2010–2019
Acha ya Baragumu Ilie
Oktoba 2015


Acha ya Baragumu Ilie

Ulimwengu unahitaji wafuasi wa Kristo ambao wanaweza kuwasilisha ujumbe wa injili kwa uwazi na kutoka moyoni.

Msimu huu wa joto uliopita mke wangu na mimi tulikaa pamoja na wajukuu wetu wawili wadogo, wakati wazazi wao walikuwa wakishiriki katika shughuli za matembezi za watangulizi pamoja na kata yao. Binti yetu alitaka kuhakikisha kwamba wavulana walijifunza piano wakiwa mbali na nyumbani. Alijua kwamba siku chache kwa mababu huifanya kuwa rahisi kidogo kusahau kufanya mazoezi. Mchana moja niliamua kukaa na mjukuu wangu mwenye umri wa miaka 13, Andrea, na kumsikiliza akicheza.

Mvulana huyu amejawa na nguvu na anapenda mambo ya nje. Kwa urahisi angetumia muda wake wote akiwinda na akivua. Wakati akijifunza piano, ningeona kwamba afadhali angekuwa akivua katika mto jirani. Nilisikiliza wakati akicheza kila toni la wimbo unaojulikana. Kila noti alioicheza ilikuwa na mkazo na sauti sawa, hivyo kuifanya kuwa vigumu kutambua tuni vizuri. Niliketi kwenye benchi karibu naye na kumweleza umuhimu wa kubofya vibao vya tuni kwa nguvu na kubofya kwa upole zile noti zinazofuatana na tuni. Tuliongea juu ya piano kuwa ni zaidi ya mtambo wa kimiujiza. Inaweza kuwa ni upanuzi wa sauti yake mwenyewe na hisia na kuwa chombo ajabu cha mawasiliano. Kama vile mtu anavyoongea kusonga vizuri kutoka neno moja hadi nyingine, hivyo ndivyo tuni inayopaswa kulainika kutoka noti moja hadi nyingine.

Tulicheka pamoja alivyojaribu tena na tena. Tabasamu lake la kubonyea liliongezeka wakati tuni yakufahamika ilipoanza kusikika tofauti na zile seti za sauti zisizolainika. Ujumbe ukawa wazi: “Mimi ni mtoto wa Mungu, naye ndiye aliyenituma hapa.”1 Nilimuuliza Andrew kama angeweza kuhisi tofauti katika ujumbe huo. Alijibu, “Ndiyo, babu, naweza kuihisi!”

Mtume Paulo anatufundisha kuhusu kulinganisha mawasiliano na vyombo vya muziki alipoandika kwa Wakorintho:

“Hata vitu visivyo na uhai vitoapo sauti, ikiwa ni filimbi, ikiwa ni kinubi, visipotoa sauti zilizo na tofauti, itatambulikanaje ni wimbo gani unaopigwa kwa filimbi au kwa kinubi?

“Kwa maana baragumu ikitoa sauti isiyojulikana, ni nani atakayejifanya tayari kwa vita?”2

Kama kuna wakati ambapo ulimwengu unahitaji wanafunzi wa Kristo ambao wanaweza kuwasilisha ujumbe wa injili kwa uwazi na kwa moyo, ni sasa. Tunahitaji mwito wazi wa baragumu.

Hakika Kristo alikuwa ndiye mfano wetu bora. Daima alionyesha ujasiri wa kutetea mambo ya ukweli. Maneno yake yanapiga mwangwi katika karne zote anapotualika kukumbuka kumpenda Mungu na wanadamu wenzetu, kushika amri zote za Mungu na kuishi kama nuru ya ulimwengu. Hakuwa na hofu ya kuzungumza juu ya wakuu wa dunia au watawala wa siku Zake, hata wakati hao waliokuwa wakipinga ujumbe wake aliopewa na Baba. Maneno yake hayakubuniwa kuwachanganya bali kuivutia mioyo ya watu. Hakika alijua mapenzi ya Baba yake katika yote aliyosema na kufanya.

Mimi pia naupenda mfano wa Petro, aliyekabiliana na watu wa dunia kwa ujasiri na uwazi katika siku ya Pentekoste. Siku hiyo watu walikuwa wamekusanyika kutoka nchi nyingi wakiwakosoa Watakatifu wa zamani kwa sababu waliwasikia wakiongea kwa lugha mbalimbali na walidhani walikuwa walevi. Petro akiwa amepandwa na Roho nafsini mwake, alisimama ili kutetea Kanisa na waumini. Alishuhudia kwa maneno haya: “Enyi watu wa Uyahudi, na ninyi nyote mkaao Yerusalemu, lijueni jambo hili, mkasikilize maneno yangu.”3

Kisha alinukuu kutoka katika maandiko yenye unabii wa Kristo na akatoa ushuhuda huu wa moja kwa moja: “Basi nyumba yote ya Israeli na wajue yakini ya kwamba Mungu amemfanya Yesu huyo mliyemsulibisha kuwa Bwana na Kristo.”4

Wengi walisikia maneno yake, walihisi Roho, na nafsi 3,000 wakawa waumini wa Kanisa la mapema. Huu ni ushahidi wenye nguvu kwamba mwanamume au mwanamke mmoja, ambaye yuko tayari kushuhudia wakati ulimwengu unaonekana kuelekea kinyume, anaweza kuleta tofauti.

Wakati sisi kama waumini tunafanya uamuzi wa kusimama kidete na kushuhudia kwa nguvu mafundisho ya Mungu na Kanisa Lake, kitu hubadilika ndani yetu. Tunachukua mfano Wake kwenye nyuso zetu. Tunakuwa karibu na Roho Wake. Yeye kisha atakwenda mbele yetu na kuwa katika “mkono [wetu] wa kuume na wa kushoto, na Roho [Wake] atakuwa katika mioyo [yetu], na malaika [Wake] atatuzingira ili kutubeba juu.”5

Wanafunzi wa kweli wa Kristo hawatafuti kuweka visingizio kwa mafundisho, wakati hayalingani na dhana ya kisasa duniani. Paulo alikuwa mwanafunzi mwingine mwema aliyetangaza kwa ujasiri kwamba “Kwa maana siionei haya Injili; kwa sababu ni uweza wa Mungu uuletao wokovu, kwa kila aaminiye.”6 Wanafunzi wa Kweli wanamwakilisha Bwana wakati unaoonekana kuwa sio rahisi kufanya hivyo. Wanafunzi wa kweli wana hamu ya kuhamasisha mioyo ya watu, sio kuwavutia.

Mara nyingi si rahisi wala hamna maliwazo kumtetea Kristo. Nina hakika hivyo ndivyo ilivyokuwa na Paulo alipoitwa mbele ya Mfalme Agripa na kuulizwa kujitetea na kuelezea hadithi yake. Paulo, bila kusita, alitangaza imani yake kwa nguvu kiasi kwamba huyu mfalme mwenye vitisho alikiri kwamba alikuwa ‘karibu’ kushawishika kuwa Mkristo.

Majibu ya Paulo yalidhihirisha nia yake kwa watu kuelewa kabisa kile ambacho angesema. Alimwambia Mfalme Agripa kwamba ilikuwa nia yake kuwa wote waliomsikiza si lazima “wote” wawe Wakristo, badala yake wote watakuwa wanafunzi wa Kristo.7 Wale wanaozungumza kwa uwazi wanaweza kutimiza haya.

Katika miaka mingi ambapo nimesoma hadithi za ndoto za Lehi katika Kitabu cha Mormoni,8 Nimefikiria kila mara juu ya jengo kubwa na pana kama mahali ambapo wale watu waasi tu huishi. Jengo lilikuwa limejaa watu, wenye tabia ya kufanya mzaha na kuwaonyesha kwa vidole vyao wale ambao walikuwa wameshikilia ile fimbo ya chuma, ishara ya neno la Mungu, na walikuwa wakielekea kwenye mti wa uzima, ishara ya upendo wa Mungu. Wengine walishindwa na shinikizo la watu ambao walikuwa wakiwakejeli na wakaondoka. Wengine waliamua kujiunga nao katika jengo hilo. Je, hawakuwa na ujasiri wa kuongea kwa ujasiri dhidi shutuma au ujumbe wa dunia?

Ninapoutazama ulimwengu wa sasa ukisogea mbali na Mungu, nadhani jengo hili linakua kwa ukubwa. Wengi wanajikuta wakitembea katika kumbi za jengo kubwa na pana bila kujua wanakuwa sehemu ya utamaduni wake. Mara nyingi wamejiingiza katika majaribu na ujumbe wake. Hatimaye wanajikuta wakifanya mizaha au kujiunga na wale wanaokosoa au kufanya mzaha.

Kwa miaka mingi nilidhani umati wa mzaha ulikuwa ukidhihaki jinsi waaminifu walivyokuwa wakiishi maisha yao, lakini sauti kutoka jengo la leo zimebadilika katika sauti zao na mbinu. Wale wanaofanya mzaha hujaribu kila wakati kupambana na ujumbe rahisi wa injili kwa kushambulia baadhi ya nyanja za historia ya Kanisa au kutoa shutuma kali kwa nabii au kiongozi mwingine. Pia wanashambulia msingi wa mafundisho yetu na sheria za Mungu, zilizotolewa tangu Uumbaji wa dunia. Sisi, kama wanafunzi wa Yesu Kristo na waumini wa Kanisa Lake, kamwe tusiache ile fimbo ya chuma. Ni lazima tuache sauti ya baragumu ilie kutoka katika roho zetu.

Ujumbe rahisi ni kwamba Mungu ni Baba yetu wa Mbinguni mwenye upendo na Yesu Kristo ni Mwana Wake. Injili imerejeshwa katika siku hizi za mwisho kupitia kwa manabii hai na ushahidi ni Kitabu cha Mormoni. Njia ya furaha ni kupitia katika taasisi ya msingi ya familia kama ilivyopangwa awali na kufunuliwa na Baba yetu wa Mbinguni. Hii ndio tuni ijulikanayo ya ujumbe ambao wengi wanaweza kutambua, kwa sababu wameisikia tangu katika maisha yao kabla ya kuzaliwa.

Kama Watakatifu wa siku za mwisho, ni wakati wetu kusimama imara na kushuhudia. Ni wakati wa noti za tuni za injili kuinuka kuliko kelele za dunia. Naongezea ushuhuda wangu kwa ujumbe wa Mwokozi na Mkombozi wa ulimwengu. Yeye yu hai! Injili yake imerejeshwa na baraka za furaha na amani zinaweza kupatikana katika maisha haya kwa kuishi amri Zake na kutembea katika njia Zake. Huu ni ushuhuda wangu katika jina la Yesu Kristo, amina.