2010–2019
Ninashangaa Sana
Oktoba 2015


Ninashangaa Sana

Ushuhuda wangu wa Yesu Kristo umejengwa kutoka uzoefu mwingi maalumu ambao  umeniwezesha kujua upendo Wake mkuu kwa kila mmoja wetu.

Wapendwa ndugu na dada zangu ulimwenguni kote, nina shukrani kubwa kwa Urais wa Kwanza kwa kunialika kushiriki ushuhuda wangu kwa unyenyekevu siku hii ya Sabato. Maneno ya wimbo niupendao wa Watakatifu wa Siku za Mwisho yanaelezea hisia nilizonazo:

Nashangaa sana ninavyopendwa na Yesu,

Nashangazwa na neema ambazo anipa kikamilifu …

Nastajabia kwamba angeweza kushuka kutoka kwenye kiti cha uungu.

Kuokoa nafsi asi sana na yenye kiburi kama yangu

Kwamba angeonyesha upendo Wake mkubwa kwa mtu kama mimi,  ...

Vya kutosha kuwa Bwana, kukomboa, na kutetea  

Ee, Inashangaza, inashangaza kwangu!1

Siku chache zilizopita nilipata fursa nzuri kukutana na Urais wa Kwanza na kupokea wito huu kutoka kwa nabii wetu mpendwa, Rais Thomas S. Monson. Nataka kutoa ushahidi kwenu nyote wa uwezo na upendo Rais Monson aliokuwa nao wakati aliponiambia, ”Wito huu unatoka kwa Bwana Yesu Kristo.”

Nimezidiwa na kutetemeka hadi ndani ya kiini cha moyo wangu kufikiria maana na umuhimu wa maneno hayo yaliyosemwa kwa upole na nabii wetu mwenye upendo Rais Monson, Rais Eyring, Rais Uchtdorf, nawapenda na nitamhudumia Bwana na nyinyi kwa moyo wangu wote, uwezo, akili, na nguvu zangu.

Ee, jinsi gani nilivyowapenda Rais Boyd K. Packer na Wazee L. Tom Perry na Richard G.Scott. Ninawakosa sana. Nimebarikiwa kuelekezwa na kufundishwa miguuni mwa hawa ndugu wapendwa. Siwezi kutembea hata kwa sehemu ndogo katika viatu vyao, hata hivyo nimeheshimiwa kusimama wima kwenye mabega yao na kuendelea katika huduma ya Bwana.

Ninapowakumbuka wale waliosaidia kunifanya mimi niwe kama nilivyo, namkumbuka kwanza kipenzi changu na asiye na makuu, mwenza wa milele, Melanie. Miaka yote, amesaidia kuniumba kama udongo wa mfinyazi, kunikwatua zaidi na kuwa mtume wa Yesu kristo. Upendo wake na msaada, na ule wa watoto wetu 5 waume na wake zao, na wajukuu wetu 24, wananiidhinisha. Kwa familia yangu kipenzi, ninawapenda.

Kama Nefi wa zamani, nilizaliwa na wazazi wema katika injili na wao na wazazi wema vizazi sita nyuma. Mababu zangu wa mwanzo waliojiunga na Kanisa walitokea Uingereza na Denmaki. Watangulizi hawa wa mwanzo walitoa vyote walivyokuwa navyo kwa injili ya Yesu Kristo na kuwaachia uridhi vizazi vyao vya baadae kufuata. Nina shukurani kubwa kwa vizazi vingi vya familia za Watakatifu wa Siku za Mwisho, na ninajua hili ni lengo linalostahili kwa sisi wote kujitahidi kuwa nalo.

Wengi wengine wamechangia kutayarisha maisha yangu kwa wito huu mpya. Inajumuisha marafiki zangu wa utotoni na familia, viongozi wa mwanzo, waalimu, na wanasihi wangu maishani. Sina budi kuwajumuisha wale kutoka misheni yangu ya mwanzo kwenye majimbo ya mashariki na wapendwa wamisionari kutoka Misheni ya New York North. Kwa wengi walioathiri na kurekebisha maisha yangu, Nashukuru sana.

Nimestahi kwa upendo mkubwa kuhudumia na ndugu zangu wa Sabini. Kwa miaka 15 nimekuwa katika moja wapo ya akidi kubwa sana na udugu katika Kanisa Asanteni sana, wapendwa watumishi wenzangu. Sasa naangalia mbele kuwa kwenye akidi mpya. Rais Russell M. Nelson, upendo wangu ni mkubwa kwako na kila mmoja wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili.

Dada Rasband nami tumebarikiwa kuwatembelea waumini wakati  wa kupangiwa katika mikusanyiko ya waumini na misheni ulimwenguni kote. Tunawapenda Watakatifu wa Siku za Mwisho kila mahali! Imani zenu zimeongeza imani zetu; shuhuda zenu zimeongeza ushuhuda wetu.

Sasa, kama ningeweza kuwaachieni ujumbe mmoja mdogo leo ungekuwa huu: Bwana amesema, ”Mpendane; kama nilivyowapenda nyinyi.”2 Nina hakika kwamba hakuna chaguo, dhambi, au makosa ambayo wewe au yoyote yule anaweza kufanya ambayo yanaweza kubadili upendo Wake kwenu au kwao. Hiyo haimaanishi anasamehe au kipuuza tabia za dhambi—Nina hakika hafanyi hivyo—lakini inamaanisha tuwafikie binadamu wenzetu kwa upendo kuwaalika, kushawishi, kuhudumu, na kuokoa. Yesu Kristo aliangalia zaidi ya ukabila wa watu, cheo, na hali ya mambo ili aweze kuwafundisha kwa undani ukweli huu

Nimeulizwa mara nyingi wakati gani nilipokea ushuhuda wangu.

Sikumbuki kutoamini katika Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo. Nimewapenda tangu nilipojifunza kuwahusu kwenye magoti ya malaika mama yangu, nikisoma maandiko na hadithi za injili. Imani ile ya mwanzo sasa imekua na kuwa uelewa na ushahidi wa Baba wa Mbinguni mwenye upendo, anaye sikiliza na kujibu maombi yetu. Ushuhuda wangu wa Yesu Kristo umejengwa kutoka uzoefu mwingi maalumu ambao  umeniwezesha kujua upendo Wake mkuu kwa kila mmoja wetu.

Nina shukrani kwa Upatanisho wa Mwokozi wetu na matamanio kama Alma kupiga yowe kwa parapanda ya Mungu.3 Najua kwamba Joseph Smith ni nabii wa Mungu wa urejesho na kwamba Kitabu cha Mormoni ni neno la Mungu. Na ninajua kwamba Rais Thomas S. Monson ni mtumishi wa kweli wa Mungu na nabii duniani leo.

Na tunapomfuata nabii wetu, naomba kwamba tuweze kuwa na upendo katika mioyo yetu kwa wengine na kwamba tutaweza kuwa mashahidi hai na hakika ”kushangaa sana tunavyopendwa na Yesu” Ee, iweze kuwa ”ajabu, ajabu kwenu [Nyinyi na mimi].” Katika jina la Yesu Kristo, amina.