila kitu wanaweza kuwa wakweli, tangazo la malengo imara, na ukweli ulioenea unakuwa kama nguvu---“Sistahili kulazimishwa kuamini kitu fulani ni cha kweli ambacho sikipendi.” Lakini hilo halibadilishi ukweli. Kutopenda sheria ya mvutano hakutamfanya mtu asianguke kama atatereza bondeni. Hiyo ni sawa na sheria za milele na haki. Uhuru hauji kwa kubisha bali kwa kuutumia. Huo ndio msingi wa nguvu pekee za Mungu. Kama isingekuwa ukweli thabiti na usiobadilika, kipawa cha wakala hakingekuwa na faida kama tusingekuwa na uwezo wa kujua nia ya matokeo ya matendo yetu. Kama vile Lehi alivyoelezea: “Na kama mtasema hakuna sheria, mtasema pia hakuna dhambi. Kama mtasema hakuna dhambi, mtasema pia hakuna utakatifu. Na kama hakuna utakatifu hakuna furaha. Na kama hakuna utakatifu wala furaha basi hakuna adhabu wala huruma. Na kama vitu hivi havipo basi hakuna Mungu. Na kama hakuna Mungu basi sisi hatupo, wala dunia; kwani hakungekuwa na uumbaji wa vitu, wala kutenda au kutendewa; kwa hivyo, vitu vyote lazima vingetokomea.”23

Ni muhimu kote kimwili na kiroho, nafasi za kuchukua majukumu ya kujitegemea wenyewe ni kipaji kutoka kwa Mungu bila hicho hatuwezi kugundua uwezo wetu kama mabinti na wana wa Mungu. Wajibu binafsi unakuja kwa haki na kazi kwamba lazima tutetee daima; imekuwa ikipingwa tangu kabla ya Uumbaji. Lazima tulinde uwajibikaji dhidi ya watu na mipango ambayo (wakati mwingine kwa nia nzuri) hutufanya sisi tujitegemee. Na lazima tuyalinde dhidi ya mielekeo yetu ili kuepusha kazi ambayo inayotakiwa kukuza vipaji, uwezo, na silka ya kama Kristo.

Hadithi9 inasimuliwa na mtu ambaye hangweza kufanyakazi. Alitaka asaidiwe katika kila kitu. Kwa mawazo yake, Kanisa au serikali, au vyote, vinadaiwa kwa sababu alilipa kodi na zaka. Hana chakula lakini hataki kufanyakazi ili ajihudumie mwenyewe. Akiwa amekata tamaa na kuchukizwa, wale waliojaribu kumsaidia waliamua kwamba kwa sababu alikuwa hataki kujisaidia mwenyewe, wao pia walikuwa tayari kumpeleka makaburini na kumwacha huko. Wakiwa njiani kuelekea makaburini, mtu mmoja alisema, hatuwezi kufanya hivi. Nina mahindi nitampa.

Hivyo wakamweleza Yule mtu, na akauliza, “Je, pumba zimeondolewa?

Wakamjibu, “La.”

“Kwa hiyo, “alisema, “nipelekeni.”

Ni mapenzi ya Mungu kwamba wanaume na wanawake kuweza kufanikisha hali yetu ya kimwili na kiroho, ili tuwe huru na tusiaibike na umaskini na kuwa watumwa wa dhambi, bali tufurahie heshima na uhuru, ili tuweze kujiandaa katika mambo yote ili kuungana Naye katika ufalme wa selestia.

Sidanganyiki kimawazo kwamba hili linawezekana kwa juhudi zetu wenyewe pekee bila ya msaada Wake muhimu wa kila mara. “Tunajua kwamba ni kwa neema ndiyo tunaokolewa, baada ya yale yote tunaweza kufanya.”24 Na hatuhitaji kupata kiwango cha chini cha uwezo au wema kabla Mungu kutusaidia---msaada wa kiungu unaweza kuwa wetu kila saa ya kila siku, bila kujali pale tulipo katika njia ya utii. Lakini najua kwamba zaidi ya kutamani msaada Wake, sisi lazima tujitahidi wenyewe, tutubu, na tumchague Mungu ili Yeye aweze kufanya kazi katika maisha yetu kwa haki na wakala wa kimaadili. Ombi langu ni kwamba tuchukue jukumu na kwenda kufanya kazi ili pawepo na kitu cha Mungu kutusaidia.

Ninatoa ushahidi kwamba Mungu Baba yu hai, kwamba Mwanawe, Yesu Kristo, ni Mkombozi wetu, na kwamba Roho Mtakatifu yu pamoja nasi. Matamanio yao ni kutusaidia bila shaka, na uwezo wao wa kufanya hivyo ni mkubwa. Acheni “tuamke na tusimame toka mavumbini, … ili maagano ya Baba wa Milele ambayo ameweka [kwetu] yaweze kutimia.”25 Katika jina la Yesu Kristo, amina.