2010–2019
Familia Ni ya Mungu
Aprili 2015


Familia Ni ya Mungu

Kila mmoja wetu ni wa familia ya Mungu na anahitajika.

Kuna kitu chochote kilicho kizuri na muhimu sana kuliko kweli sahihi na halisi za injili zinazofunzwa katika wimbo wa Msingi? Na ninyi nyote watoto wa kike wa Msingi mlio hapa jioni ya leo mnajua wimbo ambao nitaongea juu yake. Mlijifunza katika mpangilio wa masomo yenu ya Msingi mwaka uliopita,

Katika maneno ya “The Family Is of God” 1---ulioimbwa mapema katika mkutano huu---tunakumbushwa kuhusu fundisho halisi. Hatufundishwi tu kwamba familia ni ya Mungu bali pia kwamba sisi ni sehemu ya familia ya Mungu.

Mstari wa kwanza wa wimbo hufunza: “Baba Yetu ana familia. Ni mimi! Ni wewe, na wale wengine pia: sisi ni watoto Wake.” Kutoka katika tangazo la familia, tunajifunza, “Katika kipindi kabla ya kuzaliwa, wana na mabinti wa kiroho walimjua na kumwabudu Mungu kama Baba yao wa Milele.” Katika kipindi hicho, tulijifunza kuhusu utambulisho wetu wa kike wa milele. Tulijua kwamba kila mmoja alikuwa “binti … mpendwa wa wazazi wa mbinguni.” 2

Safari yetu duniani haikubadilisha kweli hizo. Kila mmoja wetu ni wa familia ya Mungu na anahitajika. Familia za duniani zote zinaonekana kuwa tofauti. Na tunapofanya vyema kadiri tuwezavyo kuunda familia za kawaida zilizo imara, ushiriki katika familia ya Mungu hautegemei hadhi ya aina yoyote--- hali ya ndoa, hali ya uzazi, hali ya kifedha, hali ya kijamii, au hata aina yoyote ya hali tunayoweka kwenye mtandao wa kijamii.

Sisi tunastahili kuwa. “Sisi ni mabinti wa Baba yetu wa Mbinguni, ambaye anatupenda, na sisi tunampenda.” 3

Mstari wa pili wa wimbo unaupanua ule wa kwanza. “Yeye alimtuma kila mmoja wetu hapa duniani, kwa njia ya kuzaliwa, ili kuishi na kujifunza katika familia.”

Katika maisha kabla ya kuzaliwa, tulijifunza kwamba tutahitaji kipindi cha maisha ya duniani. Sisi “tulikubali mpango wa [Baba wa Mbinguni] ambao watoto Wake wangeweza kupata mwili na kupata uzoefu wa duniani na kuendelea kuelekea kwenye ukamilifu na hatimaye kufikia kudra yetu takatifu kama warithi wa uzima wa milele.” 4

Mzee Richard  G. Scott alielezea kwamba “tulifunzwa katika ulimwengu wa kabla ya kuzaliwa kwamba kusudi letu ni kuja hapa kupimwa, kujaribiwa, na kupanuliwa.” 5 Kupanuliwa huku hutokea katika hali nyingi kama vile watu wanaowapatwa nayo. Mimi kamwe sijapata kupitia talaka, machungu na utovu wa usalama ambao hujitokeza kutokana na kutelekezwa, au majukumu yanayohusiana na mama ambaye hajaolewa. Sijapatwa na kifo cha mtoto, utasa, au mvuto wajinsia moja. Sijapata kupatwa na udhalimu au ugonjwa sugu au ulevi. Hazijakuwa fursa zangu za upanuzi wangu.

Kwa hiyo baadhi yenu mnafikiria, “Basi, Dada Stephens, wewe hauelewi tu!” Nami najibu kwamba mnaweza kuwa sahihi. Mimi sielewi sana changamoto zenu. Lakini kupitia mitihani na majaribio yangu binafsi---ambayo yamenisukuma kupiga magoti yangu ---Nimepata kuwa na uhusiano na Mtu ambaye anaelewa---Yule ambaye “anajua dhiki,” 6 ambaye alipatwa na yote, na anayeelewa yote. Zaidi ya hayo, nimeshapatwa na mithani yote ya duniani ambayo nimetaja kupitia jicho la binti, mama, bibi, dada, shangazi, na rafiki.

Nafasi yetu kama mabinti washika---maagano wa Mungu siyo kujifunza kutokana na changamoto zetu wenyewe; ni kuungana katika huruma na fadhili tunapowasaidia wana familia wengine wa familia ya Mungu katika shida zao, kama tulivyoagana kufanya.

Tunapofanya hivyo, pia tunapata kuelewa na kutumaini kwamba Mwokozi anajua shida za njia na anaweza kutuongoza kushinda huzuni na masikitiko yoyote yanayoweza kuja. Yeye ni mhisani wa kweli, na upendo Wake “hudumu milele”7---katika sehemu fulani kupitia sisi---wakati tunapomfuata Yeye.

Kama mabinti wa Mungu na wanafunzi wa Yesu Kristo, basi “tunatenda kulingana na ile huruma ambayo Mungu ameipanda katika [mioyo] yetu8. Sehemu yetu ya ushawishi siyo tu kwa wanafamilia yetu.

Picha
Photo of Sister Yazzi and Sister Yellowhair

Hivi karibuni nilipata nafasi ya kuzungumza na Dada Yazzie wa Kigingi cha Chinle Arizona katika nyumba yake ya udongo. Aliponikaribisha katika nyumba yake, kitu cha kwanza nilichoona ilikuwa ni picha nyingi zilizowekwa fremu za familia na wamisionari kwenye kuta zake na mezani. Basi nikamuuliza, “Dada Yazzie, una wajukuu wangapi?

Akishangazwa na swali langu, aliinua mabega yake. Nikikanganywa na jibu lake, nilimtazama binti yake, Dada Yellowhair, ambaye alijibu, “Hajui ana wajukuu wangapi. Sisi hatuwahesabu. Watoto wote humwita ‘Bibi’---yeye ni Bibi ya kila mtu.”

Dada Yazzie anatoa upendo na ushawishi wake siyo tu kwa wanafamilia wa uzao wake kibaiolojia bali kwa wote. Anaelewa kile kinamaanisha kupanua sehemu yake ya ushawishi anapoenenda akifanya mema, akibariki, akilea na kulinda familia ya Mungu. Anaelewa kwamba “mwanamke anapoimarisha imani ya mtoto, huchangia kwenye nguvu za familia, sasa na katika siku za usoni. 9

Mstari wa tatu wa wimbo unaelezea zaidi kusudi la maisha ya duniani: “Mungu alitupatia familia ili zitusaidie kuwa kile Yeye anataka tuwe.” Mwokozi alifundishaa, “Kuweni na umoja; na kama hamna umoja ninyi siyo wangu.”10 Tangazo kwa familia hutufunza kwamba kama mabinti wa kiroho wapendwa wa wazazi wa mbinguni, sisi tuna asili ya kiungu, utambulisho wa milele, na madhumuni. Mungu anataka sisi tuwe na umoja. Mungu anahitaji sisi tuwe wamoja---mabinti washika maagano tuliongana licha ya tofauti binafsi za maisha yetu,11 ambao tuna hamu ya kujifunza yote tunayohitaji ili kurudi katika uwepo Wake, tumeunganishwa Naye kama sehemu ya familia Yake ya milele.

“Ibada na maagano matakatifu yanayopatikana katika mahekalu yetu yanayotuwezesha kurudi katika uwepo wa Mungu na kwa familia kuunganika milele.”12 Ibada tunazopokea na maagano tunayofanya katika ubatizo na katika mahekalu matakatifu huunganisha familia ya Mungu katika pande zote --- kutuunganisha na Baba kupitia Mwanae ambaye aliomba “ Kwamba wote wawe kitu kimoja, kama vile Baba alivyo ndani yangu nami ndani yake, pia nanyi mwe kitu kimoja ndani yetu.” 13

Tunapotumia muda wetu katika maisha ya duniani kujifunza na kutumia mafundisho ya Mwokozi, tunakuwa zaidi kama Yeye. Tunakuja kujua kwamba Yeye ndiye njia---njia ya pekee---tunaweza kushinda changamoto za duniani, kuponywa, na kurudi tena kwenye nyumba yetu ya mbinguni.

Mstari wa mwisho wa wimbo hurudi pale tulipoanza: “Hivi ndivyo Yeye huonyesha upendo Wake, kwani familia ni ya Mungu.” Mpango wa Baba kwa watoto Wake ni mpango wa upendo, na ni mpango wa kuunganisha watoto Wake---familia Yake---pamoja Naye. Mzee Russell M. Nelson alifundisha: “Baba wa Mbinguni ana hamu mbili tu kwa watoto Wake … : maisha ya milele na uzima wa milele, ‘ambayo humaanisha maisha pamoja Naye nyumbani.’” 14 Hizo hamu zinaweza kukamilishwa tu kadiri sisi pia tunavyoonyesha upendo ambao Baba wa Mbinguni anao kwa familia Yake kwa kuwafikia na kushiriki mpango Wake pamoja na wengine.

Miaka ishiriki iliyopita, Urais wa Kwanza na Akidi ya Mitume Kumi na Wawili waliufikia ulimwengu wote wakati walipotoa tangazo kuhusu familia. Tangu wakati huo mashambulio kwa familia yameongezeka.

Kama tunataka kufanikiwa katika majukumu yetu matakatifu kama mabinti wa Mungu, ni sharti sisi tuelewe umuhimu wa milele na majukumu binafsi ya kufundisha ukweli kuhusu mpango wa Baba yetu wa Mbinguni kwa familia Yake. Rais Howard  W. Hunter alieleza:

“Kuna haja kubwa ya kuunganisha wanawake wa Kanisa ili wasimame pamoja na kwa ajili ya Ndugu katika kuzima mavimbi ya uovu ambayo yanatuzingira na katika kusogeza mbele kazi ya Mwokozi wetu. …

“… Kwa hivyo tunawasihi mhudumu kwa ushawishi wenu wenye nguvu kwa wema na katika kuimarisha familia zetu, kanisa letu, na jamii yetu.” 15

Kina dada, sisi tunastahili. Sisi tunapendwa.Sisi tunahitajika. Sisi tuna madhumuni matukufu, kazi, nafasi, wajibu katika Kanisa na ufalme wa Mungu na katika familia Yake ya milele. Je! Unajua kwa moyo wako wote kwamba Baba yako wa Mbinguni anawapenda na anatamani ninyi na wale mnaowapenda kuwa pamoja Naye? Kama vile Baba wa Mbinguni na Mwanawe, Yesu Kristo walivyo wakamilifu  …, Matumaini yao kwenu ni kamili.”16 Mpango wao kwetu ni kamili, na ahadi Zao ni hakika. Juu ya kweli hizi mimi nashuhudia kwa shukrani katika jina la Yesu Kristo, amina.

Muhtasari

  1. Ona “The Family Is of God,” in Families Are Forever: 2014 Outline for Sharing Time (2013), 28–29.

  2. “The Family: A Proclamation to the World,” Ensign or Liahona, Nov. 2010, 129.

  3. “Young Women Theme,” in Young Women Personal Progress (booklet, 2009), 3.

  4. “Familia: Tangazo kwa Ulimwengu.”

  5. Richard G. Scott, “Make the Exercise of Faith Your First Priority,” Ensign or Liahona, Nov. 2014, 92.

  6. Isaya 53:3.

  7. Moroni 7:47.

  8. Joseph Smith, in Daughters in My Kingdom: The History and Work of Relief Society (2011), 16.

  9. Daughters in My Kingdom, 159.

  10. Mafundisho na Maagano 38:27.

  11. Ona Patricia T. Holland, “‘One Thing Needful’: Becoming Women of Greater Faith in Christ,” Ensign, Oct. 1987, 26–33.

  12. “Familia: Tangazo kwa Ulimwengu.”

  13. Yohana 17:21.

  14. R.  Scott Lloyd, “God Wants His Children to Return to Him, Elder Nelson Teaches,” Church News section of LDS.org, Jan. 28, 2014, lds.org/church/news/god-wants-his-children-to-return-to-him-elder-nelson-teaches .

  15. Howard W. Hunter, in Daughters in My Kingdom, 157; see also “To the Women of the Church,” Ensign, Nov. 1992, 96.

  16. M. Russell Ballard, “Let Us Think Straight” (Brigham Young University devotional, Aug. 20, 2013); speeches.byu.edu.