2010–2019
Ripoti ya Idara ya Ukaguzi ya Kanisa, 2014
Aprili 2015


Ripoti ya Idara ya Ukaguzi ya Kanisa, 2014

Kwa Urais wa Kwanza wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho

Ndugu Wapendwa: Kama tulivyoelekezwa na ufunuo katika sehemu ya 120 ya Mafundisho na Maagano, Baraza la Mpangilio wa Zaka, linalojumuisha Urais wa Kwanza, Akidi ya Mitume Kumi na Wawili, na Uaskofu Simamizi---huidhinisha matumizi ya fedha za Kanisa. Mashirika ya Kanisa hugawa fedha kulingana na bajeti, sera na taratibu zilizoidhinishwa.

Idara ya Ukaguzi ya Kanisa, inayojumuisha wataalamu walioidhinishwa na iliyo huru kutokana na idara zingine zote za Kanisa, ina wajibu wa kufanya ukaguzi kwa lengo la kutoa uhakika kuhusu michango iliyopokelewa, matumizi yaliyofanywa, na ulinzi wa mali ya Kanisa.

Kulingana na ukaguzi uliofanywa, Idara ya Kanisa ya Ukaguzi ina maoni kwamba, katika mambo yote muhimu, michango iliyopokelewa, matumizi yaliyofanywa, na mali ya Kanisa kwa mwaka wa 2014 yamerekodiwa na kusimamiwa kulingana na bajeti ya Kanisa iliyoidhinishwa, sera na mazoea ya uhasibu. Kanisa linafuata mafunzo yanayofundishwa kwa washiriki wake ya kufuata bajeti, kuepuka madeni, na kuweka akiba dhidi ya wakati wa mahitaji.

Imewasilishwa kwa heshima,

Idara ya Ukaguzi ya Kanisa

Kevin R. Jergensen

Mkurugenzi Mtendaji