2010–2019
Roho Mtakatifu Kama Mwenza Wako
Oktoba 2015


Roho Mtakatifu Kama Mwenza Wako

Sisi tunaweza, kama tutaishi kuistahili, kuwa na baraka za Roho kuwa pamoja nasi, siyo tu sasa bali daima.

Ndugu na dada zangu wapendwa, nashukuru kuwa nanyi siku hii ya Sabato katika katika ukumbi wa Mikutano wa Kanisa la Bwana. Nimehisi, kama mlivyohisi, Roho, Roho Mtakatifu akinishuhudia ukweli wa maneno ambayo tumesikia yakiongea na kuaimbwa.

Lengo langu leo hii ni kuwaongezea matamanio na uamuzi kudai zawadi iliyoahidiwa kwa kila mmoja wetu tulipobatizwa. Wakati wa kuthibitishwa kwetu tulisikia maneno haya: “Pokea Roho Mtakatifu.”1 Kutoka wakati huo, maisha yetu yalibadilika milele.

Sisi tunaweza, kama tutaishi kuistahili, kuwa na baraka za Roho kuwa pamoja nasi, siyo tu sasa na wakati huo, na kama ilivyo uzoefu wa ajabu kama tulionao leo, bali daima. Unajua kutoka katika maneno ya sala ya sakrament jinsi gani ahadi hiyo inavyotimizwa: Ee Mungu, Baba wa Milele, tunakuomba katika jina la Mwanao, Yesu Kristo, ubariki na utakase mkate huu kwa roho za wale wote watakaoula, ili waweze kuula kwa ukumbusho wa mwili wa Mwanao, na wakushuhudie, Ee Mungu, Baba wa Milele, kwamba wako radhi kujichukulia juu yao jina la Mwanao, na daima kumkumbuka, na kushika amri zake ambazo amewapa.”

Baadaye inakuja ahadi: Ili daima Roho wake apate kuwa pamoja nao” (M&M 20:77; mkazo umeongezewa).

Kuwa na Roho pamoja nasi daima ni kuwa na mwongozo na maelekezo kutoka kwa Roho Mtakatifu katika maisha yetu ya kila siku. Tunaweza, kwa mfano, kupewa onyo na Roho kujizuia na majaribu ya kufanya maovu.

Kwa sababu hiyo peke yake, ni rahisi kuona kwa nini watumishi wa Bwana wamejaribu kuongeza matamanio yetu kumwabudu Mungu katika mikutano ya sakramenti. Kama tutapokea sakramenti katika imani, Roho Mtakatifu ataweza tena kutulinda na wale tuwapendao kutoka katika majaribu yanayokuja katika mzunguko mkali na unaoongezeka.

Uenzi wa Roho Mtakatifu unakifanya kile kilicho bora kuwa cha kuvutia zaidi na majaribu kuwa na mvuto mdogo. Hilo pekee inatosha kutufanya kujitahidi kuhitimu kwa Roho kuwa pamoja nasi wakati wote.

Kama vile Roho Mtakatifu anavyotupa nguvu dhidi ya uovu, Vile vile Yeye anatupa nguvu ya kutambua kati ya ukweli na uongo. Ukweli uliona maana sana unadhihirishwa tu kwenye ufunuo kutoka kwa Mungu. Sababu zetu za kibinadamu na utumiaji wetu wa fikra za kimwili haitatosha. Tunaishi kwenye nyakati ambazo hata wenye hekima wanapata shida kutofautisha ukweli kutoka kwa ulaghai wa ujanja.

Bwana alifundisha Nabii Wake Tomaso, ambaye alitaka udhibitisho halisi wa ufufuko wa Mwokozi kwa kugusa kovu Lake, ufunuo huo ni ushahidi salama: “Yesu akamwambia, Tomaso, kwa kuwa umeniona, umesadiki; wa heri wale wasioona, wakasadiki” (Yohana 20:29).

Ukweli ambao unaoonyesha njia nyumbani kwa Mungu unadhihirishwa na Roho Mtakatifu. Hatuwezi kwenda msituni na kuona Baba na Mwana wanaongea na kijana Joseph Smith. Hakuna ushahidi wa kimwili au hoja yenye mantiki inaweza kuelezea kwamba Eliya alikuja kama ilivyoahidiwa kutoa funguo za ukuhani ambazo sasa zinashikiliwa na kutumika na nabii anayeishi Thomas  S. Monson.

Uthibitisho wa ukweli huja kwa mtoto wa Mungu ambaye amedai haki ya kupokea Roho Mtakatifu. Kwa sababu ulaghai na uongo unaweza kuletwa kwetu saa yoyote, tunahitaji ushawishi endelevu wa Roho wa Kweli ili tusiwe na nyakati za shaka.

Wakati akiwa mshiriki wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili, George  Q. Cannon aliomba kwamba tufanye juhudi za kila mara ili Roho aweze kuwa nasi. Aliahidi, na mimi naahidi vivyo hivyo, kwamba kama tutajitahidi kutafuta njia hiyo, hatutapungukiwa na uelewa wa ukweli, “hatutakuwa kwenye wasiwasi au kwenye kiza,” na “imani yetu itakuwa imara, na kujawa na furaha  … tele.”2

Tunahitaji msaada huo endelevu kutoka kwenye urafiki na Roho Mtakatifu kwa sababu nyingine pia. Kifo cha mpendwa wetu kinaweza kuja bila kutegemewa. Ni ushahidi kutoka kwa Roho Mtakatifu wa uhalisi wa Baba wa Mbinguni mwenye upendo na Mwokozi aliyefufuka unaotupa tumaini na faraja tunapompoteza mpendwa wetu. Ushuhuda huo lazima uwe hai wakati kifo kinatokea.

Hivyo, kwa sababu nyingi, tunahitaji uenzi endelevu wa Roho Mtakatifu. Tunautamani, lakini bado tunajua kutokana na uzoefu kwamba si rahisi kudumisha. Wote tunafikiria, na kusema, na kufanya vitu katika maisha yetu ya kila siku ambavyo vinaweza kumhudhi Roho. Bwana alitufundisha kwamba Roho Mtakatifu atakuwa mwenza wa daima wakati mioyo yetu inakuwa imejazwa na hisani “wema huyapamba mawazo yako bila kukoma” (ona M&M 121:45).

Kwa wale wanaopata shida na kiwango cha juu wanahitaji kustahili uenzi wa Roho, ninatoa hamasa hii. Umekuwa na nyakati ambapo umehisi ushawishi wa Roho Mtakatifu. Inaweza kuwa imekutokea leo.

Unaweza kufikiria nyakati hizo za maongozi kama mbegu ya imani ambayo Alma aliielezea (ona Alma 32:28). Pandeni kila mmoja. Unaweza kufanya hivyo kwa kufanyia kazi hisia ulizozipata. Maongozi ya thamani sana yatakuwa ni kujua kile Mungu angependa ufanye, Kama ilikuwa ni  kulipa zaka, au kumtembelea rafiki anayeomboleza, fanya hivyo. Chochote kile, kifanye. Unapoonyesha  hamu ya kutii, Roho itakutumia hisia ambazo Mungu angetaka ufanye kwa niaba Yake.

Unapotii, hisia kutoka kwa Roho zitakuja kila mara, zikiwa karibu na karibu na uenzi wa daima. Nguvu yako ya kuchagua kilicho sahihi itaongezeka.

Unaweza kujua wakati hisia hizo za kutenda zinatoka kwenye Roho zaidi ya kwa hamu zako mwenyewe. Wakati hisia zinapokuwa kwenye maelewano na kile ambacho Mwokozi na Manabii wake wanaoishi na mitume wamekisema, unaweza kuchagua kutii kwa ujasiri. Baada ya hapo Bwana atakutumia Roho Wake kukusaidia.

Kwa mfano, kama ukipokea hisia za kiroho kuitii siku ya Sabato, hasa inapoonekana kuwa ngumu, Mungu atakutumia Roho Wake kukusaidia.

Msaada huo ulikuja kwa baba yangu miaka mingi iliyopita wakati kazi yake ilimpeleka Australia. Alikuwa peke yake Jumapili, na alitaka kushiriki sakramenti. Hakupata taarifa yeyote ile kuhusu Mikutano ya Watakatifu wa Siku za Mwisho. Hivyo basi alianza kutembea. Alisali katika kila makutano kujua ni njia gani ya kupitia. Baada ya kutembea na kugeuka kwa masaa kadhaa, alisimama kusali tena. Alipata hisia ya kukata kona kwenye mtaa mmoja. Ghafla alianza kusikia nyimbo zikitokea kwenye ghorofa ya chini ya nyumba karibu naye. Alichungulia kwenye dirisha na kuona watu wachache wamekaa karibu na meza ilivyofunikwa na kitambaa cheupe na sahani ya sakramenti.

Sasa, inaweza isiwe kuu jinsi kwako, lakini ilikuwa ni kitu kikubwa kwake. Alijua ahadi ya sala ya sakramenti ilikuwa imetimizwa: “Daima kumkumbuka na kushika amri Zake ambazo amewapa, ili daima Roho Wake apate kuwa pamoja pamoja nao” (M&M 20:77).

Huo ulikuwa ni mfano mmoja tu wakati aliposali na baadaye kufanya kile ambacho Roho ilimwambia Mungu alimtaka akifanye. Aliendelea kufanya hivyo kwa miaka mingi, kama wewe na mimi tutakavyofanya. Hakuzungumzia kamwe kuhusu hali yake ya kiroho. Aliendelea kufanya mambo madogo kwa ajili ya Bwana ambayo alikuwa ameongozwa kufanya.

Kila mara kundi la Watakatifu wa Siku za Mwisho walipomwomba kuzungumza nao, alifanya hivyo. Haikujalisha kama walikuwa watu 10 au 50 na amechoka kiasi gani. Alitoa ushuhuda wake wa Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu, na wa manabii popote Roho ilipomwelekeza kufanya hivyo.

Mwito wake wa juu katika Kanisa ulikuwa ni kwenye baraza kuu la Kigingi cha Bonneville, ambako alipalilia magugu katika shamba la kigingi, na alifundisha darasa la Shule ya Jumapili. Kwa miaka kadhaa, alipohitaji, Roho Mtakatifu alikuwepo kama mwenzi wake.

Nilisimama karibu na baba yangu kwenye chumba cha hospitali. Mama yangu, mke wake wa miaka 41, alilala kitandani. Tulikuwa tunamwangalia kwa masaa mengi. Tulianza kuona mistari ya uchungu ikipotea kutoka kwenye uso wake. Kwenye vidole vya mikono yake, ambavyo vilikuwa vimejikunja ngumi, na kulegea. Mikono yake ikatulia kwenye pande zake.

Maumivu ya miaka mingi ya saratani yalikuwa yanaisha. Niliona katika uso wake mwonekano wa amani. Alivuta pumzi fupi fupi chache, na pumzi ya mwisho, kisha akalala kimya. Tulikaa pale kuona kama pumzi nyingine ingetoka.

Mwishowe, Baba alisema kimya kimya, “Msichana amerudi nyumbani.”

Hakutokwa na chozi. Hii ni kwa sababu Roho Mtakatifu alikuwa kwa kitambo amempa picha kamili ya yeye ni nani, ametokea wapi, amekuwa nani, na alikuwa anaenda wapi. Roho ilikuwa imeshuhudia kwake mara nyingi juu ya upendo wa Baba wa Mbinguni, ya Mwokozi ambaye alivunja nguvu za kifo, na ya uhalisia wa kuunganishwa kwake hekaluni kati ya mke na familia yake.

Roho ilikuwa imempa uhakika mapema kwamba uzuri na imani yake ili imemhitimisha kurudi kwenye nyumba ya mbinguni ambapo angekumbukwa kama mtoto mzuri na kukaribishwa kwa heshima.

Kwa baba yangu, hiyo ilikuwa ni zaidi ya tumaini. Roho Mtakatifu iliifanya kuwa halisi kwake.

Sasa baadhi wanaweza kusema kwamba maneno yake na picha kwenye akili yake kuhusu nyumba ya mbinguni ilikuwa tamanio la kufikirika, wingu la hukumu la mume wakati wa msiba huu. Lakini alijua ukweli wa milele njia pekee unavyoweza kuujua.

Alikuwa ni mwanasayansi aliyetafuta ukweli kuhusu dunia hii katika maisha yake yote ya utu uzima wote. Alitumia vifaa vya kisayansi vya kutosha kupewa heshima na wenzake duniani kote. Mengi kati ya yale aliyoyafanya katika Kemia ilitoka kuwekea picha ya molekuli zikizunguka na baadaye kudhibitisha kwa majaribio katika maabara.

Lakini alikuwa amefuata njia tofauti kugundua ukweli ambao ulikuwa wa msingi zaidi kwake na kwa kila mmoja wetu. Ni kwa kupitia tu kwa Roho Mtakatifu tunaweza kuona watu na matukio kama Mungu anavyoyaona.

Zawadi hiyo iliendelea hospitalini baada ya kifo cha mke wake. Tulikusanya vitu vya mama yangu kuvipeleka nyumbani. Baba alisamama ili kumshukuru kila nesi na daktari tuliyekutana naye tukiwa njiani kuelekea kwenye gari. Nilikumbuka kwamba nilihisi kwamba tuondoke na majonzi yetu peke yetu.

Sasa natambua kwamba aliona vitu ambavyo Roho Mtakatifu angemwonyesha. Aliwaona watu hao kama malaika walitumwa kutoka kwa Mungu kumwangalia mpendwa wake. Wangeweza kuwa wamejiona wenyewe kama wataaalamu wa afya, lakini Baba alikuwa anawashukuru kwa niaba ya Mwokozi.

Ushawishi wa Roho Mtakatifu uliendelea naye mpaka tulivyofika kwenye nyumba ya wazazi wangu. Tuliongea kwa muda kidogo sebuleni. Baba aliomba kutoka kwenda chumba kulala kilicho karibu.

Baada ya dakika chache, aliingia tena sebuleni. Alikuwa na tabasamu nzuri. Alitukaribia na kutuambia kwa kunong’ona, “Nilikuwa na wasiwasi kwamba Mildred angewasili kwenye dunia ya kiroho peke yake. Nilihisi kuwa angehisi kupotea kwenye kundi la watu.”

Baadaye akasema kwa furaha, “Nimesali saa hivi. Ninajua Mildred yuko sawa. Mama yangu alikuwepo kukutana naye.”

Ninakumbuka kutabasamu alivyosema hivyo, nikimfikiria bibi yangu, miguu yake mifupi inayokimbia, ikiharakisha kupita kwenye umati wa watu kuwa na uhakika alikuwepo kukutana naye na kumkumbatia mkwe wake alipowasili.

Sasa, moja ya sababu baba yangu aliomba na kupokea faraja hiyo ni kwa sababu alikuwa akiomba kwa imani mara zote toka utotoni. Alikuwa amezoea kupata majibu kwenye maswali yaliyokuja kutoka kwenye moyo wake na kumfariji na kumpa mwelekeo. Cha kuongezea katika kuwa na tabia ya kusali, alijua maandiko na maneno ya manabii wanaoishi. Hivyo aligundua mnong’ono anaoufahamu wa Roho, ambao mnaweza kuwa mmeusikia leo.

Uenzi wa Roho ulikuwa na zaidi ya kumfariji na kumwongoza. Unaweza kumbadilisha kupitia Upatanisho wa Yesu Kristo. Tunapokubali ahadi hiyo ya kuwa na Roho pamoja nasi, Mwokozi anaweza kutupa utakaso unaohitajika kwa ajili ya maisha ya milele, moja kati ya zawadi kubwa (ona M&M 14:7).

Unakumbuka maneno ya Mwokozi: “Sasa hii ndio amri: Tubuni nyinyi nyote katika sehemu zote za dunia, na mje kwangu na mbatizwe katika jina langu kwamba muweze kutakaswa kwa kupokea Roho Mtakatifu, ili msimame mbele yangu bila mawaa katika siku ya mwisho. (3 Nephi 27:20).

Amri hizo zinakuja na ahadi hii kutoka kwa Bwana:

“Na sasa amini, amini, ninakuambia wewe, weka imani yako katika Roho yule ambaye huongoza kufanya mema—ndio kufanya haki, kutembea kwa unyenyekevu, kuhukumu kwa haki; na huyu ndio Roho wangu.

“Amini, Amini, ninakuambia nitakupa Roho wangu, ambaye ataiangaza akili yako katika Imani ukiamini katika mimi kwamba utapokea” (M&M 11:12–13).

Ninashuhudia kwamba Mungu Baba yu hai, kwamba Yesu Kristo aliyefufuka analiongoza Kanisa Lake, kwamba Thomas  S. Monson ana funguo zote za ukuhani, na kwamba ufunuo kupitia Roho Mtakatifu unaongoza na kuhimili Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho, na waumini wake wanyenyekevu.

Nashuhudia zaidi kwenu kwamba hawa wanaume wa ajabu ambao mmewaona wakiongea nasi kama mashahidi wa Bwana Yesu Kristo, kama washiriki wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili, wameitwa na Mungu. Mimi najua kwamba Roho amemwelekeza Rais Monson kuwaiita. Na mlipowasikiliza na shuhuda zao, Roho Mtakatifu alithibitisha kwenu kile ninachowaambia. Wameitwa na Mungu. Ninawaidhinisha na nawapenda na najua kwamba Bwana anawapenda na ataendelea kuwahimili katika huduma yao. Na ninafanya hivyo katika jina la Yesu Kristo, amina.

Muhtasari

  1. Handbook 2: Administering the Church (2010), 20.3.10.

  2. Ona George Q. Cannon, in “Minutes of a Conference,” Millennial Star, May 2, 1863, 275–76.