2010–2019
Furaha ya Kuishi Maisha ya Kikristo
Oktoba 2015


Furaha ya Kuishi Maisha ya Kikristo

Maisha yetu lazima yajikite kwa usahihi katika Kristo ikiwa tunataka shangwe kamili na amani katika maisha haya.

Ulimwengu tunamoishi inaweka shinikizo kubwa juu ya watu wema kila mahali ili kupunguza au hata kuachana na hali yao ya maisha ya haki. Hata hivyo, licha ya maovu na majaribu ambayo yanatuzingira kila siku, tunaweza, na tutapata furaha ya kweli leo kwa kuishi maisha ya Kikristo.

Kukita maisha yetu katika Yesu Kristo na injili Yake italeta uthabiti na furaha katika maisha yetu, jinsi mifano ifuatayo inavyoonyesha.

Mzee Taiichi Aoba wa Wale Sabini, ambaye anaishi katika kijiji kidogo cha mlima huko Shikoku, Japan, aliombwa kufundisha darasa katika mkutano wa vijana. “Simameni katika Maeneo Matakatifu” ndiyo iliyochaguliwa kama mada ya mkutano huo. Baada ya kutambua mada na kile cha kufundisha, Mzee Aoba aliamua kutumia wito wake kama chombo cha kufundishia. Kazi yake ni ya ufinyanzi.

Picha
Mzee Aoba alifanya ufinyazi pamoja na vijana

Mzee Aoba anasimulia kwamba darasa lake la vijana hakika lilipata uhai upya walipoona jinsi alivyoweza kimuujiza kubadili sura ya udongo katika mikono yake na kuwa masahani, bakuli, na vikombe. Baada ya maaonyesho yake, aliwauliza ikiwa mmoja wao angependa kujaribu. Wote wakainua mikono yao.

Mzee Aoba akaruhusu vijana kadhaa kujitokeza mbele ili kujaribu shughuli yao mpya. Walidhani, baada ya kumwangalia, kwamba hii itakuwa ni rahisi sana. Hata hivyo, hakuna hata mmoja wao aliyefanikiwa katika jitihada zao za kutengeza hata bakuli rahisi. Walitangaza: “Siwezi kufanya hivyo!” “Kwa nini hii ni vigumu sana?” “Hivi ni vigumu sana.” Matamshi haya yalifanyika huko udongo ukirushwa pande zote chumbani?

Aliwauliza vijana ni kwa nini walikuwa na ugumu kiasi hicho katika ufinyanzi. Walijibu kwa majibu mbalimbali. “Sina uzoefu wowote,” “Sijawahi kupata mafunzo,” au “Sina talanta.” Kulingana na matokeo, yote waliosema yalikuwa ya kweli; hata hivyo, sababu muhimu zaidi ya kushindwa kwao ilitokana na udongo kutokuwakwa katikati ya gurudumu. Vijana walidhani walikuwa wameweka udongo katikati, lakini kutokana na mtazamo wa kitaalamu, haukuwa katikati kabisa. Kisha akawaambia, “Hebu tujaribu tena mara nyingine.”

Picha
Mzee Aoba alifanya ufinyazi pamoja na vijana

Wakati huu, Mzee Aoba aliweka udongo katikati kabisa ya gurudumu na kisha akaanza kugeuza gurudumu, na kuweka shimo katikati ya udongo. Baadhi ya vijana walijaribu tena. Wakati huu kila mtu alianza kupiga makofi waliposema: “Ee, haitikisiki,” “Naweza kufanya hivyo,” au “Nimefanya hivyo!” Bila shaka, maumbo hayakuwa kamili, lakini matokeo yalikuwa tofauti kabisa kuliko ya jaribio la kwanza. Sababu ya mafanikio yao ilikuwa ni kuwa udongo ulikuwa umewekwa kikamilifu katikati ya gurudumu.

Ulimwengu ambako tunaishi ni sawa na gurudumu la mfinyanzi linalozunguka, na kasi ya gurudumu hiyo ikiongezeka. Kama udongo kwenye gurudumu la mfinyanzi, ni lazima sisi tuwe katikati pia. Msingi wetu, katikati ya maisha yetu, lazima iwe Yesu Kristo na injili Yake. Kuishi maisha ya Kikristo inamanisha tunajifunza kuhusu Yesu Kristo na injili Yake na kisha tunafuata mfano Wake na kushika amri Zake kwa usahihi.

Nabii wa kale Isaya alisema, “Lakini sasa, Ee Bwana, wewe u baba yetu; sisi tu udongo, nawe u mfinyanzi wetu; sisi sote tu kazi ya mikono yako.”1

Ikiwa maisha yetu ni yamewekwa kwa Yesu Kristo, Anaweza kutufinyanga vilivyo kuwa yule tunapaswa kuwa ili kurudi kwa uwepo wa Wake na wa Baba wa Mbinguni katika ufalme wa selestia. Furaha tunayiopata katika maisha haya italingana na jinsi maisha yetu yalivyowekwa juu ya mafundisho, mfano, na dhabibu ya upatanisho wa Yesu Kristo.

Ndugu na dada, nilizaliwa katika familia yenye vizazi vingi ya WSM, hivyo baraka na furaha ya kuwa na injili ya Yesu Kristo kama msingi wa utamaduni wetu wa familia ulifumwa katika maisha yetu ya kila siku. Ilikuwa wakati wangu wa misheni tu kama kijana nilipogundua matokeo chanya ambayo ukamilifu wa injili ya Yesu Kristo unao juu ya wale ambao hawajawahi kuona baraka zake katika maisha yao. Mstari huu katika Mathayo huonyesha mchakato ambao watu ambao wameongolewa katika injili ya Yesu Kristo huona: “Tena ufalme wa mbinguni umefanana na hazina iliyositirika katika shamba; ambayo mtu alipoiona, aliificha; na kwa furaha yake akaenda akauza alivyo navyo vyote, akalinunua shamba lile.”2

Acha nishiriki nanyi mfano kutoka Kitabu cha Mormoni ambao unaelezea kile mwongofu mmoja alikuwa tayari kulipa ili kupata furaha inayohusiana na kupata hazina iliyonenwa na Yesu katika fumbo la hazina iliyofichika shambani.

Kumbuka katika kitabu cha Alma, sura ya 20, Amoni na Lamoni walikuwa wakisafiri katika mji wa Middoni kwa lengo la kutafuta na kutoa Haruni ndugu yake Amoni kutoka gerezani. Wakati wa safari yao walikutana na babake Lamoni, ambaye alikuwa mfalme wa Walamani juu ya nchi yote.

Mfalme alikasirika sana kwamba mwanawe Lamoni alikuwa safarini na Amoni, mmisionari Mnefi, ambaye alimwona kama adui. Alihisi kwamba mwanawe angehudhuria karamu kubwa ambayo alikuwa amefadhili kwa ajili ya wanawe, na watu wake. Mfalme huyu Mlamani aliudhika sana kiasi kwamba aliamuru mwanawe Lamoni kumuua Amoni na upanga wake. Wakati Lamoni alipokataa, mfalme alitoa upanga wake mwenyewe ili amchinje mwanawe kwa kuasi; hata hivyo, Amoni aliingilia kati ili kuokoa maisha ya Lamoni. Hatimaye alimlemea mfalme na angeweza kumuua.

Hivi ndivyo mfalme alimwambia Amoni alipojikuta mwenyewe katika hali hii maisha-na-kifo: “Ukiniokoa nitakupa chochote utakachoniuliza, hata kama ni nusu ya ufalme.”3

Basi mfalme alikuwa tayari kulipa thamani ya nusu ya ufalme wake ili kuokoa maisha yake mwenyewe. Mfalme lazima alikuwa ameshangaa wakati Amoni aliomba tu amwachilie nduguye, Haruni na washirika wake kutoka gerezani na kwamba mwanawe Lamoni ahifadhi ufalme wake.

Baadaye, kutokana na tukio hili, kaka yake Amoni Haruni aliachiliwa kutoka gerezani Midoni. Baada ya kuachiliwa kwake alivutiwa kusafiri mahali ambapo mfalme Mlamani alitawala juu ya nchi. Haruni alijulishwa kwa mfalme na alikuwa na fursa ya kumfundisha kanuni za injili ya Yesu Kristo, ikiwemo mpango mkuu wa ukombozi. Mafundisho ya Haruni yalimvutia mfalme zaidi.

Majibu ya mfalme kwa mafundisho ya Haruni yanapatikana katika mstari 15 wa Alma, mlango wa 22 ”Na ikawa kwamba baada ya Haruni kumwelezea hivi vitu, mfalme alisema: Nitafanya nini ili nipate uzima wa milele ambao umeuzungumzia? Ndio, nitafanya nini ili nizaliwe kwa Mungu, ili hii roho mbovu ing’olewe nje ya mwili wangu, na nipokee Roho yake, ili niweze kujazwa na shangwe, ili nisitupiliwe nje siku ya mwisho? Tazama, alisema, nitatoa umiliki wangu wote, ndio, nitaacha ufalme wangu, ili nipokee hii shangwe kuu.”

Cha kushangaza sana, tofauti na kutoa nusu ya utawala wake ili kuokoa maisha yake, mfalme Mlamani alikuwa tayari kutoa utawala wake wote ili apate shangwe inayotokana na ufahamu, kukubali, na kuishi injili ya Yesu Kristo .

Mke wangu, Nancy, pia ni mwongofu wa Kanisa. Amenitajia mara nyingi kwa miaka furaha aliyoona katika maisha yake tangu kuipata, kuikubali, na kuishi injili ya Yesu Kristo. Kinachofuata ni mtazamo kutoka kwa Dada Maynes juu ya uzoefu wake:

“Kama kijana mzima katika miaka yangu ya 20, nilikuwa katika kiwango maishani mwangu wakati nilijua kwamba nilihitajika kubadilisha kitu ili kuwa mtu mwenye furaha. Nilihisi kama nilikuwa nimepotea bila kusudi halisi na mwelekeo, na sikujua wapi pa kwenda ili kuupata. Nilikuwa nikijua daima kwamba Baba wa Mbinguni alikuwepo na mara kwa mara katika maisha yangu niliwahi kuomba, nikihisi kwamba Alinisikiliza.

“Nilipoanza utafiti wangu, nilihudhuria makanisa mbalimbali lakini kila mara ningerudia hisia zile zile na kuvunjika moyo. Najisikia mwenye baraka sana kwa sababu maombi yangu kwa ajili ya mwelekeo na kusudi katika maisha hatimaye yalijibiwa, na ukamilifu wa injili ya Yesu Kristo uliletwa maishani mwangu. Kwa mara ya kwanza nilihisi kama nilikuwa na madhumuni, na mpango wa furaha ulileta furaha halisi katika maisha yangu.”

Uzoefu mwingine kutoka Kitabu cha Mormoni unaelezea wazi wazi jinsi kuishi maisha ya Kikristo kunaweza kutujaza na furaha kubwa hata wakati tumezungukwa na matatizo ya ajabu.

Baada ya nabii Lehi na familia yake kuhama Yerusalemu mnamo 600 k.k., walitanga takriban miaka minane huko nyikani mpaka hatimaye waliwasili katika nchi walioita Neema, ambayo ilikuwa karibu na pwani. Nefi anaelezea maisha yao ya dhiki nyikani kwa njia: “Tulipata mateso na masumbuko mengi,…hata mengi zaidi kwamba hatuwezi kuandika yote.”4

Wakati walipokuwa Neema, Nefi alikabithiwa na Bwana wajibu wa kujenga merikebu ambayo ingewavukisha baharini kwenda nchi ya ahadi. Baada ya kuwasili katika nchi ya ahadi, migogoro mikubwa iliendelea kujitokeza kati ya watu ambao wameweka maisha yao katika Kristo na wasioamini ambao walifuata mifano ya Lamani na Lemueli. Hatimaye, hatari ya vurugu kati ya makundi haya mawili ilikuwa kubwa sana kiasi kwamba Nefi na wale waliofuata mafundisho ya Bwana walijitenga na kukimbilia nyikani kwa usalama. Kwa wakati huu, miaka 30 baada ya Lehi na familia yake kutoka Yerusalemu, Nefi anatoa kauli ilyoandikwa vizuri na ya kushangaza, hasa baada ya kuandika katika maandiko taabu nyingi na mateso yailiyowakabili kwa muda mrefu. Haya ni maneno yake: “Na ikawa kwamba tuliishi kwa furaha.”5 Bila kujali matatizo yao, waliweza kuishi kwa namna ya furaha kwa sababu walijengwa ndani ya Kristo na Injili Yake.

Ndugu na dada zangu, kama vile udongo kwenye gurudumu la mfinyanzi, maisha yetu lazima yajikite kwa usahihi katika Kristo ikiwa tunataka shangwe kamili na amani katika maisha haya. Mifano ya mfalme Mlamani; mke wangu, Nancy; na watu wa Nefi wote wanaunga mkono kanuni hii ya kweli.

Nawatolea ushuhuda wangu leo ​​kwamba sisi pia tunaweza kupata amani, hiyo furaha, hiyo shangwe kamili tukichagua kuishi maisha ya Kikristo, katika jina la Yesu Kristo, amina.