2010–2019
Kuidhinishwa kwa Maafisa wa Kanisa
Oktoba 2015


Kuidhinishwa kwa Maafisa wa Kanisa

Kina ndugu na kina dada, Rais Monson ameomba kwamba sasa niwawasilishe kwenu Viongozi Wenye Mamlaka, Sabini wa Eneo, na marais wakuu wasaidizi wa Kanisa kwa kura yenu ya uidhinisho.

Imependekezwa kwamba tumwidhinishe Thomas Spencer Monson kama nabii, mwonaji, na mfunuaji na Rais wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho; Henry Bennion Eyring kama Mshauri wa Kwanza katika Urais wa Kwanza, na Dieter Friedrich Uchtdorf kama Mshauri wa Pili katika Urais wa Kwanza.

Wale wanaopendelea wanaweza kudhihirisha.

Wanaopinga, ikiwa kunao, wanaweza kudhihirisha

(Kura imerekodiwa.)

Imependekezwa kwamba tumwidhinishe Russell M. Nelson kama Rais wa Akidi ya Wale Mitume Kumi na Wawili na wafuatao kama washiriki wa akidi hiyo: Russell M. Nelson, Dallin H. Oaks, M. Russell Ballard, Robert D. Hales, Jeffrey R. Holland, David A. Bednar, Quentin L. Cook, D. Todd Christofferson, Neil L. Andersen, na, kama washiriki wapya wa Akidi ya Kumi na Wawili, Ronald A. Rasband, Gary E. Stevenson, na Dale G. Renlund.

Wanaopendelea tafadhali onyesheni kwa ishara ya kuinua mkono.

Wanaopinga kama kunao wanaweza kudhihirisha

(Kura imerekodiwa.)

Imependekezwa kwamba tuwaidhinishe washauri katika Urais wa Kwanza na Mitume Kumi na Wawili kama manabii, waonaji, na wafunuaji.

Wote wanaopendelea, tafadhali dhihirisheni.

Kinyume, ikiwa kuna yeyote, kwa ishara hiyo hiyo.

(Kura imerekodiwa.)

Kwa sababu ya wito wao kuhudumu kama washiriki wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili, sisi kwa hivyo tunawaachilia Ronald  A. Rasband kama mshiriki wa Urais wa Sabini, Mzee Rasband na Mzee Dale  G. Renlund kama washiriki wa Akidi ya Kwanza ya Sabini.

Wale wanaopenda kujiunga katika kura ya shukrani wanaweza kudhihirisha.

Imependekezwa kwamba tuwapumzishe kwa shukrani kwa huduma yao ya kujitolea: Mzee Don  R. Clarke kama mshiriki wa Jamii ya Kwanza ya Wale Sabini na Wazee Koichi Aoyagi na Bruce  A. Carlson kama washiriki wa Jamii ya Pili ya Wale Sabini na kuwatenga kama Viongozi Wenye Mamlaka waliostaafu.

Wale wanaopenda kujiunga nasi katika kuonyesha shukrani kwa huduma yao bora, tafadhali dhihirisheni.

Vilevile tunawasilisha kupumzishwa kwa Serhii  A. Kovalov kama Sabini wa Eneo.

Wale wanaopenda kujiunga na sisi katika kuonyesha shukrani kwa huduma yake, tafadhali dhihirisheni.

Kwa wakati huu, tunatambua kupumzishwa kwa Ndugu John  S. Tanner kama mshauri wa kwanza katika urais mkuu wa Shule ya Jumapili na Ndugu Devin  G. Durrant kama mshauri wa pili katika urais mkuu wa Shule ya Jumapili. Kama ilivyotangazwa hapo mapema, Ndugu Tanner ameteuliwa kuhudumu kama rais wa BYU–Hawaii.

Wote wanaopenda kujiunga na sisi katika kuonyesha shukrani kwa ndugu hawa kwa huduma yao na kujitolea kwao, tafadhali dhihirisheni.

Ndugu Devin  G. Durrant sasa ameitwa kuhudumu kama mshauri wa kwanza katika urais mkuu wa Shule ya Jumapili na Ndugu Brian  K. Ashton kuhudumu kama mshauri wa pili katika urais mkuu wa Shule ya Jumapili.

Wote wanaopendelea, tafadhali dhihirisheni.

Wanaopinga, ikiwa kunao.

Imependekezwa kwamba tuwaidhinishe Viongozi Wengine Wenye Mamlaka, Sabini wa Eneo, marais wasaidizi wakuu kama ilivyoundwa sasa.

Wote wanaopendelea, tafadhali dhihirisheni.

Wanaopinga, ikiwa kunao.

Kupiga kura kumerekodiwa. Tunaalika wale huenda waliopinga mapendekezo yeyote kuwasiliana na marais wao wa vigingi.

Ndugu na dada, tunashukuru imani yenu na maombi kwa niaba ya viongozi wa Kanisa.

Sasa tunawaomba washiriki wapya wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili wachukue mahali pao kwenye jukwaa. Watakuwa na fursa ya kutuhutubia hapo kesho asubuhi.