2010–2019
Kizazi Kikuu cha Vijana Wazima
Aprili 2015


Kizazi Kikuu cha Vijana Wazima

Kile tunachohitaji sasa ni kizazi kikuu cha vijana wazima katika historia ya Kanisa. Tunahitaji moyo wenu wote na nafsi zenu.

Mojawapo ya raha kuu ninayofurahia ninaposafiri duniani kote ni nafasi ya kukutana na kuwasalimu wamisionari wetu. Hawa wazee na kina dada wa ajabu wanaangaza Nuru ya Kristo, na mimi daima nimevutiwa na upendo wao kwa Bwana Yesu Kristo na huduma yao ya kujitolea Kwake. Kila mara ninapowaamkia kwa mikono na kuhisi roho na imani yao ya ajabu, mimi hujisemeza, “Hawa wana na mabinti wetu wa ajabu kwa kweli wao ni muujiza!”

Wakati wa mkutano mkuu wa ukuhani wa Oktoba 2002, mimi niliwapa changamoto maaskofu, wazazi, na wamisionari watarajiwa “kuinua kiwango” cha huduma ya wamisionari wa muda.

Kisha nikasema kwamba “kile tunachohitaji. … ni kizazi kikuu cha wamisionari katika historia ya Kanisa. Tunahitaji wamisionari wastahiki, waliohitimu, walio na nguvu kiroho. …

“… Tunahitaji moyo na nafsi zenu kunjufu. Tunahitaji wamisionari wachangamfu, wenye kufikiria, wenye ari ambao wanajua jinsi ya kusikiliza ma kujibu minong’ono ya Roho Mtakatifu.”1

Katika njia nyingi duniani leo kuna changamoto nyingi kuliko ilivyokuwa miaka kumi na mitatu iliyopita. Wavulana na wasichana wetu wana vichangamanishi vingi sana vya kuwachepusha katika yote maandalizi ya misheni na ya maisha ya furaha ya siku zijazo. Tekinolojia imepanuka, na karibu kila mtu ana uwezo wa kupata vyombo vya mkononi ambayo vinashika usikivu wa familia ya binadamu ya Mungu kwa wema mwingi na uovu mwingi.

Usiku wa leo, ninaongea na wamisionari sasa wanaohudumu, wamisionari wa siku zijazo, wamisionari waliorejea, na vijana wazima katika Kanisa. Ninaomba kuwa ninyi mtaelewa na kwa makini kufikiria kile mimi nitanena kwenu mnaposafiri katika miaka ya maisha yenu yenye kuchangamsha na magumu.

Katika miaka ya mapema ya Kanisa, wamisionari walikuwa wanahojiwa na Viongozi wenye Mamlaka kabla ya kwenda kwenye uwanda wa misheni. Siku hizi mnahojiwa ili kuhudumu kama wamisionari na maaskofu na marais wenu wa vigingi, na wengi wenu mtapitia maishani mwenu mwote bila kuhojiwa na Kiongozi mwenye Mamlaka. Hili ni onyesho la uhalisi katika kanisa la duniani kote lenye zaidi ya waumini milioni 15. Mimi najua ninaongea kwa niaba ya Ndugu zangu ninapowaambia kwamba tungependa kama ingewezekana sisi kuwajua nyinyi kibinafsi na kuweza kuwaambia kwamba tunawapenda na kuwaunga mkono.

Kwa bahati nzuri, Bwana ametoa njia kwetu za kuwafikia ninyi. Kwa mfano, mshiriki wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili humpangia kila mmisionari misheni yake. Ingawa hii inafanyika bila mahojiano ya kawaida ya ana kwa ana, tekinolojia na ufunuo kwa pamoja hutoa uzoefu ambao ni wa kindani na kibinafsi. Acheni niwaambie jinsi haya hutendeka.

Picha yako hutokeza kwenye scrini ya kompyuta na habari muhimu zilizotolewa na askofu na rais wa kigingi. Picha yako inapotokea, sisi hutazama macho na kurudia majibu yako ya maswali ya pendekezo la umisionari. Kwa huo muda mfupi, inaonekana kama wewe uko hapo na unatujibu moja kwa moja.

Tunapoitazama picha yako, tunaamini kwamba wewe umpasishwa kwa kila njia katika “kiwango kilicho juu” kinachohitajika leo kuwa wamisionari waaminifu, na wafanisi. Kisha, kwa uwezo wa Roho wa Bwana na chini ya maelekezo ya Rais Thomas S. Monson, sisi huwapangia kwenye mojawapo wa misheni 406 za Kanisa duniani kote.

La, siyo sawa na mahojiano ya kibinafsi, ya moja kwa moja. Lakini ni karibu kabisa.

Mkutano wa video ni njia nyingine ambayo hutusaidia sisi kuwafikia viongozi na waumini wa Kanisa ambao wanaishi mbali sana na makao makuu ya Kanisa.

Tukijua hayo, mimi ningependa wale wenu mnaojiandaa kuhudumu misheni, wale ambao mmerudi, na wengi wenu vijana wazima mtumie dakika chache nami kama vile mna mazungumzo ya kibinafsi ya video sasa hivi. Tafadhali nitazame kwa dakika chache kama vile wewe peke yako ndiye uliye katika chumba hiki pamoja nami jioni ya leo popote ulipo.

Kwa upande wangu, mimi nitataswiri kwamba ninatazama machoni mwako na kukusikiliza kwa makini majibu yako kwa maswali machache ambayo ninaamini yataniambia mengi kuhusu kina cha ushuhuda wako na kujitolea kwako kwa Mungu. Kama ninaweza kusema kwa maneno mengine kile nilisema kwa wamisionari miaka 13 iliyopita. Tunahitaji moyo na nafsi zenu kunjufu. Tunahitaji vijana wazima wachangamfu, wenye umaizi, wenye ari ambao wanajua jinsi ya kusikiliza na kujibu minong’ono ya Roho Mtakatifu mnapopitia njiani mwenu kupitia majaribio na majaribu ya kila siku ya kuwa kijana wa kisasa Mtakatifu wa Siku za Mwisho.

Kwa maneno mengine, sasa ni wakati wa kuinua kiwango siyo tu kwa wamisionari lakini pia kwa wamisionari waliorudi na kwa kizazi chenu chote. Kwa hayo, tafadhali tafakari katika moyo wako wote majibu yako kwa maswali haya:

  1. Je! Unapekua maandiko kila mara?

  2. Je! Unapiga magoti katika maombi ili kuongea na Baba yako wa Mbinguni kila asubuhi na kila usiku?

  3. Je! Unafunga na kuchangia matoleo ya mfungo kila mwezi---hata kama wewe ni maskini, mwanafunzi asiyejiweza ambaye hawezi kugharamia mchango wowote?

  4. Je! Unafikiria kwa kina kuhusu Mwokozi na dhabihu Yake ya Upatanisho kwako unapoombwa kutayarisha, kubariki, kupitisha, au kupokea sakramenti?

  5. Je! Unahudhuria mikutano yako na kujitahidi kuitakasa siku ya Sabato?

  6. Je! Wewe ni mwaminifu nyumbani, shuleni, kanisani, na kazini?

  7. Je! Wewe ni msafi kiakili na kiroho? Unaepukana na kutazama ponografia au kutazama mitandao, magazeti, sinema, au vipindi, vikijumuisha picha za Tinder au Snapchart, ambazo zinaweza kukuaibisha kama wazazi wako, viongozi wa Kanisa, au Mwokozi Mwenyewe angekuwa na wewe?

  8. Je! Wewe ni makini na muda wako---kuepukana na tekinolojia isiyofaa na vyombo vya kijamii, ikijumuisha michezo ya video, ambayo inaduwaza usikivu wako wa kiroho?

  9. Je! Kuna chochote katika maisha yako unachohitaji kubadili na kurekebisha, kuanzia leo?

Asanteni kwa haya mazungumzo mafupi ya kibinafsi. Natumaini umejibu kila mojawapo ya maswali haya kwa uaminifu na makini. Kama unajipata na upungufu katika mojawapo wa kanuni hizi rahisi, basi ninawahimiza ninyi mtubu kwa ujasiri na kuleta maisha yenu kwenye viwango vya injili vya wema.

Sasa kina ndugu, acha niwapatie ushauri wa ziada ambao utawasaidia kupata ushuhuda wetu wa injili kupata mizizi katika mioyo na nafsi zenu?

Ninawakumbusha wamisionari waliorejea kwamba maandalizi yenu kwa maisha na kwa familia yanafaa kuendelea. MM haimaanishi “Mmormoni Mstaafu!” Kama mmisionari aliyerejea, “unafaa kujishughulisha kwa shauku katika kazi njema, na kufanya mambo mengi kwa hiari [yenu] wenyewe, na kutekeleza haki nyingi.”2

Tafadhali tumieni ujuzi mliojifunza kwenye misheni zenu kubariki maisha ya watu walio karibu na wewe kila siku. Usiondoe uzingatifu wa kuwahudumia wengine kwa kulenga tu shughuli za shule, kazi, au kijamii. Badala yake, weka wastani maisha yako kwa uzoefu wa kiroho ambao unakukumbusha na kukuandaa kuendelea kuwahudumia wengine kila siku.

Wakati wa misheni yako ulijifunza umuhimu wa kuwatembelea watu nyumbani mwao. Ningetumaini kwamba ninyi nyote vijana wazima, kama mmehudumu misheni au la, muelewe umuhimu wa kuzungumza na watu ambao ni wapweke, wagonjwa, au waliovunjika mioyo---siyo tu kama kazi bali kwa sababu ya upendo wa kweli ulio nao kwa Baba wa Mbinguni na watoto Wake.

Wengine wenu katika shule ya upili mnaojiandaa kwa misheni, ninawahimiza mshiriki na muhitimu katika seminari. Ninyi vijana wazima mnapaswa kujisajili katika chuo cha dini.3 Kama mnahudhuria shule ya Kanisa, vivyo hivyo jumuisheni darasa kila muhula katika elimu ya dini. Wakati wa huu msimu muhimu wa maandalizi ya misheni au ndoa ya milele na maisha yenu kama watu wazima, ni sharti muendelee kutafuta njia ya kujifunza na kukua na kupokea uvuvio wa mwongozo kupitia Roho Mtakatifu. Kwa makini, maombi kujifunza injili kupitia seminari chuo, au madarasa ya elimu ya dini kunaweza kukusaidia katika hili lengo.

Kama mnahudhuria shule ya Kanisa au la, kama mnahudhuria chuo au la, msifikirie kuwa mna shughuli nyingi sana kujifunza injili. Madarasa ya seminari, chuo, au dini yanaweza kupatiana wastani wa maisha yenu, na kuongezea kwa elimu yenu ya shule kwa kuwapatia nafasi nyingine ya kutumia mkijifunza maandiko na mafundisho ya manabii na mitume. Kuna kozi nne mpya ambazo ninamhimiza kila kijana mzima kuangalia na kuhudhuria.4

Na msisahau kwamba madarasa na shughuli zinazopatikana katika chuo chenu au kupitia vijana wazima waseja wetu wa kata au kigingi pia itakuwa mahali ambapo mnaweza kuwa na wavulana na wasichana wengine. Ndugu, kama mnaweza kuweka kando simu zenu za rununu na hasa kutazama kidogo, mnaweza hata kupata mwenzi wenu wa milele wa siku zijazo.

Ambayo inanifikisha kwenye sehemu ya ushauri ambao mimi nina hakika mlijua inakuja: Niniyi vijana wazima waseja mnahitaji kufanya miadi na kufunga ndoa. Tafadhalini mkome kuchelewesha! Ninawajua baadhi yenu mnaogopa kuanzisha familia. Hata hivyo, kama mtaoa yule mtu sahihi kwa wakati sahihi na katika mahali sahihi, hamtahitaji kuogopa. Kwa kweli matatizo mengi mnayokabiliana nayo yataepukika kama “mtajishughulisha kwa bidii” katika kuweka miadi, uchumba, na ndoa njema. Usimtumie msichana ujumbe mfupi! Tumia sauti yako kujitambulisha mwenyewe kwa mabinti wema wa Mungu ambao wako karibu nawe. Hasa kusikia sauti ya binadamu kutamshangaza yeye aseme ndio.

Nashuhudia kwenu, ndugu zangu wa ukuhani, kwamba Bwana Yesu Kristo anaweza kutusaidia kurekebisha kitu chochote ambacho kinahitaji kurekebishwa katika maisha yetu kupitia dhabihu ya Upatanisho Wake.

Jioni ya leo tunapojiandaa kusherekea Jumapili ya Pasaka kesho, tafadhalini tueni pamoja nami mkumbuke kipawa cha Upatanisho wa Kristo. Kumbukeni kwamba Baba yetu wa Mbinguni na Mwokozi wetu, Yesu Kristo, wanawajua vyema na kuwapenda sana.

Kupitia kwa Upatanisho, Mkombozi alijichukulia juu Yake Mwenyewe matatizo, maumivu, na dhambi zetu. Mwokozi wa ulimwengu alikuja kumwelewa kila mmoja wetu kibinafsi kwa kupata uzoefu wa matumaini yaliyokatizwa, changamoto, na majanga kupitia mateso Yake katika Gethsemane na msalabani.5 Alikufa kama kitendo kimoja cha mwisho cha upendo kwa ajili yetu na kuzikwa katika kaburi jipya katika usiku ule.

Asubuhi ya Jumapili, Yesu alifufuka kutoka kwa wafu---akiahidi maisha mapya kwa kila mmoja wetu. Bwana mfufuka kisha akawaamuru wanafunzi Wake wakamfundishe kila mtu kuwa na imani katika Kristo, watubu dhambi, wabatizwe, wapokee kipawa cha Roho Mtakatifu, na wavumilie hadi mwisho. Ndugu, sisi tunajua kwamba Mungu Baba yetu na Mwanawe Mpendwa walimtembelea Nabii Joseph Smith na kurejesha kupitia kwake ukamilifu wa injili ya Yesu Kristo.

Mweneni imara, kina ndugu. Wekeni amri za Mungu. Bwana Yesu Kristo anaahidi vitu vyote tunavyotamani kufanya katika wema vitakuwa vyetu. Viongozi wa kanisa wanawategemea ninyi. Tunahitaji kila mmoja wenu ninyi vijana wazima kujiandaa kufunga ndoa, kuhudumu, na kuongoza katika siku zijazo, hivyo ndivyo ninavyomba katika jina ka Bwana wetu Yesu Kristo, amina.