2010–2019
”Kuchaguliwa Kushuhudia Jina Langu”
Oktoba 2015


”Kuchaguliwa Kushuhudia Jina Langu”

Ni bora kuwa wanaume wazee wenye ukomavu mkubwa wa kiroho na uamuzi kuweza kuhudumu katika nafasi za juu za uongozi wa Kanisa iliorejeshwa ya Yesu Kristo.

Katika mwaka wa 1996, Rais Gordon B. Hinckley alitokea katika kipindi cha habari cha televisheni ya kitaifa cha dakika 60. Mike Wallace, mwanahabari mwenye uzoefu na mahiri, alimhoji Rais Hinckley kuhusu mada kadhaa muhimu.

Karibu na mwisho wa mazungumzo yao, Bw. Wallace alisema, ”Kuna wale ambao wanasema, ’Huu ni usimamizi wa wazee. Hili ni Kanisa linaendesha na wazee.’”

Rais Hinckley alijibu kwa furaha na bila kusita, ”Kwani si ajabu kuwa na mwamume aliyekomaa kuwa kwenye uskani, mwamume wenye hekima ambaye hawezi kurushwa huko na kule na kila upepo wa mafundisho?” (broadcast on Apr. 7, 1996).

Kusudi langu la kuelezea kwa nini kweli ni ajabu kuwa na wazee wenye ukomavu mkuu wa kiroho na hekima wakihudumu katika nyadhifa za juu za uongozi katika Kanisa la Yesu Kristo la urejesho—na kwa nini tunapaswa “kusikia” na “kutii (Mosia 2:9) mafundisho ya wanaume hawa ambao Bwana ”amewachagua kushuhudia jina [Lake] ... miongoni mwa mataifa yote, koo, ndimi, na watu” ((M&M 112:1).

Mimi naomba sisi wote tuweze kufunzwa na Roho Mtakatifu tunapofikira pamoja hii mada muhimu.

Somo la Maisha Yote

Mimi nazungumza kuhusu mada hii kutoka kwa mtazamo wazi kabisa. Kwa miaka 11 iliyopita, mimi nimekuwa mshiriki kijana wa Akidi ya wale Kumi na Wawili kulingana na umri makuzi. Katika miaka yangu ya huduma, wastani wa umri wa wanaume wanaohudumu katika Urais wa Kwanza na Akidi ya wale Mitume Kumi na Wawili umekuwa miaka 77— uzee wa wastani wa umri wa mitume katika miaka 11 katika kipindi hiki.

Mimi nimebarikiwa kwa utume wa julma, dini, binafsi, na umahiri na umaizi wa washiriki wa akidi ambao ninahudumu nao. Mfano kutoka kwa uhusiano wangu na Mzee Robert  D. Hales huangazia fursa za ajabu nilizonazo za kujifunza kutoka kwao na kuhudumu pamoja na viongozi hawa.

Miaka kadhaa iliyopita nilichukua muda wa mchana wa jumapili moja pamoja na Mzee Hales katika nyumba yake siku ya Jumapili alipokuwa akipata ahueni kutoka na maradhi hatari. Tulizungumza kuhusu majukumu ya familia zetu, akidi yetu, matukio muhimu sana.

Wakati mmoja nilimuuliza Mzee Hales, ”Wewe umekuwa mwenye mafanikio kama mume, baba, mwana riadha, kiongozi wa biashara, na kiongozi wa Kanisa. Ni masomo gani umejifunza unapoendelea kuzeeka na umeweza kuzuiwa na upungufu wa uwezo wa kimwili?”

Mzee Hales alikaa kimya kwa muda mfupi na akajibu, ”Wakati unapokuwa hauwezi kufanya kile umekuwa ukifanya siku zote, basi wewe utafanya tu kile kilicho na maana sana.”

Nilishangazwa na urahisi na ukamilifu wa jibu lake. Mwenzi wangu katika utume alishiriki nami somo la maisha yote—somo linalofunzwa kupitia majaribu ya kuteseka kimwili na tafakari ya kiroho.

Ufinyu na Udhaifu wa Binadamu

Ufinyu ambao ni matokeo ya asili ya kuzeeka unaweza kwa hakika kuwa nyenzo ya ajabu kwa kujifunza kiroho na umaizi. Sababu zile wengi wanaweza kuaamini zinaleta ufinyu katika utenda kazi wa watumishi hawa zinaweza kuwa baadhi ya uwezo wao mkuu. Vizuizi vya kimwili vinaweza kupanua ono. Ufinyu wa siha unaweza kuchuja vipaumbele. Kutoweza kufanya vitu vingi kunaweza kuelekeza kwenye vitu vya umuhimu mkuu.

Baadhi ya watu wanapendekeza kwamba viongozi vijana wenye nguvu wanahitajika katika Kanisa ili kutatua vyema changamoto kali za ulimwengu wa kisasa. Lakini Bwana hatumii falsafa na desturi za kisasa za uongozi ili kutimiza madhumuni Yake (ona Isaya 55:8–9). Tunaweza kutarajia Rais na viongozi wakuu wa Kanisa daima watakuwa wanaume wazee na waliokomaa kiroho.

Mfumo wa Bwana uliyofunuliwa wa utawala wa mabaraza katika Kanisa Lake hutosheleza na kupunguza athari ya udhaifu wa binadamu. Cha kupendeza, ufinyu wa kibinadamu wa wanaume hawa hasa unadhibitisha chanzo kitakatifu cha mafunuo ambayo huja kwao, na kupitia kwao. Kwa kweli, wanaume hawa wameitwa na Mungu kwa unabii (ona Makala ya Imani 1:5).

Mfumo wa Matayarisho

Mimi nimeona katika Ndugu zangu angalu sehemu ya madhumuni ya Bwana kwamba wanaume wazee wenye ukomavu na hekima kuhudumu katika nyadhifa za juu za uongozi za Kanisa. Wanaume hawa wamekuwa na msimu wa kudumu wa kufunzwa na Bwana, ambaye wao humwakilisha, kumtumikia, na kumpenda. Wamejifunza kuelewa lugha takatifu ya Roho Mtakatifu na mfumo wa Bwana wa kupokea ufunuo. Hawa wanaume wa kawaida wamepitia mchakato wa ajabu wa ukuaji ambao umenoa maono yao, kufunza umaizi wao, kusababisha upendo kwa watu kutoka mataifa yote na hali zote, na kuthibitisha uhalisi wa Urejesho.

Mimi nimeshuhudia mara nyingi Ndugu zangu wakijitahidi kwa biidi sana kutekeleza na kutukuza majukumu yao wakiwa wanasumbuliwa na shida kali za kimwili. Wanaume hawa hawajazuiwa kutoka kwa mateso. Badala yake, wamebarikiwa na kuimarishwa kusonga mbele kwa ushupavu hali wanaumwa na kuteseka.

Kuhudumu pamoja na hawa wawakilishi wa Bwana, nimepata kujua hamu yao kuu ni kutambua na kutenda mapenzi ya Baba yetu wa Mbinguni na Mwanawe Mpendwa. Ninaposhauriana pamoja, maongozi yamepokewa na maamuzi kufanywa ambayo yanaakisi kiwango cha nuru na ukweli unaoshinda uerevu, mawazo, na ujuzi wa binadamu. Tukifanya kazi pamoja katika shida kanganyishi uelewa wetu jumla wa jambo umeweza kupanuliwa katika njia za ajabu kwa uwezo wa Roho Mtakatifu.

Mimi nimebarikiwa kuona kila siku sifa binafsi, uwezo, na silka tukufu za hawa viongozi. Baadhi ya watu wanaona mapungufu ya kibinadamu ya Ndugu yanatatiza na kudidimiza imani. Kwangu mimi hayo mapungufu ni ya kuhimiza na kukuza imani.

Somo la Ziada

Mimi nimeshududia wasita wa Ndugu zangu wakipokea uhamisho kupitia kifo cha kimwili hata kwenye majukumu mapya katika ulimwengu wa kiroho. Rais James E. Faust, Rais Gordon B. Hinckley, Mzee Joseph B. Wirthlin, Mzee L. Tom Perry, Rais Boyd K. Packer, na Mzee Richard G. Scott.

Hawa Ndugu washupavu walijitolea ”nafsi zao zote” (Omni 1:26) kushuhudia jina la Yesu Kristo katika ulimwengu wote. Jumla ya mafundisho yao ni ya thamani mno.

Watumishi hawa wameshiriki nasi katika miaka yao ya kutimiza huduma zao mihutasari ya nguvu kiroho ya masomo waliyojifunza kupitia miongo ya huduma ya kujitolea. Viongozi hawa wamefunza kweli za thamani kubwa wakati ambapo baadhi waliamini kuwa walikuwa na kidogo cha kutoa.

Fikiria mafundisho ya mwisho ya manabii wakuu katika maandiko. Kwa mfano, Nefi alihitimisha kumbukumbu yake kwa maneno haya: ”Kwani Bwana ameniamuru hivi, na ni lazima nitii” (2 Nefi 33:15).

Karibu na mwisho wa maisha yake, Yakobo alionya:

”Tubuni nyinyi, na muingie katika mlango uliosonga, na mwendelee katika njia ambayo ni nyembamba, hadi mtakapopokea uzima wa milele.

”Ee pokeeni hekima; niseme nini zaidi? (Yakobo 6:11–12).

Moroni alikamilisha kazi yake ya kutayarisha mabamba kwa tumaini la matarajio ya Ufufuko: ”Hivi karibuni nitaenda kupumzika katika paradiso ya Mungu, mpaka roho yangu na mwili vitakapounganishwa tena, na niinuliwe juu kwa ushindi kupitia angani, kukutana na nyinyi mbele ya kiti cha enzi cha kupendeza cha yule Yehova mkuu, Mwamuzi wa Milele wa wanaoishi na waliokufa” (Moroni 10:34).

Ninyi pamoja nami tumebarikiwa kujifunza kutoka kwa mafundisho shuhuda za tamati za manabii na mitume wa siku za mwisho. Majina yao leo si Nefi, Yakobo, na Moroni—bali ni Rais Faust, Rais Hinckley, Mzee Wirthlin, Mzee Perry, Rais Packer na Mzee Scott.

Mimi kamwe sipendekezi kuwa ujumbe wa mwisho wa wanaume hawa wapendwa ndiyo unastahili ama ni muhimu katika huduma zao. Hata hivyo, jumlisho la kujifunza kiroho na uzoefu wao wa maisha uliwawezesha viongozi hawa kutilia mkazo kweli za milele kwa uhalisi kamili na uwezo mkubwa.

Picha
Rais James E. Faust

Katika hotuba yake ya mwisho ya mkutano mkuu katika wa mwezi Aprili 2007, Rais Faust alitamka:

”Mwokozi ametupa sote amani yenye thamani kupitia kwa Upatanisho Wake, lakini hii inaweza kuja tu tunapokuwa radhi kutupa nje hisia za hasira, dharau au kulipiza kisasi. …

”Acheni tukumbuke kwamba tunahitaji kusamehe ndipo tusamehewe. … Kwa moyo na nafsi yangu yote, mimi naamini katika nguvu za uponyaji ambao huja kwetu tunapofuata ushauri wa Mwokozi ’wasameheni watu wote’ [M&M 64:10]” (“The Healing Power of Forgiveness,” Liahona, May 2007, 69).

Ujumbe wa Rais Faust ni somo la nguvu sana la maisha yote kutoka kwa mtu niliyempenda na mmoja wa watu wenye kusamehe sana ambao nimejua.

Picha
Rais Gordon B. Hinckley

Rais Hinckley alishudia katika mkutano mkuu wake wa mwisho mnamo Oktoba ya 2007: “Mimi nathibitisha uhuhuda wangu juu ya wito wa Nabii Joseph, kazi yake, na kufunga kwa ushuhuda wake kwa damu yake kama mfiadini wa ukweli wa milele ... Ninyi pamoja nami tunakabiliwa na swali la wazi wazi juu ya kukubali ukweli wa Ono la Kwanza na yale yote yaliyofuata. Juu ya swala la uhalisia wake kuna uhalali hasa wa Kanisa hili. Kama ni ukweli, na mimi nashuhudia kwamba ni kweli, basi kazi ambayo tunajishughulisha nayo ndiyo kazi muhimu sana duniani” (“The Stone Cut Out of the Mountain,” Liahona, Nov.2007, 86).

Ushahidi wa Rais Hinckley huthibitisha somo lenye nguvu sana la maisha yote kutoka kwa mtu ninayempenda na kumjua kama nabii wa Mungu.

Picha
Mzee Joseph B. Wirthlin

Mzee Wirthlin alitoa ujumbe wake wa mwisho wa mkutano mkuu katika Oktoba ya 2008.

”Mimi bado nakumbuka ushauri wa [mama yangu] uliotolewa kwangu katika ile siku ya zamani sana wakati timu yangu ilipopoteza mechi ya mpira wa miguu wa marekani: ’Lolote liwalo, na ulipende.”

“… Dhiki, kama ikichukuliwa vyema, inaweza kuwa baraka katika maisha yetu. …

”Tunapotafuta furaha, tutafute mtazamo wa milele, tuelewe kanuni za malipo, na kujongea karibu na Baba yetu wa Mbinguni, tunaweza kuvumilia hali ngumu na majaribu. Tunaweza kusema, kama alivyosema mama yangu, ’Lolote liwalo, na ulipende.’”(“Come What May, and Love It,” Liahona, Nov. 2008, 28).

Ujumbe wa Mzee Wirthlin ni somo lenye nguvu sana la maisha yote kutoka kwa mtu niliyempenda na ambaye alikuwa ni mahubiri hai ya kushinda shida kupitia imani katika Mwokozi.

Picha
Mzee L. Tom Perry

Mzee Perry alisimama kwenye nimbari hii miezi sita iliyopita. Wakati huo, hatungeweza kudhania ushuhuda wake ungekuwa wake wa mwisho katika mkutano mkuu.

”Acheni nitamatishe kwa kutoa ushuhuda (na miongo yangu tisa kwenye hii dunia inaniwezesha kusema haya) kwamba ninapozeeka, ndivyo zaidi ninavyotambua kwamba familia ndiyo kitovu cha maisha na ndiyo funguo ya furaha ya milele.

”Mimi natoa shukrani zangu kwa mke wangu, na watoto wangu, wajukuu wangu na vituku vyangu, na kwa wote … na familia yote ambao mnayafanya maisha yangu kuwa mazuri sana na, ndio, hata milele. Juu ya ukweli huu wa milele natoa ushuhuda wangu wa nguvu na mtakatifu” (“Why Family and Marriage Matter—Everywhere in the World,” Liahona, May 2015, 42).

Ujumbe wa Mzee Perry ni somo lenye nguvu la maisha yote kutoka kwa mtu ninayempenda na ambaye alielewa kupitia uzoefu mwingi wa uhusiano ufaao kati ya familia na furaha ya milele.

Picha
Rais Boyd K. Packer

Rais Packer alisisitiza katika mkutano mkuu miezi sita iliyopita mpango wa furaha wa Baba, Upatanisho wa Mwokozi, na familia za milele:

”Mimi natoa ushuhuda kwamba Yesu ndiye Kristo na Mwana wa Mungu aliye hai. Anasimama kwenye kichwa cha Kanisa hili. Kupitia Upatanisho Wake na nguvu za ukuhani, familia ambazo zilianza katika dunia ya mauti zinaweza kuwa pamoja milele yote. …

”Mimi nina shukrani kwa … Upatanisho ambao unaweza kuosha kabisa kila doa bila kujali jinsi lilivyosugu ama jinsi limekaa ama mara ngapi limejirudia. Upatanisho unaweza kuwafanya huru tena kusonga mbele, tukiwa wasafi na wastahili” (“The Plan of Happiness,” Liahona, May 2015, 28).

Ujumbe wa Rais Packer wa mwisho ni somo la maisha yote kutoka kwa mtu ninayempenda na ambaye kwa dhati na kwa kurudia alitangaza kwamba madhumuni ”shughuli zote katika Kanisa ni kuona kwamba mwanamume na mwanamke pamoja na watoto wao wana furaha, kufunganishwa pamoja kwa wakati na milele yote” (Liahona, May 2015, 26).

Picha
Mzee Richard G. Scott

Mzee Scott alitangaza katika mkutano mkuu wake wa mwisho mnamo Oktoba 2014: “Tulikuja katika maisha haya haswa kukua kutokana na majaribu. Changamoto zinatusaidia kuwa zaidi kama Baba yetu wa Mbinguni, na Upatanisho wa Yesu Kristo unawezesha kuvumilia changamoto hizo. Nashuhudia kwamba tunapokuja Kwake kikamilifu, tunaweza kuvumilia kila jaribio, kila wasiwasi, kila Changamoto tunayopitia” (“Make the Exercise of Faith Your First Priority,” Liahona, Nov. 2014, 94).

Ujumbe wa Mzee Scott ni somo lenye nguvu la maisha kutoka kwa mtu ninayempenda na shahidi maalum mpendwa wa jina la Kristo katika ulimwengu wote (ona M&M 107:23).

Ahadi na Ushuhuda

”Iwe kwa sauti yangu mwenyewe au kwa sauti ya watumishi wangu, yote ni sawa” (M&M 1:38). Na tusikie na kutii kweli za milele zinazofunzwa na wawakilishi wa Bwana walioidhinishwa. Tunapofanya hivyo, mimi naahidi imani yetu katika Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo itaimarishwa, na tutapokea mwongozo wa kiroho na ulinzi kwa hali yetu maalum na haja.

Mimi kwa nguvu zote za nafsi yangu nashuhudia Kristo aliyefufuka na anayeishi anaelekeza shughuli za Kanisa Lake la urejesho na lililohai kupitia watumishi Wake ambao amewachagua kutoa ushuhuda juu ya jina Lake. Nashuhudia hivi, katika jina takatifu la Yesu Kristo, amina.