2010–2019
Mpango wa Furaha
Aprili 2015


Mpango wa Furaha

Dhamira ya shughuli zote katika Kanisa ni kuona kwamba mwanaume na mwanamke pamoja na watoto wao wana furaha nyumbani na wamefunganishwa pamoja kwa wakati na milele yote.

Miaka mingi iliyopita, baada ya Vita vya Dunia vya II, nilikuwa nikihudhuria chuo nilipokutana na Donna Smith. Wakati nilipojifunza kwamba viungo viwili muhimu vya ndoa yenye ufanisi ni biskuti na busu. Nilidhania kwamba hiyo ilikuwa maridhawa sana.

Nilihudhuria chuo asubuhi, na kisha kurudi Brigham City ili kufanya kazi katika gereji ya baba yangu wakati wa mchana. Somo la asubuhi la mwisho lilikuwa ni sayansi kimu. Nilipitia darasani mwake kabla sijaondoka. Mlango ulikuwa na kioo cha ukungu, lakini kama ningesimama karibu na kioo angeweza kuona kuvuli changu nje. Angetoka nje na biskuti na busu. Mengineyo ni historia. Tulifunga ndoa katika Hekalu la Salt Lake, na hiyo ilianzisha safari kuu ya maisha yetu.

Miaka mingi kila mara nimefunza kanuni muhimu: dhamira ya shughuli zote katika Kanisa ni kuona kwamba mwanaume na mwanamke pamoja na watoto wao wana furaha nyumbani na wamefunganishwa pamoja kwa wakati na milele yote.

Hapo mwanzoni:

“Hivyo Miungu wakashuka chini ili kumuumba mtu kwa mfano wao, katika mfano wa Miungu wamfanye yeye, mme na mke wawafanye.

“Na Miungu wakasema: Tutawabariki. Na Miungu wakasema: Tutawafanya wazaane na kuongezeka, na waijaze dunia, na kuitiisha” (Ibrahimu 4:27–28).

Na hivyo basi msururu wa maisha ya binadamu hukaanza katika dunia hii “Na Adamu akamjua mke wake, naye akamzalia wana na mabinti, nao wakaanza kuongezeka na kuijaza nchi.

“Na … wana na mabinti wa Adamu wakaanza kugawana wawili wawili katika nchi,  … nao pia wakazaa wana na mabinti (Musa 5:2–3).

Amri ya kuzaana na kuijaza nchi kamwe haijabatilishwa. Ni muhimu katika mpango wa ukombozi na ndiyo chanzo cha furaha ya binadamu. Kupitia matumizi mema ya nguvu hizi, tunaweza kuja karibu na Baba yetu aliye Mbinguni na kupata ujalivu wa furaha, hata uungu. Nguvu za uumbaji si sehemu ya ziada ya mpango wa furaha; ni muhimu kwa furaha.

Hamu ya kujamiiana katika binadamu ni kawaida na ina nguvu sana. Furaha yetu katika maisha duniani, shangwe yetu na kuinuliwa kwetu kunategemea jinsi sisi tutajibu hizi tamaa za kimwili zinazozidi, zenye msukumo. Jinsi nguvu za uumbaji zinavyokomaa katika uanaume na uanauke hapo mapema, hisia za kibinafsi hutokea, katika njia ya kiasili, tofauti na uzoefu mwingine wowote wa kimwili.

Kwa kawaida kujamiiana huanza na mapenzi. Ingawa desturi zinatofautiana, hushamiri kama katika hisia zote za kitabu cha hadithi za mhemko na matarajio, hata wakati mwingine kukataliwa. Kuna mbala-mwezi na waridi, barua za mapenzi, nyimbo za mapenzi, mashairi, kushikana mikono, na maonyesho mengine ya mapenzi katika mvulana na msichana. Dunia hutoweka kutoka kwa wenzi hawa, na wanapata hisia za furaha.

Kama mnadhania kwamba mfumko wa penzi la ujana ndiyo jumla ya uwezekano ambao unachipuka kutoka katika birika la maisha, basi wewe haujaishi kuona upendo na faraja ya upendo wa waliooana kwa muda mrefu. Wanandoa wamejaribiwa kwa majaribu, kutoelewana, shida za kifedha, majanga ya familia, magonjwa, na wakati wote huu upendo hukua ukawa imara. Penzi pevu lina upeo wa furaha ambao kamwe haujafikirika na wana-ndoa wapya.

Penzi la kweli huhitaji kungojea mpaka baada ya ndoa kushiriki kwa hayo mapenzi ambayo hufungua hizo nguvu takatifu katika ile birika ya maisha. Humaanisha kuepukana na hali ambapo tamaa za kimwili zinaweza kuvuka mipaka. Penzi halisi limepangiwa kuwa ni tu baada ya uaminifu wa milele, sherehe kihalali na kisheria, na kwa kawaida baada ya ibada ya kufunganishwa katika hekalu, ndipo zile nguvu za uumbaji zinaachiliwa katika macho ya Mungu kwa maonyesho kamili ya upendo. Zinapaswa kushirikiwa  tu  na pekee na mtu ambaye ni mwenzi wako wa milele.

Unapofanyika kwa ustahiki, mfanyiko huu hujumuisha mhemko kimwili wa kipekee sana na wa kuinuliwa, na hisia za kiroho zinazohusiana na neno pendo. Sehemu hiyo ya maisha haina kisawe, haina kifani, katika uzoefu wote wa binadamu. Itakuwa, wakati maagano yamefanywa na kuwekwa, kudumu milele, “kwani ndani yake funguo za ukuhani mtakatifu zimewekwa, ili mpate kupokea heshima na utukufu” (M&M 124:34), “utukufu ambao utakuwa mkamilifu na kuendelea kwa vizazi milele na milele” (M&M 132:19).

Lakini pendo la mapenzi si kamili, ni mwanzo. Pendo linarutubishwa na kuzaliwa kwa watoto, ambao huchipuka kutoka katika lile birika la maisha lililothaminiwa kwa wenzi katika ndoa. Utungaji mimba hufanyika katika kumbatio la mume na mke waliooana. Mwili mdogo huanza kuumbika kwa muundo changamani wa ajabu. Mtoto hutokea katika muujiza wa uzazi, aliyeumbwa kwa sura ya baba na mama yake wa duniani. Ndani ya mwili wake kuna roho ambayo inaweza kuhisi na kujua vitu vya kiroho. Iliyo fiche katika mwili wa mtoto ni nguvu za kuzaa mtoto katika sura yake mwenyewe.

“Roho na mwili ndiyo nafsi ya mwanadamu” (M&M 88:15), na kuna sheria za kiroho na kimwili za kutiiwa kama tunataka kuwa na furaha. Kuna sheria za milele, ikijumuisha sheria inayohusiana na nguvu hizi ili kupatiana uhai, “isiyotenguliwa iliyowekwa mbinguni kabla ya misingi ya ulimwengu huu, ambapo juu yake baraka zote hutoka” (M&M 130:20). Hizi ni sheria za kiroho ambazo zinaelezea viwango vya maadili kwa mwanadamu (ona Joseph Smith—Tafsiri, Warumi 7:14–25 [katika kiambatisho cha Biblia]; 2 Nefi 2:5; M&M 29:34; 134:6). Kuna maagano ambayo yanafunga, kufunganisha, na kulinda na kutoa ahadi ya baraka za milele.

Alma alimuonya mwanawe Shibloni, “Uone kwamba ujifunze kuzuia tamaa zako zote, ili uweze kujazwa na mapenzi” (Alma 38:12). Ungwe hutumika kuongoza, kuelekeza, kuzuia. Tamaa zetu zinapaswa kuthibitiwa. Wakati zinapotumika kisheria, nguvu za uumbaji zitabariki na kutakasa (ona Teachings of Presidents of the Church: Joseph F. Smith [1998], 158).

Majaribu yapo kila mara. Kwa sababu adui hawezi kuumba uzima, yeye ana wivu dhidi ya wale wote walio na hizo nguvu za mbinguni. Yeye na wale ambao walimfuata walitupwa nje na kupoteza hali ya kuwa na mwili. “Kwani anataka wanadamu wote wawe na dhiki kama yeye(2 Nefi 2:27). Atakujaribu, kama anaweza, kukuzorotesha, kukuharibu, na kama inawezekana, kuangamiza hiki kipawa ambacho kwacho tunaweza, kama tu wastahiki, kuwa ongezeko la milele (ona M&M 132:28–31).

Kama tukichafua birika zetu za maisha au kuwafanya wengine watende dhambi, kutakuwa na adhabu “kali” zaidi na “ngumu kuvumilia” (ona (M&M 19:15)kushinda anasa za kimwili zinaweza kustahili.

Alma alimwambia mwanawe Koriantoni, “Hujui, mwana wangu, kwamba vitu hivi ni machukizo machoni mwa Bwana; ndio, ni machukizo kuliko dhambi zote isipokuwa ile ya kumwaga damu ya wale wasio na hatia au kumkana Roho Mtakatifu?” (Alma 39:5). Hatuwezi kukwepa matokeo tunapotenda dhambi.

Maonyesho yoyote yaliyo halali, yamekubaliwa ya nguvu za uumbaji ni kati mume na mke ambao wameoana kihalali na kisheria. Kitu kingine chochote isipokuwa hiki huvunja amri za Mungu. Msikubali majaribu mchafu ya adui, kwa kila deni la uvunjaji amri ni sharti lilipwe, “hata uishe kulipa senti ya mwisho” (Mathayo 5:26).

Hamna popote ukarimu na neema za Mungu zinazoonekana zaidi kuliko katika toba.

Miili yetu, inapoumizwa, inaweza kujirekebisha yenyewe, wakati mwingine tunahitaji msaada wa tabibu. Kama kuumizwa ni kubaya zaidi, hata hivyo, mara nyingi kovu hubakia kama ukumbusho wa jeraha.

Katika miili yetu ya kiroho ni jambo lingine. Roho zetu zinaumizwa wakati tunapofanya makosa na kutenda dhambi. Lakini tofauti za hali ya miili yetu, wakati mfanyiko wa toba umekamilika, hamna kovu linalobakia kwa sababu ya Upatanisho wa Yesu Kristo. Ahadi ni: “Tazama, yule ambaye ametubu dhambi zake, huyu anasamehewa, na Mimi, Bwana, sizikumbuki tena” (M&M 58:42).

Tunapoongea juu ya ndoa na maisha ya familia, kuwa jambo bila shaka huja akili, “Je! vipi walio tofauti?” Baadhi huzaliwa na mapungufu na hawezi kupata watoto. Baadhi wasio na hatia ndoa zao zimevunjika kwa sababu ya uasherati wa wenzi wao. Wengine hawaoi na wanaishi maisha ya useja wa kustahiki.

Kwa sasa, ninatoa faraja hii: Mungu ni Baba yetu! Upendo wote na ukarimu wote unaoonekana katika mfano mzuri wa baba wa duniani hupanuliwa katika Yule ambaye ni Baba yetu na Mungu wetu anayezidi uwezo wa akili za binadamu kuelewa. Hukumu yake ni ya haki; Neema yake haina kipimo; uwezo Wake wa kufidia usio na kifani. “Kama katika maisha haya tu tumemtumaini Kristo, sisi tu maskini kuliko watu wote. (1 Wakorintho 15:19).

Kwa staha sasa mimi nitatumia neno hekalu. Ninaona chumba cha kufunganisha na altari pakiwa na wenzi vijana wakipiga magoti. Hii ibada takatifu ya hekalu ni zaidi ya harusi, kwani ndoa hii inaweza kufunganishwa na Roho Mtakatifu wa Ahadi, na maandiko yanatangaza kwamba sisi “tutarithi enzi, falme, himaya, na nguvu, utawala” (M&M 132:19). Ninaona furaha ambayo inawangoja wale wanaokubali hiki kipawa cha mbinguni na kukitumia kwa kustahili.

Dada Donna Smith Packer nami tumekuwa bega kwa bega katika ndoa kwa karibu miaka 70. Ikija kwa mke wangu na mama wa watoto wetu, sina maneno ya kusema. Hisia ni za kina sana na shukrani ni za nguvu sana kwamba ninabaki na bila cha kusema. Zawadi kuu tumepokea katika maisha haya, na maisha yajayo, ni watoto wetu na wajukuu wetu. Tukielekea ukingoni wa siku zetu duniani pamoja, mimi nina shukranni kwa kila dakika ya kuwa naye kando yangu na kwa ahadi Bwana aliyoitoa ambayo haitakuwa na mwisho.

Ninatoa ushahidi kwamba Yesu ndiye Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai. Yeye anasimama katika kichwa cha Kanisa hili. Kupitia Upatanisho Wake na nguvu za ukuhani, familia ambazo zinaanza duniani zinaweza kuwa pamoja milele. Upatanisho, ambao unamkomboa kila mmoja wetu, hauna makovu. Hii inamaanisha kwamba haijalishi kile tumefanya ama pale tumekuwa ama jinsi mambao yametokea, kama kwa kweli tukitubu, Yeye ameahidi kwamba Atapatanisha. Na wakati alifanya upatanisho, alilipia hayo. Kuna wengi wetu ambao wanagaagaa, kama ilivyo, na hisia za hatia, bila kujua jinsi ya kuponyoka. Unaponyoka kwa kukubali Upatanisho wa Kristo, na machungu yote yanaweza kugeuka kuwa uzuri na upendo na umilele.

Mimi nina shukrani kwa ajili ya baraka za Yesu Kristo, kwa ajili ya nguvu za uumbaji, kwa ajili ya nguvu za ukombozi, kwa Upatanisho---Upatanisho ambao unaosha kila waa bila kujali ni vigumu jinsi gani ama itachukua mudagani ama itarudiwa mara ngapi. Upatanisho unaweza kukuweka huru tena kusonga mbele, kwa usafi na ustahiki, kufuata ile njia umechagua katika maisha.

Mimi ninashuhudia kwamba Mungu yu hai, kwamba Yesu ndiye Kristo, kwamba Upatanisho si kitu cha kawaida ambacho ni Kanisa lote. Upatanisho ni wa kibinafsi, na kama una kitu ambacho kinakusumbua---wakati mwingine almradi hauwezi kukikumbuka---weka Upatanisho kazini. Utakusafisha, na wewe, kama Yeye anavyofanya, hatakumbuka dhambi zako kamwe. Katika jina la Yesu Kristo, amina