2010–2019
Usiogope, Amini Tu
Oktoba 2015


Usiogope, Amini Tu

Tunapochagua kuamini, kuitumia imani katika toba, na kumfuata Mwokozi wetu, Yesu Kristo, tunafumbua macho yetu ya kiroho kwa mazuri tusiyoweza kuyafikiria.

Babeli na Danieli

Miaka elfu mbili na mia sita iliyopita, Babeli lilikuwa ni taifa lenye nguvu. Mmoja wa wanahistoria wa kale alizielezea kuta za Babeli ambazo ziliuzunguka mji ulikuwa na urefu wa zaidi ya futi 300 (mita 90) na unene wa futi 80 (mita 25). “Katika ukuu,” aliandika, “hakuna mji mwingine mzuri unaoukaribia.”1

Kwa wakati huo, Babeli ilikuwa ni kitovu cha dunia kujifunza sheria, na falsafa. Nguvu ya jeshi lake zilikuwa kubwa. Zilipita uwezo wa nguvu za Misri. Ilivamia, ilichoma, na kuiba vitu vya mji mkuu wa Ashuru, Ninawi. Kwa urahisi aliishinda Yerusalemu na kuwachukua watoto wazuri na wenye akili wa Israeli kwenda nao Babeli kumtumikia Mfalme Nebukadreza.

Mmoja wa mateka hawa alikuwa kijana aitwaye Danieli. Wasomi wengi waliamini kwamba Danieli alikuwa na umri wa kati ya miaka 12 na 17 wakati huo. Hebu fikirieni, vijana wangu wapendwa wa Ukuhani wa Haruni; Danieli alikuwa karibu wa rika lenu alipochukuliwa hadi kwenye mahakama ya mfalme ili kufundishwa lugha, sheria, dini, na sayansi ya ulimwengu wa Babeli.

Je, unaweza kufikiria jinsi ambavyo ungejisikia kwa kulazimishwa kutoka nyumbani kwako, kutembea maili 500 (800 km) katika mji wa kigeni, unaofundishwa mafundisho ya dini ya maadui zako?

Danieli alilelewa kama mfuasi wa Yehova. Aliamini na kumwabudu Mungu wa Ibrahimu, Isaka na Yakobo. Alijifunza maneno ya manabii, na alijua jinsi Mungu anavyoongea na wanadamu.

Lakini sasa, akiwa na umri mdogo, alikuwa mwanafunzi mfungwa huko Babeli. Shinikizo kwake lazima lilikuwa mkubwa ili aache imani zake za zamani na kuzikubali zile za Babeli. Lakini alibaki mkweli kwa imani yake—kwa maneno na kwa vitendo.

Wengi wenu mnajua inavyokuwa katika kuutetea ukweli usiopendelewa. Katika lugha ya kitovuti leo, tunazungumzia ”kuchomwa moto” na wale wasiokubaliana nasi. Lakini Danieli hakuwa anahatarisha kejeli za umma. Katika Babeli, wale wanaopingana viongozi wa dini walielewa kitakachofuata—kwa maneno mengine na kifasihi—kuchomwa “moto.” Waulize marafiki wa Danieli ambao ni Shadraka, Meshaki na Abed-nego.2

Sijui kama ilikuwa rahisi kwa Danieli kuwa mwamini katika hali kama ile. Baadhi ya watu wamebarikiwa na moyo wa kuamini—kwao, imani inakuja kama kipawa kutoka mbinguni. Lakini naona Danieli alikuwa kama wengi wetu ambao inabidi tufanyie kazi ushuhuda wetu. Nina uhakika kwamba Danieli alitumia masaa mengi kupiga magoti akisali, akitoa woga wake kwenye madhabahu ya imani, na kumsubiri Bwana kwa ajili ya uelewa na busara.

Na Bwana alimbariki Danieli. Japokuwa imani yake ilikumbwa na changamoto na kudharauliwa, alibaki mkweli kwa yale aliyoyajua kwa uzoefu wake kuwa ni kweli.

Danieli aliamini. Danieli hakuwa na shaka.

Na kasha usiku mmoja, Mfalme Nebukadireza aliota njozi ambayo ilisumbua fikra zake. Aliikusanya timu yake ya wasomi na washauri na kuwataka wailezee njozi kwake na pia watoe maana ya hiyo njozi.

Hakika, hawakuweza kuitafsiri. “Hakuna awezaye kufanya uliyoyataka,” walisema. Lakini majibu haya yalimfanya Nebukadreza akaghadhibika sana, na akatoa amri kuwaangamiza wenye hekima, waganga, wanajimu, na washauri—akiwemo Danieli na wanafunzi wengine kutoka Israeli.

Ninyi mnaokielewa kitabu cha Danileli mnajua kilichotokea baada ya hapo. Danieli alimwomba Nebukadreza apete muda zaidi, na yeye na wenza wake wema wakienda kwenye chanzo cha imani yao nguvu ya kimwili. Walimwomba kwa Mungu na kuomba msaada wa kiroho katika wakati huu muhimu katika maisha yao. Na “kisha siri ikafunguliwa kwa Danieli katika … njozi.”3

Danieli, kijana mdogo toka taifa la ushinde—alikuwa anakashfiwa na kupingwa kwa ajili ya kuamini dini yake ya geni—alikwenda kwa mfalme na kumfunulia njozi na maana yake.

Kuanzia siku ile na kuendelea, kwa matokeo ya uaminifu wake kwa Mungu, Danieli akawa mshauri wa kuaminika wa mfalme, alijulikana kwa busara zake katika Babeli yote.

Kijana aliyeamini na kuiishi imaniyake akawa mtu wa Mungu. Nabii. Mfalme wa haki4

Je, Tuko kama Danieli?

Kwetu sisi wote tulio na ukuhani wa Mungu ninawauliza, je, tuko kama Danieli?

Je, tunasimama waaminifu kwa Mungu?

Je, tunatenda yale tunayoyahubiri, au sisi ni Wakristo wa Jumapili tu?

Je, matendo yetu ya kila siku yanawiana na yale tunayoyaamini?

Je, tunawasaidia maskini na wenye shida, wagonjwa na walioteseka:5

Je, tunaongea tu, au kwa shauku kubwa tunafanya mambo yaliyo mema?

Ndugu, sisi tumepewa vingi. Tumefundishwa ukweli mtakatifu wa injili iliyorejeshwa ya Yesu Kristo. Tumeaminiwa kwa mamlaka ya ukuhani ili kuwasaidia wenzetu na kuujenga ufalme wa Mungu hapa duniani. Tunaishi katika nyakati za uwezo mkubwa wa kiroho. Tuna utimilifu wa kweli. Tuna funguo za ukuhani za kufunga duniani na mbinguni. Maandiko matakatifu na mafundisho ya manabii na mitume waliohai yanapatikana kushinda hapo mbeleni.

Wapendwa rafiki zangu, acheni tuyachukue mambo haya kwa umakini. Kwa baraka na fursa hizi yanakuja majukumu na wajibu mkubwa. Acheni tuyakubali majukumu haya.

Mji wa kale wa Babeli ni mahame sasa. Ufahari wake umetoweka. Lakini malimwengu na uovu wa Babeli bado unaendelea. Sasa ni wajibu wetu kuishi kama waumini katika ulimwengu wa kutokuamini. Changamoto ni kwetu kuzitumia kanuni za injili iliyo rejeshwa ya Yesu Kristo na kuishi katika kweli ya amri za Mungu. Tutahitaji kuwa wapole chini ya shinikizo la wenzetu, tusipendezwe na mitindo maarufu au manabii waongo, tupuuze kejeli za waovu, majaribu ya yule muovu, na tuushinde uzembe wetu wenyewe.

Hebu fikiria juu ya hili. Ingekuwa rahisi namna gani kwa Danieli kuzifuata njia za Babeli? Angeweza kuweka kando kanuni ambazo Mungu aliwapa wana wa Israeli. Angeweza kula chakula cha matajiri kinachotolewa na mfalme na kujinafasisha katika starehe za duniani za mwanadamu wa kawaida. Angeweza kuepuka kejeli.

Angeweza kuwa maarufu.

Angeweza kukubalika.

Njia zake zingeweza kuwa zenye shida kidogo.

Hiyo ni, hakika, hadi siku ambayo mfalme alitaka tafsiri ya njozi yake. Kisha Danieli angeweza kujua kwamba yeye, kama wazee wa busara wengine wa Babeli, angepoteza uhusiano wake wa chanzo cha kweli cha nuru na hekima.

Danieli alishinda mtihani wake. Wetu bado unaendelea.

Ujasiri wa Kuamini

Shetani, adui yetu, anataka sisi tushindwe. Anasambaza uongo kama sehemu ya juhudi zake za kuangamiza imani yetu. Kwa ujanja anapendekeza kwamba wenye shaka, mkosaji na mbeuzi ni wakisasa na enye akili, wakati wale wenye imani katika Mungu na miujiza yake ni wajinga, vipofu, au tusiofikiri. Shetani atapendekeza kwamba ni sawa kutilia shaka vipawa vya kiroho na mafundisho ya manabii wa kweli.

Ningependa kumsaidia kila mmoja kuelewa ukweli huu rahisi: sisi tunaami katika Mungu kwa sababu ya vitu tuvijuavyo kwa moyo na akili zetu, na siyo kwa sababu ya vitu tusivyovijua. Uzoefu wetu wa kiroho wakati mwingine ni mtakatifu sana kuelezea katika misamiati ya kilimwengu, lakini hiyo haina maana si halisi.

Baba wa Mbinguni amewaandalia watoto Wake karamu ya kiroho, akitoa kila aina ya chakula cha kifahari ambacho unachoweza kufikiria—na bado, badala ya kufurahia karama hizi za kiroho, watalia shaka wanahisi wametosheka wakitazama kutoka mbali, wakinywa kutoka kwa vikombe vya ya ubeuizi, shaka na kutoheshimu.

Kwa nini mtu yeyote atembee katika akiwa katosheka kwa nuru itokayo kwa mshumaa wao wenyewe wa uelewa, kwa kumgeukia Baba yetu wa Mbinguni, wanaweza kupata mwanga wa jua wa elimu ya kiroho ambayo ingeweza kupanua fikra kwa busara na kujaza nafsi zao kwa furaha?

Wakati wewe na mimi tunapoongea na watu kuhusu imani na kuamini, hivi hatusikii, “Natamani ningeamini kama wewe”?

Katika taarifa kama hiyo ni uongo mwingine wa Shetani: imani hiyo inapatikana kwa baadhi ya watu lakini siyo kwa wengine. Hakuna miujiza ya kuamini. Lakini kutaka kuamini ni hatua muhimu ya kwanza! Mungu hamheshimu mtu.6 Yeye ni Baba yako. Anataka kuongea na wewe. Hata hivyo, inahitaji udadisi wa kisayansi—majaribio juu ya neno la Mungu—na zoezi la ”chembe la imani.”7 Pia inachukua unyenyekevu kidogo. Na inahitaji moyo na akili kunjufu. Inahitaji kutafuta, kwa maana kamili ya neno. Na, huenda kigumu cha yote, inahitaji kuwa na uvumilivu na kumsubiri Bwana.

Kama hatufanyi juhudi za kuamini, tupo kama mtu anayezima kurunzi na kisha kuilaumu kurunzi kwa kutotoa mwanga.

Hivi karibuni nilishangazwa na kusikitishwa kusikia kijana wa Ukuhani wa Haruni aliyeonekana akijivuna kwa sababu alikuwa amejitenga na Mungu. Alisema, “Kama Mungu Atajidhihirisha kwangu, ndipo nitaamini. Pasipo hivyo, nitatafuta ukweli ninaouelewa mimi mwenyewe na kunisaidia kuelewa kile ninachokielewa.”

Sijui moyo wa kijana huyu, lakini nisingeweza kusema lolote ila kusikitikia. Kwa haraka alivyokataa vipawa vya Bwana alivyokuwa anampa. Kijan huyu alizima kurunzi na kisha akaonekana kuridhika katika uchunguzi wake wa kijanja kwamba hapakuwa na mwanga.

Kwa bahati mbaya, hii inaoneka kuwa tabia maarufu siku hizi. Kama tunaweza kuweka mzigo wa ushahidi kwa Mungu, tunafikiri tunaweza kujitetea wenyewe kwa kutochukua amri za Mungu kwa makini na bila kuwajibika katika mahusiano yetu na Baba wa Mbinguni.

Ndugu, acha niwe muwazi, hakuna kitu kizuri au cha kuvutia juu ya kuwa mjinga. Wasiwasi ni rahisi – mtu yeyote anaweza kufanya hivyo. Ni maisha mema ambayo yanahitaji nguvu ya kimaadili, kujitolea, na ujasiri. Wale wanaofunga kwa imani huenda mbali zaidi kuliko wale ambao wana shaka wakati maswali ya kimiujiza au wasiwasi unapojitokeza.

Lakini haiwezi kutushangaza kwamba imani haithaminiwi na jamii. Dunia ina historia ndefu ya kukikataa kile ambacho haikielewi. Na ina tatizo fulani la kuelewa vitu ambavyo haviwezi kuonekana. Kwa sababu tu hatuwezi kuona kitu fulani kwa macho yetu, haina maana hakipo. Hakika, “kuna vitu vingi mbinguni na duniani … ambavyo vinaweza kufikiriwa katika vitabu vyetu, majarida ya kisayansi, na falsafa za kidunia.8 Ulimwengu umejaa maajabu makubwa na yakushangaza—vitu ambavyo vinaweza kuonekana kupitia macho ya kiroho.

Ahadi ya Amini

Tunapochagua kuamini, kuitumia imani katika toba, na kumfuata Mwokozi wetu, Yesu Kristo, tunafumbua macho yetu ya kiroho kwa mazuri tusiyoweza kuyafikiria. Hivyo amini na imani yetu itaongezeka, na tutaweza kuona zaidi.9

Ndugu, ninashuhudia kwamba hata katika nyakati ngumu, Mwokozi atasema nawe kama alivyosema na mababu waliojazana kwenye mtaa wa Galilaya, “Usiogope, amini tu.”10

Tunaweza kuchagua kuamini.

Kwani katika amini, tugundua machweo ya mwanga.

Tutagundua ukweli.11

Tutapata amani.12

Kwa sababu ya imani yetu, hatutakuwa na njaa, wala kuona kiu.13 Vipawa vya neema ya Mungu vitatuwezesha kuwa wakweli katika imani yetu na kuijaza nafsi yetu kama ”chemichemi itiririkayo katika uzima wa milele.”14 Tutapata furaha ya kweli na ya milele.15

Kwa hiyo, rafiki zangu wapendwa, ndugu zangu wapendwa katika ukuhani wa Mungu:

Kuweni ujasiri wa kuamini.

Msiogope, aminini tu.

Simameni pamoja na Danieli.

Ninaomba kwamba kila mmoja wetu—kijana na mzee—tutapata nguvu mpya, ujasiri, na nia ya kuamini. Katika jina la Yesu Kristo, amina.